Kiresua
JF-Expert Member
- May 13, 2009
- 1,184
- 259
Wewe mtoa mada, pia soma hapa, tumeambiwa Porteck ni ya Singapore, sawa, Waziri kasema hivyo wal si mm..... halafu some hii post hapa chini Rostam alisema nini (kwenye RED) Eti kuwasghhawishi waje kuwekeza kwenye Usafiri wa anga, Kalangabahoo!!!!!!¬!
Tanzania Daima(January 6,2011)
Rostam alisema jambo pekee analokiri kupata kulifanya ni kuwashawishi wamiliki wa kampuni ya Dowans Holdings SA iliyorithi mkataba wa Richmond kuja kuwekeza nchini katika sekta ya umeme.
Mimi nilishiriki katika kuwashawishi Dowans kuja nchini. Nitaendelea kushawishi wawekezaji waje nchini ili nchi iendelee, ajira ipatikane na kodi ziongezeke. Juzi tu nimetoka Singapore, Malaysia na UAE (Falme za Kiarabu) kuwashawishi wawekezaji kuwekeza kwenye usafiri wa anga, alisema Rostam.
Alipotakiwa kueleza iwapo yeye ni mmoja wa watu wanaotarajia kufaidika na malipo ya shilingi bilioni 185 ambazo TANESCO inatakiwa kuilipa fidia Dowans, mfanyabiashara huyo alikana kuimiliki kampuni hiyo.
Mbali ya kukanusha hilo, Rostam aliyabeza madai ya baadhi ya wanasiasa wanaohusisha fedha hizo na yeye akisema katika mkusanyiko wa biashara zake anazofanya ndani na nje ya nchi kiasi hicho cha fedha wanazotarajiwa kulipwa Dowans ni sawa na mapato yake ya miezi minne tu.