‪DPP atumie madaraka yake kisheria ipasavyo, asisubiri maelekezo ya wanasiasa ili afanye kazi‬

Ila kuweza kusaidia wengine kuelewa hoja ya DPP kama ilivyotolewa na kina Msemakweli. Wabunge wana kazi ya kuifanyia marekebisho sheria na vile vile wanatakiwa waanza kumbana Feleshi kama hawezi kazi aachie. Jamani.. kuwa na discretion haina maana kuacha uovu utawale.
 
Tutasema yote ndugu zangu lakini ukweli unabaki palepale, mteule wa rais hawezi hata mara moja kumgeuka bosi wake, ona hata semina elekezi alivyowafunda hadi majaji ambao ni mhimili tofauti ila yeye ndo full stop wao. Katiba yetu imepitwa na wakati na kwa hali ilivyo kila mtu anao uhuru wa kuifanyia marekebisho kivyake na kuitumia anavyoona inafaa, wewe hushangai mwizi kajulikana ila jk anamuambia arudishe tu alizoiba halafu atasamehewa, na huko zilikorudi zinakutana na mwizi mwingine ambae sasa nasikia anatakz kuleta dowans yake na yeye. Ndugu zangu nchi hii sasa imekaribia kuisha, tutamaliza kalamu ila magamba haya hayawezi kusoma busara zetu na ndo maana sasa na sisi tunajiunga na wapayukaji tupige kelele bila kujua nani anasikiliza.... Kitaeleweka tu, Mheshimiwa mwanakijiji, napenda kutoa hoja.
 
Afrika lecturer akitunga paper alafu wanafunzi wakafail basi inaonekana wanafunzi wana matatizo lakini wenzetu, wanafunzi wakifail lazima mwalimu wao awe na la kujibu!

Nina maana kwamba, dpp kufail alitakiwa atimuliwe haraka sana ila tunarudi nyuma na kusema huo udhaifu wa dpp upo na kj anaujua sema wana maana yao kimaslahi ila wanasahau kuwa hizo nyazifa si za kudumu!'' ipo siku wanangu watafunguka macho na kukataa udharimu unaotendwa na wenye uchu na hira ya madaraka''
 
Wee Luckman, nani kasema DPP kashindwa kazi?. Kwa taarifa yako, Feleshi ndio the best DPP we have ever had!. Huyu ni DPP ambaye anahakikisha serikali inaheshimika kwa kutupilia mbali kesi zote zitakazoiabisha serikali. Yaani moja ya sifa kubwa za Feleshi ni saving the face ya maroroso yote ya serikali.

Hizo kesi za vigogo, ni kiini macho tuu, zilifunguliwa kabla ya uchaguzi kuwaaminisha Watanzania serikali inaweza, but before the law, ni very weak cases na zote zitapigwa chini!. Ndio maana hata Kagoda, hawezi kuifungulia mashitaka kamwe, kwa vile fedha zile zilitumika kwa kazi maalum!.

Amemfungulia kesi mbuzi yule Dalali wa Radar Vithlani, sio kwa kupaisha bei ili alete migao kwa watu ambao mgewasikia, msinge amini!. Kosa la Mzee wa Vijisenti, ni kubank kwa Waingereza, wenzake wamebank Uswisi na wamajituliza kimya, subiria wakimaliza tern zao, utasikia kila safari ni kupitia Uswiss kwa mapumziko mafupi!. Haya yote DPP anayajua na hafungui kesi za kuwadhalilisha watawala, hivyo anafanya kazi nzuri sana kwa waliomteua!.
 
Ni DPP ndiye aliye kiuzizi kikubwa cha vita dhidi ya ufisadi nchini.

You might be right, ila nionavyo mimi Rais ndiye Kizuizi kikubwa, mana kama Rais angekuwa serious na kama angekuwa hamlindi na kumsupport DPP kwa haya anayoyafanya siku nyingi angekuwa ameshamwajibisha DPP au kumtoa katika nafasi yake, lakin kwa kuwa DPP analindwa na Rais basi ndio maana anafanya upumbavu huu na kuachwa aendelee na kazi hadi leo. Pia kusema kuwa tunamwonea Rais, mimi sidhani kama tutakuwa sahihi. Kwa haya tunayoyaona ni wazi kuwa Rais anamkono kwenye uzembe wa DPP. Na inawezekana pia kuwa DPP anashindwa kufanya kazi kwa sababu ya kulinda interests za Rais, sio bure.
 
Wee Luckman, nani kasema DPP kashindwa kazi?. Kwa taarifa yako, Feleshi ndio the best DPP we have ever had!. Huyu ni DPP ambaye anahakikisha serikali inaheshimika kwa kutupilia mbali kesi zote zitakazoiabisha serikali. Yaani moja ya sifa kubwa za Feleshi ni saving the face ya maroroso yote ya serikali.

Hizo kesi za vigogo, ni kiini macho tuu, zilifunguliwa kabla ya uchaguzi kuwaaminisha Watanzania serikali inaweza, but before the law, ni very weak cases na zote zitapigwa chini!. Ndio maana hata Kagoda, hawezi kuifungulia mashitaka kamwe, kwa vile fedha zile zilitumika kwa kazi maalum!.

Amemfungulia kesi mbuzi yule Dalali wa Radar Vithlani, sio kwa kupaisha bei ili alete migao kwa watu ambao mgewasikia, msinge amini!. Kosa la Mzee wa Vijisenti, ni kubank kwa Waingereza, wenzake wamebank Uswisi na wamajituliza kimya, subiria wakimaliza tern zao, utasikia kila safari ni kupitia Uswiss kwa mapumziko mafupi!. Haya yote DPP anayajua na hafungui kesi za kuwadhalilisha watawala, hivyo anafanya kazi nzuri sana kwa waliomteua!.

Ndio hapa nashangaa kwanini wabunge hawamkomalii au kubadilisha sheria hiyo ya DPP ili iandane na mahitaji yetu ya leo? Kwa mfano kwanini hawajaweka trigger clauses za kumfanya DPP afanye kazi yake hata kama hapendi?
 
DPP wetu kizuizi mapambano dhidi ya ufisadi

M. M. Mwanakijiji

Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MAPAMBANO ya ufisadi nchini sasa hivi yanakwamishwa siyo na Rais Jakaya Kikwete kama wengi wanavyotaka tuamini, bali yanakwazwa na Mwendesha Mashtaka.

Sina wasiwasi hata kidogo kuwa kama tungekuwa na mwendesha mashtaka mzuri anayejua nguvu alizonazo za kisheria, nina uhakika baadhi ya mambo tunayoendelea kuyaimba kila kukicha, yangeisha na kusahaulika karne moja iliyopita!

Nguvu za Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kisheria ndiye mwenye nguvu kuliko hata rais, linapokuja suala la kuwashtaki watu.

Ana nguvu za kuchunguza jambo lolote linalohusu makosa ya kihalifu. Yaani, haihitaji hata kupewa ushahidi anaposikia kuna mtu anatuhumiwa hivi au vile, ana uwezo wa kuanzisha uchunguzu mara moja.

Sheria inampa DPP uwezo mkubwa wa kuhakikisha kuwa sheria za nchi zetu zinafuatwa, wahalifu wanashughulikiwa na utawala wa sheria unadumishwa.

Hadi hivi sasa, ninadai kuwa DPP wetu ameshindwa kazi hiyo na matokeo yake badala ya kuongoza, amejikuta anafuata. Nimeshaandika juu ya DPP mara kadhaa sasa, bado ninaamini kuwa yeye ndiye mtu pekee anayestahili kubebeshwa lawama za utawala wa kujichagulia sheria za kufuata!

Mwaka 2008 Sheria ilipitishwa ambayo iliunda rasmi Idara ya Mwendesha Mashtaka ya Taifa, hivyo kujaribu kutenganisha shughuli za mwendesha mashtaka zilizokuwa zikifanyika chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ikiwa na waendesha mashtaka wengi chini ya Jeshi la Polisi.

Sheria hiyo ambayo wengi tuliililia, ililenga hasa kuhakikisha shughuli za Mwendesha Mashtaka zinakuwa huru kutoka shughuli nyingine na kuondoa mgongano usio wa lazima kati ya wahusika mbalimbali katika mchakato wa utafutaji na upatikanaji wa haki nchini.

Kwa mujibu wa sheria hiyo (Ibara 1:2) uwezo wa sheria hiyo unahusu mambo yote ya uendeshaji mashtaka upande wa Tanzania Bara na vilevile kuratibu na kusimamia uchunguzi wa makosa yote ya kihalifu.

Kwa maneno mengine, linapokuja suala la uchunguzi wa makosa ya uhalifu kwa upande wa Tanzania Bara siyo Mbunge, Rais, Waziri Mkuu ama waziri mwingine yeyote anapewa wajibu huo isipokuwa ofisi hii.

Sheria hii inasisitiza kuwa linapokuja suala la kusimamia mambo ya uchunguzi wa kihalifu, bosi wa mambo hayo ni Mkurugenzi wa Mashtaka.

Ibara ya 4:4 ya sheria hiyo inasema wazi kuwa DPP au mtu anayepewa jukumu la kuendesha mashtaka kwa niaba yake anakuwa na kile ambacho kisheria kinaitwa locus stand yaani, anaweza kusimama na kuzungumza kwenye Mahakama yoyote nchini.

Yaani, hata kama kesi haimhusu moja kwa moja lakini endapo kuna ulazima wa yeye kutoa maoni yake, basi anapewa nafasi hiyo.

Ibara ya nane ya sheria hiyo inaweka kanuni kubwa tatu za utendaji kazi wa DPP (ofisi hiyo ya mashtaka) kwamba katika utendaji kazi wake kanuni hizi tatu zizingatiwe.

Kwanza, haja ya kuhakikisha haki inatendeka, pili kuhakikisha hakuna matumizi mabaya ya mchakato wa kupata haki na tatu maslahi ya umma.

Nguvu kubwa na madaraka yake yanawekwa pasipo utata katika ibara ya nane ambapo tunaambiwa nguvu za ofisi hiyo, sheria inasema ana uwezo wa kuanzisha mashtaka, kuendesha na kudhibiti uendashaji wa mashtaka ya kosa lolote isipokuwa yale ya kijeshi.

Kwa maneno mengine, DPP anaweza kuanzisha mashtaka juu ya mtu yeyote (pale ambapo kuna makosa anayotuhumiwa), kuyasimamia hadi mwisho wake.

Aidha, sheria hiyo inaeleza, DPP anao uwezo wa kutoa maagizo kwa polisi au chombo chochote cha uchunguzi kuchunguza taarifa zozote zinadokeza uhalifu na kutoa taarifa mapema.

Ni hii nguvu ya Ibara ya 9:1(e) ndiyo inayonifanya niamini kabisa kuwa DPP wetu aidha hana ubavu wa kuhakikisha haki inapatikana au amekuwa goigoi katika kutimiza wajibu wake wa kisheria na hivyo kuwa mvunjaji wa kwanza wa sheria zetu.

Kwa maneno mengine, hakukuwa na sababu ya Rais Kikwete kuunda ‘Timu ya uchunguzi wa EPA’ kwani jukumu hilo linaangukia mikononi mwa DPP. Hata ibara ya 11 ambayo yawezekana kutumika katika kesi za EPA inasema wazi kuwa kwenye makosa ambapo watu wamenufaika na mapato ya uhalifu, basi idara hii inapaswa kutimiza wajibu wake.

Nguvu hizi zinarudiwa tena kwenye ibara ya 16:2 ambapo pasipo utata wowote inasemwa wazi kuwa DPP anaweza kuleta mashtaka pale ambapo kuna tuhuma za uhalifu. Yaani hatakiwi kusubiri wabunge wapige kelele au Rais na Waziri Mkuu amuagize. Hizi ni nguvu alizo nazo.

Kwanini nimeandika haya tena (nilishawahi kuandika huko nyuma). Sababu kubwa ni kwamba DPP wetu hajatumia madaraka yake ipasavyo na amekuwa akisubiri maelekezo ya wanasiasa ili afanye kazi yake. Kuna mifano mingi michache tu nitairudia hapa.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukitoa taarifa za wazi na nyaraka kuhusu masuala mbalimbali ya uhalifu lakini naamini kwamba, DPP wetu ni mzembe, amechoka na hana ubavu wa kufanya mambo kwa mujibu wa sheria wala kuanzisha uchunguzi wakati ushahidi wote uko wazi.

Kama Rais Kikwete, asingeunda kile Kikosi Kazi cha Kuchunguza EPA, leo tungekuwa tunaendelea kuombea na kulalamika. Hata hivyo DPP ana uwezo na nguvu kubwa ya kuunda timu ya uchunguzi ule bila kuuliza Ikulu; hakufanya hivyo na hivyo kuthibitisha kutokufaa kwake kuongoza idara hiyo.

Hadi leo, tunalalamika na kuweka ushahidi wa Mwananchi Gold, Deep Green Finance na wenzao lakini DPP wetu anakaa pembeni na kusubiri Rais aunde tume au Bunge lianzishe uchunguzi.

Tuhuma za Meremeta

Tayari kuna ushahidi wa kutosha kuwa uhalifu umefanyika ambao umesababisha upotevu mkubwa wa mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu kwenda kwenye mifuko ya watu wachache ambao miongoni mwao ni watu waliowahi kushika nafasi kubwa za utawala kwenye vyombo vya usalama na ulinzi. Kwa nini DPP hajaanzisha uchunguzi?

Tuhuma za Mwananchi Gold, Deep Green Finance, Tangold

Hizi nazo ni tuhuma nzito ambazo zimeshadokezwa mara nyingi na nyaraka, tarehe, hadi majina ya watuhumiwa yako wazi (wengine wakiendelea kushika nafasi za uongozi hadi leo hii) na jinsi gani kundi hilo liliweza kutumia nafasi zao kuchota mabilioni ya fedha za Watanzania.

Kwa karibu miaka mitatu sasa nyimbo hizi zimeimbwa na kurudiwa kama kiitikio, DPP wetu yuko wapi? Ndugu zangu jibu ni jepesi.

Tuhuma za Kagoda Agriculture

Ingawa hili linaangukia kwenye sakata la EPA lakini tukilichukulia kwa upande wake peke yake naweza kusema pasipo utata wowote kuwa ni mojawapo ya mambo ya kipuuzi na kijinga kukuta utawala wa sheria nchini.

Ni ya kipuuzi na kijinga kwa sababu tunao uwezo wote wa kulishughulikia na kulimaliza kwa sekunde chache endapo tungekuwa na DPP ambaye hagwai mbele ya watawala.

Inashangaza kuwa licha ya nguvu zote ambazo DPP anazo hadi leo hii, najiuliza Kagoda ni kina nani? DPP anawajua wahusika na akitaka kuwaletea mashtaka anaweza lakini kwa sababu ya woga au kutokuwa na moyo wa kuthubutu amekaa pembeni na kuwaachia wanasiasa wazungushane kama wanaocheza ukuti ukuti.

Kwa nini DPP na idara yake wanaendelea kugwaya mbele ya mafisadi wa Kagoda? Jibu ni jepesi.

Tuhuma za manunuzi mabaya jeshini

Mojawapo ya idara ambazo zimetajwa kuhusika na ufisadi mkubwa na matumizi mabaya ya fedha za Watanzania ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kwa miaka kadhaa kundi la watu wachache wametumia usiri wa mambo yetu ya kijeshi kufanya ufisadi ambao ukiuandika tunaweza kupigiwa kelele na kina Ghasia.

Kundi hili ambalo linajulikana limeingiza nchi kwenye mikataba mibovu, kuangiza vifaa vibovu huku wao wenyewe wakimegewa mabilioni ya shilingi ambayo wametumia kuanzisha makampuni yao.

Makampuni ambayo baadaye yakapewa tenda kwenye mambo mbalimbali ya usalama! DPP wetu anajua haya na ushahidi anaujua upo (kwa kuanzia aangalie ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Serikali!).

Kwanini hajaanzisha uchunguzi? Kwanini hadi leo wahusika wanakaa pembeni na wengine kuachwa kustaafu kwa furaha huku wengine wakiendelea na biashara zao na wengine wakithubutu hata kugombea nafasi za uongozi kwa tiketi ya chama tawala (kwa wasiojua chama hicho ni CCM)? Jibu ni jepesi.

Tuhuma za ufisadi ATCL

Kwa karibu mwaka mzima tumeandika na kudokeza juu ya ufisadi uliokubuhu kule ATCL. Tukadokeza malipo yaliyofanyika na kiasi cha pesa kilichotumiwa.

Tukaonesha kuwa hata ndege tuliyotaka kujivunia ni mkwechwe; tukadokeza jinsi gani marubani hata wanafunzi (huko makwao), wanaingia kurusha ndege zetu.

Tukadokeza jinsi kundi la watu wachache kule ATCL wametumia nafasi zao kujibinafsisha magari kwa kuingia mikataba ya ajabu. DPP alifanya nini? Hakuna!

Leo hii, ati wabunge wanaulizana nini kimetokea, rais anashangaa hali imefikaje hapa na waziri mhusika anaunda tume kuchunguza ili kujua wahusika? Kama huu siyo wazimu wa watu waliosoma ni nini hiki?

DPP muda wote huu yuko wapi? Sheria inampa nguvu ya kuingilia na kuanzisha uchunguzi wa jambo lolote pale panapodaiwa kutokea uhalifu, kwanini DPP wetu amekaa pembeni kusubiri maelekezo ya wanasiasa wakati ana nguvu zote za kufanya uchunguzi na kuleta mashtaka? Jibu ni jepesi.

Tuhuma za wanafunzi waliotelekezwa Ukraine

moja ya vitendo ambavyo vinabakia katika historia kama uonevu mkubwa wa serikali dhidi ya raia wake ni suala la vijana wetu karibu 30 walipotelekezwa kule Ukraine na kuachwa kule kwenye ubaridi wa Jiji la Kiev mbele ya ubalozi wa Uingereza.

Ninatambua ndani ya moyo wangu kabisa kuwa hakuna wakati ambapo ubabe wa watumishi wachache ulivumiliwa na kuzawadiwa dhidi ya vijana wasio na mtetezi kama wakati ule.

Nakumbuka idadi ya wabunge niliowaomba wawasimamie vijana hawa. Wabunge wote wa CCM niliozungumza nao waliogopa kwa sababu ya kuonekana wanapingana na serikali!

Kama nilivyoandika wakati ule, nina shukrani yangu milele kwa wale wote waliojitokeza kusimama na vijana wale kwani kwa mara ya kwanza kikundi cha vijana wasio na lolote waliweza kusimama dhidi ya serikali yao!

Kati ya mambo yote niliyoyafanya na kuyasimamia hakuna jambo linalonigusa moyoni kama ubabe ule wa Serikali ya Rais Kikwete.

Siwezi kusahau jibu la mmoja wa watendaji wakubwa aliyenijibu kuwa yuko mezani anakula wakati vijana wetu wamelala nje ya ubalozi wa Uingereza wakililia kitu kimoja, waachwe waendelee na masomo! Sijasahau lile, na sidhani kama niko tayari kuwasamehe!

Tulionyesha wakati ule na kwa karibu kipindi cha mwaka mzima jinsi gani Bodi ya Mikopo iliwahadaa vijana hawa na kuwachuuza ugenini kwa sababu hawakutaka kuwagawia fedha zao za ada na kushiriki katika ufisadi wa bodi hiyo.

Tukaweka na nyaraka na hoja zikajengwa za kuonyesha jinsi gani bodi hiyo iliyokuwa chini ya wizara iliyoongozwa na Profesa ilivyokuwa inalipiza kisasi kwa vijana hawa na kuwatelekeza ugenini.

Leo, watu wale wale tuliowapigia kelele ati wameamka na kutambua kuna matatizo bodi ya mikopo! Kama huku siyo kulala kwa dereva kwenye usukani tukuiteje huku?

Kwa nini hadi leo DPP hajaagiza uchunguzi wa kufuatilia nini kilitokea au kuwahoji wale vijana waliorudishwa kwa maagizo ya serikali na kwa fedheha ili kujua ni nani alikuwa anahusika na kuona kama kuna mashtaka ya kuletwa mbele ya mahakama kama yakina Mramba na Yona au zaidi? Najua kwanini; jibu ni jepesi;

Tuhuma dhidi ya Rostam

Kati ya Watanzania ambao majina yao yanahusishwa na uvunjaji mkubwa wa sheria nchini ni jina la Mbunge wa Igunga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz.

Huyu anatajwa kwenye mambo mengi na kuhusishwa na baadhi ya kesi ambazo nimezitaja hapo juu. Zaidi ya yote katika suala la Dowans wengi tunafahamu kilichosemwa kwenye Kamati Teule ya Bunge na majibu aliyoyatoa mbele ya waandishi wa habari.

Lakini, tunafahamu maendeleo ya hivi karibuni ambapo mtu anayeonekana kwenye nyaraka za umiliki za BRELA (Suleiman Al-Adawi), anamtaja Rostam kuwa ni rafiki yake na baadhi ya vyombo vya habari vilikiri kuwa Mbunge huyo anamtambua Al-Adawi na kwamba alihusika katika kumshawishi kuleta mitambo ile ya majenereta.

Rostam, alikana kuwajua watu wa Dowans! Leo, ushahidi wote unamhusisha na wengine katika kujaribu kuhakikisha majenereta ya Dowans yanauzwa kwa Tanzania kwa fedha zilizotengwa tangu kwenye bajeti ya mwaka jana (Angalia Mpango wa Maendeleo wa 2008/2009).

Tulipopinga kwa sauti kali ununuzi wa mitambo ya Dowans nguvu kubwa ilitumika kujaribu kutushawishi hadi tulipowalazimisha kusalimu amri.

Hata hivyo kitu ambacho hakijaangaliwa hadi leo ni jinsi gani kampuni ya Dowans Tanzania LTD ilianzishwa kwa makusudi huko Costa Rica ili hatimaye ipate nafasi ya kujiingiza nchini.

Uchunguzi huru (ambao nimeuratibu mwenyewe) umeonyesha pasipo shaka kuwa kampuni ya Portek International, ambayo ilitajwa na Salva (wakati akiwa Habari News) kuwa ina hisa kwenye kampuni ya Dowans Tanzania haina hisa hizo! Kampuni hiyo inatajwa kwenye nyaraka za BRELA!

Kampuni ya Dowans ya Costa Rica, ilianzishwa kwenye eneo huru la biashara (Free Trade Zone) haina ofisi, haina jengo na anuani inayotajwa kwenye nyaraka za BRELA ni anuani ya hilo eneo huru!

Hata ile Dowans Holdings ambayo tuliambiwa ni ya huko Falme za Kiarabu nayo anuani yake hadi simu ni za Benki ya Canadian Royal Bank! Uchunguzi wa huko nao unaonyesha hakuna kampuni iliyoandikishwa huko.

Katika maeneo yote hayo, Rostam anahusishwa kwa namna moja au nyingine! Kwanini DPP hadi hivi sasa hajaamua kuanzisha uchunguzi huru wa Dowans na wahusika wake?

Kwanini DPP baada ya taarifa ya Bunge hakuanzisha uchunguzi dhidi ya Rostam? Kama uchunguzi huru ungefanywa na kuhakikisha haya tunayoyasema kuwa yana ukweli au uongo au ni uzushi au ni “chuki binafsi” au ni “ubaguzi” si Rostam angeondolewa hili wingu la ufisadi ambalo linamzunguka?

Ninafahamu jibu lao la kitabuni “kama mna ushahidi uwasilisheni kwa vyombo husika”! Jibu hili halina msingi kwangu kwa sababu hata tukiwawekea ushahidi hadi kwenye meza zao hawawezi kufanya lolote?

Kwani suala la DECI lilikuwaje? Watu wa usalama wa taifa waliliandikia hili kabla hata ya watu wa Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana hawajaandika ile taarifa yao kwa DCI.

Maofisa wetu wa mitaani wa Usalama wa Taifa waliandika taarifa mapema na kutoa mapendekezo yao lakini hatua hazikuchuliwa! Tena wao waliandika kuanzia 2007!

Sasa, wanataka tuwatafutie ushahidi, tuwaletee, tuwafafanulie na bado tutoe mapendekezo wakati wote huo wao wanafanya nini? Kula bila kulipa? DPP yuko wapi? Jibu ni jepesi!

Si lazima mashtaka yote yaendeshwe na ofisi yake. Wengine wanaweza kujibu na kusema mambo haya yote unayaleta dhidi ya DPP mbona ni mengi hivyo? Kwamba, hawezi kufanya kazi hizo zote na kuendesha mashtaka yoyote yeye mwenyewe kwani ni mengi na mazito. Watetezi hao wanaweza kusema kuwa DPP ana majukumu mengi na kesi nyingi za kufuatilia.

Jibu langu ni kuwa sheria iliyounda ofisi yake inatambua hilo. Ni kwa sababu hiyo sheria hiyo inasema hivi (nitainukuu) “The Director may appoint a person to be a Public Prosecutor from other departments of the Government, Local Government authority or private practice to prosecute a specified case or cases on his behalf”.

Yaani, Mkurugenzi anaweza kumteua mtu yeyote kutoka idara ya serikali kuu, serikali za mitaa au hata sekta binafsi kuendesha mashtaka ya kesi mbalimbali kwa niaba yake.

Nguvu hii ni ya ajabu na DPP wetu hajaitumia ipasavyo. Leo hii tuna wanasheria wengi ambao wanaweza kutimiza masharti ya kisheria ya kuwa PP. Wapo kwenye vyuo vikuu, kwenye mashirika mbalimbali na idara mbalimbali.

Na kama akitaka msaada wa kuwatambua ni wazi anaweza kuwasiliana na Chama cha Wanasheria au Mahakama Kuu ambao wamesajiliwa.

Yaani, katika kuendesha mashtaka DPP halazimiki kutegemea waendesha mashtaka wa serikali tu (chini ya ofisi yake) au wa Polisi bali anaweza kuwaomba hata kina Issa Shivji au watu wengine ambao wanaweza kuendesha mashtaka.

Hii ina maana gani?

Ina maana ya kwamba kwa vile tayari ana uwezo wa kuagiza chombo kufanya uchunguzi basi anaweza pia baada ya uchunguzi huo kuteua mtu au jopo la watu kuwa waendesha mashtaka kwa niaba yake na watu hao si lazima wawe watumishi serikalini.

Ninaamini, wanasheria wetu wanaweza kujitokeza au vyama vya sheria vya makundi mbalinbali vinaweza kujitokeza na kumtaarifu kuwa wanao watumishi ambao wako tayari kuendesha mashtaka kwa niaba ya DPP wakiteuliwa hata kama kwa kujitolea (pro bono) au kwa malipo ya mkataba. Wakifanya hivi tutaona kama DPP atawakatalia au atasema hana waendesha mashtaka wa kutosha.

Akiamua kufanya hivi ina maana kesi mbalimbali na hasa hizi zinazohusiana na ufisadi zinaweza kuendeshwa kwa haraka na kundi la watu waliobobea katika kazi yao na hivyo kuhakikisha kuwa karibu ya 2010 kesi hizi za ufisadi zote zinakuwa zimemalizwa na Taifa lizungumzie ajenda mpya ya uchaguzi. Lakini siamini DPP wetu atafanya hivyo. Kwanini; kwa sababu jibu ni jepesi.

Jibu Jepesi

Ndiyo! Jibu ni jepesi. DPP wetu hana uwezo wa kusimamia utawala wa sheria nchini na kuhakikisha mashtaka yanayostahili na yanayotakiwa yanaletwa dhidi ya mtu yeyote, chombo chochote na wakati wowote ule.

DPP wetu ni mwoga; anaogopa kuwaletea watu kashkash, anaogopa kuwaudhi wale waliomsaidia kufika alipofika. DPP wetu hana uthubutu wa kufanya kazi yake kwa kuangalia sheria na kwa kutumia nguvu alizopewa na Bunge limempa. Hawezi kuthubutu.

Thank you m..kijiji. God lead you through to let many tanzania know what they are supposed to knoe!!!!!
 
MMMwanakijiji mimi ni mpenzi wa makala zako. Lakini wakati mwingine naona unaoverdo. Unasema umeshawakilisha kwa DPP ushahidi ambao unatosheleza kuwafungulia mashtaka mafisadi. Sasa je unauhakika ushahidi uliwasilisha unaweza kuthibtisha kosa la jinai bila shaka yoyote? Je ushahidi ambao unthibtisha kosa la jinai unatakiwa uwe wa namna gani? Huo ushahidi uliowasilisha unakidhi vigezo vya kukubalika mahakamani kwa mujibu wa sheria ya ushahidi? Je ushahidi huo uliouwasilisha ulipatikana kwa kufuata vigezo vyote vya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai? Wewe ni mwandishi mzuri sana basi tuandikie makala yenye kuelezea ushahidi huo, uuambatanishe na uueleze ni kwa namna gani kwa kufuata reasoning ya kisheria shauri la jinai linaweza kuthibtika bila shaka yoyote. Leta humu ili tuweze kumjadili DPP vizuri. Naomba ufanye hayo niliyokueleza vinginevyo utakuwa unakurupuka katika kutoa hoja kushutumu watu bila utfiti wa kisayansi.
 
Cyberspace kama wewe sio dpp basi ni ndugu yake au mpambe wake au upo ofisi moja na dpp na kama sivyo basi ni mnufaikaji wa mfumo huo.

Ni utafiti gani wa kisayansi ambao ungependa MM auwasilishe hapa ili uridhike na kumjadili dpp? Je unaielewa Tanzania na skandali za kesi za rushwa zilizozimwa na dpp kwa kisingizio cha kukosa ushahidi japo pccb walikuwa wamekusanya ushahidi wa kutosha? Labda nikupe mfano mmoja tu kwamba Tanzania kuna sheria ya kumbana mtumishi wa umma aliye na kipato kisichopelekana na kipato chake na kwa nchi yetu ilivyo kuna watumishi wa umma ambao sasa ni mabilionea na taarifa zao zipo kwa dpp lakini bado anazui wasishitakiwe kwa kigezo cha kukosekana ushahidi!

