DOWANS na bunge la February

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
serikali imeonyesha hofu tayari,inataka malipo ya kampuni la kitapeli la dowans yafanyike haraka na tena ikiwezekana kabla ya bunge la february,waziri ngeleja anasisitiza ni lazima malipo yafanyike haraka.

MY CONCERN:
1.NINI HARAKA YA KUILIPA HILO KAMPUNI LA KITAPELI?
2.TULIKUWA NA KAMATI TEULE YA BUNGE KWNINI TUSITOE NAFASI KWAO WAKATOA TAMKO JUU YA DOWANS MAANA WALIFANYA UCHUNGUZI?
3.KWANINI SERIKALI ISISUBIRIE HADI BUNGE LINALOKUJA ILI KUWEZA KUSIKIA MAONI YA WANANCHI KUPITIA WAWAKILISHI WAO AMBAO NI WABUNGE KABLA YA MALIPO KUFANYIKA?
4.HIVI NI KWELI NI JUZI TU NDIO TANESCO WAMEWEZA KWENDA BRELA NA KUFAHAMU HAO WAMILIKI WA DOWANS KAMA ALIVYOSEMA NGELEJA?
5.WAKATI ANATAJA MAJINA YA WAMILIKI WA DOWANS HATA NGELEJA MWENYEWE ALIKUWA ANACHEKA KWANI DHAMIRA YAKE HAI ILIMWAMBIA HAO SIO,HIVI WAZIRI UNATANGAZA JANGA KAMA HILO LA KULILIPA KAMPUNI LA KITAPELI HUKU UNATABASAMU?
HAKUNA UHARAKA WA UILIPA DOWANS ENDAPO MALIPO YENYEWE YANATOKANA NA KODI ZA MASIKINI WA KITANZANIA,WADAU WASHIRIKISHWE HATA KUSOMA TENA HIYO HUKUMU YA DOWANS NA SIO KUFUATA HUO USHAURI ALIOUTOA MWANASHERIA MKUU AMBAYE SIKU ZA HIVI KARIBUNI AMEMEZWA NA KUWA MIONGONI MWA MAKADA WAAMINIFU NA WATIIFU KWA CHAMA KIZEE
 
Hawawezi kulipa hata wakijifaragua namna gani watalipa kwa kupitia bajeti ipi,kwa sababu Bunge haijaidhinisha matumizi hayo ya pesa kwa hiyo akita wabunge wa upinzani na vyama vyao waanzishe maandamano ya kitaifa kwa Tanesco na Wizara kukwapua pesa kutoka kwenye bajeti ambayo haikuidhinishwa na walipe tuwaone kweli
 
Sisi watz na serikali yetu ni wabishi sana kulipa madeni hadi wanaotudai wanaamuaga kutusamehe. Inakuwaje hawa dowans tunaharakisha kuwalipa? Tuwapotezee hadi waje watusamehe kama ambavyo wengine huwa wanatusamehe!
 
kwani nin Tanesco wameidai serikali kwa miaka sasa hwataki kulipa, leo kesi jana tu, tunataka haraja sana kulipa kabla ya Kesho
 
Ni ujinga uliojaa watawala hawa, wamelewa madaraka, hawaoni kitu tena mbele yao! wanajiona wao tu peke yao na familia zao
 
RA anasema anahela nyingi kuzidi hizi za Dowans, na Mfalme wa Ughaibuni alishasema dowans haikuwa yake basi tuwaombe watusamehe madeni kama nchi nyingine wanavyosamehe, na je kama kuna kampuni toka nje inakuja kuinvest TZ au nchi nyingine serikali ya Mtu huyu anapotoka kweli hawajui huyu mtu kafungua kampuni gani kwenye nchi nyignine au ndio kama ya Osama alivyoenda kufungua viwanda nchini Sudani, baadaye Marekani ikaviripua, je mtandao huu wa Dowans hauna nguvu za ki-alqueada maana mambo yao ni ya kimagendo mno, huenda ni wa Osama maana kote unakopita unaogopwa kutowataja mapema serikali labda inaogopa aibu kutoka marekani. Tuwe makini jamani na hawa wawekezaji wasije kuteletea mitambo ya madawa ya kulevya
 
