‪DPP atumie madaraka yake kisheria ipasavyo, asisubiri maelekezo ya wanasiasa ili afanye kazi‬

Appointing authority matters kama kweli tunataka mabadiliko na siyo business as usual.
Ndo ukweli wa kinachotendeka.
Ideal situation ( kutenda kufuatana na viapo na matakwa/matarajio ya kazi) na hali halisi kwa maana kinachotendeka katika uhalisia wake NI VITU VIWILI TOFAUTI.( DE FACTO AND DE JURE)
Kwani watu wanapoapa "nitafanya kadha kadha kadha.." does it really follow kuwa ni kweli wanatenda kama walivyoapa.
( this is my observation. Wengine mnaweza kuwa na mawazo /maoni tofauti)

Ulichosema hapa kina ukweli zaidi kuliko kauli yako ya awali. Kile kinachotendeka siyo sawa na kile kinachopaswa. Tunafahamu kuna watu wasiofuata sheria ya manunuzi serikalini (huo ni ukweli). Je watu wasifuate sheria ya manunuzi kwa sababu status quo ni kuwa haifuatwi?

Kauli yako ya awali ilisema hivi:

Kuteuliwa na Rais ina maana kutenda kadri ya matakwa na utashi wa aliyemteua.


This statement claimed to interpret what it means to be appointed by the President. Sasa, hili si kweli. Kuteuliwa na Rais haina maana ya kutenda kwa kadri ya matakwa na utashi (regardless of the law that one has been appointed to enforce or the position to which he/she has appointed into).

Sasa, kusema kuwa kauli yako haina ukweli haina maana ya tofauti ya maoni kwani huwezi kuwa na tofauti ya maoni katika ukweli. Truth is singular, intrinsic and self evident.
 
Hivi kweli MKJJ unataka kutuambia kuwa JK angependa hao jamaa washtakiwe lakini kikwazo ni DPP? Naombea niwe sikukuelewa.

Naam, uwezo wa kumfukuza hana. Lakini nani mwenye uwezo wa kumpandisha cheo? Au kumteua kwenye vijitume vya ulaji? Au kumhamisha kikazi? Kwa mfano, kumpa kaubalozi! Bajeti ya idara yake inapitishwa na nani? Tofauti na unavyosema, DPP akienda kinyume na matakwa ya Rais, Rais anaweza kufanya utendaji kazi wake ukawa mgumu hadi akaipata!

Amandla...........
 
Hivi kweli MKJJ unataka kutuambia kuwa JK angependa hao jamaa washtakiwe lakini kikwazo ni DPP? Naombea niwe sikukuelewa.


Haijalishi kama JK angependa au asingependa, DPP hatakiwi kuangalia mapenzi ya Rais.. anatakiwa kuangalia sheria. Sijui mapenzi ya Rais yanaingia vipi hapa.

Naam, uwezo wa kumfukuza hana. Lakini nani mwenye uwezo wa kumpandisha cheo? Au kumteua kwenye vijitume vya ulaji? Au kumhamisha kikazi? Kwa mfano, kumpa kaubalozi! Bajeti ya idara yake inapitishwa na nani?

DPP mbovu ndiye anafikra za namna hiyo. Maana ukifikiria hivyo utaona kuwa hakuna mtumisho yoyote anapeswa kutekeleza wajibu wake kwa kuhofia kuharibu the possibility of advancement au "kukumbukwa" huko mbeleni.


Tofauti na unavyosema, DPP akienda kinyume na matakwa ya Rais, Rais anaweza kufanya utendaji kazi wake ukawa mgumu hadi akaipata!

hawezi isipokuwa kwenye taifa la watu wanaofikiri Rais anaweza kufanya hivyo. It is the law and the law only.. it icalled the dictatorship of the law. Vinginevyo, sheria haina maana kabisa.

Tutarudi kule kule, Rais hana uwezo na nguvu za kufanya kitu nje ya zile ambazo tumempa kisheria. Hawezi kukurupuka na kumuambia polisi "mpige risasi huyu" halafu yule polisi akatekeleza agizo hilo! Hawezi kusema "chota bilioni 1 moja hapa na weka kwenye akaunti yangu" halafu mtu akatekelza.

Mtu yeyote anayetekeleza matakwa au nia hiyo ya Rais anavunja sheria kama Rais mwenyewe!
 
Ulichosema hapa kina ukweli zaidi kuliko kauli yako ya awali. Kile kinachotendeka siyo sawa na kile kinachopaswa. Tunafahamu kuna watu wasiofuata sheria ya manunuzi serikalini (huo ni ukweli). Je watu wasifuate sheria ya manunuzi kwa sababu status quo ni kuwa haifuatwi?

Kauli yako ya awali ilisema hivi:




This statement claimed to interpret what it means to be appointed by the President. Sasa, hili si kweli. Kuteuliwa na Rais haina maana ya kutenda kwa kadri ya matakwa na utashi (regardless of the law that one has been appointed to enforce or the position to which he/she has appointed into).

Sasa, kusema kuwa kauli yako haina ukweli haina maana ya tofauti ya maoni kwani huwezi kuwa na tofauti ya maoni katika ukweli. Truth is singular, intrinsic and self evident.
Mkuu,
Hakuna kilichobadilika - what I said earlier ndio hicho hicho said differently.
Pia, kama mtu anajua kabisa sheria inasema afanye x,y,z kama DPP,na bado akawa hafanyi vile, unataka kusema interpretation ni nini? na je kuna interpretation moja tu? One of them could be what i said.

I think hapa tunachangia hoja na siyo kulumbana au kujibishana.Kwa msingi huo sidhani ni vema tukawa na one-on -one - kuwa nikichangia then uniandame kwa maswali au kutafuta wapi nimesema nini.Kila mtu nadhani ana haki ya kutoa mawazo yake.Vinginevyo ni kama kufanya wengine waogope kusema kitu kwa kuchelea kuwa cross-examined.
Samahani lakini thats how I feel.
 
Last edited:
Hivi kweli MKJJ unataka kutuambia kuwa JK angependa hao jamaa washtakiwe lakini kikwazo ni DPP? Naombea niwe sikukuelewa.

Naam, uwezo wa kumfukuza hana. Lakini nani mwenye uwezo wa kumpandisha cheo? Au kumteua kwenye vijitume vya ulaji? Au kumhamisha kikazi? Kwa mfano, kumpa kaubalozi! Bajeti ya idara yake inapitishwa na nani? Tofauti na unavyosema, DPP akienda kinyume na matakwa ya Rais, Rais anaweza kufanya utendaji kazi wake ukawa mgumu hadi akaipata!

Amandla...........

Mkuu FM heshma yako Mkuu, mimi ninakuelewa vizuri sana pia ninamuelewa Mkuu Mwanakijiji vizuri sana. Wote mpo sahihi kwa falsafa tofauti. Mwanakijiji analenga uwajibikaji wa kisheria wa DPP. DPP hapaswi kumuuliza Rais juu ya nani wa kumshtaki na nani wa kumuacha. Ameapa kutekeleza wajibu wake bila kupendelea wala kuogopa. So, no excuse kwamba anamuogopa Rais kwasababu maisha yake yatakuwa si manono kwa kuwapeleka mbele ya sheria maswahiba wa Rais.

Tatizo la kuangalia upepo wa kisiasa ndilo linalotupotosha siku zote. I said sometimes kuwa tunavyozidi kuwatukuza wanasiasa ndo tunavyo haribu nchi, ni wakati sasa wa kuwawajibisha watendaji na kuwatukuza wanapofanya vizuri.

On the other side, kama JK angekuwa makini, angekwishamshangaa DPP kwa nini hachukui sheria. I mean JK angekuwa jemedari wa vita dhidi ya ufisadi angesha agiza hatua zichukuliwe. Hata hivyo tunajua kuwa JK hawezi kufanya hilo kwasababu wale ni maswahiba. On point of law, hatuwezi kumbana JK juu ya hili la kutoshtakiwa kwa hawa jamaa. Ila tunaweza kumbana DPP.
 
On the other side, kama JK angekuwa makini, angekwishamshangaa DPP kwa nini hachukui sheria. I mean JK angekuwa jemedari wa vita dhidi ya ufisadi angesha agiza hatua zichukuliwe. Hata hivyo tunajua kuwa JK hawezi kufanya hilo kwasababu wale ni maswahiba. On point of law, hatuwezi kumbana JK juu ya hili la kutoshtakiwa kwa hawa jamaa. Ila tunaweza kumbana DPP.