Haya yote yana mwisho na itawagharimu wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kuifisadi nchi kwa madaraka au rasilimali, kaa chonjo ndugu yangu kizazi hiki ndicho kitakacho shuhudia haya wala si kingine
 
Cyberspace kama wewe sio dpp basi ni ndugu yake au mpambe wake au upo ofisi moja na dpp na kama sivyo basi ni mnufaikaji wa mfumo huo.<br />
<br />
Ni utafiti gani wa kisayansi ambao ungependa MM auwasilishe hapa ili uridhike na kumjadili dpp? Je unaielewa Tanzania na skandali za kesi za rushwa zilizozimwa na dpp kwa kisingizio cha kukosa ushahidi japo pccb walikuwa wamekusanya ushahidi wa kutosha? Labda nikupe mfano mmoja tu kwamba Tanzania kuna sheria ya kumbana mtumishi wa umma aliye na kipato kisichopelekana na kipato chake na kwa nchi yetu ilivyo kuna watumishi wa umma ambao sasa ni mabilionea na taarifa zao zipo kwa dpp lakini bado anazui wasishitakiwe kwa kigezo cha kukosekana ushahidi!<br />
<br />
Haya yote yana mwisho na itawagharimu wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kuifisadi nchi kwa madaraka au rasilimali, kaa chonjo ndugu yangu kizazi hiki ndicho kitakacho shuhudia haya wala si kingine
<br />
Mimi sina undugu wowote na DPP, wala sinufaiki na chochote. Mimi naamini katika haki simtetei mtu kwa vile nina alliance nae kama ambavyo kwa akili yako finyu unaona watu ambao wako tofauti na mawazo yako basi wanaintrest na vitu wanavyovisemea. Ebu niambie mwenzangu wewe unaintrest na PCCB mpaka uawatetea kwamba walileta ushahidi wa kujitosheleza DPP akaukataa. Ebu tueeleze ni kesi zipi hizo za rushwa na ushahidi ulikuwaje? Don't take things on face value my dear. Tambua sheria ni sayansi any alleged facts lazima ziwe proved, tusiendeshwe na hisia na maneno ya mtaani.
 
Sio tuu mimi na wewe hatuwezi kumbana DPP, bali hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumbana, hata rais hawezi!.
Mzee MMKJJ, yote uliyosema kuhusu DPP ni kweli, lakini pia kwa mujibu ya sheria iliyounda ofisi ya DPP, havunji sheria yoyote kwa kutofanya uchunguzi wowote kwa vile hayo ndio mamlaka yake ambayo kisheria, anayatumia at his discretion as he pleases at his pleasure na sheria inamlinda.
Kwa maoni yangu, tatizo sio DPP, tatizo ni mamlaka ya ajabu yaliyochini ya DPP.
Niliwahi kuchangia mahali nikaainisha sheria yetu iliyounda ofisi ya DPP, amepewa mamlaka makubwa yac ajabu, na hayo aliyoyaainisha MMKJJ ni dibaji tuu, nguvu haswa za DPP ni pamoja na 'power to declare nolle proseque' yaani hakuna kesi ya kujibu. DPP huyu anauwezo wa kuingilia kesi yoyote ya jinai, ikiwa mahakama yoyote na ikiwa katika hatua yoyote kabla ya hukumu, kuisimamisha, kingilia, ama kuifuta bila kulazimika kutoa sababu zozote wala maelezo yoyote.
Sheria ya DPP inamtaka kutimiza wajibu wake bila shinikizo lolote kutoka popote na hata akiletewa kesi yoyote ni discretion yake aprosecute ama asiprosecute na hakuna chombo chochote ndani ya JMT chenye mamlaka ya kumuuliza lolote DPP, hata rais hana mamlaka hayo, sembuse MMKJJ?.

Naungana na WoS sisi mwisho wetu ni kupiga tuu kelele, japo za mlango, siku moja moja mwenye nyumba atakosa usingizi kwa sababu nyingine na atazisikia hizi kelele za mlango na ama ataamka na kuubana mlango, ama atautia kizuizi ili usiendelee kupiga kelele.

Enzi za Mwalimu kulikuwa na sheria ya 'Presidential Preventive Detention Orders' iliyompa rais mamlaka ya kumuweka mtu yoyote kizuizini kwa kipindi chochote bila kutoa sababu yoyote. Mwalimu Nyerere aliitumia kipindi chote cha utawala wake. Kipindi cha Mwinyi, wanasheria wa chuo kikuu wakiongozwa na Shivji na Mgongo Fimbo, waliichalenge sheria hii kwa 'court review' na mahakama ikatamka its a bad law, hivyo ikamlazimisha rais, kila akisaini 'preventive detention order' lazima atoe sababu. kuna detention moja ya Mwinyi ilipigwa chini na mtuhumiwa kuachiwa huru.

Kama wanasheria wetu, waliweza kufanya hivi dhidi ya mamlaka ya rais, wanashindwa nini kwenye mamlaka ya DPP?.
Kwa mawazo yangu, 'Tatizo sio Feleshi as DPP, ni mamlaka yake makubwa mno anayatumia atakavyo bila kuvunja sheria. Tazizo ni the institutional of the DPP.
Wanabodi,
Nafanya tuu mapitio ya nilichowahi kuandika kuhusu mamlaka ya DPP, ili kulinganisha na kilichofanyika kwenye kesi ya Rwakatare, nimesoma mahali kuhusu wanasheria wa Chadema, kufungua kesi, kuhoji mamlaka hii, kwa maoni yangu, its a wastage of time!.
Pasco.
 
Nadhani, watu wakisoma wataelewa wanapomtwisha JK lawama za watu kufikishwa mahakamani wanakosea. Wakumkomalia ni DPP. Huyu jamaa ndiyo kikwazo kikubwa cha mapambano haya kwani kama angekuwa anafanya kazi yake kama alivyoapa na kwa mujibu wa sheria leo hii tusingekuwa tunazungumza mambo mengine ambayo tunazungumza. Aidha afanye kazi yake au aamue kukaa pembeni aingie mtu mwingine mwenye ujasiri wa kufanya kazi hiyo.

Wa mkuu tuache ushabiki na fitina, mambo ya kutoa haki ni makubwa yanahitaji busara na akili nyingi bila kumuonea haya mtu, wala huruma, sio mambo ya kukurupuka kama wengi wetu tunavyofikilia.
 
Kusema kwel ni ndefu mno hamna video yake youbute nijaiangalie au audio yake unitumie wasap
DPP wetu kizuizi mapambano dhidi ya ufisadi

M. M. Mwanakijiji

Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MAPAMBANO ya ufisadi nchini sasa hivi yanakwamishwa siyo na Rais Jakaya Kikwete kama wengi wanavyotaka tuamini, bali yanakwazwa na Mwendesha Mashtaka.

Sina wasiwasi hata kidogo kuwa kama tungekuwa na mwendesha mashtaka mzuri anayejua nguvu alizonazo za kisheria, nina uhakika baadhi ya mambo tunayoendelea kuyaimba kila kukicha, yangeisha na kusahaulika karne moja iliyopita!

Nguvu za Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kisheria ndiye mwenye nguvu kuliko hata rais, linapokuja suala la kuwashtaki watu.

Ana nguvu za kuchunguza jambo lolote linalohusu makosa ya kihalifu. Yaani, haihitaji hata kupewa ushahidi anaposikia kuna mtu anatuhumiwa hivi au vile, ana uwezo wa kuanzisha uchunguzu mara moja.

Sheria inampa DPP uwezo mkubwa wa kuhakikisha kuwa sheria za nchi zetu zinafuatwa, wahalifu wanashughulikiwa na utawala wa sheria unadumishwa.

Hadi hivi sasa, ninadai kuwa DPP wetu ameshindwa kazi hiyo na matokeo yake badala ya kuongoza, amejikuta anafuata. Nimeshaandika juu ya DPP mara kadhaa sasa, bado ninaamini kuwa yeye ndiye mtu pekee anayestahili kubebeshwa lawama za utawala wa kujichagulia sheria za kufuata!

Mwaka 2008 Sheria ilipitishwa ambayo iliunda rasmi Idara ya Mwendesha Mashtaka ya Taifa, hivyo kujaribu kutenganisha shughuli za mwendesha mashtaka zilizokuwa zikifanyika chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ikiwa na waendesha mashtaka wengi chini ya Jeshi la Polisi.

Sheria hiyo ambayo wengi tuliililia, ililenga hasa kuhakikisha shughuli za Mwendesha Mashtaka zinakuwa huru kutoka shughuli nyingine na kuondoa mgongano usio wa lazima kati ya wahusika mbalimbali katika mchakato wa utafutaji na upatikanaji wa haki nchini.

Kwa mujibu wa sheria hiyo (Ibara 1:2) uwezo wa sheria hiyo unahusu mambo yote ya uendeshaji mashtaka upande wa Tanzania Bara na vilevile kuratibu na kusimamia uchunguzi wa makosa yote ya kihalifu.

Kwa maneno mengine, linapokuja suala la uchunguzi wa makosa ya uhalifu kwa upande wa Tanzania Bara siyo Mbunge, Rais, Waziri Mkuu ama waziri mwingine yeyote anapewa wajibu huo isipokuwa ofisi hii.

Sheria hii inasisitiza kuwa linapokuja suala la kusimamia mambo ya uchunguzi wa kihalifu, bosi wa mambo hayo ni Mkurugenzi wa Mashtaka.

Ibara ya 4:4 ya sheria hiyo inasema wazi kuwa DPP au mtu anayepewa jukumu la kuendesha mashtaka kwa niaba yake anakuwa na kile ambacho kisheria kinaitwa locus stand yaani, anaweza kusimama na kuzungumza kwenye Mahakama yoyote nchini.

Yaani, hata kama kesi haimhusu moja kwa moja lakini endapo kuna ulazima wa yeye kutoa maoni yake, basi anapewa nafasi hiyo.

Ibara ya nane ya sheria hiyo inaweka kanuni kubwa tatu za utendaji kazi wa DPP (ofisi hiyo ya mashtaka) kwamba katika utendaji kazi wake kanuni hizi tatu zizingatiwe.

Kwanza, haja ya kuhakikisha haki inatendeka, pili kuhakikisha hakuna matumizi mabaya ya mchakato wa kupata haki na tatu maslahi ya umma.