Bungeni patachimbika na izo ela ambazo CCM wanataka kujilipa kuponya majeraha/ukata baada ya uchaguzi
 
ujinga ujinga kila sehemu,uozo huu hivi utaisha lini?wazee wa jumuiya ya afrika mashrika hadi walikuwa wanamwagiwa maji ya kuwashwa kudai haki zao na hajapata hadi sasa,serikali inataka kutuongezea umasikini kwa malipo kwa kampuni hewa,damn ccm
 
Hivi Serikali hii ya JK ni kwa ajili ya wananchi gani???? Na wataifa lipi?? Wananchi karibu wote hawakubali Hilo DUDU DOWANS lilipwe fedha za jasho lao kwa nini wao wanashadadia kiivyo?????
 
Umefika wakati sasa UMMA usimamie haki ya kila mzalendo.
Haiwezekani leo hii mahakama iliyo nje ya Tanzania itoe hukumu kuwalipa hao fisadiz na serikali inakimbilia kwenye vyombo ya habari kutangaza kuwa serikali iko tayari kuwalipa. Mahakama yetu hapa nchini ilishaamua wastaafu na waliokuwa wafanyakazi wa East African Community walipwe haki zao, lakini serikali hii bado inawapiga danadana tu. Kuna nini hapa???

Watanzania tusimame pamoja kupinga huu wizi wa mchana. Wananchi ndiyo tunaamua ni nini serikali ifanye, sasa huu wakati tunatakiwa kutamka wazi si vinywa, fikra au moyo BALI kwa vitendo. Kama viongozi hao hawataki kutusikiliza basi tuwalazimishe watusikilize.
Kwani Kikwete akiiambia hiyo mahakama kuwa wenye nchi wamesema hawalipi itakuwaje?

It's time to stand up for the TRUTH.
 
Hela za kuilipa dowans wanazo lakini za kuwalipa waalimu, madakitari, na kuinua maisha ya watanzania hazipo. Hiyo maana ya ufisadi. Serikali yote imeoza inanuka sana kila kona. Ndiyo maana tunahitaji katiba mpya yenye kuwanufaisha watanzania watoe mawazo yao kwa uhuru hata jeshi lake litawalinda wananchi wakati wote, pia litalinda uhuru wa vyama vyote sio chama tawala tu.
 
Hivi deadline ya kuwalipa DOWANS ni lini?

Kinachotumika kama kigezo cha kuharakisha malipo haya eti tutakuwa tunaongeza deni kwa asilimia 7 kila siku kadiri tunapo chelewa. Mimi sioni kama hiyo ni issue watanzania ndiyo tunalipa kitu cha kwanza wangekata rufaa ili tusubiri Bunge lijadiri haya malipo ili tumapate ninani hasa anastaili kulipwa na ninani anapashwa kubeba huu mzigo.
Wanasheria tuambieni, hivi riba ya asilimia 7 ni halali na halafu mdaiwa huwa analazimishwa kulipa deni lote kwa mara moja na mahakama au anaweza kuiomba mahakama alipe kwa awamu kulingana na uwezo wake?

Kwanini viongozi wetu wako kimbelembele kulipa bila hata kuomba walipe kidogokidogo?
Hapa ndo utaona jinsi 10% zinavyofukuziwa na hawa washenzi, ngereja ana 10% yake pale ndiyo maana hana uchungu hata chembe.
Wizara ya Nishati ni wizara yenye mawaziri waliowekwa kutekeleza mambo ya wakubwa hawa wote ni ndiyo mzee ndiyo maana wanatangulizwa mbele.
Jamani hatuwezi kuwaambia mataifa yanayotupa misaada wa watch mienendo ya kifedha (account transactions) za hawa jamaa kuanzia sasa kuona kama kuna hela itaingia isiyokawaida. Nadhani hata hapa ndani inawezekana kuwafatilia hawa maana tuna watu wazalendo katika benki zetu wanaweza kututonya mara tu hela ikiingia kwenye account zao. Dr. Slaa tumia your intelligence on this we will definitely catch them.


Nina hasira, we acha tu! Peoples powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!
 
Back
Top Bottom