Nadhani tatizo umelianisha hapo mwanzo kabisa.
Tunaweza vipi sasa kumbana DPP Mkuu?
Kumbuka kwenye sakata la EPA DPP amesakamwa sana, kuulizwa maswali na hata watu kujaribu hata kumlazimisha kuwashtaki wahusika wote.Kwani aliyemteua naye hakuwa anaona au kusikia? Ni nini sasa kinampa confidence huyo DPP asichukue hatua tunazotarajia?
 
ha ha ha hii imeshakuwa kali, real i am just realizing that DPP hatuwezi kumbana, na tunapohamisha mjadala kwa JK basi ndo anapumua na kujiandaa kupata kura za bure 2010 LOL! Ni kweli kwamba DPP hatuwezi kumbana zaidi ya kupiga kelele tu. sasa tukubali yaishe?

Lets go back to Mwembeyanga, hivi Dr. Slaa alisoma ile list of shame ili kiwe nini? (nini yalikuwamatarajio ya Dr. Slaa? na wenzake?) Maybe we will find a right track.
 
Hizi kelele peke yake zinatosha? ile hotuba ya Slaa ndo iliishia vile? i mean what next?

Tatizo ni systemic - kelele zinasaidia kuonyesha kuwa watu wanaelewa nini kinaendelea, kwamba watu hawakubaliani na hali na wanataka mabadiliko.Mabadiliko hayatakuja ghafla kama mvua kwa maana tunahitaji overhaul ya systems - DPP ni taasis na siyo mtu.Taasis hiI inategemeana na nyingine kufanikisha kazi zake. Ni majuzi tu imefanyiwa marekebisho makubwa na badala ya kuwa more efficient tunaona bado kuna matatizo ya hapa na pale.

Halafu hata tunapomlaumu DPP kwenye hili LA ufisadi tusisahau pia uwezo mkubwa aliopewa kama utatumika visivyo bado tutalalamika kuwa ana powers mno...( fikiria uwezo wake kwenye entering Nolle prosequi na hahitaji kutoa sababu yeyote na ni eneo lililoleta manung'uniko sana).
 
- DPP anateuliwa kutumikia sheria za jamhuri, sio kumutumikia rais au matakwa ya rais hiyo ni dhana potofu na ndioyo imetufanya tuwe hapa tulipo as a nation,

- Mrema alipokuwa waziri wa ndani aliwafanya hata wakuu wake wa kazi kuonekana vilaza, ni kwa sababu alikuwa akitumikia sheria za jamhuri, wananchi tulimkubali ikabidi hata wakuu wake wa kazi wamkubali ingawa kwa shingo upande, na huku wakitafuta nafasi ya kumtosa.

- Sasa DPP wakweli akifuata sheria za jamhuri inavyotakiwa, hatakuwa na wasi wasi wa kuogopa rais kwa sababu hata rais atarukia treni lake linalokubalika na wananchi, Wa-Tanzania tumezoea nidhamu za uoga uoga na kuogopa kutengwa na jamii,

Hawa kina DPP uchwara ni victims wa system yetu mbovu, inayomlinda rais tu badala ya sheria za jamhuri, rais wetu ana power ya ajabu kama King George, sasa unategemea nini kama hawezi kumfukuza kazi huyu DPP basi atamhamishia Mtwara, au kumfanya kama alivyomfanyia DPP kabla ya huyu wa sasa, yaani kuwa balozi wetu Zimbabwe!

Wakulaumiwa hapa ni legal na political system yetu mbovu sana, sometimes inaudhii mpaka unajiuliza ilijengwa na nani?

Ahsante.

William.
 
Tutarudi kule kule, Rais hana uwezo na nguvu za kufanya kitu nje ya zile ambazo tumempa kisheria. Hawezi kukurupuka na kumuambia polisi "mpige risasi huyu" halafu yule polisi akatekeleza agizo hilo! Hawezi kusema "chota bilioni 1 moja hapa na weka kwenye akaunti yangu" halafu mtu akatekelza.

Mtu yeyote anayetekeleza matakwa au nia hiyo ya Rais anavunja sheria kama Rais mwenyewe!

Kwa hiyo, Mkuu, nguvu ya Rais ni ipi? Kuteua tu watendaji na kuwaachia wafanye watakavyo? Kama ulivyoulizwa, kama Rais hana nguvu ya kumsukuma DPP kufanya jambo sisi wananchi tuna uwezo gani? Mimi nilidhani nguvu yetu ipo kwenye kum-pressurize huyo tuliyempa nafasi ili nae amsukume huyo aliyemteua! Mifano yako ni off-point. Rais hawezi kuagiza kitu ambacho ni blatantly criminal.

