Dr. Bilal and the Future of COSTECH

Kwa wale waliopitia Chuku kikuu cha Dar es Salaam, wakati Dr. M. Bilal akiwa katibu Mkuu wizara ya sayansi na technologia nina uhakika kuwa wanakumbuka kuwa huyu Bwana kwanza ni mwongea hovyo na hafai hafai kabisa.

Huyu jamaa nasikia kila siku alikuwa anasimama pale katikati ya barabara na kutoa majibu ambayo hata mtoto mdogo angemzomea tu.

Huyu jamaa alikuwa anazungumza tuuuu anazungumza tuu mpaka apandishwe kwenye sturi katikati ya barabara ndipo watu wapate mikopo yao.

Kwa experience hiyo na ubishi wake pamoja na kwamba jambo analolizungumzia siyo sahii nafikiri ndio maana hata wana CCM pamoja na kuwa huwa sipendelei kuwazungumzia ndio maana huwa wanamkandamiaza.

Kitila nafikiri unauzoefu na yule Ex VC (Mathayo Luhanga) aliyekuwa UDSM nasikia hata SIDA-SWEDen na mashirika mbalimbali, huwa wanamtumia katika maswala ya research. Kama anaweza kupewa kufanya transformation ya COSTECH hata mwaka mmoja anaweza kuifanya kwa ufanisi mkubwa sana.

Hebu nitajie mtu mmoja kati ya viongozi wetu anayefaa...from both CCM na Opposition
 
Huyu jamaa wa NASA nimekuwa nikimsikia muda mrefu sana.. hivi ni nani huyu? Maana hata kabla sijaja huku kijijini alikuwa ni mmoja wa watu ati akirudi Bongo anaheshimiwa na watu wa ubalozi wa US pale.. n.k .. who is this guy, analo jina?
 
Doesnt matter siyo Mtanzania tena

maana tukianza naye utataka kuwajua wale wabongo waliojikita pale State dept na wengine waliopo MOD (UK) wakati watu walibadilisha majina,wakaachana na uaia wa kibongo na sasa wanaenjoy kazi bila majungu na wazungu

mengine wee yaache tu

JF CSI team inaonekana bado haiko effectuive kama watu wanavyofikiri
 
Mzee Mwanakijiji,

wakati wewe umesikia ni jamaa wa Kichaga, simulizi nilizosikia mimi zinadai ni Mhaya!!

Hata mimi ningependa kumjua huyo MTANZANIA mkali aliyeko NASA. pia ningependa kuipata CV yake.

GAME-THEORY,

Unaweza kutuletea CV ya Kitaalamu ya Dr.Mohamed GHarib Bilali.?
 
Mimi nadhani hizi zote ni Legends and myths, hakuna cha Mbongo kwenye nafasi za juu kwenye taasisi hizo. Maana legend moja iliwahi kusema ati kuna Mtanzania ambaye ni Brigadier katika jeshi la Marekani na ni mchagga na amekuwa huku kwa muda mrefu sana..
 
Mimi nafikiri badala ya kupata mcheche nani anafaa na nani hafai kuiongoza COSTECH, tujaribu kutafakari njia ambazo wizara zetu za elimu (chini na juu) zitumie kuhamasisha wanafunzi kuchukua mkondo wa sayansi kwa wingi.

Ukweli ni kwamba, ukiondoa mkondo wa udaktari na matawi yake (pharmacy, nursey, ets), wanafunzi hawako interested na sekta nyingine za sayansi. Hebu tujiulize leo hii tuna environmentalists wangapi nchini, vipi kuhusu nutritionists, biotech scientists, wakemia, zoologists, etc?

Unajua, system ya elimu yetu inakatisha tamaa mchepuo wa sayansi. System yenyewe imejijenga around the obvious careers only: Accountancy, Medical, Law, Journalism, Engineer, and now Human Resource. I bet kuwa 70% ya Watz wanao hold a professional job wako kwenye among mentioned careers. Sasa hebu niambie, ni vipi tutaitengeneza COSTECH kuwa a competitive scientific commision wakati hata system ya elimu yetu haitilii mkazo kwenye sayansi?

Mimi kwa maoni yangu, pengine challenge kubwa ya COSTECH (na taasisi zingine za sayansi) ni kuangalia njia za kushirikiana na taasisi za elimu kujaribu kuinua elimu ya mchepuo wa sayansi kwa wanafunzi. Ni process ambayo inalenga kwenye long-term goals.

