DOUBLE STANDARDS ZA CHADEMA, Lwakatare angekuwa kiongozi wa CCM wangeandamana kushinikiza ajiuzuru

Mh Lowassa, Mzee Mwinyi, Mh Mrema...
Mrema hakujiuzulu bali alifukuzwa Uwaziri na Mwinyi ndio akaamuwa kuhama CCM, Lowasa alifukuzwa na Bunge, kajipange upya naona dose ya Dr Pauline bado haijakusaidia, wewe unahitaji mtu kama Dr Murray akupe over dose ukajifie Uyole kabisa.
 
Matola zamani nilikuwa nakuona kama Great thinker lakini kwa sasa nazani umezeeka sana kiasi kwamba unakosa memory.
Mrema na Mzee Mwinyi walijiuzuru baada ya kashfa ya mauaji ya vikongwe kule shinyanga miaka ya themanini, wakati huo Mrema alikuwa usalama wa taifa na Mzee Mwinyi alikuwa waziri wa mambo ya ndani. Pia Mheshimiwa Llowassa alijiuzuru baada ya nafasi yake na tena alijiuzuru nafasi kubwa ambayo ukiacha Mwl Nyerere kustaafu kwa hiari Urais ni Lowassa pekee ambaye ameweza kuachia wadhifa mkubwa kabisa serikalini kwa hiari.
Hivi kwa staili hii ya Chadema si tutakuja tawaliwa na ma dictators ambao ukiwanyooshea kidole watakuua??
 
Ndugu Zanguni

Nimesoma barua ile iliyowekwa hapa ikidaiwa kuwa imeandikwa na Mh Zitto na pia nimesoma maelezo yake hapa leo na kushangazwa sana na hizi double standards za CHADEMA , chama ambacho ndio kikubwa cha upinzani nchini na ambacho tunategemea ndio kiwe cha kwanza kutuonyesha mfano kuwa wakipewa dola watafanya nini pale viongozi wao wakiharibu au kukumbwa na kashfa yoyote inayohitaji uchunguzi wa polisi.

Wote tunajua kuwa ikitokea kashfa sehemu fulani ndani ya serikali CHADEMA huwa ni wa kwanza kushinikiza mhusika ajiuzuru au asimamishwe kupisha uchunguzi jambo ambalo na mimi nakubaliana nalo kwani huwezi kumchunguza mtuhumiwa wakati bado ni kiongozi. Ili uchunguzi uwe wa huru na haki inabidi muhusika asimamishwe kupisha uchunguzi huo ili asiwe na nafasi yoyote ya kuweza kuharibu ushahidi au kuwanyima nafasi wapelelezi kufanya uchunguzi wa kina kwa kumuonea aibu au huruma. Uchunguzi/upelelezi ukiisha basi hatima yake ndio itajulikana.

Sasa leo chadema wanashindwa kumsimamisha kwa muda Kiongozi wao na wanapinga kwa nguvu zote kuwa ameonewa, Hivi ikija kuonekana kuwa huyo kiongozi ana hatia tutawaelewaje? Kesho mtawezaje kuwanyooshea kidole CCM pale watakapoonekana wana kashfa?

Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi mazito kama aliyochukua Mh Lowassa pale alipojiuzuru uwaziri mkuu.

Ndugu yangu umetumia dose uliyopewa na Dr? au dawa zimekushinda?
 
Ushuri wa buure hubiri mafanikio ya serikali ya chama chako kipya sio kufuatilia mambo ya mumeo wa zamani hiyo inakufanya uonekane mjinga na ----- tu.......again "unafikiri kwa kutumia tumbo lako na si akili yako"
 
Kwani umesikia kuwa CDM wanafanya uchunguzi kuhusu swala la Lwakatare? Uchunguzi unafanywa na serikali na wameshagundua kuwa ana kesi ya kujibu ndio maana wamempeleka Mahakamani. Sasa ajiuzulu ili iweje? CDM hawana shida na Lwakatare wana shida la CCM na hawa askari uchwara wnaotengeneza kesi ili CDM wakataliwe na wananchi. Wewe ni mmoja wa watu wanaofaidika na udhalimu huu. Muda utafika utajikana Mwenyewe. Lukosi nashukuru Mungu kwa wewe kuongozwa na Mungu urudi CCM kwani shetani alikushauri uhamie CDM ili uvuruge lakini kwa sababu CDM iko na Mungu, umefail.
Shame on you
 
Dr. Slaa ameruhusu barua ya Zitto uvuje kwa makusudi.

Kama kuna mtu anayetakiwa kuwajibika kwa kujiuzuru ni Dr. Slaa kwa kushindwa kutunza siri za ofisi yake.

Acha kumbwelambwela...hoja za Fesibuku unazileta huku. Na kwa nini tusiseme kwamba ni Zitto ndiyo alishindwa kutunza siri? Kwa waliohusika na hiyo barua ni wangapi? Sender (Zitto) na Receiver (Katibu Mkuu). Acheni longolongo..mmeshikwa kila mahali; hamuwezi kupumua
 
Slaa ndio anayetunza makaburasha. Siri za chama zikivuja anapaswa kuwajibika...
 
Hata kama utakuwa gaidi kama upo Chadema wewe ni shujaa.
 
Matola zamani nilikuwa nakuona kama Great thinker lakini kwa sasa nazani umezeeka sana kiasi kwamba unakosa memory.
Mrema na Mzee Mwinyi walijiuzuru baada ya kashfa ya mauaji ya vikongwe kule shinyanga miaka ya themanini, wakati huo Mrema alikuwa usalama wa taifa na Mzee Mwinyi alikuwa waziri wa mambo ya ndani. Pia Mheshimiwa Llowassa alijiuzuru baada ya nafasi yake na tena alijiuzuru nafasi kubwa ambayo ukiacha Mwl Nyerere kustaafu kwa hiari Urais ni Lowassa pekee ambaye ameweza kuachia wadhifa mkubwa kabisa serikalini kwa hiari.
Hivi kwa staili hii ya Chadema si tutakuja tawaliwa na ma dictators ambao ukiwanyooshea kidole watakuua??

---- of the day! Lowassa alijiuzulu mwenyewe? Ni kweli unaumwa, na tiba ilitolewa na Dkt Paurine lakini umeipuuzia. Kwa taarifa yako, Lowassa alijiuzulu kwa kuwa alikuwa implicated moja kwa moja na sakata la Richmond. Kamati teule ilipendekeza apime uzito wa tuhuma na aamue mwenyewe. Na hata wachangiaji wa findings and recommendations za kamati ile Teule (mfano Ole Sendeka) walishinikiza ajiuzulu. Kama alijiuzulu kwa kupenda, kwa nini aliendelea kulia lia kwa kuona kuwa AMEONEWA? AMEDHALILISHWA? AMESIKITISHWA? Kama alikuwa INNOCENT si angeamua kukomaa mpaka mwisho?
 
Mimi nadhani kama kweli mna wataalam wenu na nyinyi mngefanya uchunguzi kuliko kumtetea wakati nyie wenyewe hamjui ukweli ukoje

Kilio cha CHADEMA siku zote ni watuhumiwa kufikishwa mahakamani...na hata Lwakatare walisisitiza afikishwe mahakamani...
Kama mtuhumiwa,tuhuma zake hazimpeleki mahakamani moja kwa moja kama JAIRO au WAZIRI KAWAMBWA inabidi kujiuzulu kupisha uchunguzi!
Kwa suala la Lwakatare hiyo itakuwa fujo kupishana na polisi kufanya uchunguzi...ndio maana hata CUF wamewaachia polisi huko Zanzibar...
Mbona yule mbunge wa bahi (CCM) ajajiuzulu...na hujalisimamia hili kuwa kama chama mfanye uchunguzi wakati akiwa kajiuzulu..na badala yake mmewaachia polisi...
ONDOA BOLTI KWANZA....
 
Acha kumbwelambwela...hoja za Fesibuku unazileta huku. Na kwa nini tusiseme kwamba ni Zitto ndiyo alishindwa kutunza siri? Kwa waliohusika na hiyo barua ni wangapi? Sender (Zitto) na Receiver (Katibu Mkuu). Acheni longolongo..mmeshikwa kila mahali; hamuwezi kupumua

CHRIS MKOSI NAONA BAADA YA KUPEWA DIAGNOSIS YA MAGONJWA YANAYO KUSIBU UNAJITAHIDI SANA UONEKANE WA MAANA. MIE NAPITA TUU. ILA HABARI NDO HIYO , HIVO JITAHIDI KUUZA SURA KWENYE MTANDAO KWA ID NYINGI. LILO WAZI NI KUWA HUTABADILISHA UKWELI KUWA WALIKUTOA NDUKI. NA KWELI KAMA NAWE UNAJIITA GREAT THINKER, NAONA KWANINI ULITIMULIWA HUKO. MAANA UNATIA KINYAA, " JARIBU KUWA SENSIBLE LAU MARA MOJA !!!! YANI POVU LAKO LIME VUNJA UNGO!!!!. ANYWAY FOR THE DAY!!!!

Wabaya wa CHADEMA wavurugana

na Mwandishi wetu

SIKU moja baada ya Mkurugenzi wa Mambo ya Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu kufichua njama zinazofanywa ili kutengeneza ushahidi wa uongo kwa ajili ya kuutumia katika kesi ya ugaidi inayomkabili Wilfred Lwakatare, baadhi ya wahusika wameanza kuvurugana.

Kwa mujibu wa Lissu, njama hizo zinafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na ujasusi ili kutumia ushahidi huo mahakamani dhidi ya Lwakatare ambaye ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA.

Alisema kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA wa Idara ya Ulinzi na Usalama wanaopewa fedha na kuahidiwa kufundishwa namna ya kuzungumza katika kesi hiyo ya Lwakatare.

Lissu alisema kuna baadhi ya vijana wakiongozwa na Saumu Mulugu ambaye alifukuzwa kazi CHADEMA mwanzoni mwa mwaka jana, wamepokea fedha kutoka kwa kigogo mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa) ili kufanikisha mpango huo.