Kudai kuwa Rais hana nguvu ya ushwaishi juu ya wale aliowateua ni kuwa disingenous. Hata Marekani, that bastion of democracy, hiyo si kweli. Tumemshuhudia Albert Gonzales. Tumewashuhudia mawakili wakitoa justification kwa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria. Sheria ni interpretation. Na si wote tuna-interpret sawasawa.

Kutuambia kuwa tuache kumwandama mtu ambae tuna uwezo wa kumshughulikia na kutuambia tumbane huyu ambae unatuambia kuwa hakuna mwenye mamlaka juu yake ni kutotutendea haki. Kwa kifupi, Rais hawezi kuepuka lawama kutokana na vitendo au mapungufu ya wale aliowateua. Hata kama lawama ni kwa ajili ya kuteua mtu asiyefaa tu.

Amandla.......
 

...rais wetu ana power ya ajabu kama King George, sasa unategemea nini kama hawezi kumfukuza kazi huyu DPP basi atamhamishia Mtwara, au kumfanya kama alivyomfanyia DPP kabla ya huyu wa sasa, yaani kuwa balozi wetu Zimbabwe!

Nadhani hata hilo la kumhamishia ubalozini hawezi. Rais yuko stuck na DPP aliyemteua. Akiteua ameteua.
 
-
Hawa kina DPP uchwara ni victims sasa unategemea nini kama hawezi kumfukuza kazi huyu DPP basi atamhamishia Mtwara, au kumfanya kama alivyomfanyia DPP kabla ya huyu wa sasa, yaani kuwa balozi wetu Zimbabwe!

Wakulaumiwa hapa ni legal na political system yetu mbovu sana, sometimes inaudhii mpaka unajiuliza ilijengwa na nani?

Ahsante.

William.

Sahihisho: Aliyepelekwa ubalozini Zimbabwe siyo former DPP ni former DCI.
 
Ni kweli " wewe na mimi" hatuwezi kumbana DPP.Sana sana tutapiga kelele na kumlalamikia kuwa ana powers lakini hazitumii.
Sio tuu mimi na wewe hatuwezi kumbana DPP, bali hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumbana, hata rais hawezi!.
Mzee MMKJJ, yote uliyosema kuhusu DPP ni kweli, lakini pia kwa mujibu ya sheria iliyounda ofisi ya DPP, havunji sheria yoyote kwa kutofanya uchunguzi wowote kwa vile hayo ndio mamlaka yake ambayo kisheria, anayatumia at his discretion as he pleases at his pleasure na sheria inamlinda.
Kwa maoni yangu, tatizo sio DPP, tatizo ni mamlaka ya ajabu yaliyochini ya DPP.
Niliwahi kuchangia mahali nikaainisha sheria yetu iliyounda ofisi ya DPP, amepewa mamlaka makubwa yac ajabu, na hayo aliyoyaainisha MMKJJ ni dibaji tuu, nguvu haswa za DPP ni pamoja na 'power to declare nolle proseque' yaani hakuna kesi ya kujibu. DPP huyu anauwezo wa kuingilia kesi yoyote ya jinai, ikiwa mahakama yoyote na ikiwa katika hatua yoyote kabla ya hukumu, kuisimamisha, kingilia, ama kuifuta bila kulazimika kutoa sababu zozote wala maelezo yoyote.
Sheria ya DPP inamtaka kutimiza wajibu wake bila shinikizo lolote kutoka popote na hata akiletewa kesi yoyote ni discretion yake aprosecute ama asiprosecute na hakuna chombo chochote ndani ya JMT chenye mamlaka ya kumuuliza lolote DPP, hata rais hana mamlaka hayo, sembuse MMKJJ?.

Naungana na WoS sisi mwisho wetu ni kupiga tuu kelele, japo za mlango, siku moja moja mwenye nyumba atakosa usingizi kwa sababu nyingine na atazisikia hizi kelele za mlango na ama ataamka na kuubana mlango, ama atautia kizuizi ili usiendelee kupiga kelele.