Nguvu kubwa na madaraka yake yanawekwa pasipo utata katika ibara ya nane ambapo tunaambiwa nguvu za ofisi hiyo, sheria inasema ana uwezo wa kuanzisha mashtaka, kuendesha na kudhibiti uendashaji wa mashtaka ya kosa lolote isipokuwa yale ya kijeshi.

Kwa maneno mengine, DPP anaweza kuanzisha mashtaka juu ya mtu yeyote (pale ambapo kuna makosa anayotuhumiwa), kuyasimamia hadi mwisho wake.

Aidha, sheria hiyo inaeleza, DPP anao uwezo wa kutoa maagizo kwa polisi au chombo chochote cha uchunguzi kuchunguza taarifa zozote zinadokeza uhalifu na kutoa taarifa mapema.

Ni hii nguvu ya Ibara ya 9:1(e) ndiyo inayonifanya niamini kabisa kuwa DPP wetu aidha hana ubavu wa kuhakikisha haki inapatikana au amekuwa goigoi katika kutimiza wajibu wake wa kisheria na hivyo kuwa mvunjaji wa kwanza wa sheria zetu.

Kwa maneno mengine, hakukuwa na sababu ya Rais Kikwete kuunda ‘Timu ya uchunguzi wa EPA' kwani jukumu hilo linaangukia mikononi mwa DPP. Hata ibara ya 11 ambayo yawezekana kutumika katika kesi za EPA inasema wazi kuwa kwenye makosa ambapo watu wamenufaika na mapato ya uhalifu, basi idara hii inapaswa kutimiza wajibu wake.

Nguvu hizi zinarudiwa tena kwenye ibara ya 16:2 ambapo pasipo utata wowote inasemwa wazi kuwa DPP anaweza kuleta mashtaka pale ambapo kuna tuhuma za uhalifu. Yaani hatakiwi kusubiri wabunge wapige kelele au Rais na Waziri Mkuu amuagize. Hizi ni nguvu alizo nazo.

Kwanini nimeandika haya tena (nilishawahi kuandika huko nyuma). Sababu kubwa ni kwamba DPP wetu hajatumia madaraka yake ipasavyo na amekuwa akisubiri maelekezo ya wanasiasa ili afanye kazi yake. Kuna mifano mingi michache tu nitairudia hapa.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukitoa taarifa za wazi na nyaraka kuhusu masuala mbalimbali ya uhalifu lakini naamini kwamba, DPP wetu ni mzembe, amechoka na hana ubavu wa kufanya mambo kwa mujibu wa sheria wala kuanzisha uchunguzi wakati ushahidi wote uko wazi.

Kama Rais Kikwete, asingeunda kile Kikosi Kazi cha Kuchunguza EPA, leo tungekuwa tunaendelea kuombea na kulalamika. Hata hivyo DPP ana uwezo na nguvu kubwa ya kuunda timu ya uchunguzi ule bila kuuliza Ikulu; hakufanya hivyo na hivyo kuthibitisha kutokufaa kwake kuongoza idara hiyo.

Hadi leo, tunalalamika na kuweka ushahidi wa Mwananchi Gold, Deep Green Finance na wenzao lakini DPP wetu anakaa pembeni na kusubiri Rais aunde tume au Bunge lianzishe uchunguzi.

Tuhuma za Meremeta

Tayari kuna ushahidi wa kutosha kuwa uhalifu umefanyika ambao umesababisha upotevu mkubwa wa mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu kwenda kwenye mifuko ya watu wachache ambao miongoni mwao ni watu waliowahi kushika nafasi kubwa za utawala kwenye vyombo vya usalama na ulinzi. Kwa nini DPP hajaanzisha uchunguzi?

Tuhuma za Mwananchi Gold, Deep Green Finance, Tangold

Hizi nazo ni tuhuma nzito ambazo zimeshadokezwa mara nyingi na nyaraka, tarehe, hadi majina ya watuhumiwa yako wazi (wengine wakiendelea kushika nafasi za uongozi hadi leo hii) na jinsi gani kundi hilo liliweza kutumia nafasi zao kuchota mabilioni ya fedha za Watanzania.

Kwa karibu miaka mitatu sasa nyimbo hizi zimeimbwa na kurudiwa kama kiitikio, DPP wetu yuko wapi? Ndugu zangu jibu ni jepesi.

Tuhuma za Kagoda Agriculture

Ingawa hili linaangukia kwenye sakata la EPA lakini tukilichukulia kwa upande wake peke yake naweza kusema pasipo utata wowote kuwa ni mojawapo ya mambo ya kipuuzi na kijinga kukuta utawala wa sheria nchini.

Ni ya kipuuzi na kijinga kwa sababu tunao uwezo wote wa kulishughulikia na kulimaliza kwa sekunde chache endapo tungekuwa na DPP ambaye hagwai mbele ya watawala.

Inashangaza kuwa licha ya nguvu zote ambazo DPP anazo hadi leo hii, najiuliza Kagoda ni kina nani? DPP anawajua wahusika na akitaka kuwaletea mashtaka anaweza lakini kwa sababu ya woga au kutokuwa na moyo wa kuthubutu amekaa pembeni na kuwaachia wanasiasa wazungushane kama wanaocheza ukuti ukuti.

Kwa nini DPP na idara yake wanaendelea kugwaya mbele ya mafisadi wa Kagoda? Jibu ni jepesi.

Tuhuma za manunuzi mabaya jeshini

Mojawapo ya idara ambazo zimetajwa kuhusika na ufisadi mkubwa na matumizi mabaya ya fedha za Watanzania ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kwa miaka kadhaa kundi la watu wachache wametumia usiri wa mambo yetu ya kijeshi kufanya ufisadi ambao ukiuandika tunaweza kupigiwa kelele na kina Ghasia.

Kundi hili ambalo linajulikana limeingiza nchi kwenye mikataba mibovu, kuangiza vifaa vibovu huku wao wenyewe wakimegewa mabilioni ya shilingi ambayo wametumia kuanzisha makampuni yao.

Makampuni ambayo baadaye yakapewa tenda kwenye mambo mbalimbali ya usalama! DPP wetu anajua haya na ushahidi anaujua upo (kwa kuanzia aangalie ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Serikali!).

Kwanini hajaanzisha uchunguzi? Kwanini hadi leo wahusika wanakaa pembeni na wengine kuachwa kustaafu kwa furaha huku wengine wakiendelea na biashara zao na wengine wakithubutu hata kugombea nafasi za uongozi kwa tiketi ya chama tawala (kwa wasiojua chama hicho ni CCM)? Jibu ni jepesi.

Tuhuma za ufisadi ATCL

Kwa karibu mwaka mzima tumeandika na kudokeza juu ya ufisadi uliokubuhu kule ATCL. Tukadokeza malipo yaliyofanyika na kiasi cha pesa kilichotumiwa.

Tukaonesha kuwa hata ndege tuliyotaka kujivunia ni mkwechwe; tukadokeza jinsi gani marubani hata wanafunzi (huko makwao), wanaingia kurusha ndege zetu.

Tukadokeza jinsi kundi la watu wachache kule ATCL wametumia nafasi zao kujibinafsisha magari kwa kuingia mikataba ya ajabu. DPP alifanya nini? Hakuna!

Leo hii, ati wabunge wanaulizana nini kimetokea, rais anashangaa hali imefikaje hapa na waziri mhusika anaunda tume kuchunguza ili kujua wahusika? Kama huu siyo wazimu wa watu waliosoma ni nini hiki?

DPP muda wote huu yuko wapi? Sheria inampa nguvu ya kuingilia na kuanzisha uchunguzi wa jambo lolote pale panapodaiwa kutokea uhalifu, kwanini DPP wetu amekaa pembeni kusubiri maelekezo ya wanasiasa wakati ana nguvu zote za kufanya uchunguzi na kuleta mashtaka? Jibu ni jepesi.

Tuhuma za wanafunzi waliotelekezwa Ukraine

moja ya vitendo ambavyo vinabakia katika historia kama uonevu mkubwa wa serikali dhidi ya raia wake ni suala la vijana wetu karibu 30 walipotelekezwa kule Ukraine na kuachwa kule kwenye ubaridi wa Jiji la Kiev mbele ya ubalozi wa Uingereza.

Ninatambua ndani ya moyo wangu kabisa kuwa hakuna wakati ambapo ubabe wa watumishi wachache ulivumiliwa na kuzawadiwa dhidi ya vijana wasio na mtetezi kama wakati ule.

Nakumbuka idadi ya wabunge niliowaomba wawasimamie vijana hawa. Wabunge wote wa CCM niliozungumza nao waliogopa kwa sababu ya kuonekana wanapingana na serikali!

Kama nilivyoandika wakati ule, nina shukrani yangu milele kwa wale wote waliojitokeza kusimama na vijana wale kwani kwa mara ya kwanza kikundi cha vijana wasio na lolote waliweza kusimama dhidi ya serikali yao!

Kati ya mambo yote niliyoyafanya na kuyasimamia hakuna jambo linalonigusa moyoni kama ubabe ule wa Serikali ya Rais Kikwete.

Siwezi kusahau jibu la mmoja wa watendaji wakubwa aliyenijibu kuwa yuko mezani anakula wakati vijana wetu wamelala nje ya ubalozi wa Uingereza wakililia kitu kimoja, waachwe waendelee na masomo! Sijasahau lile, na sidhani kama niko tayari kuwasamehe!

Tulionyesha wakati ule na kwa karibu kipindi cha mwaka mzima jinsi gani Bodi ya Mikopo iliwahadaa vijana hawa na kuwachuuza ugenini kwa sababu hawakutaka kuwagawia fedha zao za ada na kushiriki katika ufisadi wa bodi hiyo.

Tukaweka na nyaraka na hoja zikajengwa za kuonyesha jinsi gani bodi hiyo iliyokuwa chini ya wizara iliyoongozwa na Profesa ilivyokuwa inalipiza kisasi kwa vijana hawa na kuwatelekeza ugenini.

Leo, watu wale wale tuliowapigia kelele ati wameamka na kutambua kuna matatizo bodi ya mikopo! Kama huku siyo kulala kwa dereva kwenye usukani tukuiteje huku?

