Dr. Dalali Peter Kafumu rasmi ndani ya Bunge

ray jay

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,084
485
Baada ya Dr Kafumu kuapishwa rasmi bungeni hivi leo.,Chama cha CCM kimemuandalia sherehe fupi ya kumpongeza na kumkaribisha rasmi akiwa kama mbunge mpya kupitia chama iko kutoka katika Jimbo ambalo lilikuwa na ushindani wa hali ya juu..,katika maneno yake Dr Kafumu amedai kuwatumikia watanzania, wanaccm lakini hasa wanaigunga ndio hasa msingi wa msukumo wake katika kuwania ubunge ambao anashukuru kuwa wanaigunga wamemteuwa.

Dr kafumu ameendelea kudai kuwa kwa sasa hana jambo lingine linalomsubiri mbele yake isipokuwa kutimiza azma yake ya muda mrefu ya utumishi kwa umma na katika hilo hatojali ama kuzingatia nani alikuwa adui kwake kipindi cha harakati za uchaguzi bali anawakaribisha watu wote katika kumshauri, kumrekebisha na kushikamana nae katika Dhamira yake hii.

Sherehe hizo fupi zinafanyika ukumbi wa CCM-Dodoma, Makao Makuu, ambapo msafara wa Dr Kafumu utapokelewa na Mheshimiwa Nape ambae amerejea jana kutoka Marekani alikokwenda kukagua uhai wa chama na maendeleo yake.
 
Hongera Kafumu, Hongera Igunga, Hongera Rostam, Hongera CCM. Magwanda waandamane tu, sisi tunakata mawimbi tartiiiibu.
 
Hongera Kafumu, Hongera Igunga, Hongera Rostam, Hongera CCM. Magwanda waandamane tu, sisi tunakata mawimbi tartiiiibu.

umesahau na hawa,hongera cuf,hongera polisi,hongera mafisadi,hongera rushwa,hongera kambi ya misigirihongera kipindi cha njaa.

na mimi kwa upande wangu nawapongeza.kazenibuti kwa maana jua linataradad.
 
Magamba bana wanachekesha sana. Nape ameenda kukagua uhai wa ccm marekani? Ujinga. kwani kule si kuna Democratic ya akina Obama na Republican ya akina Bush? Hivi Democratic ya Obama ipo hapa Tanzania? Huu ujinga wa magamba ndo huwa siutakagi kabisa. Yaani ninahasira jinsi kodi zetu zinavyotumika vibaya. wasijidai kuwa ni za chama. vyama vya waTZ vinaendeshwa kwa kodi zetu na wao wapo pale kama dhamana na si kutufilisi. Pumbafu yao.
 
Hongera Dr. Kafumu.
Uliwagaragaza magwanda wote...umeleta heshima..sasa hivi wanaiogopa CCM sana, mpka wenyewe wanakimbila kujificha gerezani.
 
Magamba bana wanachekesha sana. Nape ameenda kukagua uhai wa ccm marekani? Ujinga. kwani kule si kuna Democratic ya akina Obama na Republican ya akina Bush? Hivi Democratic ya Obama ipo hapa Tanzania? Huu ujinga wa magamba ndo huwa siutakagi kabisa. Yaani ninahasira jinsi kodi zetu zinavyotumika vibaya. wasijidai kuwa ni za chama. vyama vya waTZ vinaendeshwa kwa kodi zetu na wao wapo pale kama dhamana na si kutufilisi. Pumbafu yao.
waelevu waliwahi kusema ficha ujinga wako.,na usivimbe kifua hasa kwa lile ulilokosea kwa kudhani umepatia...!
 
Kafumu huyuhuyu alie sababisha watu kuuwawa ndio anakaribisha ushauri?! Kabla ya kukaribisha ushauri angehakikisha wote walioshiriki mauwaji wanafikishwa mbele ya sheria.
 
Hata waandae sherehe mwezi mzima bado wananchi wa Igunga wanapata shida a matatizo yaliyopo hayawezi kumalizwa na huyu Kafumu ambaye alikuwa pale madini na hakufanya lolote kuwasaidia,kwangu mimi ninaona ni kama kutoa shoka na kuingiza panga pale Igunga.
Furahini mwisho mwisho maana siku zenu zinahesabika.
 
Magambaaaaaa!!! Nape alikwenda kukagua uhai wa watu wanane! kweli mna wananchaman wengi.
 
Hongera Kafumu, Hongera Igunga, Hongera Rostam, Hongera CCM. Magwanda waandamane tu, sisi tunakata mawimbi tartiiiibu.

hongera nyerere,hongera mfumo kristo,hongera lowasa hongera chenge hongera nape
tuko pamoja sana ..magwanda waandamane tu
 
Back
Top Bottom