Enzi za Mwalimu kulikuwa na sheria ya 'Presidential Preventive Detention Orders' iliyompa rais mamlaka ya kumuweka mtu yoyote kizuizini kwa kipindi chochote bila kutoa sababu yoyote. Mwalimu Nyerere aliitumia kipindi chote cha utawala wake. Kipindi cha Mwinyi, wanasheria wa chuo kikuu wakiongozwa na Shivji na Mgongo Fimbo, waliichalenge sheria hii kwa 'court review' na mahakama ikatamka its a bad law, hivyo ikamlazimisha rais, kila akisaini 'preventive detention order' lazima atoe sababu. kuna detention moja ya Mwinyi ilipigwa chini na mtuhumiwa kuachiwa huru.

Kama wanasheria wetu, waliweza kufanya hivi dhidi ya mamlaka ya rais, wanashindwa nini kwenye mamlaka ya DPP?.
Kwa mawazo yangu, 'Tatizo sio Feleshi as DPP, ni mamlaka yake makubwa mno anayatumia atakavyo bila kuvunja sheria. Tazizo ni the institutional of the DPP.
 
Pasco.. na wengine.. ninachosema ni kuwa DPP amekuwa kimya kwa sababu the pressure is not on him. Watu bado wanataka tumbane JK wakati hana uwezo wala nguvu ya kisheria ya kuendesha mashtaka au kumshtaki mtu. Nguvu hizo ziko kwa DPP.

Nilikuwa miongoni mwa watu waliopinga kabisa kwa DPP kuwa sehemu ya tume inayoundwa na Rais kuchunguza EPA.. kwangu DPP ndiye alitakiwa aunde tume hiyo au kusimamia uchunguzi huo. Watu walipofurahia kuwa hatimaye tume imeundwa hawakujua wanafurahia nini.

Ndiyo maana nasema hata kule Bungeni, Wabunge wamlilie DPP kwenye Meremeta, Mwananchi, Deep Green na wengine.. kuililia "serikalii" tu haitoshi.

We have to put the pressure where it matters! Kusema JK JK JK might be politically popular lakini kiukweli ni kuwa kwenye uwanja wa sheria ni DPP ndiye tunatakiwa kumbana. Kwanini?

a. Kwa sababu ndiye mwenye wajibu wote wa kisheria kwenye mambo ya mashtaka
b. Rais au mtu mwingine yoyote hawezi kumtimua au kuingilia uchunguzi wake.
c. Ana uwezo wa kuteua mtu mwingine kuendesha uchunguzi kwa niaba yake hata Mwanasheria binafsi!

So, kisiasa tunaweza kufanya sawa kupiga kelele kwa Rais lakini itabakia kuwa ni siasa tu; tukitaka kweli sheria ifuate mkondo wa kumbana ni DPP.
 
Tatizo ni systemic -

Halafu hata tunapomlaumu DPP kwenye hili LA ufisadi tusisahau pia uwezo mkubwa aliopewa kama utatumika visivyo bado tutalalamika kuwa ana powers mno...( fikiria uwezo wake kwenye entering Nolle prosequi na hahitaji kutoa sababu yeyote na ni eneo lililoleta manung'uniko sana).
Asante WoS kwa hili la nolle prosequi. Ni mamlaka kubwa ya ajabu, haswa sheria inapotamka hawajibiki kutoa sababu yoyote!.
Mwingine mwenye mamlaka ya kutenda lolote bila kutoa sababu zozote ni rais pekee kwenye mamlaka ya uteuzi, ama excecutive powers za utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.
Wako watendaji wengi serikalini wenye independent powers akiwemo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, kumbe ili Ripoti ya Ukaguzi, anaikabidhi kwanza kwa rais, rais akishaiona (kutoa go ahead) ndipo anaikabidhi bungeni na kufanywa public.
Ni DPP tuu na rais ndio wenye absolute independeence na powers ambazo hawajibiki kwa yoyote na maamuzi yao ndiyo ya mwisho.
Hakuna mtendaji mwingine yoyote serikalini ambaye hawajibiki popote zaidi ya rais na DPP.
The Judiciary yetu chini ya Jaji Mkuu, haina absolute independence, ana uamuzi wa mwisho kwenye baadhi ya masuala, lakini uamuzi huo unaweza kuwa challenged kwenye court review, na mahakama ikitoa capital punishment, haitekelezwi mpaka rais asaini.
Hata the Legistlature yetu, Bunge na Spika ana ukomo wa madaraka kwa sheria yoyote inayopitishwa na bunge, haiwi sheria mpaka rais accent. Pia rais kama sehemu ya Bunge, ana mamlaka ya kulivunja bunge.
 
Back
Top Bottom