Dovutwa amshambulia Dk. Slaa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
JUMATATU, OCTOBA 01, 2012 04:59 NA KHAMIS MKOTYA

fahmi%20dovutwa%20-%20updp.jpg


Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa


MWENYEKITI wa Chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, amemshangaa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, kutokana na uamuzi wake wa kutoa angalizo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Dovutwa alisema Dk. Slaa hakupaswa kutoa angalizo hilo, kwani kufanya hivyo kunaonyesha wazi kuwa kiongozi huyo si mpinzani wa kweli na pia lengo lake ni kutaka CCM iendelee kubaki madarakani.

Dovutwa, ambaye aligombea urais mwaka 2010, amekosoa kauli ya Dk Slaa ambayo aliitoa hivi karibuni akiwa jijini Mwanza, akisema kuwa CCM inakufa kutokana na kushindwa kujisafisha na tuhuma za ufisadi kupitia uchaguzi wake wa ndani.

Dk. Slaa alisema kuwa chama hicho kikongwe sasa kimeonyesha dalili za wazi za kifo, kwa kushindwa kuwaengua katika uchaguzi wa NEC, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Mbunge wa Bariadi Mgharibi, Andrew Chenge, ambao ni watuhumiwa wakubwa wa ufisadi.

"Dk. Slaa hana dhamira ya dhati ya kutaka CCM iondoke madarakani, kama yeye anaona kurudishwa NEC kwa akina Lowassa na Chenge ndiyo kifo cha CCM hakupaswa kusema hayo.

"Alipaswa kunyamaza ili waweze kuishughulikia CCM na mwisho wa siku Chadema ishinde uchaguzi iingie Ikulu, lakini kwa maneno hayo ni sawa na kuifungua macho CCM, hivi wakisimamisha mtu strong (anayekubalika) Chadema itapitia mlango gani kuingia Ikulu?

"Kauli ya Dk. Slaa inashangaza na imevitia doa vyama vya upinzani, hii inaonyesha kumbe Dk Slaa anaogopa na hataki CCM ianguke mwaka 2015, swali la kujiuliza huyu bwana anamfanyia kazi nani? Nilitarajia Dk Slaa angefurahia CCM kuanguka ili Chadema iingie Ikulu, lakini yeye anasikitika CCM inakufa.

"Hivi CCM ikifa Dk. Slaa anaathirika na nini hadi atoe angalizo? CCM inatakiwa kufa kama UNIP (chama) ya Kaunda ilivyokufa Zambia au MMD ya Banda ilivyokufa Malawi au UPC ya Obote ilivyokufa kule Uganda," alisema Dovutwa.

Dovutwa alisema kuwa kauli hiyo inaonyesha kuwa Dk. Slaa bado ana mapenzi na CCM, licha ya kujitoa katika chama hicho mwaka 1995, vinginevyo atoe ufafanuzi kuhusu mantiki ya kutoa hoja ya angalizo na kuishauri CCM.

Kwa mujibu wa Dovutwa, akiwa Mwanza Dk. Slaa pia alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wakati akiwa bungeni aliwahi kumtaka Lowassa amtaje mtu aliyesababisha yeye awajibike kisiasa kwa kujiuzulu, ili kwa kufanya hivyo chama chake kiweze kumsafisha na tuhuma za ufisadi.

"Kwa maneno haya, Dk. Slaa alikuwa amejipanga kucheza mchezo mchafu baada ya Lowassa kumkatalia kumtaja huyo mtu, hii inaonyesha kuwa Dk. Slaa anafanya siasa za chuki za kulazimisha," alisema.


 
ALIANZA WA CCK sasa DOVUTWA; Kwanini wasiitishe mikutano na Wananchi kwanza ? Waone na Wajue Matakwa ya Wananchi? Kuliko kurukia MPINZANI aliyejuu zaidi yao?

AU NDIO PAYBACK VYAMA VYAO HAVITAFUTWA na MZEE ? TOENI HOJA, TUELEZE SABABU yenu kuwa VYAMA!!!
 
Dovutwa ni kibaraka cha magamba..anaishi mjini hapa kwa msaada wa magamba.chama chake ndio ASSET yake.
 
watakupinga dovutwa ila mioyoni mwao wanajua umetoa hoja ya msingi sana
 
Huyu hastahili kujadiliwa hapa jamvini abakie huko huko popo bawa yalipo makao makuu ya hako ka-NGO kake.
 
Umri nao ni tatizo kwenye siasa sasa ndo mtaanza kumwelewa zitto alikuwa ana maanisha nini
 
Huyu jamaa alinikuna sana kipindi kile cha uchaguzi alipodai eti akichagulia kua Raisi atajenga Kiwanda cha Silaha!
 
Davutwa ! malayaa Mujarabu wa Siasa ! hahahaaah , Mtu ambae hata mamake Mzazi hajui chama anachoongoza . . . .

Takataka huyu , tupa kule
 
Mzee Dovutwa hafai hata kuwa Mjumbe wa nyumba kumi,ufahamu wake ni mdogo sana alishindwa hata kuchangia kwenye kipima joto anaulizwa hivi yeye anajibu vingine.Hivi anafanyaga kazi gani tofauti na uenyekiti wa chama
 
Mimi binafsi sitaki ccm ife nataka ibakie kuwa chama cha upinzani ili waone maendeleo japo nchi iwe safi tu .....dar mvua ikinyesha maji yasijae mjini kama mto ruvu
 
Huu ujinga sijui utaisha lini, yeye badala ya kuongelea sera za chama chake ili ajaribu tena uraisi 2015 anakwenda kutumiwa kumzungumzia Dr Slaa.

Watu wengine ni wakubwa kiumri lakini kichwani bure kabisa!
 
ALIANZA WA CCK sasa DAVATWA; Kwanini wasiitishe mikutano na Wananchi kwanza ? Waone na Wajue

Matakwa ya Wananchi? Kuliko kurukia MPINZANI aliyejuu zaidi yao ?

AU NDIO PAYBACK VYAMA VYAO HAVITAFUTWA na MZEE ? TOENI HOJA, TUELEZE SABABU yenu kuwa VYAMA!!!

Hivi yulle kiongozi wa chama cha upinzani aliyesema kura zake za urais uchaguzi 2010 apewe Kikwete ,alikuwa nani vile nimesahau .naomba umnikumbushe
 
Mimi nlijua tu kuwa hii kauli ya dr slaa ama itaeleweka vinaya au itatafsiriwa vibaya na watu wenye akili kama dovutwa...
kauli aliyotoa dr slaa ni sahihi na ni ya kisiasa kwa maana kuwa kubeza teuzi za ccm...which is right...
au dovutwa alitaka dr slaa awapongeze ccm???
kwanza kabisa dovutwa hivi sio wewe ulijitoa dk za mwisho na kuwaambia wapiga kura wako wampigie JK? wewe ni mpinzani kweli?

i hate wanafiki wanaotafuta maslahi binafsi.
hivi nyie wapinzani gani kila siku mnashambuliana wenyewe kwa wenyewe? kila siku chadema...
dont you see the monster ahead of you????
come on.
 
Kama kuna wafia tumbo mashuhuri hapa duniani basi Dovutwa ni mmojawapo. Sijui kama kumbukumbu zangu ziko vizuri au lah, lkn huyu mgagagigikoko aligombea urais kwa tiketi ya UPDP kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 na siku chache kabla ya siku ya kupiga kura alitangaza kujitoa na kuwaomba wafuasi wake waelekeze kura zao kwa Kikwete kwani ukiondoa CCM (kwa mtazamo wake) hakuna chama kingine chenye sera nzuri.

Kinachonishangaza ni kumuona leo hapa kesho pale akidandia dandia mambo yanayowahusu watu ambao siyo level yake. Huyu na yule mwenzake Hashim Rungwe ni kichefuchefu cha uwani kwa kweli.
 
Dovutwa alishindwa kabisa kujenga hoja kwenye malumbano ya hoja ITV wiki iliyopita. Mwongoza kipindi alijitahidi kumrejesha zaidi ya mara 3 akashindwa. Sisi tunajadili madara ya Rais, yeye anajadili muungano. Akatolewa hewani kwa nguvu.
Hoja hii ilivyojengwa vizuri kiufundi lazima amelishwa, si yake nina uhakika. Safari ya ukombozi ni ndefu lakini tutafika.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom