DPP: Ushahidi Kagoda unakaribishwa

Miaka si mingi iliyopita tulikuwa tunashangaa na wengine kuwacheka babu zetu jinsi walivyoendeshwa na wakoloni. Sasa leo hii sii na midigrii yote hiyo, vyombo vya habari, exposure etc. Kwa utaratibu huu Historia itakuja kutuhukumu bila huruma na tutachekwa kupita mno and this is just within the coming ten years!
 
Miaka si mingi iliyopita tulikuwa tunashangaa na wengine kuwacheka babu zetu jinsi walivyoendeshwa na wakoloni. Sasa leo hii sii na midigrii yote hiyo, vyombo vya habari, exposure etc. Kwa utaratibu huu Historia itakuja kutuhukumu bila huruma na tutachekwa kupita mno and this is just within the coming ten years!

Wakoloni walikuwa na vibaraka na mbwa wao wa kuwalinda, vivyo hivyo siku hizi mafisadi wana vibaraka na mbwa wao!
Vibaraka na mbwa hao ni hatari kuliko hata mafisadi wenyewe kwa mafisadi wanawategemea hao.
Kwa bahati mbaya sana, mara nyingi wananchi wanategemea vibraka na mbwa wa mafisadi kuwasaidia katika vita dhidi ya ufisadi.
Ili kushinda vita dhidi ya ufisadi, mapambano yanatakiwa yaelekezwe kwanza kwa vibaraka na mbwa wa mafisadi ambao ndio wanaowalinda mafisadi na baada ya kuwamaliza itakuwa rahisi kuwashughlikia mafisadi.
 
yani MH. RAIS ROSTAM AZIZ kajipanga wee and dealt with all trails that implicate him for those 4 years and then he was like ''DPP, now let the CIRCUS begin''
 
Enough said

Pelekeni ushahidi acheni kulalamika kama wenzenu walivyobumbulua mambo ya watergate.
 
Tukuletee ushahidi,huo mshahara wako tutagawana?..ninyi leteni ujanjaujanja,ila yana mwisho haya,.wapi Mubaraka,Mobutu n.k
 
Ni bora kukaa kimya watu wakakudhania kuwa u mpumbav kuliko kuongea watu wakathibitisha kuwa u mpumbavu, DPP ni taasisi ya mashtaka nt investigatory organ, nlikuwa napita tu anyway.

Mbuki Feleshi, umeisema vizuri na katika hili Eleizer Feleshi kwa kufungua mdomo wake amethibitisha 'upumbavu' wake. Bora angekaa kimya.



Mwanyika, Mwema na Hosea walivyotayarisha report yao na kumkabidhi Rais, walitumia ushahidi gani? Na Rais alivyowapongeza kwa kazi nzuri waliyofanya na kuweza kuwabana wezi wa EPA wakarudisha Shs 53 Bilioni (kati ya Shs 133 Bilioni zilizoibiwa), walitumia ushahidi gani?

Na Quality Group (Manji) alivyofungua kesi ya madai dhidi ya Kagoda (Rostam), alitumia ushahidi gani?

Sasa kwa nini huyu Feleshi leo aseme "leteni" ushahidi, au anataka ushahidi gani? Makoye matale!!!!!
 
Hapa ndipo maneno ya zamani kama "Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, tumedhalilishwa kiasi cha kutosha, tumeonewa kiasi cha kutosha, tumedharauliwa kiasi cha kutosha" yanapokuwa na maana sana.

Haikubaliki DPP kusema anataka taarifa kutoka kwa watu wasio na uwezo kwa kupata taarifa hizo kisheria. Benki Kuu na CRDB zina wafanyakazi na sheria zinazitaka ziwe na kumbukumbu ya financial transactions ZOTE!!! Ananiomba mtu kama mimi anategemea naweza kupata kumbukumbu hizo kutoka vyombo hivyo vya fedha???

Namuuliza DPP, je amefungua kesi yoyote kuishitaki KAGODA??? Au anaizungumzia tu?? Nadhani akifungua kesi kuna uwezekano wa kupata taarifa kwa watu watakaojitoa muhanga na kuanika mambo haya. Ingekuwa busara kukaa kimya kuliko kuleta jambo hili katika hadhara ya watu wenye ufahamu mkubwa.

