Dola za Mwaka 1999 na kurudi nyuma

CPU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
3,863
686
Nimekuwa nikiathirika sana na hili suala. una baadhi ya sehemu wanakataa kabisa kupokea Dola za Kimarekani ambazo ni za mwaka 1999 kurudi nyuma, mfano Exim Bank pale Mliman City wakati sijawahi kusikia Serikali ya USA ikisema chochote kuhusu hizo noti. Je wanavyofanya ni sahihi???
 
hope so,
nilienda nchi moja ya kiarabu hapa africa kufika uhamiaji kulipia viza kutoa dola ya 2002 jamaa anakataa halafu nashindwa kumuelewa kwa sababu ya kiarabu hadi akaja jamaa mwingine(bosi?)ndiyo akapokea
 
Nikweli bureau awapokei nasikia zinatumika usa tu!

Mkuu sio USA tu, nchi nyingi zinatumika., ila nilisikia kuwa series hasa ya 1999 kuna fake nyingi sana with high tech zilitoka pia, so ni ngumu sana kuzigundua. Thus bureau nyingi sana Bongo hawapokei.
But huku nilipo wanazipokea njema kabsaaa..)
 
hiyo nadhani ni bongo tu, Ulaya yote wanapokea na wala haina tatizo. ajabu wala bot hawajawahi kutoa ufafanuzi kwa nn bongo tu ndio zinakataliwa
 
jamani sikuwai kuelewa kwa nn wanafanya hivi asante mtoa mada naamini tutapata majibu sahihi hapa
 
Ohh...Ok Ok....Na Hili la exchange rates,....kutofautia kati ya USD1,10,50,100 Likoje mnaweza nisadia wadau?
 
Ohh...Ok Ok....Na Hili la exchange rates,....kutofautia kati ya USD1,10,50,100 Likoje mnaweza nisadia wadau?

Mbona hesabu ni ya kawaida tu!!! Reja reja na jumla bei ni tofauti.

Hii series ya 1999 hapa Arusha haitumiki kabisa ila Money Changer akikuona ni wakuja anakutwanga za zamani. Ni Juzi tu nilikuwa Kampala pale Simba night Club, Garden City ndani kuna tangazo la bei na Dola za series 1999 kwenda chini ni bei kubwa!!!
 
Ni katika kujilinda tu,dola za kuanzia 2002 zimetengenezwa kitaalam zaidi na ni nadra kugushiwa,lakini kama unazo na umeshindwa kuzibadili nenda bureau za Kariakoo wanabadili lakini bei iko chini kama 1300 badala ya 1500.
 
Mbona hesabu ni ya kawaida tu!!! Reja reja na jumla bei ni tofauti.

Hii series ya 1999 hapa Arusha haitumiki kabisa ila Money Changer akikuona ni wakuja anakutwanga za zamani. Ni Juzi tu nilikuwa Kampala pale Simba night Club, Garden City ndani kuna tangazo la bei na Dola za series 1999 kwenda chini ni bei kubwa!!!

Mkuu yaani Nasema umetoka zako nje ukapatia labda pale freee duty shop ukanunua vitu vyako...ulikuwa na dola zaiko 150 then umebaki na dola 98,...kwanini wanabagua ile 50 ambayo iko moja..na hizo kumi,tano...wakati wewe unazibadilisha kiujumla as dola 98 na sio dola hamsini,Kumi etc?
 
Ohh...Ok Ok....Na Hili la exchange rates,....kutofautia kati ya USD1,10,50,100 Likoje mnaweza nisadia wadau?

Huu ni wizi mtupu. Maana wao hawaziuzi kwa bei hiyo ndogo wanauza kwa bei moja yaani denomination kubwa na ndogo. Ukienda nchi zingine hawana huu mtindo.

Mbona hesabu ni ya kawaida tu!!! Reja reja na jumla bei ni tofauti.

Hii series ya 1999 hapa Arusha haitumiki kabisa ila Money Changer akikuona ni wakuja anakutwanga za zamani. Ni Juzi tu nilikuwa Kampala pale Simba night Club, Garden City ndani kuna tangazo la bei na Dola za series 1999 kwenda chini ni bei kubwa!!!

Mkuu rejareja gani hiyo? Mbona kama mtu unazo dola 100 lakini ni za dola moja moja bei mbona haibadiliki na kuwa ya jumla kama mwenye noti moja ya dola 100? Huu ni wizi mtupu.
 
Bongo hapa dola za nyuma 2006 hazipokelewi, lakini december last year nilifanikiwa kubadilisha dola za 2002 y jumla ya USD350, Unique Forex pale posta kwa rate ya chini sana ya 1000 eti ananisaidia tu, zimeexpire. Ntafanyaje nilipinda, nilisalim amri
 
Kama kuna mwana Jf anafanya kazi CRDB anambie: nilitaka ku deposit $ tano (199) ya kichwa kidogo wakaikataa, kwa nini?
 
Mwisho wa mwaka jana tulikuwa Japan na tulitaka kubadilisha US$ to Yen, mwenzetu mmoja alikuwa na dola ya 2004 mashine ya bank ilikataa kabisa.

Walisema hawapokei za nyuma ya 2006. Kwa hivyo nchi nyengine pia huwa hazipokei dola hizo.
 
Lol! Hii sasa balaaa
 
Back
Top Bottom