Kwa nini hadi leo DPP hajaagiza uchunguzi wa kufuatilia nini kilitokea au kuwahoji wale vijana waliorudishwa kwa maagizo ya serikali na kwa fedheha ili kujua ni nani alikuwa anahusika na kuona kama kuna mashtaka ya kuletwa mbele ya mahakama kama yakina Mramba na Yona au zaidi? Najua kwanini; jibu ni jepesi;

Tuhuma dhidi ya Rostam

Kati ya Watanzania ambao majina yao yanahusishwa na uvunjaji mkubwa wa sheria nchini ni jina la Mbunge wa Igunga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz.

Huyu anatajwa kwenye mambo mengi na kuhusishwa na baadhi ya kesi ambazo nimezitaja hapo juu. Zaidi ya yote katika suala la Dowans wengi tunafahamu kilichosemwa kwenye Kamati Teule ya Bunge na majibu aliyoyatoa mbele ya waandishi wa habari.

Lakini, tunafahamu maendeleo ya hivi karibuni ambapo mtu anayeonekana kwenye nyaraka za umiliki za BRELA (Suleiman Al-Adawi), anamtaja Rostam kuwa ni rafiki yake na baadhi ya vyombo vya habari vilikiri kuwa Mbunge huyo anamtambua Al-Adawi na kwamba alihusika katika kumshawishi kuleta mitambo ile ya majenereta.

Rostam, alikana kuwajua watu wa Dowans! Leo, ushahidi wote unamhusisha na wengine katika kujaribu kuhakikisha majenereta ya Dowans yanauzwa kwa Tanzania kwa fedha zilizotengwa tangu kwenye bajeti ya mwaka jana (Angalia Mpango wa Maendeleo wa 2008/2009).

Tulipopinga kwa sauti kali ununuzi wa mitambo ya Dowans nguvu kubwa ilitumika kujaribu kutushawishi hadi tulipowalazimisha kusalimu amri.

Hata hivyo kitu ambacho hakijaangaliwa hadi leo ni jinsi gani kampuni ya Dowans Tanzania LTD ilianzishwa kwa makusudi huko Costa Rica ili hatimaye ipate nafasi ya kujiingiza nchini.

Uchunguzi huru (ambao nimeuratibu mwenyewe) umeonyesha pasipo shaka kuwa kampuni ya Portek International, ambayo ilitajwa na Salva (wakati akiwa Habari News) kuwa ina hisa kwenye kampuni ya Dowans Tanzania haina hisa hizo! Kampuni hiyo inatajwa kwenye nyaraka za BRELA!

Kampuni ya Dowans ya Costa Rica, ilianzishwa kwenye eneo huru la biashara (Free Trade Zone) haina ofisi, haina jengo na anuani inayotajwa kwenye nyaraka za BRELA ni anuani ya hilo eneo huru!

Hata ile Dowans Holdings ambayo tuliambiwa ni ya huko Falme za Kiarabu nayo anuani yake hadi simu ni za Benki ya Canadian Royal Bank! Uchunguzi wa huko nao unaonyesha hakuna kampuni iliyoandikishwa huko.

Katika maeneo yote hayo, Rostam anahusishwa kwa namna moja au nyingine! Kwanini DPP hadi hivi sasa hajaamua kuanzisha uchunguzi huru wa Dowans na wahusika wake?

Kwanini DPP baada ya taarifa ya Bunge hakuanzisha uchunguzi dhidi ya Rostam? Kama uchunguzi huru ungefanywa na kuhakikisha haya tunayoyasema kuwa yana ukweli au uongo au ni uzushi au ni "chuki binafsi" au ni "ubaguzi" si Rostam angeondolewa hili wingu la ufisadi ambalo linamzunguka?

Ninafahamu jibu lao la kitabuni "kama mna ushahidi uwasilisheni kwa vyombo husika"! Jibu hili halina msingi kwangu kwa sababu hata tukiwawekea ushahidi hadi kwenye meza zao hawawezi kufanya lolote?

Kwani suala la DECI lilikuwaje? Watu wa usalama wa taifa waliliandikia hili kabla hata ya watu wa Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana hawajaandika ile taarifa yao kwa DCI.

Maofisa wetu wa mitaani wa Usalama wa Taifa waliandika taarifa mapema na kutoa mapendekezo yao lakini hatua hazikuchuliwa! Tena wao waliandika kuanzia 2007!

Sasa, wanataka tuwatafutie ushahidi, tuwaletee, tuwafafanulie na bado tutoe mapendekezo wakati wote huo wao wanafanya nini? Kula bila kulipa? DPP yuko wapi? Jibu ni jepesi!

Si lazima mashtaka yote yaendeshwe na ofisi yake. Wengine wanaweza kujibu na kusema mambo haya yote unayaleta dhidi ya DPP mbona ni mengi hivyo? Kwamba, hawezi kufanya kazi hizo zote na kuendesha mashtaka yoyote yeye mwenyewe kwani ni mengi na mazito. Watetezi hao wanaweza kusema kuwa DPP ana majukumu mengi na kesi nyingi za kufuatilia.

Jibu langu ni kuwa sheria iliyounda ofisi yake inatambua hilo. Ni kwa sababu hiyo sheria hiyo inasema hivi (nitainukuu) "The Director may appoint a person to be a Public Prosecutor from other departments of the Government, Local Government authority or private practice to prosecute a specified case or cases on his behalf".

Yaani, Mkurugenzi anaweza kumteua mtu yeyote kutoka idara ya serikali kuu, serikali za mitaa au hata sekta binafsi kuendesha mashtaka ya kesi mbalimbali kwa niaba yake.

Nguvu hii ni ya ajabu na DPP wetu hajaitumia ipasavyo. Leo hii tuna wanasheria wengi ambao wanaweza kutimiza masharti ya kisheria ya kuwa PP. Wapo kwenye vyuo vikuu, kwenye mashirika mbalimbali na idara mbalimbali.

Na kama akitaka msaada wa kuwatambua ni wazi anaweza kuwasiliana na Chama cha Wanasheria au Mahakama Kuu ambao wamesajiliwa.

Yaani, katika kuendesha mashtaka DPP halazimiki kutegemea waendesha mashtaka wa serikali tu (chini ya ofisi yake) au wa Polisi bali anaweza kuwaomba hata kina Issa Shivji au watu wengine ambao wanaweza kuendesha mashtaka.

Hii ina maana gani?

Ina maana ya kwamba kwa vile tayari ana uwezo wa kuagiza chombo kufanya uchunguzi basi anaweza pia baada ya uchunguzi huo kuteua mtu au jopo la watu kuwa waendesha mashtaka kwa niaba yake na watu hao si lazima wawe watumishi serikalini.

Ninaamini, wanasheria wetu wanaweza kujitokeza au vyama vya sheria vya makundi mbalinbali vinaweza kujitokeza na kumtaarifu kuwa wanao watumishi ambao wako tayari kuendesha mashtaka kwa niaba ya DPP wakiteuliwa hata kama kwa kujitolea (pro bono) au kwa malipo ya mkataba. Wakifanya hivi tutaona kama DPP atawakatalia au atasema hana waendesha mashtaka wa kutosha.

Akiamua kufanya hivi ina maana kesi mbalimbali na hasa hizi zinazohusiana na ufisadi zinaweza kuendeshwa kwa haraka na kundi la watu waliobobea katika kazi yao na hivyo kuhakikisha kuwa karibu ya 2010 kesi hizi za ufisadi zote zinakuwa zimemalizwa na Taifa lizungumzie ajenda mpya ya uchaguzi. Lakini siamini DPP wetu atafanya hivyo. Kwanini; kwa sababu jibu ni jepesi.

Jibu Jepesi

Ndiyo! Jibu ni jepesi. DPP wetu hana uwezo wa kusimamia utawala wa sheria nchini na kuhakikisha mashtaka yanayostahili na yanayotakiwa yanaletwa dhidi ya mtu yeyote, chombo chochote na wakati wowote ule.

DPP wetu ni mwoga; anaogopa kuwaletea watu kashkash, anaogopa kuwaudhi wale waliomsaidia kufika alipofika. DPP wetu hana uthubutu wa kufanya kazi yake kwa kuangalia sheria na kwa kutumia nguvu alizopewa na Bunge limempa. Hawezi kuthubutu.
 
DPP wetu kizuizi mapambano dhidi ya ufisadi

M. M. Mwanakijiji

Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MAPAMBANO ya ufisadi nchini sasa hivi yanakwamishwa siyo na Rais Jakaya Kikwete kama wengi wanavyotaka tuamini, bali yanakwazwa na Mwendesha Mashtaka.

Sina wasiwasi hata kidogo kuwa kama tungekuwa na mwendesha mashtaka mzuri anayejua nguvu alizonazo za kisheria, nina uhakika baadhi ya mambo tunayoendelea kuyaimba kila kukicha, yangeisha na kusahaulika karne moja iliyopita!

Nguvu za Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kisheria ndiye mwenye nguvu kuliko hata rais, linapokuja suala la kuwashtaki watu.

Ana nguvu za kuchunguza jambo lolote linalohusu makosa ya kihalifu. Yaani, haihitaji hata kupewa ushahidi anaposikia kuna mtu anatuhumiwa hivi au vile, ana uwezo wa kuanzisha uchunguzu mara moja.

Sheria inampa DPP uwezo mkubwa wa kuhakikisha kuwa sheria za nchi zetu zinafuatwa, wahalifu wanashughulikiwa na utawala wa sheria unadumishwa.

Hadi hivi sasa, ninadai kuwa DPP wetu ameshindwa kazi hiyo na matokeo yake badala ya kuongoza, amejikuta anafuata. Nimeshaandika juu ya DPP mara kadhaa sasa, bado ninaamini kuwa yeye ndiye mtu pekee anayestahili kubebeshwa lawama za utawala wa kujichagulia sheria za kufuata!

Mwaka 2008 Sheria ilipitishwa ambayo iliunda rasmi Idara ya Mwendesha Mashtaka ya Taifa, hivyo kujaribu kutenganisha shughuli za mwendesha mashtaka zilizokuwa zikifanyika chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ikiwa na waendesha mashtaka wengi chini ya Jeshi la Polisi.

Sheria hiyo ambayo wengi tuliililia, ililenga hasa kuhakikisha shughuli za Mwendesha Mashtaka zinakuwa huru kutoka shughuli nyingine na kuondoa mgongano usio wa lazima kati ya wahusika mbalimbali katika mchakato wa utafutaji na upatikanaji wa haki nchini.

Kwa mujibu wa sheria hiyo (Ibara 1:2) uwezo wa sheria hiyo unahusu mambo yote ya uendeshaji mashtaka upande wa Tanzania Bara na vilevile kuratibu na kusimamia uchunguzi wa makosa yote ya kihalifu.

Kwa maneno mengine, linapokuja suala la uchunguzi wa makosa ya uhalifu kwa upande wa Tanzania Bara siyo Mbunge, Rais, Waziri Mkuu ama waziri mwingine yeyote anapewa wajibu huo isipokuwa ofisi hii.

Sheria hii inasisitiza kuwa linapokuja suala la kusimamia mambo ya uchunguzi wa kihalifu, bosi wa mambo hayo ni Mkurugenzi wa Mashtaka.

Ibara ya 4:4 ya sheria hiyo inasema wazi kuwa DPP au mtu anayepewa jukumu la kuendesha mashtaka kwa niaba yake anakuwa na kile ambacho kisheria kinaitwa locus stand yaani, anaweza kusimama na kuzungumza kwenye Mahakama yoyote nchini.

Yaani, hata kama kesi haimhusu moja kwa moja lakini endapo kuna ulazima wa yeye kutoa maoni yake, basi anapewa nafasi hiyo.

Ibara ya nane ya sheria hiyo inaweka kanuni kubwa tatu za utendaji kazi wa DPP (ofisi hiyo ya mashtaka) kwamba katika utendaji kazi wake kanuni hizi tatu zizingatiwe.

Kwanza, haja ya kuhakikisha haki inatendeka, pili kuhakikisha hakuna matumizi mabaya ya mchakato wa kupata haki na tatu maslahi ya umma.

Nguvu kubwa na madaraka yake yanawekwa pasipo utata katika ibara ya nane ambapo tunaambiwa nguvu za ofisi hiyo, sheria inasema ana uwezo wa kuanzisha mashtaka, kuendesha na kudhibiti uendashaji wa mashtaka ya kosa lolote isipokuwa yale ya kijeshi.

Kwa maneno mengine, DPP anaweza kuanzisha mashtaka juu ya mtu yeyote (pale ambapo kuna makosa anayotuhumiwa), kuyasimamia hadi mwisho wake.

Aidha, sheria hiyo inaeleza, DPP anao uwezo wa kutoa maagizo kwa polisi au chombo chochote cha uchunguzi kuchunguza taarifa zozote zinadokeza uhalifu na kutoa taarifa mapema.

Ni hii nguvu ya Ibara ya 9:1(e) ndiyo inayonifanya niamini kabisa kuwa DPP wetu aidha hana ubavu wa kuhakikisha haki inapatikana au amekuwa goigoi katika kutimiza wajibu wake wa kisheria na hivyo kuwa mvunjaji wa kwanza wa sheria zetu.

Kwa maneno mengine, hakukuwa na sababu ya Rais Kikwete kuunda &#8216;Timu ya uchunguzi wa EPA' kwani jukumu hilo linaangukia mikononi mwa DPP. Hata ibara ya 11 ambayo yawezekana kutumika katika kesi za EPA inasema wazi kuwa kwenye makosa ambapo watu wamenufaika na mapato ya uhalifu, basi idara hii inapaswa kutimiza wajibu wake.

Nguvu hizi zinarudiwa tena kwenye ibara ya 16:2 ambapo pasipo utata wowote inasemwa wazi kuwa DPP anaweza kuleta mashtaka pale ambapo kuna tuhuma za uhalifu. Yaani hatakiwi kusubiri wabunge wapige kelele au Rais na Waziri Mkuu amuagize. Hizi ni nguvu alizo nazo.

Kwanini nimeandika haya tena (nilishawahi kuandika huko nyuma). Sababu kubwa ni kwamba DPP wetu hajatumia madaraka yake ipasavyo na amekuwa akisubiri maelekezo ya wanasiasa ili afanye kazi yake. Kuna mifano mingi michache tu nitairudia hapa.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukitoa taarifa za wazi na nyaraka kuhusu masuala mbalimbali ya uhalifu lakini naamini kwamba, DPP wetu ni mzembe, amechoka na hana ubavu wa kufanya mambo kwa mujibu wa sheria wala kuanzisha uchunguzi wakati ushahidi wote uko wazi.

Kama Rais Kikwete, asingeunda kile Kikosi Kazi cha Kuchunguza EPA, leo tungekuwa tunaendelea kuombea na kulalamika. Hata hivyo DPP ana uwezo na nguvu kubwa ya kuunda timu ya uchunguzi ule bila kuuliza Ikulu; hakufanya hivyo na hivyo kuthibitisha kutokufaa kwake kuongoza idara hiyo.

Hadi leo, tunalalamika na kuweka ushahidi wa Mwananchi Gold, Deep Green Finance na wenzao lakini DPP wetu anakaa pembeni na kusubiri Rais aunde tume au Bunge lianzishe uchunguzi.

Tuhuma za Meremeta

Tayari kuna ushahidi wa kutosha kuwa uhalifu umefanyika ambao umesababisha upotevu mkubwa wa mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu kwenda kwenye mifuko ya watu wachache ambao miongoni mwao ni watu waliowahi kushika nafasi kubwa za utawala kwenye vyombo vya usalama na ulinzi. Kwa nini DPP hajaanzisha uchunguzi?

Tuhuma za Mwananchi Gold, Deep Green Finance, Tangold

Hizi nazo ni tuhuma nzito ambazo zimeshadokezwa mara nyingi na nyaraka, tarehe, hadi majina ya watuhumiwa yako wazi (wengine wakiendelea kushika nafasi za uongozi hadi leo hii) na jinsi gani kundi hilo liliweza kutumia nafasi zao kuchota mabilioni ya fedha za Watanzania.

Kwa karibu miaka mitatu sasa nyimbo hizi zimeimbwa na kurudiwa kama kiitikio, DPP wetu yuko wapi? Ndugu zangu jibu ni jepesi.

Tuhuma za Kagoda Agriculture

Ingawa hili linaangukia kwenye sakata la EPA lakini tukilichukulia kwa upande wake peke yake naweza kusema pasipo utata wowote kuwa ni mojawapo ya mambo ya kipuuzi na kijinga kukuta utawala wa sheria nchini.

Ni ya kipuuzi na kijinga kwa sababu tunao uwezo wote wa kulishughulikia na kulimaliza kwa sekunde chache endapo tungekuwa na DPP ambaye hagwai mbele ya watawala.

Inashangaza kuwa licha ya nguvu zote ambazo DPP anazo hadi leo hii, najiuliza Kagoda ni kina nani? DPP anawajua wahusika na akitaka kuwaletea mashtaka anaweza lakini kwa sababu ya woga au kutokuwa na moyo wa kuthubutu amekaa pembeni na kuwaachia wanasiasa wazungushane kama wanaocheza ukuti ukuti.

Kwa nini DPP na idara yake wanaendelea kugwaya mbele ya mafisadi wa Kagoda? Jibu ni jepesi.

Tuhuma za manunuzi mabaya jeshini

Mojawapo ya idara ambazo zimetajwa kuhusika na ufisadi mkubwa na matumizi mabaya ya fedha za Watanzania ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kwa miaka kadhaa kundi la watu wachache wametumia usiri wa mambo yetu ya kijeshi kufanya ufisadi ambao ukiuandika tunaweza kupigiwa kelele na kina Ghasia.

Kundi hili ambalo linajulikana limeingiza nchi kwenye mikataba mibovu, kuangiza vifaa vibovu huku wao wenyewe wakimegewa mabilioni ya shilingi ambayo wametumia kuanzisha makampuni yao.

Makampuni ambayo baadaye yakapewa tenda kwenye mambo mbalimbali ya usalama! DPP wetu anajua haya na ushahidi anaujua upo (kwa kuanzia aangalie ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Serikali!).

Kwanini hajaanzisha uchunguzi? Kwanini hadi leo wahusika wanakaa pembeni na wengine kuachwa kustaafu kwa furaha huku wengine wakiendelea na biashara zao na wengine wakithubutu hata kugombea nafasi za uongozi kwa tiketi ya chama tawala (kwa wasiojua chama hicho ni CCM)? Jibu ni jepesi.

Tuhuma za ufisadi ATCL

Kwa karibu mwaka mzima tumeandika na kudokeza juu ya ufisadi uliokubuhu kule ATCL. Tukadokeza malipo yaliyofanyika na kiasi cha pesa kilichotumiwa.

Tukaonesha kuwa hata ndege tuliyotaka kujivunia ni mkwechwe; tukadokeza jinsi gani marubani hata wanafunzi (huko makwao), wanaingia kurusha ndege zetu.

Tukadokeza jinsi kundi la watu wachache kule ATCL wametumia nafasi zao kujibinafsisha magari kwa kuingia mikataba ya ajabu. DPP alifanya nini? Hakuna!

Leo hii, ati wabunge wanaulizana nini kimetokea, rais anashangaa hali imefikaje hapa na waziri mhusika anaunda tume kuchunguza ili kujua wahusika? Kama huu siyo wazimu wa watu waliosoma ni nini hiki?

DPP muda wote huu yuko wapi? Sheria inampa nguvu ya kuingilia na kuanzisha uchunguzi wa jambo lolote pale panapodaiwa kutokea uhalifu, kwanini DPP wetu amekaa pembeni kusubiri maelekezo ya wanasiasa wakati ana nguvu zote za kufanya uchunguzi na kuleta mashtaka? Jibu ni jepesi.

Tuhuma za wanafunzi waliotelekezwa Ukraine

moja ya vitendo ambavyo vinabakia katika historia kama uonevu mkubwa wa serikali dhidi ya raia wake ni suala la vijana wetu karibu 30 walipotelekezwa kule Ukraine na kuachwa kule kwenye ubaridi wa Jiji la Kiev mbele ya ubalozi wa Uingereza.

