DPP amfutia mashtaka ya ufisadi kigogo wa Maliasili

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233



DPP amfutia mashtaka ya ufisadi kigogo wa Maliasili

Na Hellen Mwango, Nipashe

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuachia huru Naibu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Dk. Ismail Kelly Alloo, baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kusema kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki.

Aidha, DPP amemfutia Mkurugenzi huyo mashitakiwa chini ya kifungu namba 91 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kinampa moja kwa moja mamlaka ya kumwondolea mashitaka mtuhumiwa.

Bosi huyo wa Misitu na Nyuki, alifikishwa mahakamani hapo Novemba, mwaka jana ambapo alisomewa mashitaka mawili ikiwemo matumizi mabaya ya ofisi na kutoa taarifa za uongo kuhusu rushwa.

Mashitaka hayo dhidi ya Alloo ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Paul Kimicha.

Mwendesha Mashitaka Kasuni Nkya kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), aliyemsomea mashitaka hayo, alidai kuwa Mei 2, mwaka 2005, mshitakiwa anadaiwa kutenda kosa la matumizi mabaya ya ofisi kwa kuruhusu mauzo ya magogo kinyume cha sheria.

Nkya alidai katika shitaka la pili kuwa Machi 17, mwaka 2005 katika ofisi za makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam, wakati wa uchunguzi wa matumizi mabaya ya rushwa, mshitakiwa alitoa taarifa za uongo kuhusu tangazo la mazao ya misitu mali ya Kampuni ya Aqeel Traders Ltd. Pamoja na kwamba upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa umekamilika, kesi hiyo ilikuwa ikitajwa mahakamani hapo hadi alipofutiwa mashitaka na DPP.





My take: Hivi katika kesi hiyo iliyofutwa, wahusika waliosafirisha magogo kinyume cha sheria walifikishwa mahakamani? Hawajulikani ni akina nani? Jamani, sheria zetu zinakaa vipi? Hii ni moja ya madudu ya utawala wa JK kuhusu kushughulikia mafisadi -- hana ubavu kabisa, anachofanya ni geresha tu.
 
Matumizi ya kifungu 91 CPA yanapaswa kuangaliwa upya, kinaweza kutumika kulinda wahalifu wakubwa au wakati mwingine DPP akitumie kwa maslahi binafsi!
Kama DPP hana nia ya kuendesha kesi dhidi ya mafisadi, wakati jamii ina nia hiyo, nini kifanyike?
DPP anapaswa kutoa sababu za msingi na siyo kusema tu hana nia.
This should be taken as an impurity in the stream of justice!
 
Matumizi ya kifungu 91 CPA yanapaswa kuangaliwa upya, kinaweza kutumika kulinda wahalifu wakubwa au wakati mwingine DPP akitumie kwa maslahi binafsi!
Kama DPP hana nia ya kuendesha kesi dhidi ya mafisadi, wakati jamii ina nia hiyo, nini kifanyike?
DPP anapaswa kutoa sababu za msingi na siyo kusema tu hana nia.
This should be taken as an impurity in the stream of justice!

Zak kwanza za siku kaka,naona kumekunogea huko,kijiweni wanakummis saana,fanya urudi.

Tz hakuna mafisadi bali wanachukua ni zao wenyewe hao,waache wale,halafu tuendelee kuwapigia kura kama kawaida yetu..
 
Back
Top Bottom