Dr. Hassan Mshinda, DG wa COSTECH...

Kama alikuwa anafanyakazi nzuri huko Ifakara ameondoka kwa nini kuja COSTECH? Ninyi wanasayansi na watafiti mliobobea nini tofauti ya taasisi hizi mbili? NIMR nao wanafanya nini?
 
Waungwana

Mimi niliwahi kufanya kazi pale COSTECH, kabla ya Dr. Mshinda kuteuliwa kushika nafasi hiyo. Ninachowaambia ni hiki:

  1. COSTECH haieleweki. Jaribu kumwuliza mwanafunzi wa shule yoyote ya Sekondari, akuelezee COSTECH ni nini. Halafu sikilizia majibu yake.
  2. Tafiti nyingi sana zimefanyika na zimesimamiwa na COSTECH, lakini matokeo yake yanawekwa kwenye makabati. End of story.
  3. Wakurugenzi waliohamishwa walikuwa wamepoteza dira, walisahau kwamba kazi kuu ya COSTECH ilikuwa ni kufanya tafiti na kuishauri serikali kuhusu namna ya kutatua matatizo yanayoikabili Tanzania kupitia Sayansi na Teknolojia, ndio maana inaitwa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia!
Anachokitaka Mshinda ni damu mpya, ili COSTECH ifufuliwe. Kwa sasa, COSTECH ni sawa na taasisi mfu, haina dira, malengo yake yanajulikana, lakini kuna dereva tu, makondakta wa kumsaidia dereva hawapo. Bora waende watu watakaohakikisha kazi inafanyika, kuliko watakaopiga bla bla!

Ninakijua ninachokiongelea. Kwa sasa tunahitaji damu mpya, fikra mpya, mtazamo mpya, malengo mapya na dira mpya!

Vinginevyo, hata hizo tafiti zinazofanyika hazitasaidia kitu! Hivi mnafahamu kwamba ndani ya miaka 10 ijayo tunao uwezo wa kumaliza kabisa tatizo la umeme, tena bila kutumia nishati itokanayo na petroli?
 
mshinda yuko sahihi na kufukuza hao ilikuwa sahihi...ni kichwa hasa na anachofanya ni kusafisha uchafu uliopo costech....by the way huyu si aliteuliwa na rais sasa mambo ya kukwalify yanakujaje....udini ni mdini dana kwa msiojua fba walimuweka chini ya uangalizi maana kuna mtu aliyelipua ubalozi wa usa kenya ana links na mkewe mshinda....ushanifahamu
 
waliohamishwa ni ma-directors wa 3 ( dr matheo raphael, dr rose kingamkono na mr eliab chijoriga) wengine ni scientific staff...nao ni dr makene, lambo mayenga (chief accountant), elikira mathew(mhasibu), wengine nao scientific staff ni charles yongolo, enock mpenzwa, jonas kamaleki, PC chuwa, salvatory mushi, rogers alfayo, godlease malisa, jumanne bwamkuu..

Siwafahamu hao wengine, lakini kwa hao niliowawekea red nawafahamu...Mume wa Dr Rose Kingamkono (tulikuwa tunamuita mzee Kinga) alikuwa Financial and Administration Manager pale IHI wakati Dr Mshinda akiwa mkurugenzi, huyu anakuwa 2nd or 3rd in command pale IHI baada ya DG na walikuwa marafiki (nachelea kuamini kama anaweza mfanyia 'faulo' mke wa rafiki na colleague yake for years!). Jumanne (Africa) Bwamkuu hakufukuzwa, alipata kazi kama consultant Uholanzi (Nedherland) ambako yuko mpaka sasa, sio fitina ya Dr Mshinda. bado sijaona hoja...
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hii thread haitoshi kuongelea mafanikio ya Dr Mshinda..google na utaona hundreds of pages!

Dr Mshinda alipanua IHI toka kuwa na field offices 2 (STILF Ifakara na Rufiji) mpaka kuwa 5 accredited centre (Ifakara, Rufiji, Bagamoyo, Mtwara na Dar es salaam), kufungua demographic surveilance sites 3 Africa (Kilombero, Ulanga, Rufiji) na kaondoka akifungua ya 4 Kigoma (hii ndio iliyompa uwenyekiti wa INDEPTH Africa)...Bagamoyo centre ilifunguliwa chini ya uongozi wake is one of the centres of excellence for clinical research in Africa...IHI has an accredited entomological lab (Ifakara) in Africa, and a very strong entomology team...etc! Ingia hapa uone mafanikio ya IHI Mshinda akiwa DG, na mafanikio ya Mshinda binafsi kama mwanasayansi: www.ihi.or.tz

Riwa,

Kwa mgonjwa anayeugua malaria au mtu aliyefiwa na mtoto, ndugu, e.t.c hayo bolded success kwake hayana maana kabisa!

