Dovutwa amshambulia Dk. Slaa

Dovutwa haelewi anachoamini kabisa tukitrace historia yake kwenye siasa... Ila kwa leo,nilivyomwelewa hapa ni kama anakerwa na kile anachofikiri kuwa dr. Slaa anasympathize CCM inapofanya teuzi za hovyo na hivyo kuharakisha kifo chake. Nadhani yupo on track kwa kuwa angependa CCM ife kama UNIP, MMD, UPC n.k. kwamba itoweke isibaki hata traces. Kwa kuwa dhamira ya kauli yake ni dhidi ya CCM, anajidhihirisha ni mpinzani, ila hakumuelewa dr. alimaanisha nini aliposema vile. Hebu tulieni mtafakari hoja yake bila kulink mambo yake ya nyuma... Mnaweza kuona ukweli?
 
CCM ina mapapeti kibao!. Hajui kwa nini aligombea urais. Hata kura yake alimpa JK!.
 
ALIANZA WA CCK sasa DOVUTWA; Kwanini wasiitishe mikutano na Wananchi kwanza ? Waone na Wajue Matakwa ya Wananchi? Kuliko kurukia MPINZANI aliyejuu zaidi yao?

AU NDIO PAYBACK VYAMA VYAO HAVITAFUTWA na MZEE ? TOENI HOJA, TUELEZE SABABU yenu kuwa VYAMA!!!

Natafuta Utingo wa Daladala ya Ubungo Masaki.....Mpeni number yangu kilaza huyu..
 
[h=2]Wakati Dovutwa anasema Dkt. Slaa anamwogopa Lowasa; Godigodi amtaka Dkt. Slaa aache kuwaandama Lowasa, Chenge - Siasa jama, teh teh![/h]
Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa, amemshangaa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbrod Slaa, kutokana na uamuzi wake wa kutoa angalizo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Dovutwa alisema Dkt. Slaa hakupaswa kutoa angalizo hilo, kwani kufanya hivyo kunaonyesha wazi kuwa kiongozi huyo si mpinzani wa kweli na pia lengo lake ni kutaka CCM iendelee kubaki madarakani.

Dovutwa, ambaye aligombea urais mwaka 2010, amekosoa kauli ya Dkt. Slaa ambayo aliitoa hivi karibuni akiwa jijini Mwanza, akisema kuwa CCM inakufa kutokana na kushindwa kujisafisha na tuhuma za ufisadi kupitia uchaguzi wake wa ndani.

Dkt. Slaa alisema kuwa chama hicho kikongwe sasa kimeonyesha dalili za wazi za kifo, kwa kushindwa kuwaengua katika uchaguzi wa NEC, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Mbunge wa Bariadi Mgharibi, Andrew Chenge, ambao ni watuhumiwa wakubwa wa ufisadi, “Dk. Slaa hana dhamira ya dhati ya kutaka CCM iondoke madarakani, kama yeye anaona kurudishwa NEC kwa akina Lowassa na Chenge ndiyo kifo cha CCM hakupaswa kusema hayo. Alipaswa kunyamaza ili waweze kuishughulikia CCM na mwisho wa siku Chadema ishinde uchaguzi iingie Ikulu, lakini kwa maneno hayo ni sawa na kuifungua macho CCM, hivi wakisimamisha mtu strong (anayekubalika) CHADEMA itapitia mlango gani kuingia Ikulu?”

“Kauli ya Dkt. Slaa inashangaza na imevitia doa vyama vya upinzani, hii inaonyesha kumbe Dkt. Slaa anaogopa na hataki CCM ianguke mwaka 2015, swali la kujiuliza huyu bwana anamfanyia kazi nani? Nilitarajia Dkt. Slaa angefurahia CCM kuanguka ili CHADEMA iingie Ikulu, lakini yeye anasikitika CCM inakufa. Hivi CCM ikifa Dkt. Slaa anaathirika na nini hadi atoe angalizo? CCM inatakiwa kufa kama UNIP (chama) ya Kaunda ilivyokufa Zambia au MMD ya Banda ilivyokufa Malawi au UPC ya Obote ilivyokufa kule Uganda,” alisema Dovutwa.

Dovutwa alisema kuwa kauli hiyo inaonyesha kuwa Dkt. Slaa bado ana mapenzi na CCM, licha ya kujitoa katika chama hicho mwaka 1995, vinginevyo atoe ufafanuzi kuhusu mantiki ya kutoa hoja ya angalizo na kuishauri CCM.

