Download hapa katiba ya Chama Cha Kijamii (CCK)

Wabongo bwana, yaani tumeshindwa kuvipa nguvu vyama vilivyopo tunang'ang'ania kuanzisha vipya? Demokrasia hailetwi na wingi wa vyama vya siasa bali uimara wa vichache vilivyopo. Utitiri kama huu nauona kama evidence ya UBINAFSI!

Kwa maoni yako, nini ni tofauti ya msingi iliyopo baina ya vyama vyote vikubwa vya upinzani vilivyopo Tanzania (nje ya chama kipya cha CCK)?
 
Kwako Mhusika wa CCK humu Jamiiforums:

Huu ni mwanzo mzuri sana kwa CCK, haswa kitendo cha kuiweka katiba yenu hadharani ili mpate mawazo. Katiba za CCM, CUF, NCCR, CHADEMA, hazikuchukua mawazo ya wananchi. Hakika hii ni dalili kwamba hiki ni chama cha wananchi. Mimi ni mwana ccm lakini naamini katika ushindani wa hoja, sio uadui wa kisiasa, kwani mwisho wa siku, taifa huja kwanza kabla ya vyama. Nina maoni machache kuhusu katiba yenu kama ifuatavyo:

1. Kwanza ni pale mnaposema mnasimamia haki na maslahi ya makundi yafuatayo: wakulima, wafugaji; wafanya kazi wote. Lakini kwenye wajasiriamali mnasema "inapobidi". Hii ni hatari kwa sababu kuu mbili:
Moja – inaweza kutoa tafsiri kwamba nia ya CCK ni kuwaacha wajasiriamali wapambane wenyewe na nguvu za soko, ambalo tumekwishaona huko Mbeya, Mwanza, na hata DSM jinsi gani nguvu hii inawapa tabu wajasiriamali wadogo wadogo, ambao asilimia karibia 70 ni vijana. Na vijana ndio nguzo muhimu ya chama chochote cha siasa Tanzania i.e. asilimia 70% ya watanzania hawajavuka miaka 30, na asilimia 60 ya wapiga kura Tanzania ni vijana wa kati ya umri wa miaka 16 na 35. Hakikisheni hamtoi tafsiri kwamba mnawatupa hawa.

Mbili – hatari ya pili ya kuzungumza suala la CCK na ujasiriamali katika hali ya ‘ikibidi', ni kwamba, kwa hali ya sasa, mfanyakazi, mkulima, mfugaji, pia ni mjasiriamali kwa njia moja au nyingine. Inawezekana CCK mnajaribu kukwepa hali ya Chama kutekwa na wafanyabiashara au kuonekana ni chama cha wafanyabiashara kama ilivyo CCM, lakini ukweli unabakia wazi kwamba ili CCM, Chadema, NCCR, CCK wafanikiwe, lazima wawe na ukaribu sana na wafanyabiashara. Ni muhimu kwa vyama kukwepa hilo ‘kisiasa', ila sidhani kama ni sahihi sana kuliweka kama inavyosomeka kwenye hivi sasa. Jaribuni kulitafutia maneno mengine ya kufikisha ujumbe huo huo mnaokusudia.

2. Katika itikadi mmelenga pazuri, kwani ni ‘unique' from CCM, CDM n.k. Itikadi hii pia ipo more practical na pia realistic kwa mazingira ya wananchi walio wengi. Vyama vingine havionyeshi jinsi gani vitamkomboa mtanzania kutoka kwenye soko huria lililokuwa so unfair kwa maskini. Havitoi tafsiri kwa wananchi kwamba wapo tayari kukaa meza moja na maadui watatu wa Maendeleo na kufikia makubaliano juu ya masuala ya Maendeleo, na badala yake tafsiri ni kwamba wote wanashindana kwenda ikulu kutekeleza yale yale ya maadui hawa kaka yalivyo bila kuhoji: WorldBank, IMF na WTO. Hili suala ni muhimu sana kwani ni wadudu hawa watatu ambao wamemwacha Mtanzania ameduwaa ndani ya soko huru. Na kama mnamthamini Nyerere, jaribuni kuweka mkazo hapa. Lengo sio kuwafukuza hawa bali kuweka msimamo badala ya kuwakenulia kama inavyofanya CCM na Chadema kwa sasa.