Haiitaji Phd kumi kupunguza au kuondoa ugonjwa wa Malaria hapa Tanzania ...

Na kama anaenda kufanya hayo hayo hapo COSTECH, kwa mtizamo wangu tutaendelea kuwa taifa la mazuzu!
 
Na kama tunasubiri watu wenye PhD waje kututokomezea Malaria au kuzuia vifo vya watoto wetu kwa Malaria basi na tuendelee tu kuwa mazuzu! Haingii akilini mtu mwenye PhD kafanya tafiti akapublish, akasababisha policy change, strategies zikatengenezwa na zikawa implemented huku donor wakimwaga lot of money....halafu wewe hutaki badili tabia zako hatarishi, unaugua Malaria, mwanao anakufa kwa Malaria, mkeo mimba inatoka kwa Malaria....halafu you blame it on success of Dr Mshinda!

The biggest failure of Malaria control in Tanzania is behavioural change...twende moja baada ya nyingine:

National Malaria Control Program imeweka strategies kadhaa kama mwelekeo wa vita dhidi ya Malaria
- Case management: ALu is one of the best Malaria treatment drugs katika ulimwengu wa leo, watu hawataki kutumia simply tu vidonge vingi na kwa siku tatu. Am a doctor, na simu ninazopata nyingi zinauliza dawa gani atatumia kwa mfupi kutibu Malaria aendelee kunywa pombe, au amekunywa dawa za Malaeria hajamaliza dozi lakini yuko poa kabisa, anaulizia kama anaweza kukatisha dozi ili anywe pombe.
- Vector control:
Vyandarua kila siku vinashushiwa hadithi, mara ukilalia vyeupe unasikia kama sanda, mara vina sumu vinadhuru, mara vinapunguza nguvu ya kiume, mara kuvulia samaki, wengine wanafunikia mchicha ndege wasile...hii ni intervention imethibitishwa na tafiti kuwa inapunguza maambukizi ya malaria.

IRS Lake zone watu wanalalamika kama hapo juu na wanakataa nyumba zao zisipulizwe

Watu nyumba manyasi kibao wanangoja mtu mwenye PhD aje awaambie watoe madimbwi na vichaka kwani ni mazalia ya mbu

Sasa hapo hata ukiwa na honors kwenye Malaria, watu hawabadiliki tabia, unategemea nini? Tuwabeze wanasayansi wetu kisa tu we umegoma kubadilika pamoja na elimu yote inayomwagwa kwa jamii kwa gharama kubwa!
 
thank you for clearing the air!!! no research no right to speak......NB: hassan kazaliwa, kalelewa hapa hapa tanzania.!! for more reference nendeni Moshi mtaa wa Liwali nyumba ya shehe Abdallah kuulizia vizuri, tupunguze umbea jamani heeee!!!
 
Sitaki ku koment maeneo mengine ya tuhuma hizi kwa kuwa siyajui. Ila Saidi Mwema asili yake ni Mngazija wa Comoro na mama yake ni mchaga ila Saidi mwenyewe alikulia ujombani kwake Moshi.... hivyo kwa kukiri kama Dr. Mshinda naye ni Mngazija inawezekana kweli kuna uhusiano wa kidugu kati ya Saidi na Hassan.

Kikwebo.

Wa Tng sasa imekuwa kali hii. Mnachunguzana mpaka asili zenu. Mbona hamukumchunguza Nyerere na kusema kuwa ana asili ya Kenya.

Sie yetu macho kwani kabisaaaa hapo kuna harufu kali sana ya UDINI na uvundo wa ukabila.

Poleni sana
 
Na kama tunasubiri watu wenye PhD waje kututokomezea Malaria au kuzuia vifo vya watoto wetu kwa Malaria basi na tuendelee tu kuwa mazuzu! Haingii akilini mtu mwenye PhD kafanya tafiti akapublish, akasababisha policy change, strategies zikatengenezwa na zikawa implemented huku donor wakimwaga lot of money....halafu wewe hutaki badili tabia zako hatarishi, unaugua Malaria, mwanao anakufa kwa Malaria, mkeo mimba inatoka kwa Malaria....halafu you blame it on success of Dr Mshinda!

The biggest failure of Malaria control in Tanzania is behavioural change...twende moja baada ya nyingine:

National Malaria Control Program imeweka strategies kadhaa kama mwelekeo wa vita dhidi ya Malaria
- Case management: ALu is one of the best Malaria treatment drugs katika ulimwengu wa leo, watu hawataki kutumia simply tu vidonge vingi na kwa siku tatu. Am a doctor, na simu ninazopata nyingi zinauliza dawa gani atatumia kwa mfupi kutibu Malaria aendelee kunywa pombe, au amekunywa dawa za Malaeria hajamaliza dozi lakini yuko poa kabisa, anaulizia kama anaweza kukatisha dozi ili anywe pombe.
- Vector control:
Vyandarua kila siku vinashushiwa hadithi, mara ukilalia vyeupe unasikia kama sanda, mara vina sumu vinadhuru, mara vinapunguza nguvu ya kiume, mara kuvulia samaki, wengine wanafunikia mchicha ndege wasile...hii ni intervention imethibitishwa na tafiti kuwa inapunguza maambukizi ya malaria.

