Dowans,Dowans

Utata mtupu.. afu ikiwashwa deni linaongezeka au tunaanza kuwalipa bili mpya

Mitambo Ya Dowans ndio yenye kuuza umeme bei rahisi kuliko mitambo yeyote ya aina hiyo iliyopo Tanzania. Of-course, ukiiwasha unailipia usiiwashe unailipia. Hapo ndipo nikasema aliyezowea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi. Wengi wetu wanadhani kwa kuizima ile mitambo ndio hauilipii, la hasha, hata hilo deni lililoamriwa na wasuluhishi wa biashara wa kimataifa ICC mitambo ilikuwa imesimamisha uzalishaji wake lakini ki-mkataba inabidi uwalipe, kwa nini uliwapa "go-ahead" ya kuileta? halafu huitumii? hiyo sijui ni akili ya wapi?

Mitaambo ipo, imeshaungwa kwenye gridi, tunailipia/tutailipia hata kama hatuitumii, labda tuamuwe kufanya dhulma, na hilo pia kwa dunia ilivyo sasa hatutapata nafasi kwani hata nyerere aliwahi kutaifisha mali za Lonrho, alishindwa, ilibidi walipwe pamoja na interest alipobisha eti tu kwa sababu yeye ni Rais wa Tanzania na kusema hatazami nyuma atageuka jiwe, watu wakayafikisha palipo mbana pabaya nyerere, mwenyewe aksalimu amri, akailipa Lonrho kwa riba. Akaulizwa mbona hukugeuka jiwe? umelamba matapishi yako mwenyewe? akawa kimyaaaaa kama kamwagiwa maji. nyerere alifikiri haya mashirika makubwa utayanyang'anya kama ulivyo wanyang'anya wahindi nyumba zao?

Mfano huo ndio huu wa Dowans, cha kufanya cha hekima na busara ni kukaa nao chini na kuinunuwa hii mitambo isizidi kututia hasara, kwani tunailipia na hata ikifikia tammat na kusema rasmi hatuwalipi. Hapo ndipo Dowans watapoyapeleka kule kuliko mbana pabaya nyerere, huko hakuna ujanja utalipa ukitaka usitake.
 
duh!!mkuu majimshindo kumbe sisi tunaopiga makelele kuwa mitambo isiwashe tumekalia mti huku tunaukata sio?..so bora mitambo iwashwe kama vipi na kwa nini watu wengine hawataki iwashwe kama all in all tunawalipa kutokana na mkataba? Na ile gesi ya kuendeshea ile mitambo ni ya nani?
 
Hivi ulikuwa hujui kuwa hata zile fedha zilizoamriwa na ICC zinalipwa na huku mitambo imekaa tu? Hapo ndipo utapojuwa kuwa tunafanya maamuzi mengine bila kufikiria, Rashid, Zitto walisema jamani, hawa wamekwenda mahakamani na mitambo wameleta, ipo, na imejaribiwa na imetumika kwa muda, inafanya kazi vizuri, kama sasa mvuwa zimenyeesha na ndio tunaona hatuihitaji, tuinunuwe. Watu wakawaona wabaya. Matokeo ndi hayo mabillioni ya kuwalipa. Na bado tumeizuwiya kiubabe, na bado deni linaongezeka. Jee, huo ndio uamuzi wa busara? mimi nasema hapana, tukae chini na wamiliki wa Dowans, hawa ni wafanya biashara, na pesa ya leo kwa mfanya biashar ni bora kuliko ya kesho. Tukubaliane nao moja lenye tija kwetu na kwao. Hilo ndio suluhisho jema.

Unajuwa madhara ya kuwanyima haki yao Dowans si tu tutawalipa, tunakosa kuzalisha mabilioni zaid ya thamani ya hiyo mitambo kwa ujinga wetu. Pia, picha gani tunawapa wawekezaji tunaowaomba kila siku waje kuwekeza Tanzania? jibu, ni picha mbovu na ndio maana unaona hatupati wawekezaji wa viwanda zaidi ya wachina.

