Dr. Bana: CCM bado ni chama imara, kinasikiliza watu!

Bana ndio kauwa REDET...ni mropokaji na haongei kama msomi. Kauli zake zote ni za kujipendekeza kwa serikali kitu ambacho sio sahihi kwa msomi wa siasa kama yeye. Wafadhili wamejitoa REDET kutokana na kuboronga kwa taasisi hii kwa kuonesha upendeleo wa wazi kwa serikali katika tafiti zake na huyu mzee ndio kahusika kwa sehemu kubwa. Anatia huruma hata katika kauli zake

Hata mi ningekuwa Dr Bana ningesema hivyo maana ukiwasifia magamba hufi njaa hasa mkwr anafurahi sana huenda akamkaribisha magogoni wanywe chai pamoja
 
hata usome vipi ukijiunga ccm unakuwa na akili za chekechea

Huyu ni baadhi tu ya wasomi wetu leo hii, ambao wamejiwekea wigo na wananchi na vile vile wamevaa miwani za mbao hawaoni mbele. sitomshangaa Dr. Bana leo, amekwishafanya madudu mengi tu! anauwezo wa kuwafundisha wanafunzi wetu waende wakawe wabunifu, thinkers? Jibu unalo hapo
 
Ningesema hana habari na hali halisi ya kisiasa nchini. Dkt. wa sayansi ya siasa unapojiunga na propaganda za kukandia vyama vingine kwamba havipo kila mahali (hadi vijijini) kama vile huna habari na mfumo wa utawala uliopo unavyodhibiti hilo lisitokee (rejea kidogo tu tukio la juzi Tunduma - ambako ni mjini!), unashangaza.

Lakini, maneno mengi pembeni, huyu naye ni mmoja wa wahanga wa fursa zilizominywa na CCM hadi ulambe viatu vya wakulu ndipo angalau uruhusiwe kuuona mwanga. Hakuna haja ya kuumiza vichwa na blabla za watu wa aina hii. Siku mabadiliko ya kweli yakitokea utawaona wakijibaraguza kwamba ukweli walikuwa wakiujua lakini "system" ilikuwa imewatia kabali.
 
Sina tatizo na maoni ya huyu Dr. Bana maana kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake. Tatizo langu ni kwamba CCM wanamtegemea huyu bwana kama mshauri! Tragedy!
 
Benson Bana, a fourm four leaver - Ihungo Secondary School, sat for A level examinations as a private Candidate, He's a mature entrant at UDSM, where he struggled to acquire his master in Political Science
He worked with TCC before securing sponsorship for his Phd in UK.
All in all, nani zaidi kati yake na Dr. Azaveli Rwaitama?
 
kama msomi na elimu yake ananunulika na kuamua kuwasaliti wananchi ambao wamemsomesha kwa kodi zao ili kusudi aje kuwatetea leo ndo anakuwa wa kwanza kuwaangamiza,eti ilani yao nzuri je inatekelezeka au anasifia cover anasau ujumbe uliomo,hakika kiama chao kipo karibu najua wanajipa moyo kwa kuwa wao wanavyombo vya dora ila sisi tuna mungu ipo siku mwananchi maskini naye atafurahia kuwa mtanzania walau kufaidi rasilimali za nchi yake,hatuwezi tukalia milele ipo cku tutanyamaza
 
...Anasema CCM bado ni imara kwenye utawala,chama kinachoonesha kina vision na kinasikiliza watu/wananchi na kutoa masuluhisho kwa wakati mfano dhana ya kujivu gamba,ni imara kwenye mfumo wa uongozi,anasema ina-policy nzuri kuliko vyama vingine akasema hata ukisoma ilani ya chama ya uchaguzi ni nzuri kuliko vyama vingine,na anasema ni chama kinachoongozwa kwa utaratibu na sio kama NGO..hapa anaongea kupitia THIS WEEK IN PERSPECTIVE muda huu...

My take:
Huyu Doctor anaelekea pabaya,kama hata hasomi majira na nyakati lol!!

The world is not fair. Huyu Bana ambaye alikuwa mchechemeaji, aliyeamua kusomea Developments Studies (DS), somo ambalo kila mmoja alikuwa akilidharau na kuonekana somo la wapiga majungu, leo anapewa coverage kiasi hata cha kusikilizwa na wenye akili! To me this is non-material at any standard.
 
Idadi ya wabunge, madiwani, kura za Urais na matokeo ya chaguzi za hivi karibuni ni jibu tosha, halihitaji uwe na PhD kulitambuwa hilo.
 
Back
Top Bottom