IRS Lake zone watu wanalalamika kama hapo juu na wanakataa nyumba zao zisipulizwe

Watu nyumba manyasi kibao wanangoja mtu mwenye PhD aje awaambie watoe madimbwi na vichaka kwani ni mazalia ya mbu

Sasa hapo hata ukiwa na honors kwenye Malaria, watu hawabadiliki tabia, unategemea nini? Tuwabeze wanasayansi wetu kisa tu we umegoma kubadilika pamoja na elimu yote inayomwagwa kwa jamii kwa gharama kubwa!

Daktari Riwa nakubaliana na maelezo yako kwa kiasi kikubwa.

Jambo moja ambalo sikubaliani nawe moja kwa moja ni hili la kupambana na malaria. serikali yetu haijawekeza vya kutosha katika kupambana na malaria kwa kuwa ndio gonjwa linaloua watu wengi sana kuliko hata ngoma.

Serikali inategemea wafadhili ndio watoe fedha kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya, haitumii fedha za ndani kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya afya, bajeti ya 2011/2012 tulishuhudia bajeti ya afya ikipungua na mbaya zaidi sehemu kubwa ikitegemea fedha za wafadhili, wasipoleta fedha tutafanyeje? Mathalani zanzibar tunaambiwa wameweza kudhibiti malaria kwa kiasi kikubwa sana kwahiyo malaria kwao imeanza kuwa historia. Je SMZ imewezaje kumaliza malaria? je serikali yetu imefanya nini katika kukabiliana na malaria?kuna lolote imejifunza toka zanzibar?

Sidhani kama ni sahihi kupambana na malaria kwa ALU hata kama ni dawa nzuri kiasi gani wakati mazalia ya mbu hayajakabiliwa ipasavyo. Na katika hili la kupambana na vyanzo vya malaria kwa maana ya mazalia, wananchi peke yao hawawezi kufanikiwa bila usaidizi mkubwa wa serikali.

Kwa mfano tumeshuhudia mbu wakiwa wamezaliana katika mito na mabonde ambayo hayakaliwi na wananchi lakini ndiyo yenye mazalia ya kutisha ya mbu. Tunakumbuka ni kwa kiasi gani mbu wanazaliana bonde la msimbazi, je serikali imechukua hatua gani kukabiliana na mazalia ya mbu bonde la mto msimbazi? Ilifika mahali hospitali ya muhimbili kukawa hakukaliki wala hakulaliki mbu wanashambulia raia kama nyuki!!

Tukitaka kufanikiwa vita dhidi ya malaria serikali yetu iwekeze vya kutosha kwenye sekta ya afya kwa kutumia fedha zetu za ndani. Lakini hii ya kutegemea hisani ya watu wa marekani kila siku hatuwezi kufika popote, na bahati mbaya sana ukiongezea na tabia ya ufisadi miongoni mwa watumishi wa serikalini katika sekta ya afya ambao hutumia sehemu kubwa ya hayo mafungu ya wafadhili kuendesha semina na makongamano badala ya kuleta madawa ya kuua mazalia ya mbu.
 
Labda anaiboresha hii COSTECH, kwanza tupe list ya waliohamishwa.

UDINI NA UBAGUZI UPO PALE PALE, HAUHITAJI PhD la cheti, kama unabisha uliza selikari ya awamu hii na chambua kila mtu aliyepewa cheo kikubwa kma si ZAWADI na Uswahiba.

Kusema ana PhD ni hoja dhaifu, je hii ni kigezo cha ku-qualify COSTECH?
 
The biggest failure of Malaria control in Tanzania is behavioural change...

Kwahiyo mafanikio ya IHI yanapimwa vipi? Kama hawa Ma-Phd holder wanaondesha DFP na kulipwa na D hawajui kuwa tatizo letu la malaria lipo kwenye mienendo ya watu and yet wewe unashadidia kuwa wao ni VICHWA, then, I doubt, u-vichwa wao ni sawa na wale wanaotumia vyandarua kuvulia samaki...

Honestly, I can not see the reason why IHI ilianzishwa!

Tuwe wakweli na tuambiane ukweli, I do not care kuhusu the so called U-DINI wa huyo Dr M or I do not have anything personal against him ... But... Kama anafanyia kazi kwenye mazingira HAYA HAYA ambayo top scientists ni top politicians, HAWEZI kufanya lolote la maana hapo COSTECH ...! PERIOD
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Sidhani kama ni sahihi kupambana na malaria kwa ALU hata kama ni dawa nzuri kiasi gani wakati mazalia ya mbu hayajakabiliwa ipasavyo. Na katika hili la kupambana na vyanzo vya malaria kwa maana ya mazalia, wananchi peke yao hawawezi kufanikiwa bila usaidizi mkubwa wa serikali.

