DOWANS waisamehe TANESCO deni lote!

du hapa bado nipo sipo (d'lema) kumbukeni kunasiku ilikuja ama kuwa budget za kila wizara zilipunguzwa kulipa dowans je amuoni kuwa yawezekana wamelipwa halfu wanatupiga chenga la macho hawa mafisadi
mie ninaomba kama kuna udhibitisho wa kusamewa uwekwe jamvin tuusome
 
Mimi nachofikiri deni lilishalipwa kinyemela sasa wanakaushia mbali huko kwa kusema walishasamehe.
 
Kusamehe ni pale ulipokosewa...sasa Tanesco(na Watanzania) iliwakosea nini hao Dowans

Tanesco ilikiuka mkataba na ICC ikawaona kuwa wanakosa na walipe kutokana na kukiuka mkataba. Hayo ndio makosa ya Tanesco. Na kwa kuwa Tanesco ni shirika la umma, umma ni nani?
 
Hapa tunaweza danganywa kirahisi hivi hata kama wakolipwa tutajuaje? Inawezekana washamalizana hafu wanatudangaya tu!
 
Tanesco ilikiuka mkataba na ICC ikawaona kuwa wanakosa na walipe kutokana na kukiuka mkataba. Hayo ndio makosa ya Tanesco. Na kwa kuwa Tanesco ni shirika la umma, umma ni nani?
You Al-Hadaiwi's JF Agent!...YOU CANT HIDE YOUR FACE ANYMORE!
 
Aliyeibiwa ndio anayemsamehe mwizi.
Dowans hawezi kuisamehe TANESCO bali kinyume chake.
Dowans ni matapeli wanapaswa kuilipa fidia TANESCO
 
hajasamehe zote, anataka alipwe Bil. 36 (USD 24 M) anazodai zilijumuishwa katika Bil. 94 deni lililokuwa hadi june 2010 (kwamba bil. 36 ni malipo ya umeme waliokuwa washazalisha na kuuza tanesco bali walikuwa hawajalipwa----kiini macho hapo!!!!!!!!). Kwa sasa linatakiwa kuwa Bil. 99 (deni kwa tanesco baada ya nyongeza ya malipo stahili yao ya kila siku (wawe wanazalisha au la-kwa mujibu wa mkataba wao na tanesco). SASA waliwaandikia tanesco kusamehe kwa masharti kuwa waruhusiwe kuendelea na mkataba wao!!!!!!!!!!! na wamalize kesi nje ya mahakama...... tanesco hawajajibu kitu, nani amufunge paka kengele!!!!!! vikao kila siku usiku kucha (wizara, manegment tanesco, kurugenzi, mara kamati ya nishati). CHANGAMOTO kwao (1) wakikubaliana na dowans, watajiepushaje na azimio la bunge-maana liliagiza kufutwa kwa dowans na ikafutwa na kuvunjwa mkataba wake na tanesco???!!!! (2) Dowans hawajataka samehe deni na kuendelea kukubali vunjika mkataba!!!! (3) wakisema wanunue mitambo-wanaogopa azimio la bunge na sheria ya manunuzi???!! wananchi nao ndo hao unawaona mwanza-wanaojua kila kitu.....hapo kizunguzungu!!!!!!!
 
Kama ni kweli tayari wameshaona kuna namna nyingine ya kuzipata hizo hela. Utaja sikia wameingia mkataba na serikali wa kuzalisha umeme huku wakilipwa mil 150 kwa siku!

Au watawasha mitambo yao. Nadhani wanatuona kama MAITI tu ndo maana wanatuambia kila wanachotaka nasi tunajadiri!
 
Dowans sasa yalainika, wafuta deni kwa Tanesco

Na Richard Makore

25th February 2011

headline_bullet.jpg
Sasa wataka walipwe tu Sh. bilioni 36



Januari(4).jpg

January Makamba

Kampuni ya Dowans Tanzania Limited ya kufua umeme wa dharura ambayo ilishinda kesi dhidi ya Tanesco katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kupewa tuzo ya Sh. bilioni 94, sasa imelainika na imetangaza kusamehe deni hilo.
Uamuzi huu ambao unatangazwa baada ya kuwapo kwa malumbano makali nchini juu ya hukumu ya ICC na kiasi cha fedha kilichotolewa, sasa Dowans wanataka Tanesco ilipe tu Dola za Marekani milioni 24 (Sh. bilioni 36 tu). Fedha hizo ni gharama halisi ya umeme uliouzwa kwa Tanesco.

Uamuzi wa Dowans ulitangazwa na Stanley Munai ambaye ni Mkurugenzi wake wa Fedha, akiwa pia mwakilishi wa kampuni hiyo nchini.

Mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Munai alisema kuwa wamechukua hatua ya kufuta deni hilo kutokana na kusikia kilio cha Watanzania.

Hata hivyo Dowans imesema licha ya kutoa msamaha huo, Tanesco bado imeshindwa kujibu kama imeukubali msamaha huo au la ili mazungumzo yaanze.

Munai alidai fedha wanazolidai shirika hilo kwa sasa zinakaribia Sh. bilioni 99 badala ya Sh. bilioni 94 za mwaka jana.
Alisema ongezeko hilo limetokana na kampuni ya Dowans kuitoza Tanesco kila siku Dola za Marekani 11, 800 (Sh. milioni 15.3) kama gharama za kuweka mtambo hata kama hauzalishi umeme na kwamba nyongeza ya gharama hizo ilianza kutozwa kila siku tangu Juni 15, mwaka 2010 hadi sasa.

Alisema deni la Sh. bilioni 94 liliishia Juni 14, mwaka 2010 na baada ya hapo limekuwa likiongezeka siku hadi siku. Munai aliwaambia waandishi wa habari walioambatana na kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuwa kampuni yake haina tatizo kuhusu kusamehe deni hilo, lakini Tanesco muda wote imekuwa haitaki kukubali msamaha huo.
Aliongeza kuwa ikiwa Tanesco na Serikali watakataa kupokea msamaha huo nje ya mahakama na wao wataacha sheria iendelee kuchukua mkondo wake.

Munai alisema mkataba kati ya Dowans na Tanesco unasema kuwa ikiwa pande hizo mbili zitatofautiana na zikaenda kwa msuluhishi maamuzi yatakayotolewa yatatakiwa kuheshimiwa na pande zote na hakuna upande utakaoruhusiwa kukata rufaa.
"Kwa mujibu wa mkataba huu, Tanesco haiwezi kukata rufaa kwa kuwa kipengele hicho kinawazuia na wao wanajua, lakini hajui ni kwanini hawataki kuwaambia wananchi ukweli," alisema.

Alifafanua kuwa endapo serikali na Tanesco wataendelea na msimamo wa kugoma kupokea msamaha huo wataendelea na utaratibu wa kimahakama ili wapate kibali cha kukamata mali za Tanesco za ndani na nje ili ziuzwe ili kufidia fedha za Dowans.
"Tumewandikia barua Tanesco kwamba tukae meza moja kwa maelekezo ya mmiliki wa Dowans ili tuwasamehe deni, lakini hawataki kujibu, sasa tuwafanyeje?" alihoji Munai.

Alisema Dowans inaidai Tanesco Dola milioni 24 (Sh. Bilioni 31.2) kutokana na kuwauzia umeme kabla ya kuvunjwa kwa mkataba.

Alifafanua kuwa deni la umeme lazima lilipwe kwa kuwa waliwauzia Tanesco nishati hiyo na wakawauzia wateja wao hivyo wana uhakika fedha hizo walizichukua na wanazo.

Mtambo huo wa Dowans jana ulikuwa umezimwa lakini, Munai alibainisha kwamba muda wowote wakitakiwa kuwasha watafanya hivyo.

Alisema mtambo huo una uwezo kuzalisha megawati 120 na kwamba endapo watauwasha una uwezo wa kuanza kuzalisha umeme baada ya dakika 12 tangu kuwashwa.

Wakati huo huo, kampuni ya Dowans imekiri kudaiwa na benki ya Baclays Tanzania Dola za Marekani milioni mbili na kusema kuwa wanaendelea kulipa kama ilivyo kwa wateja wengine wanaokopa katika taasisi za fedha.

Jumapili iliyopita mmiliki wa Dowans, Brigedia Jenerali Mstaafu Suleiman Yahya Al Adawi, alikutana na wahariri wa vyombo vya habari na kueleza kuwa alikuwa radhi kukukana na Tanesco kwa mazungumzo. Alisema walikuwa tayari kusamehe sehemu ya deni hili kwa masharti wakubaliwe kuendelea kuzalisha umeme.

Wakati huo huo, Kamati ya Nishati na Madini jana ilitembelea mitambo ya gesi ya Tanesco iliyopo Ubungo, mitambo ya Dowans na ya Songas ambayo pia inatumia gesi.

Akizungumza wakati wa kutembelea mitambo hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, January Makamba, alihoji ni kwa nini mitambo hiyo ya Dowans isihamishwe eneo la Tanesco kwa kuwa haifanyi kazi.

"Sasa hii mitambo inafanya nini hapa wakati haifanyi kazi na mmeizima au mna malengo gani nayo," January alimhoji Munai.
Akijibu swali la January, Munai alisema awali walitaka kuondoa mitambo yao lakini Tanesco wakawazuia.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando, akizungumzia maamuzi ya Dowans, hakutaka kutoa ufafanuzi badala yake alisema kinachosababisha matatizo yote hayo ni kauli za kisiasa na wanasiasa.

Naye January alipoulizwa kuhusiana na maamuzi ya Dowans, alijibu kwa kifupi kuwa suala hilo ni la Tanesco.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, hakupatikana kuzungumzia msamaha wa Dowans kutokana na simu zake za kiganjani kuzimwa.




CHANZO: NIPASHE
 
Hakuna haja ya kuingia mkataba na cambuni inayoendeshwa kitapeli,
nibora kuvunja mkataba na dowans na kutangaza tenda ya kuzalisha
umeme kwa nchi mbalimbalina kuchagua ambayo, ambayo itatoa nafasi kwa tanenesco kupata kampuni bora na inayojulikana na si kambuni ya vichochoroni kama dowans, tenda itanagazwe na vigezo viwe wazi, kwani ni bora tuendelee kukosa umeme kwa miezi hata sita ila tupate kambuni yenye uwezo wa kuzalisha umeme kwa beii nafuu. Haya mambo ya kuwapa tenda matapeli kama rosta na adawi ndiyo yanaleta matatizo, na hili ni kosa la mkurugenzi wa tanesco kupenda 10% kwani kama mambo ya 10% yasingekuwepo uzembe huu usinge tokea.
 
Kilichosababisha hatua hiyo kufikiwa ni nguvu ya umma! Ya chadema....na bado lazima wote waliotufikisha hapo washughulikiwe kwani nguvu ya umma bado ipo na inakuja si utani.....watu lazima wawajibishwe wangatuke....bado maswala ya mbagala,gongo la mbota nk
 
Na kwanini Radio Tumaini iwe ndio source ya hiyo habari kubwa hivi, wakati tunajua hiyo redio inaishia Magomeni, na sisi wa huku SWEKA hatuijui!

JK anangoja ROSTAM amwelekeze cha kusema...Otherwise asingekaa kimya wakati nchi ipo kwenye hali ya hatari hivi!

nafuu hata wangetumia radio free africa ambayo ipo karibu eneo lote la maziwa makuu. au hata redio maria ambayo iko kwenye intaneti, huwasaidia sana wazawa walio ughaibuni. tembelea the World Family of Radio Maria
 
Dowans sasa yalainika, wafuta deni kwa Tanesco


Munai alidai fedha wanazolidai shirika hilo kwa sasa zinakaribia Sh. bilioni 99 badala ya Sh. bilioni 94 za mwaka jana.
Alisema ongezeko hilo limetokana na kampuni ya Dowans kuitoza Tanesco kila siku Dola za Marekani 11, 800 (Sh. milioni 15.3) kama gharama za kuweka mtambo hata kama hauzalishi umeme na kwamba nyongeza ya gharama hizo ilianza kutozwa kila siku tangu Juni 15, mwaka 2010 hadi sasa.


Akizungumza wakati wa kutembelea mitambo hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, January Makamba, alihoji ni kwa nini mitambo hiyo ya Dowans isihamishwe eneo la Tanesco kwa kuwa haifanyi kazi.


CHANZO: NIPASHE

Nisaidieni jamani mimi kichwa changu cha panzi. Mitambo imewekwa kwenye eneo la Tanesco, halafu tanesco inatakiwa kuwalipa walioweka mitambo kwenye eneo lao?
 
Ni kwamba Dowans ndio wamesamehe Deni lote Tanesco ila kwa sharti kwamba lazima waendelee kutoa huduma, (Yaani wataendelea kuzalisha umeme na kuiuzia Tanesco). Ukiangalia tunarudi kulekule. Na kwa taarifa za uhakika tayari Dowans wamesha washa mitambo yao.
Kiini macho hicho, watauziwa umeme kwa bei ghali ili kufidia Bil 94 wanazodai,
Hii Dowans kama vile ya Watanzia walioikana nchi yao. Lazima Dowans ni kampuni ya Watanzania, hawa watu wana akili mno ya kuibia serikali. Akili kama hizi za kiwizi na kifisadi Watanzania ndo wanasifika duniani,
Kwa vile TZ ni nchi ya amani ndo maana haya yanafanyika,
Tanzania imekuwa kama nchi ambayo haina Rais. Hv Rais haoni uchafu huu unaomdharirisha,
Haya bwana endeleeni kulipua kambi za Jeshi.
 
Achana na huyo kijana kiziwi na siyejifunza!
Anatakiwa kwanza kabisa anywe sumu kabla hatujamshika, maana ametudanganya mchana hadharani kuwa wamiliki wa Dowans ni wale jamaa 6!...Sasa imekuwaje hasemi kitu, au kukanusha taarifa yake ya awali baada ya kuja kwa Al- Hadaiwi??

Hivi kweli Ngeleja anataka tufanye maandamano ndipo ajue watanganyika tuna hasira.Wizara imemshinda hatumtaki aende Sengerema akavue samaki au arudi kwenye kampuni la kifisadi alikokuwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom