eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 15,653
- 13,794
Ok sasa nisije kuwa natibua mambo; tuliambiwa tatizo la umeme linahitaji Dowans kuwashwa haraka na bila ya hivyo nchi itazidi kuwa gizani. Katika kauchunguzi kangu kadogo kanaonesha umeme unapatikana si kwa mgao mkali sana kama wiki chache zilizopita. Sasa nimejiuliza labda kwa vile tulikuwa tunafuatilia mambo ya Loliondo yawezekana tumeshindwa kujau hatua zilizochukuliwa. Yawezekana:
a. Mitambo ya Dowans imewashwa
b. Umeme kwenye Migodi umehamishwa uraiani? - ili na wao waonje uchungu?
c. Tanesco wametafuta umeme wa ziada...
d. ...
Lakini mkulu hata kama nina mawazo ya kikombe cha babu/bibi; nina swali
mosi: mitambo imewashwa kwa mapatano/makubaliano gani?
pili: imewashwa kwa idhini ya nani?
tatu: Kuwashwa kwa mitambo kutaathiri kwa kiasi gani mvutano uliopo sasa kati ya wamiliki [dowans] na tanesco?
nne: Sheria zimefuatwa kununua huduma hiyo [procurement procedure].