Hivi ni kweli tuna wanasayansia wengi nje ya nchi?
 
Game Theory,

Naona nimeanza hii Chrismas break hapa JF vibaya. Umeshambulia post yangu haraka haraka sana.

Kwanza kama umesoma vizuri maandiko yangu, sikusema kuwa jamaa huyu siyo mtaalam wa Nuclear Physics, ila nilisema kuwa siyo kati ya world class Nuclear Physicists anayeweza kuchimba na kuibua jambo jipya la kisayansi. Ana Ph.D ya Nuclear Phyisics kama walivyo wengine wengi tu.

Ni kweli kabisa kuwa kuandika paper siyo kipimo cha uwezo wa mtu kitaalamu; kwa hiyo endapo mtu ana majukumu ambayo hayamhitaji kuandika papers za kitaalam ni dhahiri kuwa hataandika lolote. Ndiyo maana hao watu wawili uliowataja hapo juu hawakupublish lolote. Lakini huyu jamaa alifundisha pale UDSM huku akijua kuwa mojawapo ya majukumu yake ni ku-publish na alishindwa kufikiria na kupublish mawazo yake ya kisayansi ipasavyo kulingana na standard zilizokuwapo wakati huo. Kwa vyovyote vile hakuwa anaweza kufikiria kisayansi outside his box. Ndiyo maana naamini kabisa kuwa jamaa huyu hawezi kuongoza taasisi ya kisayansi kama COSTECH.

Kuhusu yeye kuwa consultant wa NSA kwanza sijui una maana gani unaposema NSA. Kama una maana ya "Nuclear Systems Associates;" basi ni lazima ufahamu kuwa hii ni kampuni ya watu binafsi na kati ya consultant wanaowatumia ni watu wenye Bachelor's degree tu. Hiyo inaonyesha kuwa kuwafanyia kazi siyo lazima uwe world class material.

NSA nyingine ni "Nuclear Safety Associates", ambayo nayo ni kampuni ya watu binafsi sawa kabisa na NSA ya hapo juu.

Inawezekana una maana ya ANS (American Nuclear Society). Hii ni society ambayo mtu yeyote mwenye interest na Nucrelar science anaweza kuwa member kuanzia na wanafunzi klwa hiyo siyo kipimo cha kumfanya mwanachama wake awe ni world class scientist.

Ingawa ni kweli kuwa Mzee Bilal ni mmoja wa watanzania wachache waliosomea Nuclear Physics, lakini tusiwe tunapiga ngoma sana kudai kuwa ni mtaalamu mkubwa sana katika field hiyo wanayetambulika duniani duniani kote.

Kurekebisha record yako moja, tambua kuwa A.Q Khan aliiba michoro yote ya nuclear reactors, accelerators na centrifuges kutoka Uholanzi na kuja kuzireproduce huko Pakistan; hakufanya jambo jipya la kumfanya awe world class scientist. Kitaalam, yeye ni Metallurgical Engineer, na wala siyo Nuclear Physicist. Kinachofanya ajulikane sana ni kwa vile alianza kusambaza michoro hiyo kwa nchi mbalimbali na hiyo kutishia usambazaji wa silaha na Nuclear.
 
Mimi nadhani hizi zote ni Legends and myths, hakuna cha Mbongo kwenye nafasi za juu kwenye taasisi hizo. Maana legend moja iliwahi kusema ati kuna Mtanzania ambaye ni Brigadier katika jeshi la Marekani na ni mchagga na amekuwa huku kwa muda mrefu sana..

nashangaa kwa mtu aliyesafiri kama wewe unaona hilo haliwezekani na haswa kwa nchi kama USA

Suala la kuwa na briegadier silijui lakini i can confirm kuna watanzania 2 wako MOD hapa uk na najua watanzania 3 ambao wako State.Position ambayo mtu ambaye hajazalia wUSA hawezi kuishika ni URAIS tu zinginezo ziko Open mzee

Thats not a myth my brother thats the truth

PRITI PATEL alizaliwa UGANDA na ni mmoja kati ya hao waliopekwa majina yao katika hiyo A list ya kuwania ubunge wa CONSERVATIVE (uk)

_42384470_pritipatel203_bbc.jpg

Baroness Usha Kumari Prashar kazaliwa KENYA

Baroness&
 
Game Theory,

Naona nimeanza hii Chrismas break hapa JF vibaya. Umeshambulia post yangu haraka haraka sana.