Kwa mujibu wa Dovutwa, akiwa Mwanza Dkt. Slaa pia alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wakati akiwa bungeni aliwahi kumtaka Lowassa amtaje mtu aliyesababisha yeye awajibike kisiasa kwa kujiuzulu, ili kwa kufanya hivyo chama chake kiweze kumsafisha na tuhuma za ufisadi, “Kwa maneno haya, Dkt. Slaa alikuwa amejipanga kucheza mchezo mchafu baada ya Lowassa kumkatalia kumtaja huyo mtu, hii inaonyesha kuwa Dkt. Slaa anafanya siasa za chuki za kulazimisha,” alisema.

---
Hiyo ni habari kwa mujibu wa hgazeti la Mtanzania, Oktoba Mosi, 2012
---

MKURUGENZI wa Taasisi ya Islamic Peace Foundation (TIPF), Sadiki Godigodi, amemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, kuacha kumuandama Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa na Mbunge wa Bariandi Magharibi, Andrew Chenge.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Godigodi, alisema uamuzi uliofanywa na Kamati Kuu (CC), kuwaacha wanachama hao wagombee nafasi walizoomba ulikuwa sahihi hivyo Dkt. Slaa hakupaswa kuupinga.

Alisema kupitishwa kwa majina ya Lowassa na Chenge kutakiimarisha chama hicho, kujenga umoja na mshikamano kwani kama majina yao yasingerudi, kungetokea mpasuko mkubwa.

Aliwataka wana CCM kumpa ushirikiano Lowassa kwani dalili zinaonesha kuwa wapinzani wanamuogopa, “Watanzania wanaelewa jinsi alivyokuwa mchapa kazi hodari, amejituma sana pia ni mtu anayejitoa kwa watu na kuwapa misaada ya hali na mali,” alisema.

Godigodi aliongeza kuwa, Lowasa ni mfano wa kuigwa na anastahili pongezi kwa jinsi anavyojitoa kuisaidia jamii ya kada mbalimbali, taasisi za dini na binafsi, “Hivi karibuni alikabidhi msaada wa madawati 500 katika Shule ya Msingi Kipawa, hoja ya ufisadi inayotolewa na Dkt. Slaa hazina mashiko kwani suala la rada lilishatolewa maelezo na Serikali ya Uingereza sasa kama yeye anao ushahidi, kwanini asimpeleke mahakamani,” alihoji Bw. Godigodi.

Alisema wao kama taasisi na sehemu ya jamii ya Watanzania wanapongeza uamuzi mzuri uliofanywa na CCM kupitisha majina yao ili waweze kuwania uongozi na kumpinga Dkt. Slaa.

---
Habari kwa mujibu wa Anneth Kagenda via gazeti la Majira



Source: wavuti.com - wavuti

MENGI YATAJIRI MI SIUZI KURA YANGU, NA BIBI YANGU KAGUNDUA JANA KUA NYERERE SIO RAISI WA Tanzania....
 
CCM ngoma nzito wanamgwaya Dr Slaa mpaka wamechukua majeshi ya kukodi, mara Bakwata, mara vyama mfu mara mapandikizi ndani ya Chadema, mara polisi, TISS, Majaji wa makakama kuu, lakini yote bure hawawezi kuepuka kuondoka madarakani.
 
Unatakiwa kujua chama tawala cha Tanzania ni CHADEMA cauze CCM ,CUF ,UDP,NCCR MAGEUZI ,TLP,na vingine ni vyama vya upinzani cauze vinaipiga CDM vita hvyo sishangai
 
Tunafahamu Dovutwa ni ana chama maslahi. Ni pandikizi la Ccm. Ikumbukwe wakati wa kugombea urais alichukua hela za ruzuku halafu kaingia mitini. Siku ya siku akatokea akimwombea Kikwete kura.
Hata jana wakati anasoma tamko la kumlaumu Dr Slaa alionekana kusoma kitu ambacho hajakiandaa yeye. Huwezi kuandaa speech halafu unaidodosa kama hujui kilicho andikwa.
Kwa ufupi aliandikiwa na magamba yeye kaenda kuisoma.
Tunawajueni jamani! Kaeni kimya! Njaa zenu ndio mauti yenu.
 
Naikumbuka kauli ya Dovutwa 2010 "kama hamnipi kura mie basi mpeni Kikwete" huyo ndio mgombea wa upinzani.

dovutwa ni kilaza, anatoa kushoto anapeleka kulia, anatoa kulia anapeleka kushoto, anateleza kwa mlenda kwenye tiles! Dovutwa ni gamba kama yalivyo magamba mengine, na dr Slaa analijua hili ndo mana kampuuzia
 
Look who is talking.. WaBongo kwa unafiki hawajambo..Dovutwa mwaka 2010 aliondoa jina lake akisema kura zake apewe JK, leo amekuwa msemaji wa upinzani eeeh!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom