Dondoo za majina ya wabunge wanaoibia TANESCO

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
1.jpg
images



Kitendo cha shule zinazomilikiwa na Mchungaji Rwekatare kuhusishwa na kashfa ya kuiba unit za Luku Tanesko ni jambo la kushtusha, na pengine kuna mengi zaidi kwa wakubwa uchunguzi ukifanyika, huyu ni dagaa tu.

Mmiliki wa shule hizo akiwa Mbunge na mchungaji ingawa haimhusinshi moja kwa moja au hajatajwa wazi wazi, lakini ananaswa na kitanzi cha umiliki wa shule hizo, jambo ambalo alitakiwa kuwa na uangalifu wa hali ya juu kufuatili matumizi na mapato ya shule zake kwamba hayawezi kuleta utata wo wote, na hata bodi za shule hizo zimeshindwa kufuatilia kinachoendelea kuliibia shirika la umeme mapato.

Mbunge ambaye ana tenda ya kuuzia TANESCO matairi ya magari si kazi kumpata, tuvute subira kwani ataanikwa na wajuaji soon hapa jamvini. Huyo ana kashfa nzito zaidi kuliko Rwakatare.

Kwa vyo vyote wabunge ambao wametoka kifua mbele kutetea hatua za Waziri wa Nishati na Madini kusafisha shirika kuna kila dalili za kuhusika na ufisadi ndani ya shirika hili, wengi wao ni wajanja wajanja ambao hutumia njia za panya ili wasishikwe kirahisi, lakini zipo njia nyingi tu za kuwanasa, moja wapo kauli zao zimeshawatilia doa tayari kabla utafiti haukajamilika, ingwa wamejenga utetezi wa kwamba walitetea taratibu zifanyike.
 
Uogzo kila mahala na hata wabunge wa upinzani kuhusishwa nani wa kumnyoshea kidole mwezake?
 
Naomba kuuliza, hao wabunge pichani kwenye gazeti la mtanzania ndio wanaotuhumiwa kwa kula mlungula au?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Inamaana Mnyika anahusika kwenye huo uchafu?Au Mimi ndo simjui Mnyika vizuri
 
Naomba kuuliza, hao wabunge pichani kwenye gazeti la mtanzania ndio wanaotuhumiwa kwa kula mlungula au?


  • Hapana, ni wale wanaohusika katika kujadili jambo hili bungeni akiwapo mmoja wapo Mnyika ambaye aliibua madudu mengi tu.
  • Picha ya pili ya mchungaji Rwakatale anahusika kutokana na kashfa ya shule anazozimilika kuhusika na kuiba unit za luku. Baadhi ya wabunge hao wamo kwenye ile kamati ya nishati na madili ambayo jana ilivunjiliwa mbali.
  • Hata hivyo wanaweza baadhi kuhusika na kashfa hii kutokana na kunyoshewa kidole bungeni kwamba baadhi wanahusika na kulihujumu shirika kwa njia mbalimbali ikiwepo rushwa ili kuwakingia kifua bungeni na kwenye kamati.
 
Inamaana Mnyika anahusika kwenye huo uchafu?Au Mimi ndo simjui Mnyika vizuri

Nakumbuka kama Nyika yupo kwenye kamati ya nishati na madili kama sijakosea nisahihisheni ndiyo iliyovunjiliwa mbali jana kutokana na kashfa hizi.
NB: Kuvunjwa kwa kamati ya nishati na madini haimaanishi kila mwanakamati anahusika na kashfa hiyo, ila ni baadhi tu, lakini kwa sasabu ya kuijenga upya kwa ajili ya kutoa uozo wote wanawajibika, kwani walifanya kazi pamoja na madudu hayo wanayajua, kwa nini hawakuyaibua?
 
inawezekana mkuu, always remember that never trust politician especialy thos of 3rd world countries.


Sikuamini kinachoendelea Zitto alipoamua kumkingia kifua Mhando wakati bodi na wazirwameona uozo uliopo. Angefanya hivyo baada ya kufanya utafiti wa kutosha, sasa angalia waziri alivyowaumbua kuwa kukokotoa madudu ya Mhando na kuwavua nguo baadhi ya wabunge. Wamebaki uchi mbele ya hadhara.
 
Wiki iliyopita niliandika hapa kuwa kuna siku mtanikuta naandamana peke yangu kwa sababu nimechoka kusikia haya mambo ya rushwa, ufisadi na kila aina ya uovu. Nasikitika hata watumishi wa Mungu wanatajwa katika sakata la wizi wa umeme, sasa tutaponea wapi??? Kumbe utajiri wa wengi sio halali ni ujanja ujanja tu, na kumbe ni wizi mtupu!!!

Sasa tunawapeleka kwenye kamati ya uongozi na maadili na kwa CAG ni kwanini wasipelekwe rumande halafu uchunguzi uendelee sawasawa na mwizi wa Kuku au kibaka wa pale mtaa wa Kongo.


Kama sio hivyo basi kuna tatizo katika system yote all are lost, we need God!!!!
 
I wish bunge letu sikuzote lingekuwa active kama lilivyofanya katika jambo hili, natamani uchunguzi huo ufanyike haraka na kufata haki ili wahusika/watuhumiwa wote watiwe hatiani na wahukumiwe kwa adhabu kali, na hili lisiishie hapa bali kwa tuhuma zote! lakini napata shaka... tatizo letu kubwa kesi za wanasiasa siku zote huishia kwenye kuchunguza... tujiulize wakina Lowasa, Karamagi na Msabaha nini kiliendelea???? Kina Blandina Nyoni nini kiliendelea???? Jairo kapewa adhabu gani????????
 
Wizi ni wizi tu hata kama unajipakaa rango ua tamzanite. Wizi unaoendana na utanganyifu ni hatari sana, wote akina Rwakatari haijalishi ni mchungaji afungwe pingu na kushindishwa mahabuhu Ukonga wakati kesi ikiendelea.

Yule Mbunge aliyeuzia TANESCO matairi mabovu apelekwe Gereza la Keko aonje harufu mbaya ya kule kando ya mifereji ya keko Magurumbasi.

Wengine watafuata.
 
Ze comedy tu hamna lolote! Subiri uone! Unaweza kiambiwa hata Nyumba ya spika hailipiwi bill
 
Mama mchungaji dokta askofu mkuu rwakatare wajibika mama achia nyazifa zako kuonyesha ukomavu wako mbele za Mungu na jamii.
 
Ze comedy tu hamna lolote! Subiri uone! Unaweza kiambiwa hata Nyumba ya spika hailipiwi bill

Yes! Kuanzia serikali ya mapinguzi Zanzibar ni wadaiwa wakubwa ambao ndio wanaolikosesha shirika la TANESCO mapato ya mabilioni kila mwezi. Nashangaa bungeni wamerukwa hao wanaofikiria wabara tunafaidika na Muungano wakati tunanyonywa.
 
Mama mchungaji dokta askofu mkuu rwakatare wajibika mama achia nyazifa zako kuonyesha ukomavu wako mbele za Mungu na jamii.

Subirini waangalie na kodi nyingine kama analipa kwani anaweza kuwa mkwepaji mkuwa sana wa kodi kwa kisingizio cha wadhifa wa uchungaji na uaskofu.
 
Back
Top Bottom