Hi, wanaJF mkumbuke katika serikali ya awamu ya tatu Mhe. Dr Abdallah Kigoda alikuwa waziri wa mipango na uchumi na mambo yalikwenda vizuri shilingi yetu ilikuwa na thamani mfumko wa bei haukuwa kabisa nakumbuka wakati Mkapa anamalizia kipindi chake cha mwisho 2005 kilo ya sukari ilikuwa sh600 tu hivi sasa imefikia sh.2,400. Mhe. rais nakupongeza kwa kuona utendaji wa Dr. Kigoda na hivyo kumrudisha kwenye Baraza la mawaziri. Lakini ingekuwa vema kama ungempa wizara ya fedha na uchumi kwani ni mtu mwenye uzoefu na angesaidia kurekebisha hali tuliyo nayo hivi sasa ya maisha kupanda.