Kwanza kama umesoma vizuri maandiko yangu, sikusema kuwa jamaa huyu siyo mtaalam wa Nuclear Physics, ila nilisema kuwa siyo kati ya world class Nuclear Physicists anayeweza kuchimba na kuibua jambo jipya la kisayansi. Ana Ph.D ya Nuclear Phyisics kama walivyo wengine wengi tu.

Ni kweli kabisa kuwa kuandika paper siyo kipimo cha uwezo wa mtu kitaalamu; kwa hiyo endapo mtu ana majukumu ambayo hayamhitaji kuandika papers za kitaalam ni dhahiri kuwa hataandika lolote. Ndiyo maana hao watu wawili uliowataja hapo juu hawakupublish lolote. Lakini huyu jamaa alifundisha pale UDSM huku akijua kuwa mojawapo ya majukumu yake ni ku-publish na alishindwa kufikiria na kupublish mawazo yake ya kisayansi ipasavyo kulingana na standard zilizokuwapo wakati huo. Kwa vyovyote vile hakuwa anaweza kufikiria kisayansi outside his box. Ndiyo maana naamini kabisa kuwa jamaa huyu hawezi kuongoza taasisi ya kisayansi kama COSTECH.

Kuhusu yeye kuwa consultant wa NSA kwanza sijui una maana gani unaposema NSA. Kama una maana ya "Nuclear Systems Associates;" basi ni lazima ufahamu kuwa hii ni kampuni ya watu binafsi na kati ya consultant wanaowatumia ni watu wenye Bachelor's degree tu. Hiyo inaonyesha kuwa kuwafanyia kazi siyo lazima uwe world class material.

NSA nyingine ni "Nuclear Safety Associates", ambayo nayo ni kampuni ya watu binafsi sawa kabisa na NSA ya hapo juu.

Inawezekana una maana ya ANS (American Nuclear Society). Hii ni society ambayo mtu yeyote mwenye interest na Nucrelar science anaweza kuwa member kuanzia na wanafunzi klwa hiyo siyo kipimo cha kumfanya mwanachama wake awe ni world class scientist.

Ingawa ni kweli kuwa Mzee Bilal ni mmoja wa watanzania wachache waliosomea Nuclear Physics, lakini tusiwe tunapiga ngoma sana kudai kuwa ni mtaalamu mkubwa sana katika field hiyo wanayetambulika duniani duniani kote.

Kurekebisha record yako moja, tambua kuwa A.Q Khan aliiba michoro yote ya nuclear reactors, accelerators na centrifuges kutoka Uholanzi na kuja kuzireproduce huko Pakistan; hakufanya jambo jipya la kumfanya awe world class scientist. Kitaalam, yeye ni Metallurgical Engineer, na wala siyo Nuclear Physicist. Kinachofanya ajulikane sana ni kwa vile alianza kusambaza michoro hiyo kwa nchi mbalimbali na hiyo kutishia usambazaji wa silaha na Nuclear.

NSA nilimaanisha NATIONAL SECURITY AGENCY

samahani sikueleza hilo katika post yangu ya awali

Pili hiyo unaposema WORLD CLASS sijakuelewa unamana gani kwani kama ni kilingustic sidhani kama tunaweza kulinyambua kwa mapana lakini inshort ni watu ambao wamekuwa exposed by the media au otherwise kama vile interest groups and so on.

Sasa hebu fafanua unamaana gani na nani ana decide who should be WORLD CLASS and who shouldnt?

Vile vile kuhusu AQ KHAN kuiba michoro ni sawa kabisa lakini hiyo haiondoi ukweli bado alikuwa ni mtaalam mzuri wa fani yake kwani kusingekuwa na faida ya kuiba bila ya kuwa na utaalam wa kufanyia kazi hivyo vilivyoibiwa.
 
National Security Agency ya Marekani haihitaji scientists; inahitaji ma-spy tu. Hata babu yangu ananaweza kuwa agent wao kama anajua siri za kispy wanazotaka.
Pili hiyo unaposema WORLD CLASS sijakuelewa unamana gani kwani kama ni kilingustic sidhani kama tunaweza kulinyambua kwa mapana lakini inshort ni watu ambao wamekuwa exposed by the media au otherwise kama vile interest groups and so on.

