Dowans, mauaji Arusha - ni kipi kipo mahakamani na hakipaswi kuongelewa?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wanaJF, kuna mambo yanayotokea hapa Tz na wakati mwingine nashindwa kuelewa kwa nini inakuwa vile. Mfano, hoja ya Dowans imeachwa kujadiliwa bungeni kwa madai kuwa ni suala ambalo bado liko mahakamani.

Lakini mauaji ya raia Arusha yalitolewa kauli na Waziri Mkuu Mizengo Pinda huku akikishtumu Chadema kwa kuwa chanzo cha mauaji hayo wakati kesi bado iko mahakamani. Je, Waziri Mkuu kutoa "hukumu" nani alaumiwe kuhusu vurugu hizo wakati kesi iko mahakamani siyo kuingilia uhuru wa mahakama? Kwa nini inakuwa rahisi kuongelea vurugu zilizotokea Arusha ambapo kesi bado iko mahakamani na wakati Dowans inaonekana kama taboo wakati kesi pia bado iko mahakamani? Ni kitu gani kimejificha hapa?
 
Back
Top Bottom