Disappointed!!!
 
Yaani nimekasirikaaaa hadi unajiuliza hawa watu hata kufanya maigizo ya kwenye movie hawawezi? Anataka tumpatie vipengele vya sheria vinavyompa yeye madaraka ya kufanya kazi ya Mwerndesha Mashtaka Mkuu wa Taifa hili? gademu!! Halafu utasikia keshokutwa "Rais amwagia sifa DPP"!!!

Inakatisha tamaa lakini 'time will tell' tena hatuta tafuta mwenye kagoda bali wote walioilinda kwamaana kwamba muda ukifika viongozi wote waliochangia kutumaliza watalipa kwa kuwajibishwa na umma
 
Huu sasa ni uhuni - DPP acha ujinga na ubabaishaji. Kwa taarifa yako huko mahakamani kuna kesi iliwahi kufunguliwa na mtu anayejiita Yusufu Manji akidai ni yeye aliidhamini Kagoda kuchota hela Benki Kuu, je ulifuatilia ? Katika kukusaidia hebu soma hapa;
Taarifa zinasema Manji, kupitia kampuni yake – Quality Finance Corporation Limited (QFCL) – ambayo anamiliki na baba yake, Mehboob Manji, “anakabwa koo na serikali” ili arudishe dola za Marekani 28 milioni (Sh. 31 bilioni) zikiwa sehemu ya fedha zote zilizoibwa na Kagoda.

Nyaraka zilizopo zinaonyesha kuwa Manji na kampuni yake walikopa kiasi hicho cha fedha kutoka kampuni ya Kagoda chini ya mkataba wao wa tarehe 12 Septemba 2005.

Kampuni ya Kagoda ilikwapua jumla ya dola za Kimarekani 30,732,658.82 (Sh. 40 bilioni) katika Akanuti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya BoT. Fedha hizi na nyingine zipatazo Sh. 73 zilichotwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Manji anadaiwa chini ya kinachoitwa urejeshaji kiasi fulani cha madeni ya EPA kwa mpango wa Rais Jakaya Kikwete wa msamaha kwa wezi au washirika wao watakaokubali kurejesha sehemu ya fedha zilizoibwa.

Barua ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika, Kumb. Na. JC/B.20/29/16 ya 20 Mei 2008 iliyotumwa kwa Manji, inamtaka Manji alipe fedha hizo katika kipindi alichokubaliana katika mkataba wake na serikali.


Mwanyika alikuwa akijibu ombi la Manji la 28 Agosti 2008 la kutaka kusogeza mbele muda wa kurejesha mabilioni hayo kadri ya makubaliano.

Manji alikuwa akimkumbusha Mwanyika kuwa makampuni yake yalitoa dhamana ya mali isiyohamishika na vilevile kutoa hundi nane zenye tarehe za mbele.

“Bahati mbaya tumeshindwa kufanya malipo ambayo yalikuwa yafanywe tarehe 1 na 15 Aprili 2008 kutokana na upatikanaji kwa viwango vidogo wa fedha za kukulipa…Tunaona pia kuwa hatutaweza kukamilisha wajibu wetu hata kwa tarehe 1 Mei 2008,” anaandika Manji.

Katika barua hiyo, Manji anaomba kusogeza mbele muda wa kulipa na kwamba warejeshewe hundi zao ili waweke tarehe mpya. Kagoda inaeleza katika mkataba wake na Manji kuwa mkopo huo ulipaswa kulipwa katika muda wa miaka mitatu (3), kwa riba ya asilimia 11 kwa mwaka. Haijafahamika Kagoda walipata wapi mamlaka ya kukopesha fedha iliyodaiwa kukusanywa kutoka kwa wadai wa serikali wa nje ya nchi.

Manji na baba yake Mehboob, ndio wanaonyeshwa kuwa walisaini mkataba huo kwa niaba ya QFCL, huku waliosaini kwa niaba ya Kagoda, wakitajwa kuwa ni Francis William na John Kyomuhendo ambaye tangu sakata la Kagoda ametajwa kuwa mfanyakazi wa Rostam Aziz.

Mbali na Manji na baba yake kuwa wakurugenzi wa QFCL, ni haohao ambao pia ni wadhamini binafsi wa mkopo ili kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa.