Lakini katika malengo na madhumuni – CCK inasema kwamba "itahakikisha shughuli za uchumi haziruhusu ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi kwa manufaa ya watu wachache binafsi". Itikadi yenu ya Social Economic Conservatism haiwezi shamiri bila kukubali ubepari ambao mtaji wake mkubwa ni umiliki binafsi wa mali. Mnachotakiwa kuonyesha kwamba mnaukubali ubepari na soko huria, ili mradi muwe na uwezo wa kukemea vitu hivi pale vitapomkandamiza maskini. Vinginevyo moja ya criticisims kubwa wanazopata Social Democrats ni kwamba wana restrict sana individual rights, sana sana economic freedom kutokana na kuwa na an intrusive government. CCK inatakiwa kukimbia hoja hii kwa kufafanua hicho kipengela cha "mali na njia kuu za uchumi" kwa lugha ambayo itatoa tafsiri nzuri kwa mfano kwamba CCK inaamini katika soko huria n.k, ili mradi kunakuwa na involvement ya serikali katika uchumi nia kubwa ikiwa ni kuzuia unequal distribution of resources n.k, kwani mnaamini kwamba kufanya hivyo kutapelekea uwepo wa soko huria lenye faida kwa wengi n.k. katika maelezo yenu, ionekane kwamba restrictions of individual rights ni muhimu katika kufanikisha hilo i.e. kufanya ‘soko' liwe fairer kwa kila mtu.

Pia kwenye itikadi ni vizuri muweke msisitizo kwenye imani ya chama kwamba mnaamini itikadi yenu ndio njia pekee ya kujenga jamii mnayoitaka au envision kama CCK. Asset kubwa na unique katika Jina la CCK ni "JAMII", itumieni vizuri hii.

3. Kuhusu ukomo wa mwanachama:
Sijaone maelezo kuhusu ni kikao gani kinahusika na hili. Inawezekana imeelezwa kwenye katiba lakini nikapitiwa. Pia sijaona sehemu inayoelezea iwapo mtu atafukuzwa uanachama, ataendelea kuwa mwanachama kwa mfano kupitia vitengo vingine kama vijana, wazee, wanawake?

4. Kuhusu Miiko ya uongozi – hili halijazungumzwa. Ni muhimu kwa sehemu juu ya sifa za uongozi ziendane sambamba na miiko ya uongozi. Suala la ‘hasi na chanya'

5. Pia ni muhimu mkazungumzia ngazi ya JIMBO kama mlivyofanya kuhusu Shina, Kata/Wadi, Mkoa na Taifa. Ngazi ya majimbo ni muhimu sana katika shughuli za chama.

6. Na mwisho ni ushauri tu kwamba CCK kianzishe utamaduni wa kuchapisha literature mbalimbali mfano mipango ya CCK kati ya sasa na mwaka 2015 n.k. Chama pia kije na mwongozo, lakini muhimu zaidi kwa sasa ni kuja hata na vipeperushi vidogo tu vya rangi, hata kurasa hata moja, vinavyoelezea kwa muhtasari kuhusu CCK, huku pakiwa na kauli mbiu ya CCK ambayo ni ‘catchy', ‘inspiring', ‘easy to remember' and ‘unique' from other parties. Chadema, CCM, CUF hawatumii mbinu hii ambayo ni very powerful. Badala yake, huwa wanasubiri wakati wa uchaguzi mkuu, na kupelekea hali ya wananchi kuchananyikiwa kutokana na idadi ya vipeperushi kutoka vyama mbalimbali. Kauli mbiu yenu ya sasa ni nzuri: 'mabadiliko ni sasa, mabadiliko ni sisi'

Ni hayo machache niliyoyabaini kwa haraka haraka.
 
CCK wanaonesha wana mbinu za kutumia mtandao, maana wewe inaonesha utakuwa mpiga debe wao mkubwa. Kwakwakwa. Hongera, lakini hao ni pumba tu hawana lolote jipya, CCJ sasa CCK ikishadondokea puwa kutakuwa na CCL.

