VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini,Mheshimiwa Eliezer Feleshi,amewasilisha Kusudio la kukata Rufaa dhidi ya Hukumu iliyomweka huru Prof. Costa V. Mahalu na Bi.Grace Martin. Hii inamaana kuwa Jamhuri itakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi,Ilvin Mgeta pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.
Kama Jamhuri,ikiwa na muda wa kutosha wa kuthibitisha shtaka pale Kisutu,ilishindwa kufanya hivyo,itaweza kuthibitisha Mahakama Kuu? DPP haoni kuwa kama hana ushahidi wa kutosheleza,Rufaa hii itagharimu fedha za walipakodi wa kitanzania bure? Kimsingi,naiona Rufaa ya DPP kama ni butu.Hatahivyo,Mahakama Kuu itatupa jibu kamili siku itakapofika...