DPP amfutia mashtaka ya ufisadi kigogo wa Maliasili

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307





Na Hellen Mwango



17th June 2010












TAkukuru(9).jpg

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuachia huru Naibu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Dk. Ismail Kelly Alloo, baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kusema kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki.
Aidha, DPP amemfutia Mkurugenzi huyo mashitakiwa chini ya kifungu namba 91 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kinampa moja kwa moja mamlaka ya kumwondolea mashitaka mtuhumiwa.
Bosi huyo wa Misitu na Nyuki, alifikishwa mahakamani hapo Novemba, mwaka jana ambapo alisomewa mashitaka mawili ikiwemo matumizi mabaya ya ofisi na kutoa taarifa za uongo kuhusu rushwa.
Mashitaka hayo dhidi ya Alloo ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Paul Kimicha.
Mwendesha Mashitaka Kasuni Nkya kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), aliyemsomea mashitaka hayo, alidai kuwa Mei 2, mwaka 2005, mshitakiwa anadaiwa kutenda kosa la matumizi mabaya ya ofisi kwa kuruhusu mauzo ya magogo kinyume cha sheria.
Nkya alidai katika shitaka la pili kuwa Machi 17, mwaka 2005 katika ofisi za makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam, wakati wa uchunguzi wa matumizi mabaya ya rushwa, mshitakiwa alitoa taarifa za uongo kuhusu tangazo la mazao ya misitu mali ya Kampuni ya Aqeel Traders Ltd. Pamoja na kwamba upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa umekamilika, kesi hiyo ilikuwa ikitajwa mahakamani hapo hadi alipofutiwa mashitaka na DPP.




CHANZO: NIPASHE


0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
 
Hii ndiyo Tanzania yetu, wanaohusika na rushwa kubwa ndio hawana matatizo. Iba mihogo ukale uone. Utakaa rumande hata miaka minane ukisubiri uchunguzi kukamilika.
 
Ukiona hivyo jua yeye alikuwa natumiwa tu, ni lazima alikuwa na backup ya mkubwa fulani....! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!
 
Back
Top Bottom