Dr. Bana, Heche, Mkosamali na Kafulila LIVE ON STAR TV

Halafu ndugu Yahya kuna wakati mnaonekana kabisa mnafanya kazi ambayo radio uhuru wanatakiwa waifanye,kuna siku mlikuwa mnafanya spining live live....hasa ile siku CHADEMA walipokataa kuhudhuria sherehe za kumwapisha waziri mkuu.Mlipoteza credibility ya kuwa professional Journalists.Thanks kwa kutuhabarisha though!
Hilo linawezekana,Tunashukuru kwa positive criticism, japo hakuna msamaha when damage has caused already.
Nimependezwa na ushiriki wa wanaJF kwa leo na tutaendelea kupokea na kufanyia kazi mawazo yenu.
 
Binafsi naona ujumbe wa Chadema umefika sababu ujumbe ni nini: Chadema wanalalamika juu yakubadilisha Mfumo ambapo source ya tatizo ni Katiba mfumo utakaopelekea kuwa na Tume huru ya Uchaguzi.

Iwapo hiyo Ishu isingeku raised na Wabunge wa Chadema kwakutoka nje hata nyie hapo na huyo Kafulila msingekuwa mnaongelea Ishu ya Katiba,Tanzania nzima saiv watu wanaongelea Katiba.

Mchakato wa Ishu ya Katiba umeanza siku nyingi lakini CCM hawako tayari coz ina wafavour so hi Ishu inatakiwa iwekwe mezani na idaiwe kwa nguvu zote c kuongelea Chini ya meza kwakujikomba komba.
Shukran kwa ushiriki wako mzuri
 
Shukrani Yahya kutushirikisha kwa njia hii.
Dr. Bana, mshauri wa siasa wa mgombea wa CCM wa nafasi ya Rais amesema madai ya Chadema yanazungumzika, na yalianza 1995. Je anakubali kuwa kilichojiri Dodoma kimeliibua suala hilo kwa nguvu mpya?
La pili Yahya, kwa sababu unapata wageni mbalimbali hapo studio, NAOMBA TUFAFANULIWE hayo MAADILI YA KISIASA YA KITANZANIA wakati hatujui kama taifa letu linaelekea kwenye ujamaa au ubepari, ni yepi?
Ushiriki kama huu tunategemea kuuboresha kwa kuincooperate mawazo yenu critical thinkers. Shukrani kwa kushiriki
 
ila kafulila na yule bwana mdogo nawashangaa sana wanaeleza vitu ambavyo sikuwategemea kabisa na huyo bwana mdogo ole wake angekua
UDSM MGONGO FIMBO ANGEKUKAMATA WEWE BAHATI YAKO NATUNGEKUTOA MAGAZETINI UNGEJUA SIASA ZA BONGO
 
Safi sana Yahya:hail: ila naomba kukiwa nakitu kama hichi uwe unatupa clue mapema ili nasi tujongee pamoja kwenye runinga zetu na laptop zetu ili tuweze kwenda pamoja.. hii kitu ni nyeti sana kwa ustawi wa taifa la kesho na inabidi tuijadili kwa umakini kwa pamoja
 
Swali zuri sana mzee, kwa mtu sahihi na ndani ya muda mwafaka kabisa!!!!!!!!!!!!!!!

Nadhani kwa sasa hivi atakua anakunja vyombo vyake vya utangazaji tayari kuondoka home, hivyo jibu mpaka kesho tena.
 
Back
Top Bottom