Jana gazeti hili lilimnasa Saumu akiwa anawasiliana na wenzake, huku akiwatuhumu baadhi yao kuwa ndio waliovujisha siri kwa Lissu.

Vile vile alionekana akiwasiliana na kigogo mmoja wa CCM ambaye alikuwa akimwita ‘mkuu’ huku akimsomea baadhi ya taarifa zilizoandikwa magazetini jana kuhusu kuvuja kwa siri zao.

Saumu akiwa katika grosari maarufu kwa jina la Kwa Kimaro jirani na eneo la Benki Kuu ya Damu Salama Mchikichini jijini Dar es Salaam, alisikika akiwalalamikia wenzake kwa kumsaliti na kuvujisha mkakati wao kwa Lissu.

“Kwanini mmelikisha siri zetu kwa Lissu hadi amejua tulikutana katika hoteli ya kifahari na Mwigu? Sasa nitawaonesha, maana laki tano zenu ninazo mimi. Siwapi bali nitazitumia kujilinda,” alitamba.

Saumu ambaye alikuwa akizungumza kwa sauti kubwa ya ghadhabu kupitia simu, aling’aka: “Nyie kwanini mmeniuza kwenye ishu ambayo tumeipanga wote?”

Baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa ‘mkuu wake’ aliendelea kupiga simu akimlalamikia mtu ambaye hakumtaja, kuwa alikuwa amezima simu yake makusudi kwa kuwa ndiye alivujisha siri zao kwa CHADEMA.

“Mimi sitakubali na nimehakikishiwa na bosi wetu kuwa huyo aliyetusaliti tutatumia wale askari kumwekea hata unga. Haiwezekani fedha tumepokea za kwanza, za pili na tatu kwanini tuuzane dakika za mwisho?” alidai Saumu huku akiendelea kugida bia yake.

Huku akihaha huku na kule, Saumu alikuwa akiwapigia simu baadhi ya madereva wa CHADEMA makao makuu na kuwaomba simu za baadhi ya watu, na hata wakati mwingine kuwafokea akidai ndio waliofichua siri hiyo.

Hata hivyo, baada ya kutilia shaka nyendo za chanzo chetu kudaka siri zake, ghafla alitokomea na kuzima simu zake mara moja kwani hata alipotafutwa baadaye hakupatikana.

Katika madai yake, Lissu alisema hadi sasa vijana hao wameshapewa sh 400,000 ili wakubali kwenda kufundishwa jinsi ya kuzungumza mahakamani kuwa CHADEMA ni chama cha kigaidi, kwamba Lwakatare alipanga mikakati ya kigaidi.

“Awali walipewa 400,000, wakapewa tena 300,000, pia wakapewa 35,000 mara mbili. Na fedha zote hizi walikuwa wanapewa kwa njia ya M-Pesa,” alisema Lissu.

Alidai kuwa Saumu ndiye anayeratibu mpango wote kati ya Jeshi la Polisi na vijana hao wa CHADEMA kwa kuwarubuni kwa fedha.

Alisema vikao baina ya vijana hao wa CHADEMA na Saumu vimewahi kufanyika mara kadhaa katika moja ya hoteli maarufu nchini juu ya mambo ya kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari au mahakamani kwenye kesi ya Lwakatare.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba hakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo kama anahusika nazo kwa namna yoyote.
 
Matola zamani nilikuwa nakuona kama Great thinker lakini kwa sasa nazani umezeeka sana kiasi kwamba unakosa memory.
Mrema na Mzee Mwinyi walijiuzuru baada ya kashfa ya mauaji ya vikongwe kule shinyanga miaka ya themanini, wakati huo Mrema alikuwa usalama wa taifa na Mzee Mwinyi alikuwa waziri wa mambo ya ndani. Pia Mheshimiwa Llowassa alijiuzuru baada ya nafasi yake na tena alijiuzuru nafasi kubwa ambayo ukiacha Mwl Nyerere kustaafu kwa hiari Urais ni Lowassa pekee ambaye ameweza kuachia wadhifa mkubwa kabisa serikalini kwa hiari.
Hivi kwa staili hii ya Chadema si tutakuja tawaliwa na ma dictators ambao ukiwanyooshea kidole watakuua??
Wewe fani yako ni kuropoka tu na kuimba taarabu hakuna unalolijuwa Nyerere alishaachia Uwaziri mkuu Akachukuwa nafasi Kawawa najuwa kwa umri wako na akili zako huweza kulifahamu hili.

Pili Lowasa ni Waziri Mkuu aliyeondolewa na Bunge, kama akili zako umezifungia kabatini hiyo ni hiyari yako. na Mrema alifukuzwa kazi ya Uwaziri na Mwinyi Period.

Habari ya Usalama wa Taifa haina uhusiano wowote na politics status. acha kutuchanganyia habari hapa.
 
Wewe unachokumbuka ni Mrema kufukuzwa Uwaziri lakini hukumbuki kuwa Mrema alijiuzuru pale mauaji ya vikongwe yalipotokea.
Katika wapinzani ambao naweza kuwapa kura zangu ni Mh Lyatonga Mrema mzee wa siku saba
Chadema bado sana
 
Back
Top Bottom