Dokta Bana Alipuka Tena

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,764
Kuna busara moja inayotuasa kuwa mpuuzi husema kwa vile anajiskia kusema (hata kama ni upuuzi) ilhali mwenye busara husema tu pale anapokuwa na kitu cha kusema (ikimaanisha kama hana cha kusema,au haoni umuhimu wa kusema kitu,atakaa kimya). Busara zaidi zinatuasa kuwa makini na tunayosema hadharani kwa vile mara nyingi jamii humtambua zaidi mtu kwa kauli zake.Sema upuuzi,utaonekana mpuuzi.Sema ya busara,utaonekana mwenye busara.Sasa kuna huyu msomi,Dokta Benson Bana,ambaye licha ya kuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam,ni mkuu wa idara ya Sayansi za Siasa na Uongozi na pia ni Mwenyekiti Mwenza wa REDET.Yayumkinika kusema Dkt Bana amekuwa mahiri zaidi wa kutoa kauli zisizoendana na wasifu wake kitaaluma kuliko umahiri wa wa usomi wake.....Mjadala zaidi unapatikana: http://chahali.blogspot.com/2010/04/dkt-bana-alipuka-tena.html
 

Attachments

  • Benson Bana.jpg
    Benson Bana.jpg
    11.4 KB · Views: 110
Sura za watu huwa zinasema mengi. Sasa huyo Bana sura yake pia inasema kachanganyikiwa!

Hapana hakuchanganyikiwa, ila tatizo ni kuwa akipiga mswaki anaishia kusukutua meno tu bila kuusafisha ulimi. Matokeo yake kinywa kinamuawasha na kutoa harufu mbaya, na njia mojawapo ya kupunguza hayo ni pamoja na ...............
 
Sioni kama kuna sababu ya kumtukana na kumwandama sana, Yeye ni mtu wa pili kinafasi katika taasisi ambayo inatumia pesa nyingi sana kuwadanganya watanzania. Hiiimefanyika katika kipindi kisichopungua miaka kumi sasa. Utafiti ni ghali sana sasa ubabaishaji kama huu unofanywa na hii taasisi ni wa kuangamiza taifa kwa masilahi binafsi. Aliyemtangulia alipewa zawadi yake, kwa hiyo na yeye anaitafuka zawadi yake.
 
Walimu wa Chuo Kikuu njaa kali, ni kweli, ila heshimuni taaluma zenu. Shame to all those who are not objective. By the way, mwanaume mzima utakuwaje na mawazo ya kupandikizwa? Tena Daktari wa Falsafa. Dr. Bana unaboa big time!
 
Sura za watu huwa zinasema mengi. Sasa huyo Bana sura yake pia inasema kachanganyikiwa!

Nimefungua ile picha nikashangaa, sura yake kwa kila inatoa ujumbe unaoendana na anayosema. Mumsamehe bure, hajui atendalo!!!!
 
Back
Top Bottom