Elections 2010 DOWUTA yataka mafisadi CCM kung’olewa bila ubaguzi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
DOWUTA yataka mafisadi CCM kung’olewa bila ubaguzi


na Mwandishi wetu


amka2.gif
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA), Abdallah Kibunda, amemshauri Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutekeleza haraka uamuzi wake wa kuwang’oa chamani wote wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi bila kujali nyadhifa zao.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Tanzania Daima kuhusu hatua ya Mwenyekiti wa CCM kueleza dhamira yake ya kukifumua chama hicho kama mkakati wa kukijengea uimara mbele ya safari.
“Nampongeza Kikwete kwa hatua yake ya kutaka kukisafisha chama, kama anataka kukiimarisha chama hicho namshauri achukue haraka hatua hizo madhubuti kukinusuru kwani kimekuwa kikinyooshewa kidole kwa muda mrefu sasa,” alisema Kibunda.
Kwa mujibu wa Kibunda inashangaza kuona kiongozi fisadi akiteuliwa kuingia katika chombo cha maamuzi ya juu kama vile Kamati Kuu ya CCM na kusema kwamba watu hao hawafai hata kidogo kushirikishwa katika maamuzi.
Alishauri chama hicho kuwa na mchanganyiko maalumu wa kuwa na wanachama vijana wa jinsia zote pamoja na wazee wenye hekima.
Pia alishauri chama kurejesha taratibu zake za miaka ya nyuma kuwa na chuo cha kufundishia makada wa chama kwa kuwa wengi waliopo wanafanya kazi kwa maslahi yao binafsi.
Wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya CCM yaliyofanyika Dodoma, Kikwete ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema chama hicho kitafanya mabadiliko makubwa ikiwemo kuwaengua watendaji mzigo na wanaopakana matope.



h.sep3.gif

 
PHP:
"Nampongeza Kikwete kwa hatua yake ya kutaka kukisafisha chama, kama anataka kukiimarisha chama hicho namshauri achukue haraka hatua hizo madhubuti kukinusuru kwani kimekuwa kikinyooshewa kidole kwa muda mrefu sasa," alisema Kibunda.
  Kwa mujibu wa Kibunda inashangaza kuona kiongozi fisadi akiteuliwa kuingia katika chombo cha maamuzi ya juu kama vile Kamati Kuu ya CCM na kusema kwamba watu hao hawafai hata kidogo kushirikishwa katika maamuzi.

Tuwe wazi kwa kutaja wahusika kwa majina ili huyo tunayemshauri aelewe vyema tunalenga wapi na haya mashinikizo...........................it is time to call a spade a spade but not a big spoon......................
 
Back
Top Bottom