Dogo ananiambia yule sio mpenzi wangu, lakini ni zaidi ya rafiki

nonino

Member
Apr 11, 2012
32
12
Kuna mtoto wa ndugu yangu msichana yuko chuoni tayari,kuna mvulana wanasoma naye wako very close,mara nyingi nawakutaga au nawaona katika mikao yenye utata,sasa kwa vile nilishawahi kumuuliza kama ana rafiki wa kiume akanijibu hana na siku akipata boyfriend ataniambia,sasa nilivyomuona na huyo kijana,ikabidi nimuulize mwenzangu vipi ndio tayari umepata,jibu alilonipa limeniacha hoi;akasema yule sio mpenzi wangu lakini ni zaidi ya rafiki,nikashindwa hata kuendelea kuuliza,maana nina uhakika yeye na huyo kijana wameshakutana kimwili mara nyingi tu,kuna siku nilimsikia akimsimulia shosti wake hapa home,wakijua mi nimelala. Hebu nielezeni jamani ,mtu wa opposite sex kuwa zaidi ya rafiki kwako ndio inakuwaje kuwaje?
 
au unamtaka ww tuambie ndugu unamfuatilia wa nn keshakwambia zaid ya rafikia hata kufunguka mtu mzma hakuna kunguka
 
ishimaisha yako ya huyo dada muachie.....

Na kujibu swali lako inawezekana kama wite mnajitambua na mnajuz mipaka ya urafiki wenu
 
Duh!nyie ndo mnakosesha dada zenu waume,asa kisa cha kumfuatilia hvyo ni nin?
 
Sasa mtu yuko chuo unamfuatilia wa nini?
Binadamu hachungwi kama mbuzi..
 
Kama huyo msichana mtoto wa ndugu yako kakujibu hivyo na hujaridhika na jibu lake, siyo vibaya kama utakwenda kumilza na huyo kijana uliyomkuta nae, umsikilize nae atakupa jibu gani.
 
Hakuna urafiki kati ya mwanaume na mwanamke.
Paka na panya hawawezi kuwa marafiki, watachezeana weee mwisho wa siku Paka atamla Panya
 
Acha utoto yanini kufuatilia maisha ya dada yako hasa katika suala la mahusiano pengine uniambie unataka kula mzigo mwenyewe

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom