Dollar versus Shilling

Arsenal

Senior Member
Aug 12, 2008
190
71
Wakuu naomba kuuliza ivi kubandika bei ya bidhaa au services in us dollars but you pay in Tanzanian shiilings na pia kubandika bei ya bidhaa au services in Tanzanian shilling na you pay in Tanzanian shilling vina athari au uzuri gani katika uchumi?
 
Hii tanzania inanikera siku hizi kila kitu wanauza kwa dollar sijui ni ushamba au nini dolla yenyewe inakwenda chini kila siku leo inanunuliwa kwa 114,155.91 na kuuzwa kwa 116,462.09(BOT)
Huu niuite ulimbukeni au ni ushamba wa dollar kuanzia kwenye pango za nyumba ni dollar tu tutakuja kuuziwa chupi kwa dollar
 
Tafadhali Mr. YO YO kama unafahamu msaidie, maana haujagusa anapotaka. Mimi sifahamu kwa kweli, watakusaidia wanaofahamu
 
Bank kuu ya Tanzania (BOT) ndiyo inayotowa miongozo ya matumizi ya fedha. Wanashindwa kuzuia kwa sababu BOT ndiye cashier wa Serikali. Zinapotakiwa pesa kuhudumia mkutano mkuu wa UVCCM zinatoka kwa haraka. Zinapotakiwa pesa za shoping nje ya nchi vimemo vinapelekwa kwa cashier na pesa hutolewa bila matatizo.

Kazi ya BOT ni kuhakikisha sarafu ya tanzania ndiyo inayotumika kwa matumizi yote ya ndani, sina hakika kama kuna sheria yenye adhabu kwa wanaokiuka taratibu za matumizi ya sarafu ambayo siyo ya Kitanzania.
 
Wakuu naomba kuuliza ivi kubandika bei ya bidhaa au services in us dollars but you pay in Tanzanian shiilings na pia kubandika bei ya bidhaa au services in Tanzanian shilling na you pay in Tanzanian shilling vina athari au uzuri gani katika uchumi?

Arsenal,

Athari za kiuchumi zitategemea na uwingi wa wauzazi wanye tabia hiyo au(na) umuhimu wa bidhaa au huduma wanazozitoa katika uchumi au shughuli za kimaendeleo.

Wanaobandika bei katika $USA, na kupokea sh: Hawa kama ni wengi na (au) bidhaa/huduma zao ni muhimu katika kuendesha uchumi, wanaweza ku-distabilize bei ya dola dhidi ya shilingi na hivyo kusababisha kupungua kwa pato la taifa (other factors held) na kupanda holela kwa bidhaa (inflation). Kwa mantiki kwamba wanalazimisha wateja kununua $USA kwa bei isiyowiana na ya soko. Kwa mfano bei ya petrol ikiwa katika dola wakati petrol stations zinapokea Tz shs, automatically kila petrol station itakuwa 'beaural de change' kwa sababu mteja akijaza mafuta lazima kuwe na convertion kutoka $USA kwenda Tz sh. Matokeo yake bei ya mafuta itakuwa inapanda kituo hadi kituo, huku wenye vituo wakifaidika. Na kwasababu mafuta ni muhimu katika shughuli za uchumi, bidhaa nyingine zitapanda bei in response, hivyo kusababisha mfumuko wa bei.

Sambamba na hili, in the long-run, wateja wa mafuta watagundua kwamba wanaibiwa katika convertion kutoka $USA kwenda Tz shs, na watagundua kwamba ni bora walipe kwa $USA kama ilivyobandikwa. Hivyo basi kabla hawajaenda katika vituo vya mafuta watanunua dola, na kadri dola inavyonunuliwa kwa wingi ndivyo Tz sh inavyopoteza thamani na kuongeza mfumuko wa bei mara dufu. Kana kwamba haitoshi, $USA zikijaa mitaani imports zitaongezeka na hivyo kupunguza pato la taifa (other factors at constant)

Wanaobandika bei katika Tz sh, na kupokea Tz shs: Hawa ni wazalendo wanaotakiwa kuigwa. Kwasababu wakifanya kinyume chake wanasababisha hayo niliyoyasema hapo juu.
 
Leo ni Dollar kesho itakuwa Euro.

Nadhani ni kutaka kufanya biashara na ionekane bei ni ndogo. Maana ukitaja dola 500 inaonekana ndogo kuliko kutaja Tshs 600,000

Zimbabwe majuzi tu wameondowa tufuri tisa kama si kumi katika sarafu yao ili pesa ionekane ndogo, bilioni moja ya zamani ni sawa na dola mpya ya Zimbabwe moja. Iko siku kwetu napo wataondowa masufuri ili sarafu iwe inapendeza kuliko hivi sasa. Jirani zetu Uganda wamewahi kuondoa sufuri tatu tatu mara kadhaa pia.

