Dovutwa amtetea Ridhiwani; awaponda Dr. Slaa na Mtikila

Mdau

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,789
470
Wadau,nasikiliza redio hapa, taarifa ya saa 12 jioni hii, kwamba Dovutwa- mwenyekiti wa UDPD ameitisha press confernce na kutetea hatua ya Ridhiwani kutaka kuwapeleka court Dr Slaa na Mch Mtikila.....kaongea mengi, ila zaidi kawashangaa kushusha tuhuma za uwongo kwa Ridhiwani wakati wao ni zaidi ya wanasiasa, yaani ni watu wa dini,,,eti wasiongee kama 'watu wa mitaani'...

Kwa wasiomjua DOVUTWA, ni huyu anayeongea na rais Kikwete pichani (chini)

Dovutwa.jpg

 
yule ni kibaraka kuanzia mwaka juzi na mwka jana wakati wa uchaguzi ndo alonyesha makucha yake
 
Kura yangu nampa JK kwa kumnukuu alichosema wakati wa uchaguzi ni sababu tosha naye yumo kundini hana jipya.
 
Sasa huyu Dovutwa wa nini naye, nani anamjua?? Anajipendekeza kwa Riz??

Jamani, mimi nasema kila siku: Njaa mbaya sana na hasa ukiibebea kwenye sinia, hata mtoto mdogo anajua una njaa. Kinachomsumbua huyu bwana ni njaa tu, hakuna kingine.

Kama kweli yeye ni mwanasiasa tena mwenyekiti wa chama chake sijui kinaitwaje, anataka kutuambia tangu uchaguzi mkuu uishe amefanya nini kukitambulisha chama chake. Anasubiri wanaume waibue tuhuma ndo anadandia, sasa hiyo itamsaidia nini.

Nashauri: Dr Slaa kuna watu wanataka kupata umaarufu kupitia kwako, hebu achana nao chapa kazi ya chama. Sasa huyu naye anataka mjibizane ili iweje. Forget about him halafu tuone atakuja na sera gani tena.
 
Mzee naona njaa inataka kumuua sasa inabidi ajikombe kombe kinamna ili mafisadi wamtoe kimaisha
 
nafikiri hayo hayamhusu huyu jamaa, asijiingize vinginevyo naye atakuwa kwenye mkumbo mmoja. Hakumsikia Ridhiwani alivyowaambi kwamba mabo hayo ni yake na familia yake. sasa nauliza je DOVUTWA NI MWANA FAMILIA YA RIDHIWANI AU MSEMAJI WA FAMILIA HIYO????? Aweke wazi kwanza.
 
Hivi kwenye uchaguzi alipata kura ngapi ni moja au nntakuwa nimekosea!!?maana kila mtangazaji wa matokeo alipokuwa akilitaja jina la Dovutwa,,,,!!!
 
Dovutwa huna authority ya kuita press conference kumtetea dogo wa bwana mkubwa, unajiaibisha sana kujishusha kiasi hicho maana ukifanya hivyo utakutana na fire.....acha unafiki na kutuuza sisi kwa akili ya kutetea tumbo lako,
 
Mimi napendekeza tusitishe mjadala huu kwa sababu kadri mnavyo post thread munamuongezea umaarufu
 
Dovutwa ataka CHADEMA ichukuliwe hatua za kisheria

Thursday, 10 March 2011

Mwandishi Wetu

CHAMA cha UPDP kimesema ni uhaini na uasi kwa vyama vya siasa kuratibu maandamano ya kuing'oa serikali iliyomadarakani kwa mabavu.

Chama hicho kimetoa kauli hiyo jana kupitia Mwenyekiti wake Fahmi Dovutwa, na kimehoji kitendo cha serikali kutokichukulia hatua chama cha Chadema kama ilivyomchukulia Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema, mwaka 2001, alipokutwa na nyaraka za vifo vya watu Bulyankulu.

Alisema hivi sasa taifa linakabiliwa na tatizo la baadhi ya vyama vya siasa kubadili mwelekeo wa kisiasa unaokidhi mahitaji ya kidemokrasia na hivyo kulielekeza taifa katika machafuko ili kufikia malengo yao ya kisiasa.

"Jambo hili lazima likemewe kwa nguvu, kitendo cha Chadema kuingiza nchi katika vurugu kama zitokeazo Misri na Tunisia, haliwezi kuvumilika," alisema Dovutwa.

Alisema Tanzania inatawaliwa na siasa za kidemokrasia na utaratibu wa kuruhusu kubadilishana uongozi kwa njia ya sanduku la kura. "Hivyo Tanzania haiwezi kulinganishwa na mataifa ya Kaskazini ya Afrika ambako kuna tawala za kimila."

Hata hivyo, alisema katika nchi za Misri na Tunisia vyama vya siasa haviko mbele kuratibu maandamano yanayoendelea na kama vingefanya hivyo hali isingekuwa kama ilivyo hivi sasa.

Alisema kutokana na kauli za kichochezi za Chadema, wanaostahili kulaumiwa ni Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kuwa chama hicho hakikuanza leo kuzurura na nyaraka za Serikali bila kuchukuliwa hatua.

"Kitendo cha chama hiki kupeleleza mwenendo wa vikosi vya ulinzi na kutumia taarifa za kijeshi katika majukwaa ya siasa limeonekana kuzoeleka na viongozi wenye mamlaka na dola wameshindwa kulikemea.

Dovutwa alisisitiza kuwa ifike wakati sasa kwa serikali kutazama mbele zaidi ili kunusuru maisha ya watanzania ambao alisema wamekuwa wepesi wa kulaghaiwa.


Dovutwa ataka CHADEMA ichukuliwe hatua za kisheria
 
Hivi hicho ki-Dovutua ndio ki-mdudu gani tena????

Wadau,nasikiliza redio hapa, taarifa ya saa 12 jioni hii, kwamba Dovutwa- mwenyekiti wa UDPD ameitisha press confernce na kutetea hatua ya Ridhiwani kutaka kuwapeleka court Dr Slaa na Mch Mtikila.....kaongea mengi, ila zaidi kawashangaa kushusha tuhuma za uwongo kwa Ridhiwani wakati wao ni zaidi ya wanasiasa, yaani ni watu wa dini,,,eti wasiongee kama 'watu wa mitaani'...
 
kinachomsumbua Dovutwa ni kujipendekeza na uislamu ulioibuka sasa nchini wa kuteteana hata mahali ambapo ukweli ni dhahiri. kama siyo kujipendekeza kwa nini kumsemea mtu ambaye kasema anaenda mahakamani? si aende ndo tujue ukweli na uongo? Tabia mbaya ya waislam ya kuteteana kwa kila kitu eti kwa sababu tu ni dini moja iachwe.kwa sisi tunaoelewa, uislamu ni dini ya haki na siyo kuteteana hata mahali ambapo ukweli haujawa dhahiri. tusubiri aende mahakamani kama anasingiziwa. na kumbuka yeye ni ofisa wa mahakama, ni wakili, acha atafute mkondo wa sheria. tuache tabia ya kuteteana bila legal ground na kushiriki dhambi za watu wengine.
 
Huyo hana msimamo kisiasa.
Wana-CCM ndiyo wanamsikiliza. Kwa nini asiweke strategy na Ridhiwani wake kuweka mawakili kuwasaidia iwapo wataamua kwenda mahakamani?
 
Anataka na yeye watu wajue kwamba yupo ndio maana anaongea pumba. Si ndio yule aliyesema kura zake apewe JK naona hana jipya.
 
Back
Top Bottom