Dowans kujadiliwa udsm leo

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
kutakuwa na mjadala leo pale ukumbi wa nkrumah saa nane kuhusu malipo ya dowans. kutakuwa na watoa mada wazuri ukipata nafasi njoo tuendelee kupiga kelele kuhusu huu wizi wa mchana kweupe
 
Hii ni muhimu sana. Taarifa kama hizi ziwe zinaletwa hapa mapema ili tujipange kuhudhuria. Ukisoma ujumbe huo hapo juu, mwambie na mwenzako, wote tuhudhurie.
 
Hii ni habari njema,lazima niwepo. Hata kama watailipa Dowans wajue Watanzania tulikataa. Utawala bora kwenye kulipa makampuni feki tu? Mbona wazee wetu wa East Africa ni miaka 30+ hawajalipwa stahiki zao kama ilivyotaakiwa???? Huo ni utawala bora????

Nalia sana na Mzee wa POWER OF ATTORNEY, sijui ana mpango gani na hii nchi. Maana angekuwa na huruma hata kidogo. Tunaangamia yeye anafurahia tu. Ingekuwa ni uharabuni watu wangejilipua nae tu.
 
Wakuu naomba mtakaokwenda huko kama uwezekano wa mtu kwenda na Camera au hata recorder tupate Audio ili muweze kutuwekea Youtube.... Thanks is Advance
 
Watanzania wenye uchungu na nchi nawaomba mliweke priority suala hili,kama ratiba yako inaruhusu hapa si pa kukosa
Panelists;
Mr James Jesse
Mr Bashiri
Dr Aldof H Mkenda
Hon Tundu Lissu
Panel Chair Dr A.Lwaitama
 
Labda kwa wanasheria mtuelekeze kidogo, kuna watu wamefungua kesi kuhusu hii issue ya dowans, sasa discussions kama hizi wakati kesi iko mahakamani ni sahihi au? mm sijui, labda wnasheria watuelekeze.
 
:clap2:Safi sana UDSM, hii Dowans lazima isilipe kwani ni ya ROSTAM AZIZI, huyu gabachori hawezi kula pesa za wavujajasho wa TZ kiurahisi kiasi hicho, japo kuwa CCM na JK wao wanataka kumlipa kama Ahsante kwa kugharamia helkopta za JK wakati wa Kampeni.:clap2:
 
Habari zilizonifikia ni kwamba kuna nafasi chache sana za kuingia ukumbini. Panel discussion inafanyikia council chamber badala ya Nkurumah Hall. Hivyo anayependa kuingia awahi sana, saa 7.30 uwepo eneo la tukio. Mimi niko hapa tayari na watu wengi wanapanga kuhudhuria. I will post what has been discussed.
 
Back
Top Bottom