Mwita Manyara,

Hapo ndipo na mimi ninapoona tatizo la Malaria na magonjwa mengine yatokanayo lilipojikita ...

Chukulia mji kama Dar es Salaam - Asilimia 95 ya households wanatiririsha maji taka kwenye mitaro ya maji ya mvua! Mvua inapoanza kunyesha Mitaa ya Dar es Salaam INANUKA - Hii inawezekana according to Riwa ni ULIMBUKENI wa watu lakini kwa upande wa pili Ni nani anastahili kuweka miundo mbinu ya MAJI TAKA?

One very serious note, Hata uwe na VICHWA 1000 IHI, bila kuzuia mazalia ya mbu, HAITASAIDIA lolote! Donors & DFP & whatever have you ni kazi bure ... This applies in every single scientific research tunayotaka kufanya ...

Kwa mfano, ICT development haiwezzekani kuleta mabadiliko yoyote katika nchi kama nishati ya UMEME ipo kwenye hali kama hii... No NEVER!
 
Sikukimbia…nilikuwa na udhuru kidogo.

Wengi wenu mmemtetea Dr. Mshinda kwa kutumia kigezo cha usomi. Usomi wake hauna utata…buku tu amelichimba. Lakini nafikiri mmejisahaulisha ya kwamba usomi bila utendaji kazi mahili ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Wengine mmethubutu kusema kuwa the guy alifanya “wonders” kwenye mradi wa Malaria pale IHI. Kama ni kweli msemayo, mbona Malaria bado inaongoza kwa kuua nchini? Inaua kuliko ukimwi.

Acheni ushabiki wa kitabuni. Wangapi tuliwaamini na kuwapa dhamani ya uongozi kwa kutumia elimu yao, lakini wakalitenda taifa letu. Vipi kuhusu Andrew Chenge and co!!! Kitabu pekee sio kigezo kamili cha amana.

Huyu Dr. Mshinda mnaempamba humu amekaa COSTECH kwa miaka 3 sasa. Amefanya nini akiwa kama head wa taasisi, zaidi ya kulipendezesha jengo kwa kulipaka rangi na kuongeza uzio wa parking? Mpaka leo hii wanafunzi bado wanaogopa mchepuo wa sayansi kama ukoma. Hivi mmeshaenda kuzitembelea taasisi za utafiti mbalimbali nchini kuona jinsi zilivyozorota? Nyingi hazina hata single computer, let alone maabara. Kwa kipindi cha miaka 3 amefanya nini cha maana? Ni nini ameshauri serikali kuhusu njia ya kuongeza morali ya wanafunzi kwenye mchepuo wa sayansi?

Hivi nani alishawahi kuhudhuria kongamano lililoandaliwa na COSTECH, ambalo Dr.Mshinda nae alikuwepo? Huwezi kuamini….jamaa huwa anakaa kimya kama bubu. Muda wote anakuwa na arrogance look, kana kwamba wote mliokuwa mle ndani ni mambumbu. Na akihamua kufungua mdomo, basi hatataka kukosolewa. Ni type ya watakao “ndio mzee”muda wote.

Dr. Mshinda ilibidi aondoke IHI. Mambo yalishaanza kumshinda kule. Alikuwa ameshashtukiwa na alikuwa hana muda aonyeshwe mlango. Alilijua hilo, na ndio maana aliposikia post ya u-DG wa COSTECH ipo wazi, akaenda kulamba miguu ya mkulu kwa kupitia IGP (mtabisha, lakini kuna uhusiano wa karibu sana kati ya Dr. Mshinda na IGP Mwema). Kwanza ile post ya u-DG wa COSTECH ilikuwa bound kwa Dr. Kingamkono (huyu mama ni mmoja wa top ten female scientists nchini. Google ina kila aina ya info zake). Kuanzia uongozi wa wizara ya Sayansi na Teknolojia, mpaka bodi yake, walikuwa wameshamkubali huyu mama. Na ndio maana baada ya Gen. Kohi kuoneshwa mlango, huyu mama alikamata ile post kama acting DG kwa karibu mwaka mzima. Taa ilikuwa green kwake, mpaka memo ilipotoka kwa Mr. Prezidaa, na ndipo Dr. Mshinda alipobisha hodi COSTECH.