Katiba yao itatusaidia nini?

vyama tuliko ni kama makoti yakitubana tutayavua siku moja hivyo kama makoti yanaongezeka namna ni jambo zuri hii itatupa wigo mpana wa kubadilishia makoti yenye kututia joto,tusikasirikie ujio wa cck na vingine vije tu,haina shida ni faida kwetu wavaaji wa makoti
 
Nimejaribu kuipitia katiba yao,hawa jamaa nawatabiria kufika mbali,na kama hii ni katiba ya muda na uongozi uliopo ni wamuda bila shaka wanatoa nafasi kubwa kwa demokrasia kuchukua mkondo wake.Mimi muumini wa demokrasia ya ndani kwanza,hiki kinaweza kuwa chama changu baada ya kuwa nje ya siasa za vyama kwa muda mrefu kutokana na kukerwa na ubakaji wa demokrasia za ndani ya vyama karibu kwa vyama vyote vilivyo ikiwemo ccm,watu hawachugui na kuchaguliwa kuwa viongozi kwa uhuru,bali kwa kudumisha ule utaratibu wa zidumu fikra "sahihi" za mwenyekiti hata kama mbovu unalazimika kuzidumisha ukileta ukaidi unashughulikiwa,nikaona ya nini malumbano,bora nijiweke pembeni.
 
Nimefurahi tu kuona jinsi wanavyotaka kuwa karibu na CCM, maana hawataki kuachana na hizi herufi za C, ngoja tuone.
 
mkuu mchambuzi unajichosha bure. Nani atawapa dola?

Kwa kweli mchango wa mawazo yangu haujanichosha kabisa, badala yake najisikia faraja sana. Nitazidi kufanya hivyo kwa chama chochote ambacho kitajitokeza kuzidi kuziba nyufa zilizopo hivi sasa ki-itikadi au iwapo vyama vilivyopo vikibadilika kimtazamo. Na kuhjusu swali lako juu ya Dola, dola hutolewa na wananchi, lakini muhimu zaidi ni kwamba, mafanikio ya chama hayapimwi kwa kushika dola peke yake. Chadema wamekamata dola? Mbona wana mafanikio mengi tu. Hawa wana CCK ni vijana wanaotia sana moyo. Unakumbuka Chadema ilivyoanza jinsi gani ilikuwa inabezwa? Pengine ulikuwa bado una umri mdogo. CCK wakijipanga, ndio atakuwa mpinzani wa kweli wa Chadema. Au hamtaki Chadema awe na mpinzani?

Wacha tu tuwe hata na vyama mia moja, wananchi wenyewe ndio watakao engage katika Process of Elimination. isitoshe, katika siasa za bara, hakuna chama chenye upinzani wa kweli kwa Chadema. Na hata upinzani wa chadema sasahivi ni wa vitu vya mpito kama nilivyosema huko nyuma. Chadema ina potential kubwa lakini imekwama ki-itikadi. Lakini kwa vile wengi humu walikataa hoja yangu ju ya umuhimu wa itikadi kwa mafanikio ya kudumu ya chama cha siasa Tanzania, mimi yangu ni macho, masikio, akili timamu, na sala zisizokwisha kuombea kuombea uhai mrefu nizidi kuwa shuhuda wa ushindani huu wa demokrasia ya vyama vingi.
 
Nimefurahi tu kuona jinsi wanavyotaka kuwa karibu na CCM, maana hawataki kuachana na hizi herufi za C, ngoja tuone.

Mbona na Chadema ina 'C'? Jamani, tuwe wastaarabu na wenye hekima, na tutoe hoja baada ya kuangalia katiba na itikadi ya chama hiki, na either kupingana nao au kukubaliana nao, kwa hoja. Sidhani hata umesoma katiba yao. Na kukubaliana nao haina maana unaacha uanachama wako wa Chadema, CCM au CUF. Sio lazima uanachama na misimamo wako kwa chama fulani ubadilike kutokana tu na kukubaliana na vyama vingine kihoja, kisera n.k. Kikubwa ni uwe umeshiba itikadi unayoiamini. Vinginevyo utakuwa mtu wa kuyumba.
 
Ngoja tuisome vizuri,sasa mkuu naomba ulijibu hili kwenye kituo kimoja wewe pamoja na katibu wako mlisema serikali ifute rudhuku kwenye chama,sasa we unafikiri vyama vitajiendeshaje? Si ndio vitakua mali zenu sasa?

kuhusu swala la ruzuku,msimamo wetu kama chama ni kuwa ifutwe kwakuwa
1: haifanyi kazi iliyokusudiwa na hata CAG ameonyesha wazi kuwa vyama vinavyochukua pesa zetu walipa kodi vimeshindwa kupeleka ripoti za namna walivyotumia ruzuku.
2.kama hoja ni namna gani vyama vitaendeshwa,jaribu kuangalia,nini hasa hoja ya kutolewa kwa ruzuku,is it for uenezaji wa vyama au ni kwa ajili ya kuendeleza malumbano ndani ya vyama? ni vyama vingapi havijawahi hata kuiona hiyo ruzuku kama lengo la ruzuku ni kuendesha vyama?
3: nchi kama marekani hakuna chama kinachopata ruzuku kutoka serikalini,kila chama kina miradi yake ya kukiendesha chama husika,na hapa kwetu tumekuwa walemavu kwa kutegemea ruzuku,imefika wakati tuseme ruzuku hapana,ingeongezwa kwenye mishahara ya waalimu na madaktari kusingekuwapo na migomo ya kipuuzi kama hii,angalia akinamama wa kimasikini walivyoteketea pale muhimbili na mahospitali mengine nchini!
CCK tunasema " RUZUKU NI UFISADI" na watanzania lazima tuungane katika hili
 
CCK wanaonesha wana mbinu za kutumia mtandao, maana wewe inaonesha utakuwa mpiga debe wao mkubwa. Kwakwakwa. Hongera, lakini hao ni pumba tu hawana lolote jipya, CCJ sasa CCK ikishadondokea puwa kutakuwa na CCL.

Katiba yao itatusaidia nini?

itatusaidia kuujua ukweli kuhusu chama chao,na kumpa utayari wa kujiunga ama kutojiunga yeyote yule ambaye ataridhia yaliyomo ndani ya katiba,na inavyoonyesha jamaa wamejipanga sana kuhakikisha wanaleta mabadiliko,toka CCM foxy! wananuka ufisadi kila kona!
 
CCK wanaonesha wana mbinu za kutumia mtandao, maana wewe inaonesha utakuwa mpiga debe wao mkubwa. Kwakwakwa. Hongera, lakini hao ni pumba tu hawana lolote jipya, CCJ sasa CCK ikishadondokea puwa kutakuwa na CCL.

Katiba yao itatusaidia nini?

hahaaaa! nyani bana huwa haoni................???? wewe hujioni ulivyo mpiga debe wa magamba??? nasikia mabosi zako akina nape,sitta,na wengineo wanatembea wakiwa wamejipaka mafuta ya kuzuia sumu mikononi!! heheeeee! na wewe chunga watakulisha!
 
Bobuk "Husna naomba unitumie namba yako ya simu (Tongue in cheek). BTW hii CCK sio Prototype ya CCJ?"

ngoja nimuombe mume wangu ruhusa akinikubalia knitakupa no zangu za simu,thawa eeeee???
 
KWENYE UTANGULIZI WENU MNASEMA

""kuwa lengo hili kuu la kuijenga na kuimarisha
nguvu za umma nauwezo wa wananchi inawezekana tu ikiwa wananchi wataungana na kuongozwa naChama cha siasa kilicho madhubuti na chenye matumaini mapya kwao na kisichoyumba kwenye masuala ya msingi, Chama chenyeitikadi na sera za kimaendeleo, chama kinachoweka hai matarajio ya wananchibaada ya uhuru wa kiuchumi na kijamii chama kinachopiga vita aina zote zaubaguzi wa kimaumbile kwa kauli na vitendo na pia chama chenye msimamo thabitiwa kujali nchi na watu wake kwanza kabla ya Maslahi mengine yoyote.""


MSISITIZO WANGU NI NGUVU YA UMMA NI ALAMA YA CHAMA FULANI HAPA ,KWA NINI MSIJIUNGE NACHO TUU KAMA MNAKUBALIANA NA MWELEKEO WAO??
 
nimeipitia katiba ya CCK,ni katiba nzuri na inaonyesha kweli inadai mabadiliko ya ukweli,ila kama mtaongea kitu kuhusu muungano hakika nawahakikishia zile kambi za maalim seif na HR zitahamia kwenu CCK
 
ndio tumetumwa kuunda chama hiki na watanzania!

WATANZANIA GANI WALIOWATUMA NA WKO WANGAPI KILA MKOA WANAOWAUNGA MKONO??

JE NI KWELI KUWA MWAKYEMBE,SITTA,NAPE,ANNA KILANGO,LEMBELI ,NA KIMARO NDIO VIONGOZI HALISI WA CCK,KAMA SIO IKITOKEA MBELENI WAKAJIUNGA NA KUSEMA WAO NDIO WALIOKIANZISHA UTARUDI HAPA NA KULA MATAPISHI YAKo??
 
...hakuna mwenye akili yeyote anayeweza kukubali kuwa CCK ni chama,maybe mngeiita NGO
 
Back
Top Bottom