Lakini kubwa zaidi ni hii inayofuatia;
Taarifa zinaonyesha pia kuwa ni Yusuf Manji aliyedhamini Kagoda kufungua akaunti katika tawi la CRDB Benki la Holland jijini Dar es Salaam ambako mabilioni ya shilingi yalipitia.

Mkataba wa makampuni hayo mawili ulisimamiwa na mwanasheria Nasir Rattansi na mkopo wenyewe ulitakiwa kuwa umemalizwa kulipwa ifikapo 28 Desemba 2008.


Kufumuka kwa taarifa hizi za Kagoda kunaiweka serikali ya Kikwete katika mazingira magumu. Serikali imekuwa ikikana kufahamu wamiliki wa Kagoda na kwa zaidi ya miaka mitano sasa imekaa kimya juu ya wizi wa kampuni hiyo.

Aidha, serikali imekuwa ikijikanyaga kuhusu wizi huu. Aliyekuwa waziri wa fedha, Zakia Meghji aliwaandikia maodita wa kampuni ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini akisema, fedha za Kagoda zilitumika kwa “kazi za usalama wa taifa.”

Katika barua yake ya 15 Septemba 2006, Meghji anasema, “Kama unavyofahamu vema, mamlaka ya serikali huwa na siri, vilevile haja ya kugharamia matumizi ya busara.

“Kwa hiyo... malipo ya dola 30,732,658.82 za Marekani yaliyofanywa na BoT kwa Kagoda Agriculture Limited, yaliidhinishwa na serikali kugharamia matumizi yake nyeti na ilikuwa lazima kuchukua hatua hii ya kudumisha usiri huu.” Hatua hii inaleta maswali mengi kuliko majibu; yakiwa ni pamoja na iwapo Manji na wakwapuaji wa Kagoda ndio hasa wanaitwa “Usalama wa taaifa.”
Na katika kuongezea chumvi kwenye kidonda;
Hata hivyo, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, 12 Septemba 2005, siku ambayo kampuni ya Manji na baba yake wanadai kufunga mkataba wa kukopa mabilioni ya shilingi, Kagoda yenyewe ilikuwa haijasajiliwa.

Cheti cha usajili wa Kagoda Na. 54040 kilichotolewa na ofisi ya Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara na Makampuni (BRELA), kinaonyesha Kagoda ilisajiliwa 29 Septemba 2005, siku 17 baada ya Manji kufunga mkataba na kampuni ya kitapeli.

Watu muhimu katika siri ya Rais Kikwete kuhusu wezi wa fedha za BoT ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP), Said Mwema, Mkurugezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hoseah na Mwanyika, ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Maalum ya rais ya kufuatilia walioiba benki.

Kazi za kamati hii zimebaki siri ya watu hao wanne; hata idadi ya watu waliogundulika, walioahidi kulipa na kiasi watakacholipa imebaki siri yao.

MwanaHALISI lina taarifa, tangu miaka mitatu iliyopita, kuwa mwenye kampuni ya Kagoda au anayejua shughuli zake ni Rostam Aziz.

Wakili Bhyidinka Sanze wa kampuni ya mawakili ya Malegesi – Malegesi Law Chambers – ya Dar es Salaam, katika andishi rasmi kwa Kamati ya rais ya kushughulikia wizi kwenye akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), anakiri kuwa ni yeye alishuhudia “…mikataba ya Kagoda na makampuni mengine ya nje.”

Anasema alishuhudia mkataba wa Kagoda ndani ya ofisi za kampuni ya Caspian Construction Limited ambayo inamilikiwa na Rostam iliyoko Mtaa wa Milambo Na. 50 katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Sanze anasema, “Niliitwa na Bw. Malegesi ofisini kwa Bw. Rostam Aziz…Nilipofika…niliwakuta Bw. Rostam Aziz, Peter Noni (Mkurugenzi Mtendaji wa sasa wa benki ya raslimali) na Bw. Malegesi; wakaniambia fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kugharamia uchaguzi wa CCM na rais wake.”