Gas wanayoitumia ni ya Tanzania na wanailipia inapotumika, hawapewi bure, na kama sasa haitumiki, hiyo gas inapotea bure, kwani gas ukiitowa inabidi uitumie, hatuna vifaa vya kuhifadhi Gas kwa wingi katika Tanzania. Hapo utaona ni hasara tu, umeme hatuna, gas haiuziki, mitambo tuna/tutailipia bila ya kuiwasha.

Aliyezowea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.
 
Mtoa mada umesahau kitu. Napenda kukuuliza, unataka mitambo iwashwe kwani tumeshalipa? Kati ya wafuatao niambie nani alikuwa na ujasiri wa kukutana na muwekezaji? a) Ngereja b)Mr.President c)Mnyika d)JMakamba d)waziri kivuri nishat na madini wa chadema e)mkuu wa mkoa ambapo mitambo ipo f) wanaharakati wote waliokuwa wanaongea saaaana kuhusu dowans.

ukimaliza hapo uniambie kati ya Mr.Dowanz na wale watanzania waliohusika kwenye mikataba nani sisi watanzania tunapaswa kufa nae? Mie naona Mr.Dowanz kama muwekezaji hana makosa kwani hana uzalendo na sisi lakini je hawa watanzania ambao tumeona walihusika na hawakuweka uzalendo mbele tuwafanyeje?

Mwisho naomba unijulisheje wakati wabunge under Sitta wanaishawishi serikali kuvunja mkataba ni kweli walikuwa hawajui madhara ya kuvunja mkataba kwa muwekezaji wa kimataifa?
 
Tutalipaje wakati mkataba hauleweki? Na anayetakiwa kukutana na mwekezaji ni wizara husika na wala sio mtu , kuna wizara husika wao ndio wanahusika.mr dowans ana makosa kwa sababu anajua /alijua analolifanya kuwa anatupiga changa la macho na anataka kutuibia aka kutunyonya kirahisi. Hawa watanzania ambao hawajaweka uzalendo mbele inatakiwa wajiuzulu kama kina karamagi lakini hawataki wanadhani kuwa wako right. Wabunge tumewatuma sisi na nina uhakika walikuwa wanajua wanalolifanya na si unajua mchuma janga hula na wakwao? Hawa nao inabidi wawajibike katika kusolve hili tatizo but nashangaa wanaongea na magazeti tu mpaka sasa hivi..
So tufanye nini sisi? Nafikiri unajua kilichotokea Tahrir square
 
Mtoa mada umesahau kitu. Napenda kukuuliza, unataka mitambo iwashwe kwani tumeshalipa? Kati ya wafuatao niambie nani alikuwa na ujasiri wa kukutana na muwekezaji? a) Ngereja b)Mr.President c)Mnyika d)JMakamba d)waziri kivuri nishat na madini wa chadema e)mkuu wa mkoa ambapo mitambo ipo f) wanaharakati wote waliokuwa wanaongea saaaana kuhusu dowans.

ukimaliza hapo uniambie kati ya Mr.Dowanz na wale watanzania waliohusika kwenye mikataba nani sisi watanzania tunapaswa kufa nae? Mie naona Mr.Dowanz kama muwekezaji hana makosa kwani hana uzalendo na sisi lakini je hawa watanzania ambao tumeona walihusika na hawakuweka uzalendo mbele tuwafanyeje?

Mwisho naomba unijulisheje wakati wabunge under Sitta wanaishawishi serikali kuvunja mkataba ni kweli walikuwa hawajui madhara ya kuvunja mkataba kwa muwekezaji wa kimataifa?

Kwani mkataba ulivunjwa na DOWANZ au na RIchmond? Nilidhani kuwa mkataba ulikuwa zaidi na Richmond - ,ambao walihaurisha mkataba kwa Dowans
 
Back
Top Bottom