Ninatambua ndani ya moyo wangu kabisa kuwa hakuna wakati ambapo ubabe wa watumishi wachache ulivumiliwa na kuzawadiwa dhidi ya vijana wasio na mtetezi kama wakati ule.

Nakumbuka idadi ya wabunge niliowaomba wawasimamie vijana hawa. Wabunge wote wa CCM niliozungumza nao waliogopa kwa sababu ya kuonekana wanapingana na serikali!

Kama nilivyoandika wakati ule, nina shukrani yangu milele kwa wale wote waliojitokeza kusimama na vijana wale kwani kwa mara ya kwanza kikundi cha vijana wasio na lolote waliweza kusimama dhidi ya serikali yao!

Kati ya mambo yote niliyoyafanya na kuyasimamia hakuna jambo linalonigusa moyoni kama ubabe ule wa Serikali ya Rais Kikwete.

Siwezi kusahau jibu la mmoja wa watendaji wakubwa aliyenijibu kuwa yuko mezani anakula wakati vijana wetu wamelala nje ya ubalozi wa Uingereza wakililia kitu kimoja, waachwe waendelee na masomo! Sijasahau lile, na sidhani kama niko tayari kuwasamehe!

Tulionyesha wakati ule na kwa karibu kipindi cha mwaka mzima jinsi gani Bodi ya Mikopo iliwahadaa vijana hawa na kuwachuuza ugenini kwa sababu hawakutaka kuwagawia fedha zao za ada na kushiriki katika ufisadi wa bodi hiyo.

Tukaweka na nyaraka na hoja zikajengwa za kuonyesha jinsi gani bodi hiyo iliyokuwa chini ya wizara iliyoongozwa na Profesa ilivyokuwa inalipiza kisasi kwa vijana hawa na kuwatelekeza ugenini.

Leo, watu wale wale tuliowapigia kelele ati wameamka na kutambua kuna matatizo bodi ya mikopo! Kama huku siyo kulala kwa dereva kwenye usukani tukuiteje huku?

Kwa nini hadi leo DPP hajaagiza uchunguzi wa kufuatilia nini kilitokea au kuwahoji wale vijana waliorudishwa kwa maagizo ya serikali na kwa fedheha ili kujua ni nani alikuwa anahusika na kuona kama kuna mashtaka ya kuletwa mbele ya mahakama kama yakina Mramba na Yona au zaidi? Najua kwanini; jibu ni jepesi;

Tuhuma dhidi ya Rostam

Kati ya Watanzania ambao majina yao yanahusishwa na uvunjaji mkubwa wa sheria nchini ni jina la Mbunge wa Igunga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz.

Huyu anatajwa kwenye mambo mengi na kuhusishwa na baadhi ya kesi ambazo nimezitaja hapo juu. Zaidi ya yote katika suala la Dowans wengi tunafahamu kilichosemwa kwenye Kamati Teule ya Bunge na majibu aliyoyatoa mbele ya waandishi wa habari.

Lakini, tunafahamu maendeleo ya hivi karibuni ambapo mtu anayeonekana kwenye nyaraka za umiliki za BRELA (Suleiman Al-Adawi), anamtaja Rostam kuwa ni rafiki yake na baadhi ya vyombo vya habari vilikiri kuwa Mbunge huyo anamtambua Al-Adawi na kwamba alihusika katika kumshawishi kuleta mitambo ile ya majenereta.

Rostam, alikana kuwajua watu wa Dowans! Leo, ushahidi wote unamhusisha na wengine katika kujaribu kuhakikisha majenereta ya Dowans yanauzwa kwa Tanzania kwa fedha zilizotengwa tangu kwenye bajeti ya mwaka jana (Angalia Mpango wa Maendeleo wa 2008/2009).

Tulipopinga kwa sauti kali ununuzi wa mitambo ya Dowans nguvu kubwa ilitumika kujaribu kutushawishi hadi tulipowalazimisha kusalimu amri.

Hata hivyo kitu ambacho hakijaangaliwa hadi leo ni jinsi gani kampuni ya Dowans Tanzania LTD ilianzishwa kwa makusudi huko Costa Rica ili hatimaye ipate nafasi ya kujiingiza nchini.

Uchunguzi huru (ambao nimeuratibu mwenyewe) umeonyesha pasipo shaka kuwa kampuni ya Portek International, ambayo ilitajwa na Salva (wakati akiwa Habari News) kuwa ina hisa kwenye kampuni ya Dowans Tanzania haina hisa hizo! Kampuni hiyo inatajwa kwenye nyaraka za BRELA!

Kampuni ya Dowans ya Costa Rica, ilianzishwa kwenye eneo huru la biashara (Free Trade Zone) haina ofisi, haina jengo na anuani inayotajwa kwenye nyaraka za BRELA ni anuani ya hilo eneo huru!

Hata ile Dowans Holdings ambayo tuliambiwa ni ya huko Falme za Kiarabu nayo anuani yake hadi simu ni za Benki ya Canadian Royal Bank! Uchunguzi wa huko nao unaonyesha hakuna kampuni iliyoandikishwa huko.

Katika maeneo yote hayo, Rostam anahusishwa kwa namna moja au nyingine! Kwanini DPP hadi hivi sasa hajaamua kuanzisha uchunguzi huru wa Dowans na wahusika wake?

Kwanini DPP baada ya taarifa ya Bunge hakuanzisha uchunguzi dhidi ya Rostam? Kama uchunguzi huru ungefanywa na kuhakikisha haya tunayoyasema kuwa yana ukweli au uongo au ni uzushi au ni "chuki binafsi" au ni "ubaguzi" si Rostam angeondolewa hili wingu la ufisadi ambalo linamzunguka?

Ninafahamu jibu lao la kitabuni "kama mna ushahidi uwasilisheni kwa vyombo husika"! Jibu hili halina msingi kwangu kwa sababu hata tukiwawekea ushahidi hadi kwenye meza zao hawawezi kufanya lolote?

Kwani suala la DECI lilikuwaje? Watu wa usalama wa taifa waliliandikia hili kabla hata ya watu wa Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana hawajaandika ile taarifa yao kwa DCI.

Maofisa wetu wa mitaani wa Usalama wa Taifa waliandika taarifa mapema na kutoa mapendekezo yao lakini hatua hazikuchuliwa! Tena wao waliandika kuanzia 2007!

Sasa, wanataka tuwatafutie ushahidi, tuwaletee, tuwafafanulie na bado tutoe mapendekezo wakati wote huo wao wanafanya nini? Kula bila kulipa? DPP yuko wapi? Jibu ni jepesi!

Si lazima mashtaka yote yaendeshwe na ofisi yake. Wengine wanaweza kujibu na kusema mambo haya yote unayaleta dhidi ya DPP mbona ni mengi hivyo? Kwamba, hawezi kufanya kazi hizo zote na kuendesha mashtaka yoyote yeye mwenyewe kwani ni mengi na mazito. Watetezi hao wanaweza kusema kuwa DPP ana majukumu mengi na kesi nyingi za kufuatilia.

Jibu langu ni kuwa sheria iliyounda ofisi yake inatambua hilo. Ni kwa sababu hiyo sheria hiyo inasema hivi (nitainukuu) "The Director may appoint a person to be a Public Prosecutor from other departments of the Government, Local Government authority or private practice to prosecute a specified case or cases on his behalf".

Yaani, Mkurugenzi anaweza kumteua mtu yeyote kutoka idara ya serikali kuu, serikali za mitaa au hata sekta binafsi kuendesha mashtaka ya kesi mbalimbali kwa niaba yake.

Nguvu hii ni ya ajabu na DPP wetu hajaitumia ipasavyo. Leo hii tuna wanasheria wengi ambao wanaweza kutimiza masharti ya kisheria ya kuwa PP. Wapo kwenye vyuo vikuu, kwenye mashirika mbalimbali na idara mbalimbali.

Na kama akitaka msaada wa kuwatambua ni wazi anaweza kuwasiliana na Chama cha Wanasheria au Mahakama Kuu ambao wamesajiliwa.

Yaani, katika kuendesha mashtaka DPP halazimiki kutegemea waendesha mashtaka wa serikali tu (chini ya ofisi yake) au wa Polisi bali anaweza kuwaomba hata kina Issa Shivji au watu wengine ambao wanaweza kuendesha mashtaka.

Hii ina maana gani?

Ina maana ya kwamba kwa vile tayari ana uwezo wa kuagiza chombo kufanya uchunguzi basi anaweza pia baada ya uchunguzi huo kuteua mtu au jopo la watu kuwa waendesha mashtaka kwa niaba yake na watu hao si lazima wawe watumishi serikalini.

Ninaamini, wanasheria wetu wanaweza kujitokeza au vyama vya sheria vya makundi mbalinbali vinaweza kujitokeza na kumtaarifu kuwa wanao watumishi ambao wako tayari kuendesha mashtaka kwa niaba ya DPP wakiteuliwa hata kama kwa kujitolea (pro bono) au kwa malipo ya mkataba. Wakifanya hivi tutaona kama DPP atawakatalia au atasema hana waendesha mashtaka wa kutosha.

Akiamua kufanya hivi ina maana kesi mbalimbali na hasa hizi zinazohusiana na ufisadi zinaweza kuendeshwa kwa haraka na kundi la watu waliobobea katika kazi yao na hivyo kuhakikisha kuwa karibu ya 2010 kesi hizi za ufisadi zote zinakuwa zimemalizwa na Taifa lizungumzie ajenda mpya ya uchaguzi. Lakini siamini DPP wetu atafanya hivyo. Kwanini; kwa sababu jibu ni jepesi.

Jibu Jepesi

Ndiyo! Jibu ni jepesi. DPP wetu hana uwezo wa kusimamia utawala wa sheria nchini na kuhakikisha mashtaka yanayostahili na yanayotakiwa yanaletwa dhidi ya mtu yeyote, chombo chochote na wakati wowote ule.

DPP wetu ni mwoga; anaogopa kuwaletea watu kashkash, anaogopa kuwaudhi wale waliomsaidia kufika alipofika. DPP wetu hana uthubutu wa kufanya kazi yake kwa kuangalia sheria na kwa kutumia nguvu alizopewa na Bunge limempa. Hawezi kuthubutu.
Asante Pascal. Wewe ni noma, kwa lugha ya mtaa ni.
 
Back
Top Bottom