Andishi la wakili linaeleza kuwa Rostam Aziz, Peter Noni na Bered Malegesi walimthibitishia Sanze kuwa Rostam alikuwa kwenye kikao ambako rais mstaafu Benjamin Mkapa alitoa maelekezo kwa Gavana Ballali kutoa fedha hizo kwa Rostam kwa ajili ya uchaguzi.

Bali taarifa zilizoenea Dar es Salaam zinasema Rostam aliamua “kumuuzia kesi Manji ili kujinusuru na kashfa ya Kagoda.” MwanaHALISI lilipowasiliana na Manji kutaka kufahamu iwapo madai hayo ni kweli alijibu, “Hivi sasa ni vita.” Hata hivyo, Manji hakufafanua vita hivyo vinalenga kuangamiza nani.

Nyaraka zilizo mikononi mwa gazeti hili zinaonyesha risiti kadhaa za serikali zinazodaiwa na wa ndani wake kuwa ndizo zilizotolewa na serikali kuthibitisha Manji kurejesha fedha za Kagoda.

Miongoni mwa risiti hizo ni Na. 31494282 yenye thamani ya Sh. 4.5 bilioni; 31494264 ya Sh. 4.5 bilioni na 31494283 ya Sh. 4.5 bilioni. Bali tarehe za risiti hizo zinagongana na zile ambazo Manji alielekeza katika mawasiliano yake na Mwanyika ya tarehe 28 Aprili 2008.

Juhudi za kuthibitisha uhalali wa risiti hizo na malipo yanayodaiwa kufanyika hazikufanikiwa. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile hakupatikana kwa maelezo ya Katibu Muhtasi wake kuwa alikuwa katika mkutano akijiandaa kwenda bungeni Dodoma.

Baada ya mwandishi kusisitiza ni lazima aonane na Likwelile kwa sababu kuna jambo la dharula, katibu huyo alisema Likwelile hawezi kuwa na muda huo.

“Kwanza umepitia mapokezi? Huwezi tu kuja ofisini kwa mtu kwa vile wewe ni mwandishi na ukapewa nafasi ya kuzungumza naye. Ukitaka labda nikupangie miadi uje siku nyingine,” alisema mwanamama huyo.

Mwandishi aligoma kuondoka kutoka katika ofisi hiyo na ndipo katibu huyo aliposema kuwa bosi wake (Likwelile) ameagiza kama kuna maswali yapelekwe katika ofisi ya uhusiano ya wizara.

Risiti hizo zilipelekwa kwenye ofisi ya uhusiano ambayo nayo ilizipeleka kwenye ofisi inayohusika na hundi zilizolipwa na hazina, lakini majibu hayakuweza kupatikana kwa madai kwamba jambo linalozungumziwa ni la miaka mitatu

Jamaa wote waliotajwa hapo juu hakuna hata moja aliyewajibishwa hadi leo. Feleshi, ni kama unatutukana Watanzania unapodai mwenye ushahidi kuhusu Kagoda akuletee, ili uufanyie nini ? Unataka kuuchakachua huo ushahidi kwa kuwasafisha mabosi wako waliokuteua ambao hawawezi kusafishika hata kama watavua magamba hadi damu ziwatoke ? Ningekuwa wewe, ningejinyamazia kuliko kuonyesha huu ubumbumbu na ukilaza huu wa kutisha, pambafu.

Wizi wa Kagoda - Chama tawala iliwala Watanzania !
1. Msimamizi Mkuu - Benjamin Mkapa, Raisi na Mwenyekiti wa CCM.
2. Mnufaikaji Mkuu - Jakaya Kikwete, mgombea Uraisi kutoka CCM.
3. Mnufaikaji Mkuu Msaidizi - Rostamu Azizi, Mweka Hazina wa CCM.
4. Mnufaikaji Msaidizi - Yusufu Manji, mfadhili wa CCM.
5. Mtekelezaji Mkuu - Zakia Meghji, Waziri wa Fedha.
6. Mtekelezaji Mkuu Msaidizi - Daudi Balali, Gavana Benki Kuu
Listi itaendelea .......................................
 
Huyu jamaa anaongea akiwa nyuma ya kivuli cha mtu mwenye nguvu sana, hasa mwajiri wake. Hawezikani kwa mtu kama yeye kusema upuuzi huu halafu eti mwajiri wake asimchukulie hautua za kinidhamu. Ni lazima mwajiri huyo awe ndiye aliyemtuma jamaa kumwaga upupu huo kwenye mikrofoni.
 
