Dr Deo Mtasiwa(mganga mkuu wa serikali) asimamishwa uanachama wa MAT!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Tamko la Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT)

Kikao cha mkutano mkuu wa dharura wa chama cha madaktari Tanzania (MAT) kilichofanyika leo siku ya jumamosi, tarehe 14/01/2012 ukumbi wa JAFFARY COMPLEX kimejadili kwa kina yafuatayo:

1. Kwamba, chama cha madaktari Tanzania kimejadili na kuazimia kutoa masaa 72 kwa serikali kuwa “Intern doctors” wote waliohamishwa warudishwe Muhimbili mara moja wakamalizie muda wao. Na kwamba ifahamike kuwa interns huomba kwenda kufanya internship katika hospitali Fulani kutegemeana na malengo ya baadaye waliojiwekea. Na pili kuna baadhi ya vifaa vipo mf. Muhimbili na huko kwingine haviko. Madaktari wemesikitishwa sana na uamuzi huu kwa vile haieleweki ni kwa nini “intern doctors” waadhibiwe wakati walidai walipwe mishahara yao tu na serikali ilikiri kosa hilo. Wanachama wangependa kuona waliofanya uzembe huo wanawajibishwa mara moja na sio kuachwa waendelee kuwaadhibu madaktari wasio na kosa.

2. Kwamba, kwa kuwa Intern doctors wamekuwa wakifanya kazi bila malipo kwa muda mrefu na hali hiyo ikapelekea kusitisha kazi ndipo serikali ikaamua kuwalipa mishahara yao. Kufuatia kuendelea kusababisha adha kwa madaktari na wataalamu wengine wa afya na hatimaye kusababisha huduma mbovu kwa wagonjwa, Chama cha madaktari kimeona kimshauri Mh. Rais atafute ajira nyingine kwa ajili ya maafisa waandamizi wafuatao:
a. Katibu Mkuu, wizara ya Afya , Ms. Blandina Nyoni b. Mganga Mkuu wa serikali, Dr. Deo Mtasiwa
3. Kwamba waziri wa afya Dr. Hadji Mponda (MB) afute kauli yake inayoashiria kwamba “intern doctors” ni wanafunzi wa udaktari wa mwaka wa 5. Ieleweke kwamba ni madaktari kamili, waliohitimu mafunzo yao na kula kiapo rasmi cha udaktari. Na chama cha madaktari kimesikitishwa sana na upotoshwaji huuu wa mara kwa mara. Kutokana na hayo hapo juu basi chama cha madaktari Tanzania kina msamehe kwani inaonekana hajui atendalo. Ijulikane kwamba mjadala wa hivi ulishawahi kuibushwa mwaka
2005 na waziri wa afya kipindi hicho alikiri bayana kwamba intern ni daktari kamili aliyefuzu.

4. Kwamba, chama cha madaktari Tanzania kimeamua kumsimamisha uanachama wa chama hiki Dkt. Deo Mtasiwa, ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Serikali (CMO), kwa kosa la kusaliti fani ya udaktari na pia kwa kushindwa kumshauri waziri wa afya vizuri kuhusiana na mambo yanayohusu fani ya udaktari Tanzania. Mkutano huu unamsimamisha rasmi Uanachama huo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Taratibu za kumrejesha zitajadiliwa kwenye Mkutano mkuu wa kawaida wa chama. Hii itakuwa fundisho kwa madaktari wengine wote nchini.

5. Kwamba chama cha madaktari Tanzania (MAT) kimeazimia kuitisha mkutano mwingine mkubwa wa wanachama wote siku ya jumatano tarehe
18/01/2012, kuanzia saa tatu asubuhi na kuendelea kwenye ukumbi
utakaotangazwa. Agenda za mkutano huo, pamoja na mambo mengine, zitakuwa zifuatazo:
i. Hatma ya heshima ya fani ya udaktari na mustakabali wa huduma za afya kwa watanzania
ii. Kwa nini serikali haijaanza kulipa posho ya kazi muda wa ziada (on call allowance) kama ilivyopitishwa mwaka 1990 na kufanyiwa maboresho mwaka 2008.
iii. Mshahara mpya wa daktari unaoendana na elimu, ujuzi, umuhimu, hadhi, majukumu, na hali ya uchumi wa sasa na mfumuko wa bei.
iv. Maslahi mengine ya madaktari kama nyumba, posho ya mazingira magumu, ufadhili wa masomo ya elimu ya juu na posho ya kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi( Risk allowance).
v. Kuhamishwa hovyo hovyo kwa madaktari bingwa 61
vi. Mengineyo (kwa idhini ya mwenyekiti) IMETOLEWA NA

DR. NAMALA MKOPI
 
Safi saaaaana. Hili ni fundisho kwa vilaza wengine wanaojisahau fani zao na kudhania siasa ndio msingi wa ofisi zao. Vyema akaeleza kuwa yeye ni Daktari au mwanasiasa?
 
