Double-standards ya serikali na Jeshi la Polisi

Joss

JF-Expert Member
May 28, 2009
765
191
Dr. Kitila Mkumbo kushitakiwa na Serikali kwa kutoa lugha ya matusi katika mkutano wa hadhara.

Livingstone Lusinde kutoshitakiwa kwa kutoa lugha ya matusi katika mkutano wa hadhara/ kampeni.

Tunaposema polisi wapo kwa maslahi ya ccm na kukandamiza upinzani,ni kama hivi. Kama kweli polisi wanatenda haki, kwanini mmoja ashitakiwe mwingine aachwe?

Kutoka gazeti la Mwananchi:

Waandishi Wetu
VIGOGO watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema); Mshauri wa chama hicho Dk Kitila Mkumbo na madiwani wawili, wametiwa mbaroni wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali.

Wakati Dk Mkumbo ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida, akituhumiwa kutoa lugha ya matusi kwa mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi (CCM), Mwigullu Nchemba, Diwani wa Kata ya Mabogini Wilaya ya Moshi, Albert Msando na Alex Umbella wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki, wamehojiwa na polisi kwa makosa ya jinai.

Dk Mkumbo amepandishwa kizimbani jana akiunganishwa katika kesi inayomkabili Ofisa wa Sera na Utafiti wa chama hicho kikuu cha upinzani, Mwita Waitara Mwikwabe (37).

Mwanasheria wa Serikali, Maria Mudulugu alidai mbele ya Hakimu Ruth Massamu kuwa, Julai 14 mwaka huu saa 10.00 jioni, mshtakiwa Dk Mkumbo alitoa lugha ya matusi dhidi ya mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi.

Mwanasheria aliiambia mahakama kuwa, Dk Mkumbo alitamka kuwa mbunge huyo ni malaya, mzinzi na ni 'the comedy' (msanii), huku akijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.
............

 
''We know through painful experience that freedom is never voluntarily given by the oppressor; it must be demanded by the oppressed"
 
Back
Top Bottom