Mwenzenu anaelekezwa jamani,hatumii taaluma yake,yeye na kina Hosea wamefyata mkia kwa sab wanaelekezwa cha kufanya,ndio maana hosea kalalamika kupitia weki leaks
Cha kufanya ni kuweka ofisi,taasisi hizi huru kupitia ktb mpya,wakuu wake wasitokane na rais,vinginevyo hawawezi kufanya kitu kwa sababu wanahofia usalama wao,ni sawa na kumtoa mbwa meno na makucha yote halafu utegemee kutenda kazi,haitawezekana!
 
This mo<^&*$@%)@|\}r is a%@&#*le. Yaani huyu anamwakilisha huyo aliyemteua katika kazi zake. Jamaa pamoja na mamlaka hayo yote aliyonayo anashindwa kwenda pale CRDB na BoT kujua upupu uliofanywa na marafiki wa huyo aliyemteua?!!:A S cry:

Mkiona namna gani vipi, mfungulie Dr. Slaa na CHADEMA kesi kuwa wanaeneza chuki kwa kutoa habari za uongo kuhusu Kagoda. Hapo ndipo utapata ushahidi BUT ndani ya MAHAKAMA. Msitake kuwahadaa watanzania, they know better than that crap.
 
Hivi hawaoni hata aibu mbona sanaa hizi . ............. nisije kupigwa ban

Ndio maana

  • chenge na vijisenti vya jrsey mambo yameisha. "wanachi" hatuna ushaudi

kwani serikali iliyopo madarakani si ya wananchi. feleshi anataka kuseme ameshindwa kuorganise resources alizonazo ukupata ushaidi.


Disgusting
 
Mimi nautafsiri huu wito kama ni mwendelezo wa hila inayofanywa na uongozi mpya wa chama cha magamba wa kutaka kuionyesha jamii kwamba sasa wapo serious wanataka kupambana na ufisadi kumbe ni usanii mtupu! Watanzania lazima tupuuze wito wa kipumbavu namna hii na tuendelea na mapambano yetu kwa namna nyingine. Nawasihi sana viongozi wa chadema waendelee kuhamasisha wananchi kukichukia chama hiki cha magamba ili ifikapo 2015 tukifutilie mbali na uso wa dunia kupitia kwenye masanduku ya kura. Namshangaa sana DPP kwa kukubali kuendesha ofisi kwa maelekezo ya chama. Aibu gani hii isiyo na kifani!!
 
Feleshi, watu wakishindwa kazi tunawafukuzwa. Ondoka ofisini bila kupoteza muda wowote ule. Msitufanye sisi ni wajinga kama nyie. Nani Tanzania anauwezo wa kukusanya ushahidi zaidi ya wewe na vyombo vya usalama? Tanzania inavyombo vingapi vya ulinzi na upelelezi, mnafundishwa nini vyuoni nyie? Hizi njia zakutaka kuwaachia mafisadi nchini kwa kutumia hizi tactics ndizo zitawaweka clean sio? Fanya kazi na kama huwezi muondoke na kumwacha Dr Slaa apendekeze wanaoweza na kufanya kazi za wananchi. I am tired of you guys and real I hope ushetani wenu uwarudi. Ushahidi upo nenda wizara ya madini, treasure, BOT na ofisi ya raisi, wote wanajua wanayoyaficha au muulize makamba alipata wapi pesa ya kumpa mtoto wake January kuweza kufanya kampeni.

Vichwa bure kabisa na iko siku yenu nyie...Hamwangalii international news.
 
Huyu jamaa anaongea akiwa nyuma ya kivuli cha mtu mwenye nguvu sana, hasa mwajiri wake. Hawezikani kwa mtu kama yeye kusema upuuzi huu halafu eti mwajiri wake asimchukulie hautua za kinidhamu. Ni lazima mwajiri huyo awe ndiye aliyemtuma jamaa kumwaga upupu huo kwenye mikrofoni.


That is ezactly, how i also see it......and is no different but the usual pres. RA
 
Back
Top Bottom