Kwa mara ya kwanza professional body inaonyesha njia sahihi ya kufuata dhidi ya wanasiasa. Trust me tukiwafuata hawa wanasiasa wetu waliochanganyikiwa,ambao wanaenda kunywa kikombe cha babu au kutibiwa apollo india, tutakuwa tumepotea njia.
Tulinde hawa madaktari tunaowatengeneza wenyewe dhidi ya wanasiasa ambao sasa hivi kazi yao ni kula tu hela ya umma.
 
tatizo ni kuingiza siasa kwenye taaluma za watu hasa kwenye sector nyeti kama ya afya
 
Na huyo mwanasiasa daktari ujue kesho asubuhi atafunguliwa, maana siasa yetu is above the lawa,lol!!
 
ndio maana tunasikia vifaa vya uchunguzi wa HIV ni feki,siasa inaendekezwa sana.sasa ni wakati wa kutenganisha siasa na taaluma.tumeanzia fani ya udaktari tuendelee na kwenye taaluma nyingine.
 
Hii topic moderator nashauri ihamishiwe kule hoja mchanganyiko, si sahihi kuwekwa hapa
 
Well done,kama mtu anaona wenzake wanamwagiwa upupu na anakenua mimeno tu. Huyo ni, 'nyoka'.
Mnampa za kichwa fasta.
 
Wale wa profession ya maaccountant wangefanya hivyo hivyo kwa CAG=Utouh!!
 
Tamko la Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT)

4. Kwamba, chama cha madaktari Tanzania kimeamua kumsimamisha uanachama wa chama hiki Dkt. Deo Mtasiwa, ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Serikali (CMO), kwa kosa la kusaliti fani ya udaktari na pia kwa kushindwa kumshauri waziri wa afya vizuri kuhusiana na mambo yanayohusu fani ya udaktari Tanzania. Mkutano huu unamsimamisha rasmi Uanachama huo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Taratibu za kumrejesha zitajadiliwa kwenye Mkutano mkuu wa kawaida wa chama. Hii itakuwa fundisho kwa madaktari wengine wote nchini.

IMETOLEWA NA

DR. NAMALA MKOPI

Whaat!!!!!! Nilifikiri chama cha madakari ni cha kitaalamu zaidi kinachohusika na mambo ya kitaalamu kwenye mambo ya chumba cha matibabu na theatre.Hebu waweke katiba yao hapa tuisome. Nilifikiri Kwamba ukichemka mfano ukapasua mtu kichwa badala ya mguu una haki ya kufukuzwa au kusimamishwa uanachama maana umekiuka proffession.Lakini kusema unaweza simamishwa hata kwa kutomshauri mwanasiasa aliyeteuliwa kisiasa asiyewajibika kwa MAT bali kwa mwanasiasa mwenzie Raisi unafukuzwa hii kali ya kufungulia mwaka 2012.Sijajua maamuzi haya ya ni ya chama cha madaktari Tanzania au ya chama cha wapiga ramli cha Tanzania.Vyama vya kitaalamu vibaki kwenye mambo ya kitaalamu tu zikianza kuingia siasa mara hukumshauri mwanasiasa tutageuza vyama vya kitaalamu kuwa vyama vya wahuni.Kama ni kweli wasomi wataalamu madaktari waliamua hivyo kuna mtu nadhani anatikiwa kwenda kufanyiwa matibau mirembe au chama cha madaktari sasa ni chama cha siasa na si cha madaktari tena.
 
Hekooooo Madakitari. Sijui lini itatokea kwa ndg zangu wa NBAA.

Long LIVE MAT!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Whaat!!!!!! Nilifikiri chama cha madakari ni cha kitaalamu zaidi kinachohusika na mambo ya kitaalamu kwenye mambo ya chumba cha matibabu na theatre.Hebu waweke katiba yao hapa tuisome. Nilifikiri Kwamba ukichemka mfano ukapasua mtu kichwa badala ya mguu una haki ya kufukuzwa au kusimamishwa uanachama maana umekiuka proffession.Lakini kusema unaweza simamishwa hata kwa kutomshauri mwanasiasa aliyeteuliwa kisiasa asiyewajibika kwa MAT bali kwa mwanasiasa mwenzie Raisi unafukuzwa hii kali ya kufungulia mwaka 2012.Sijajua maamuzi haya ya ni ya chama cha madaktari Tanzania au ya chama cha wapiga ramli cha Tanzania.Vyama vya kitaalamu vibaki kwenye mambo ya kitaalamu tu zikianza kuingia siasa mara hukumshauri mwanasiasa tutageuza vyama vya kitaalamu kuwa vyama vya wahuni.Kama ni kweli wasomi wataalamu madaktari waliamua hivyo kuna mtu nadhani anatikiwa kwenda kufanyiwa matibau mirembe au chama cha madaktari sasa ni chama cha siasa na si cha madaktari tena.
mbona unabweka???unahitaji kuelimishwa ili ujue MAT ni nini na MCT(medical council of Tanganyika) ni nini.nyie wagonjwa wa india mna kashfa sana kwa madaktari wa tanzania lakini kaa ukijua ukipata ajali hutakuwa na muda wa kwenda india bali utapelekwa dispensary ya karibu halafu amana,muhimbili na mwishoni huko india kwako.hao hao wapiga ramli ndio utakaokutana nao.
 
sikujua yule waziri wa afya ni mpuuzi namna ile.., kweli nimeamn kusoma sio kuelimika, anasahau taaluma amelewa vipesa vya kwny siasa.., shenzz,, nadhani yule katibu wake ni problem na am sure ndo anamfanyia maamuzi.., kama msukule vile..,

Alichoongea jana ni pumba hata mtoto wa nursery hazikubali,, eti watu inabd wakumbuke viapo na wawe wazalendo.., unamnyima mtu haki zake afu unamwambia awe mzalendo.., shennzzzz
 
Back
Top Bottom