Dr. Matheo Raphael was no joke either. Huyu nae ni mtaalam aliyebobea kwenye masuala ya technology transfer. Unaweza kupata info zake kupitia google. Kuna bwana mmoja humu jamvini alinena kuwa alichofanya Dr. Mshinda nikukosea steps. Huwezi kuwaondoa wanasayansi waliobobea wote kwa mpigo, ingali unajua ya kuwa taifa letu lina upungufu wa wajuvi wa hiyo sekta. Mabadiliko COSTECH ilikuwa ni lazima. Taasisi ilikuwa imelala usingizi. Lakini kutimua watu wengi hivyo kwa pamoja sio solution ya kuiamsha. Ni kuipa dozi ya “nusu kaputi”…itachukuwa muda mrefu kuamka. Anataka fresh blood…ataitoa wapi, na wakati kuna upungufu wa wanasayansi? Au ndo atawakusanya wataalam wa Bcomm, Journalism, na Hotel management na kuwageuza kuwa wanasayansi? Maana huko ndo kimbilio la wanafunzi wengi. What a joke!!!

So usomi wa Dr. Mshinda hauna ubishi. Books, journals, na makaratasi mengine mengi tu yana prove usomi wake. Lakini utendaji kazi wake una walakini. Kitu ambacho watetezi wake mmefumbia macho (ingawaje mnajua) ni kuwa huyu bwana ni notorious wa fitna. Huyu bwana mnaweza mkacheka nae na even kuswali nae, lakini ukigeuka tu anaku-stab mgongoni vibaya sana. Ana rangi mbili. Kwa hiyo, kwa wale mnaofanya nae kazi na kumtetea hapa, all I can advise you is “watch your back.”

Kuhusu suala la udini, kusema kweli sina uhakika na hilo. Kuna tetesi zilikuwa IHI kuwa jamaa ndio hivyo tena. Lakini ni tetesi tu, siwezi kuzishikia bango. Inawezekana ni uzushi tu!

Of course, comparing with former COSTECH DG, Gen. Kohi, Dr. Mshinda is much better kiutendaji. Gen Kohi was a punk! Yeye alichokuwa anajali ni kwenda kuwinda kwa kutumia magari ya COSTECH kila weekend. He was living a lavish style kwa kutumia rasilimali za taifa.
 
  • Katika TZ kuna mambo mengi yanayofanywa hovyo hovyo na wataalam wetu (technocrats)wakishirikiana na wanasiasa za maji taka haswa pale ambapo wataalam hawa waliopewa dhamana ya kusimamia taasisi nyeti wanapoingiza siasa katika kazi zao kimaslahi.Hili tumeliona kwenye sekta nyingi muhimu(kama madini na nishati and others).Udhaifu huu kiutendaji umeongezeka sana kwasasa kiasi kwamba tunawaona hata baadhi ya hawa wataalam wakijiingiza kwenye siasa za maji taka na kusahau kutumikia fani zao.That said, niseme tu pia wapo wanataaluma wachache ambao kwa kweli wamefanya kazi kubwa kwa taifa na kazi zao zimeonekana ndani na nje ya nchi. Mtafiti (researcher)makini anatambulika kwa vigezo mbalimbali mfano: ubora na wingi wa machapisho/maandiko ya kazi zake(publications),implementation ya kazi zake katika sekta husika na hata kufikia kwenye policy change...na pia matumizi ya kazi zake katika kutengeneza guidelines, na pia kiwango cha innovations kwenye kazi zake (hili laweza kupimwa kwa wingi wa patents za innovations alizofanya mtafiti).Ubora na utendaji wa mtafiti haupimwi kwa mtazamo wake kidini bali kwa kazi zake.
  • Kwa kuwa siasa zimeingilia sana fani za wataalamu wetu TZ basi mtu kuwa associate Prof au Prof si kipimo tena cha ubora wa mtafiti TZ(hili tumeliona sana vyuoni).Labda niongeze tu kuwa Professor wa kitanzania nionavyo huwezi kumlinganisha na Professor wa China au US au Europe ukitazama ubora wa kazi zao na jinsi zinavyokuwa implemented na kuleta tija.Niseme tu kuwa inasikitisha sana TZ nimeona....maprofessor wetu wanakaa maofisini wakati ukiwa kwa wenzetu nje wanachapa kazi kwelikweli.Pia niongeze tu kuwa nimeona wanafunzi wa PhD nje wakifanya mambo ambayo maprofessor wetu hawawezi kuyafanya.(hata kama wakipewa nyenzo).
  • Kwa mtazamo huo nakubaliana na Riwa kuwa kweli Dr.Mshinda ni kichwa na amefanya mambo ambayo yameonekana kitija na anakubalika kwa kweli.Pale IHI ameacha legacy kama mtendaji makini.Ni kweli TZ tuna wataalam wachache ambao wanaendelea kutetea nfani zao....bila kujiingiza kwenye hizi siasa za maji taka na huyu bwana amejitahidi.Niseme tu hapimwi mtu kwa msimamo wake kidini please.Mabadiliko ya hao jamaa costec yawezekana kabisa yametokana na capacity zao kwani kwa kweli costec ilikua haipo.....na haisikiki zaidi ya kukaa maofisini na kukalia pesa na proposal za watafiti za miradi.Ifike mahali wa TZ tuwe watu wa kukubali mabadiliko........tunadai mabadiliko kila kukicha .....yakifanyika tunalalama....kama kuna fitna za udini i don't know lakini huwezi kuondoa watu 15 eti kwasababu ya udini..
  • Nizidi kuongeza tu kuwa tusiharibu jina zuri la taasisi ya Ifakara kwani ni taasisi kati ya chache sana tulizo nazo TZ ambazo ni makini sana....hawa jamaa wana venture kali sana na swiss tropical institute na wanatoa shule za kufa mtu kwa watafiti pale.(Ifakara and swiss tropical institute)...if you are a serious medical researcher ifakara its a good place to be kwa kweli..Hata hizi dawa za malaria mnazosikia zinabadilika kila leo.....haya ni matokeo ya research za IHI (si NIMR please!).Mimi kwa mtizamo wangu IHI ni makini by far kuzidi NIMR. NIMR is just a national body ambapo ethical clearance lazima zipite pale, patent applications lazima zipite pale.....n.k .k lakini kwa research per se......Ifakara is the best my friends.Sasa huwezi kuzungumzia mafanikio ya ifakara bila kumzungumzia Dr.Mshindo....(hicho ndicho kipimo wazee si dini).
  • Labda kwa kumalizia niongeze tu kuwa.....ifike mahali siasa za chooni nchi hii zitenganishwe na fani za kitaaluma ili mambo yaende nchi hii.....hakuna nchi duniani iliyoendelea bila matumizi ya research.......zungumzia USA au europe au china zote zimeendelea kwasababu viongozi wao wanajali umuhimu wa research and development.Tanzania imebaki kuwa nchi ya viongozi kuwa ombaomba tu.......hata vyuo vyetu hatuvijali.......yaani imekuwa watu wanataka wawe wanasiasa tu.....i swear we will never develop like this never......wanataaluma wanataka kuwa wanasiasa.............matechnocrats wanafanya kazi kisiasa, sasa nani atajenga nchi???????
  • Nimeona mmegusia suala la research za malaria.................imekuwa badala ya viongozi wetu kukazia mkazo kwenye tafiti za malaria haswa kwenye kinga........(ambazo hufanyika pale ifakara)...wao viongozi wamebaki kukimbilia marekani kwa wafadhili kuomba eti nchi ipatiwe vyandarua vya kujikinga na mbu!!!!!!ndugu zangu hatuwezi kamwe kungamiza malaria kwa kutumia vyandarua........unapotumia vyandarua haumwui mbu bali unamkimbia.....na hili kamwe si suluhisho la tatizo la malaria TZ.
 
mshinda yuko sahihi na kufukuza hao ilikuwa sahihi...ni kichwa hasa na anachofanya ni kusafisha uchafu uliopo costech....by the way huyu si aliteuliwa na rais sasa mambo ya kukwalify yanakujaje....udini ni mdini dana kwa msiojua fba walimuweka chini ya uangalizi maana kuna mtu aliyelipua ubalozi wa usa kenya ana links na mkewe mshinda....ushanifahamu

Mkuu hapo sikubaliani nawewe kwamba ukiwekwa tu kwenye FBI watchlist basi tafsiri yake ni kuwa wewe ni mdini!... Hii imenistua kama watu wanaweza kustrecth mambo hivi. Hivi unaijua FBI watchlist ina mapana na marefu gani? Si ajabu hata kuna baadhi ya viongozi wetu wa hapa na hata wa huko kwao U.S wakawepo kwenye FBI watchlist... Na pengine hata wewe upo kwenye watchlist bila kujijua.

Halafu taarifa za kuwa kiongozi wa IHI yuko kwenye FBI watchlist kutokana na link ya mkewe ni Dr. Salim Abdullah, na sio Dr. Hassan Mshinda. Ingawa baadae walikuja kumclear Dr. Abdullah na hata vyombo vyetu vya usalama viliarifiwa the guy is cleared.
 
Na kama tunasubiri watu wenye PhD waje kututokomezea Malaria au kuzuia vifo vya watoto wetu kwa Malaria basi na tuendelee tu kuwa mazuzu! Haingii akilini mtu mwenye PhD kafanya tafiti akapublish, akasababisha policy change, strategies zikatengenezwa na zikawa implemented huku donor wakimwaga lot of money....halafu wewe hutaki badili tabia zako hatarishi, unaugua Malaria, mwanao anakufa kwa Malaria, mkeo mimba inatoka kwa Malaria....halafu you blame it on success of Dr Mshinda!

The biggest failure of Malaria control in Tanzania is behavioural change...twende moja baada ya nyingine:

National Malaria Control Program imeweka strategies kadhaa kama mwelekeo wa vita dhidi ya Malaria
- Case management: ALu is one of the best Malaria treatment drugs katika ulimwengu wa leo, watu hawataki kutumia simply tu vidonge vingi na kwa siku tatu. Am a doctor, na simu ninazopata nyingi zinauliza dawa gani atatumia kwa mfupi kutibu Malaria aendelee kunywa pombe, au amekunywa dawa za Malaeria hajamaliza dozi lakini yuko poa kabisa, anaulizia kama anaweza kukatisha dozi ili anywe pombe.
- Vector control:
Vyandarua kila siku vinashushiwa hadithi, mara ukilalia vyeupe unasikia kama sanda, mara vina sumu vinadhuru, mara vinapunguza nguvu ya kiume, mara kuvulia samaki, wengine wanafunikia mchicha ndege wasile...hii ni intervention imethibitishwa na tafiti kuwa inapunguza maambukizi ya malaria.

IRS Lake zone watu wanalalamika kama hapo juu na wanakataa nyumba zao zisipulizwe

Watu nyumba manyasi kibao wanangoja mtu mwenye PhD aje awaambie watoe madimbwi na vichaka kwani ni mazalia ya mbu

Sasa hapo hata ukiwa na honors kwenye Malaria, watu hawabadiliki tabia, unategemea nini? Tuwabeze wanasayansi wetu kisa tu we umegoma kubadilika pamoja na elimu yote inayomwagwa kwa jamii kwa gharama kubwa!

Umesema sawa kabisa lakini pia badala ya kulaumu commoners angalia pia hizi research zetu zinafanywaje; wamekaa tu watu wa bio-medical sciences kuangalia scientific findings pekee bila kuangalia anthropological na socio-logical issues za consumers wa tafiti zao then unakuja na lawama badala ya kuona wapi hizo strategy zime fail kuleta expected results. Behavioural change ni one of the research agenda zilizotakiwa kwenda pamoja na scientific research za transmition chain-break down.

Watu wa basic research na hasa hard core scientist wakubali kuwa research zao bila kwenda na applied research basi finding zao zitabaki kupamba Cv zao tu bila kuleta impact yeyote at society's level.
 
  • Katika TZ kuna mambo mengi yanayofanywa hovyo hovyo na wataalam wetu (technocrats)wakishirikiana na wanasiasa za maji taka haswa pale ambapo wataalam hawa waliopewa dhamana ya kusimamia taasisi nyeti wanapoingiza siasa katika kazi zao kimaslahi.Hili tumeliona kwenye sekta nyingi muhimu(kama madini na nishati and others).Udhaifu huu kiutendaji umeongezeka sana kwasasa kiasi kwamba tunawaona hata baadhi ya hawa wataalam wakijiingiza kwenye siasa za maji taka na kusahau kutumikia fani zao.That said, niseme tu pia wapo wanataaluma wachache ambao kwa kweli wamefanya kazi kubwa kwa taifa na kazi zao zimeonekana ndani na nje ya nchi. Mtafiti (researcher)makini anatambulika kwa vigezo mbalimbali mfano: ubora na wingi wa machapisho/maandiko ya kazi zake(publications),implementation ya kazi zake katika sekta husika na hata kufikia kwenye policy change...na pia matumizi ya kazi zake katika kutengeneza guidelines, na pia kiwango cha innovations kwenye kazi zake (hili laweza kupimwa kwa wingi wa patents za innovations alizofanya mtafiti).Ubora na utendaji wa mtafiti haupimwi kwa mtazamo wake kidini bali kwa kazi zake.
  • Kwa kuwa siasa zimeingilia sana fani za wataalamu wetu TZ basi mtu kuwa associate Prof au Prof si kipimo tena cha ubora wa mtafiti TZ(hili tumeliona sana vyuoni).Labda niongeze tu kuwa Professor wa kitanzania nionavyo huwezi kumlinganisha na Professor wa China au US au Europe ukitazama ubora wa kazi zao na jinsi zinavyokuwa implemented na kuleta tija.Niseme tu kuwa inasikitisha sana TZ nimeona....maprofessor wetu wanakaa maofisini wakati ukiwa kwa wenzetu nje wanachapa kazi kwelikweli.Pia niongeze tu kuwa nimeona wanafunzi wa PhD nje wakifanya mambo ambayo maprofessor wetu hawawezi kuyafanya.(hata kama wakipewa nyenzo).
  • Kwa mtazamo huo nakubaliana na Riwa kuwa kweli Dr.Mshinda ni kichwa na amefanya mambo ambayo yameonekana kitija na anakubalika kwa kweli.Pale IHI ameacha legacy kama mtendaji makini.Ni kweli TZ tuna wataalam wachache ambao wanaendelea kutetea nfani zao....bila kujiingiza kwenye hizi siasa za maji taka na huyu bwana amejitahidi.Niseme tu hapimwi mtu kwa msimamo wake kidini please.Mabadiliko ya hao jamaa costec yawezekana kabisa yametokana na capacity zao kwani kwa kweli costec ilikua haipo.....na haisikiki zaidi ya kukaa maofisini na kukalia pesa na proposal za watafiti za miradi.Ifike mahali wa TZ tuwe watu wa kukubali mabadiliko........tunadai mabadiliko kila kukicha .....yakifanyika tunalalama....kama kuna fitna za udini i don't know lakini huwezi kuondoa watu 15 eti kwasababu ya udini..
  • Nizidi kuongeza tu kuwa tusiharibu jina zuri la taasisi ya Ifakara kwani ni taasisi kati ya chache sana tulizo nazo TZ ambazo ni makini sana....hawa jamaa wana venture kali sana na swiss tropical institute na wanatoa shule za kufa mtu kwa watafiti pale.(Ifakara and swiss tropical institute)...if you are a serious medical researcher ifakara its a good place to be kwa kweli..Hata hizi dawa za malaria mnazosikia zinabadilika kila leo.....haya ni matokeo ya research za IHI (si NIMR please!).Mimi kwa mtizamo wangu IHI ni makini by far kuzidi NIMR. NIMR is just a national body ambapo ethical clearance lazima zipite pale, patent applications lazima zipite pale.....n.k .k lakini kwa research per se......Ifakara is the best my friends.Sasa huwezi kuzungumzia mafanikio ya ifakara bila kumzungumzia Dr.Mshindo....(hicho ndicho kipimo wazee si dini).
  • Labda kwa kumalizia niongeze tu kuwa.....ifike mahali siasa za chooni nchi hii zitenganishwe na fani za kitaaluma ili mambo yaende nchi hii.....hakuna nchi duniani iliyoendelea bila matumizi ya research.......zungumzia USA au europe au china zote zimeendelea kwasababu viongozi wao wanajali umuhimu wa research and development.Tanzania imebaki kuwa nchi ya viongozi kuwa ombaomba tu.......hata vyuo vyetu hatuvijali.......yaani imekuwa watu wanataka wawe wanasiasa tu.....i swear we will never develop like this never......wanataaluma wanataka kuwa wanasiasa.............matechnocrats wanafanya kazi kisiasa, sasa nani atajenga nchi???????
  • Nimeona mmegusia suala la research za malaria.................imekuwa badala ya viongozi wetu kukazia mkazo kwenye tafiti za malaria haswa kwenye kinga........(ambazo hufanyika pale ifakara)...wao viongozi wamebaki kukimbilia marekani kwa wafadhili kuomba eti nchi ipatiwe vyandarua vya kujikinga na mbu!!!!!!ndugu zangu hatuwezi kamwe kungamiza malaria kwa kutumia vyandarua........unapotumia vyandarua haumwui mbu bali unamkimbia.....na hili kamwe si suluhisho la tatizo la malaria TZ.

Siasa ndiyo activity/investment inayo produce big marginal returns na kwa muda mfupi; ebu cheki kuna prof mmoja alistaafu akapewa kiinua mgongo cha 16M baada ya kulitumikia taifa lake kwa takribani 30 years tena kama mtu mkubwa tu huko chuoni; bahati yake akapata ubunge mwaka huo huo na baada ya miaka mitano akapata more than 70M na bado ameendelea na hiyo kazi ya kuuza maneno/uwongo mtaani and on top miradi yake kadhaa inaendelea kupata monopoly kwa sera wanazozitengeneza then wewe unakuja na hadithi za paukwa pakawa nani atakuelewa?

Mpaka tutakapo ifanya siasa isiwe sehemu ya poverty alleviation at individual level ndipo ambapo wataalamu na wengine watakapo ondoa siasa kwenye shughuli zao vinginevyo endelea tu kulia mpaka uamue kuwa active kwenye kuwapa raia elimu ya uraia ili hizi externality ziwe cleared na policies zetu.
 
Mkuu kinachofanyika hapo COSTECH ndicho kinafanyika UDOM, kuna ubaguzi wa kidini. Ukiwa mtu wa dini amabayo wanailalamikia hupati kazi na walioajiriwa wanatishiwa kufukuzwa. Nasikia fukuza fukuza imepamba moto UDOM. Kwa kweli huu upendeleo utaliangamiza taifa hili. Nasikia hawa jamaa wanajiita wao kwa wao (watu dini moja) na siyo qualification, kupeana kazi zote za senior. Madai yao wao tu ndiyo wawepo chuo kizima.

we mtu acha unafiku..embu toa data stahiki.. una habari kuwa total number ya stuff udom wakristo ni zaidi ya mara mbili ya waislam.. sasa huo udini wa kikwete upo wapi.. hivi watanzania sijui tumerogwa yani chuo kimoja kuwa ni vc na dvc waislam ndio tatizo.. na wao walalamikie sua udsm mzumbe kuwa wameonewa itakuwaje sasa.. acha udini mbwa ww..
 
Back
Top Bottom