Nono
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 1,536
- 643
Niliwahi kusema haya huko nyuma kuwa walioko nje ya nchi ambao ni wapenzi wa ccm wengi ni wanufaika na system ya kibongo (Mtoto kama baba). Ndio maana pamoja na kubahatika kwa vipindi fulani kuwepo huko UK, sikuweza kuwa na imani na vijana wa kibongo niliokuwa nikikutana nao kwa upenzi wa nchi yao. Inanikumbusha hata wale wenye kampuni za kuthibitisha ubora wa magari yaingizwayo kutoka uk. Naamini hii mbegu iliyopandwa na ccm ni mbaya, na matunda yake bila kujali yanachumwa kutoka tawi gani (uk au US) bado ni mabovu!
Haiingii akilini mnafursa za kubeba maboksi huko mkatengeneza paundi kuliko daladala hapa bongo, halafu fedha ya msukuma mkokoteni huku ndio tunakutumieni. Kweli hiki chama kimetunajisi!
Haiingii akilini mnafursa za kubeba maboksi huko mkatengeneza paundi kuliko daladala hapa bongo, halafu fedha ya msukuma mkokoteni huku ndio tunakutumieni. Kweli hiki chama kimetunajisi!