Sasa hebu fafanua unamaana gani na nani ana decide who should be WORLD CLASS and who shouldnt?
Inawezekana nimekuwa Fuzzy hapa. Niliposema World Class scientist nina maana ya mwanasayansi ambaye anajulikana na kuheshimiwa kitaalam duniani kiasi cha kuaminiwa kutoa ushauri wa kitaalamu. Ina maana kuwa asilimia kubwa ya wataalamu katika field yake wanamtambua. Tunao Watanzania wachache wa namna hiyo kama akina Professor Mwandosya, Professor Lipumba, na wengineo lakini Dr. Bilal siyo mmja wao.

Vile vile kuhusu AQ KHAN kuiba michoro ni sawa kabisa lakini hiyo haiondoi ukweli bado alikuwa ni mtaalam mzuri wa fani yake kwani kusingekuwa na faida ya kuiba bila ya kuwa na utaalam wa kufanyia kazi hivyo vilivyoibiwa.

Dr. Khan ni mtu smart sana; lakini siyo world class scientist. Tanzania tutapiga hatua kubwa sana kama tutakuwa na watu kama Dr. Khan, na serikali ikawasupport.
 
nashangaa kwa mtu aliyesafiri kama wewe unaona hilo haliwezekani na haswa kwa nchi kama USA

Hapa ndio nachoka, sijui mimi kusafiri kunahusiana vipi na mimi kujua kila kitu. Na sijui kama nimesema "hilo" haliwezekani na hata kama ningesema hilo linahusiana vipi na kusafiri kwangu?

Suala la kuwa na briegadier silijui lakini i can confirm kuna watanzania 2 wako MOD hapa uk na najua watanzania 3 ambao wako State.Position ambayo mtu ambaye hajazalia wUSA hawezi kuishika ni URAIS tu zinginezo ziko Open mzee

You confirming it doesn't make it true. Sasa tuyachukulie maneno yako at face value because ume "confirm"? Itakuwa hatari. Hata mimi nafahamu Watanzania kadhaa ambao wanamsaidia Rais Bush pale White House, na yupo yule anayefanya kazi Jeopardy na kina Alex Trebek. Halafu usimsahau yule Mtanzania anayefanya kazi pale NASA Houston.

Thats not a myth my brother thats the truth

according to...

PRITI PATEL alizaliwa UGANDA na ni mbunge wa CONSERVATIVE (uk)

irrelevant!
 
Mwanakijiji, hebu nipe hayo majina ya Wabongo (1) anayefanya kazi White House, (2) anayemsaidia Trebek, na (3)anayefanya kazi NASA.

Hivi mnajua kuna wengine 4 wanaofanya kazi hapa CDC (Centers For Disease Control)?
 
Hapa ndio nachoka, sijui mimi kusafiri kunahusiana vipi na mimi kujua kila kitu. Na sijui kama nimesema "hilo" haliwezekani na hata kama ningesema hilo linahusiana vipi na kusafiri kwangu?

You confirming it doesn't make it true. Sasa tuyachukulie maneno yako at face value because ume "confirm"? Itakuwa hatari. Hata mimi nafahamu Watanzania kadhaa ambao wanamsaidia Rais Bush pale White House, na yupo yule anayefanya kazi Jeopardy na kina Alex Trebek. Halafu usimsahau yule Mtanzania anayefanya kazi pale NASA Houston.

according to...

irrelevant!

Interesting...
 
GAME-THEORY,

hivi NSA ya USA si wako ktk level moja na CIA na FBI? ninavyoelewa taasisi nyeti kama hizo haziajiri watu ambao hawana URAIA wa USA.

Naomba utuweke sawa hapa. Ina maana Dr.Mohamed Gharib Bilali, waziri kiongozi mstaafu wa SMZ, yuko ktk pay-roll ya US NATIONAL SECURITY AGENCY?
 
[/QUOTE] Hivi mnajua kuna wengine 4 wanaofanya kazi hapa CDC (Centers For Disease Control)?[/QUOTE]

Mhe. unaweza kutupatia majina?
 
Hivi mnafahamu kuna wabongo kama 10 hivi wanaofanya kazi MI5? N.K. n.k. nk.......
 
Back
Top Bottom