So nadhani kuweka pesa in dollars na kulipia in Tshs ni kuipamba na kuisitiri sarafu yetu isionekane ina masufuri mengi.
 
Sababu ya kubandika bei kwa dolla naamini ni relative stability ya dollar Vs Shilling, ("historicaly at least") wanaogopa kwa mfano shilling ikiporomoka thamani kama Zim Dollar watapata hasara. Labda pia inakua rahisi kwenye mambo ya accounting kama ni multinational company.

Sidhani kama ina athari kiuchumi, labda uzuri wake ni inaongeza efficiency kunakua hakuna haja ya kubadili bei kila saa ("kama shillingi inaflactuate"), so wanaavoid cost associated with that.
 
Naona wachangiaji tumetunga swali tunaoloona linajibika. Alienzisha mada hii ameuliza athari za kiuchumi, hakuuliza sababu za kubandika bei kwa dola na kupokea shilingi. Ni bora tukabaki kwenye mada na ku-focus kwenye swali tuliloulizwa hapa chini.

Wakuu naomba kuuliza ivi kubandika bei ya bidhaa au services in us dollars but you pay in Tanzanian shiilings na pia kubandika bei ya bidhaa au services in Tanzanian shilling na you pay in Tanzanian shilling vina athari au uzuri gani katika uchumi?
 
Mwanzoni watu wakiweka bei za bidhaa na services katika US Dollar kwa sababu ya kutokuwa na imani katika umadhubuti wa shilingi, hasa katika viwango vya kubadilisha fedha ukilinganisha na fedha za kigeni kama dola za Kimarekani.

Siku hizi ambapo dola inashuka, hii imekuwa siyo swala kubwa sana, imebaki kwa maoni yangu kwa sababu katika mipango ya muda mrefu, bado dola ya kimarekani inaonekana kuwa madhubuti zaidi ya shilingi, lakini vitu vingine vinavyopangiwa dola haviko katika mahesabu ya muda mrefu, na kwa kweli katika wakati huu ambao dola ya kimarekani inaweza kuwa inashuka thamani kwa kasi na kusababisha uwiano wake na Shilingi kuipa shilingi nguvu zaidi, mtu anayelipwa kwa shilingi kwa kufuata thamani ya dola anaweza kupunjwa.
 
...to peg the price in dollars kwa sheria za Tanzania ni illegal na hairuhusiwi,people just dont care ndio maana watu wanajifanyia mambo bila kufuata sheria,kama una muda/resources unaweza kuwapelekesha under illegal price fixing...na hata ukipata srvices na ukakataa kulipa in $$$ hakuna kitu watakufanya under the law na unaweza kuwashtaki na wakaishia kukulipa wewe!
 
...to peg the price in dollars kwa sheria za Tanzania ni illegal na hairuhusiwi,people just dont care ndio maana watu wanajifanyia mambo bila kufuata sheria,kama una muda/resources unaweza kuwapelekesha under illegal price fixing...na hata ukipata srvices na ukakataa kulipa in $$$ hakuna kitu watakufanya under the law na unaweza kuwashtaki na wakaishia kukulipa wewe!

Haulipi in $ unalipa the Sh equivalent ya $ price. Sidhani kama kuweka bei in dollars inafall under price fixing.
 
Mgonjwa wa ukimwi,

Umenena na info zako thanks..nakuombea upone haraka..tehe tehe...
 
tunapolazimisha matumizi ya dola kwenye biashara za ndani tuna create demand kubwa ya dollar, hence shiling depreciation, katika hali hiyo tunachochea mfumuko wa bei
 
from what i know,

Ukimpa mtu US $, unakua hujamshwishi kununua bidhaa kwa TSh. kwa mfano kama mimi nategemea my sources of income will earn me US $ and other sources will earn me Tsh,
i'll purchase goods using the Tsh. but i wont use the US$ unless am going outside the country.
Only continous consumption of domestic goods and services makes an economy stronger. sasa kama napokea dola alaf sizitumii, muuza nyanya atauza nini?

Alaf nashangaa kuona foreigners wengi wanalipwa in US$ hapa Tz. huu ni ulimbukeni. Kwa nini tusiwalipe in Tshs? ili waweze kununua maparachichi pale kariakoo?

Consultancy works nyingi hapa Tz, payments zinakua in dollars. sometimes hata agencies za serikali zinalipa consultants in dollars.

I think inabidi tuanze kufundisha uzalendo kanisani na msikitini cz shule zimeshindwa.
 
Back
Top Bottom