Dogo aliyeandika bongo fleva mtihani wa kidato cha nne 2011

clouds walijuaje kama huyo julius ndiye aliyeandika bongo fleva? Ana uhakika gani kama ni yeye peke yake? Na ana uhakika gani kama ndalichako alimtumia yeye kama mfano?

Na huyo kijana anaona ni busara kuandika bongo fleva kwenye mtihani? Ndo jinsi ya kutambua kipaji hivyo????
 
ila asome kiingereza kitamsadia kimataifa!

Siyo kiingereza tu,anatakiwa asome shule aongeze ufahamu ndipo baadaye aende akasomee hiyo miziki anayotaka.La sivyo ataibiwa sana kazi zake na ataishia kuimba nyimbo zitakazochuja baada ya siku mbili.
 
Hata akina Thomas Edison elimu rasmi iliwapa taabu; na Bill Gates ni drop out. Nakubaliana na "Dogo" kuwa formal education (elimu rasmi) si kigezo pekee cha mafanikio, lkn bado elimu ni kigezo cha mafanikio. Sijakijua kipaji chake, lkn kwa Bongo fleva amepotea.

Lakini kutokuwa na formal education ni sawa na kutembea kwenye msitu wenye chui bila hata ya kuwa na mkuki wa kujihami.
 
Sio kwa mbali dogo kasema ukweli. Lazima tubadilishe mifumo tuweze ku-accomodate kila kipaji. Kwa ukweli katoa changamoto.
 
Kunahitajika kuwa na waalimu wenye uwezo wa kubaini talent za wanafunzi na kuwasaidia kuziendeleza lakini kwa sasa hivi kama hujui kutafuta X na Y. Na kuwezi kubana pua na kuongea kizungu kidogo huna nafasi katika mfumo wetu wa elimu.
 
Walau baada ya kupewa fursa ya kuongea dogo kafunguka....Ila Shanghazi wa NECTA alivyoipaisha hiyo stori duh!
 
Sasa ndugu yangu kama ni form four failure without certificate sasa ataenda wapi??? Ndio anataka kwenda kutunga hizi ambazo hazina maudhui yoyote?? Basi badala ya kuandika hiyo bongo flavour alihitaji mshauri ili amsaidie. Kwani angemaliza hata na D mbili au tatu potelea mbali angepata cheti akaenda chuo cha music akiwa na cheti cha kumsaidia. Ndugu yangu si kweli kuwa watu huimba tu bila mpango sahihi wewe si unakumbuka tulivyotunga mashairi na ngonjera p/school?? Anahitaji mtu wa kumsaidia kumfikisha kwenye destiny yake.
 
Lakini kutokuwa na formal education ni sawa na kutembea kwenye msitu wenye chui bila hata ya kuwa na mkuki wa kujihami.

Ni kweli kabisa, km tutazungumzia jamii kwa ujumla na mfumo wa elimu tulionao, k/sbb informal educ. inahitaji self discipine, ambayo si kila mtu anayo. Vilevile, huu mfumo wa kumpima mtu kwa vyeti vyake nao ni sbb tosha ya kuendelea kuwepo na formal ed., na hivyo kutozitambua informal ones. O/wise, formal ed. si lazima kwa mtu mmoja mmoja.
 
akili dhaifu tu! wa tz tumezidi kutetea akili dhaifu! sasa hii ndiyo ilikuwa njia sasa ya kufikisha ujumbe kweli? inamaana alikosa njia nyingine zote ili atufikishie ujumbe watanzania na hasa wahusika wa elimu! malengo na nia yake ni nzuri ila njia aliyotumia sio nzuri! kwakuwa wanaosahihisha mitihani wao wanamuda wa kusoma majibu ya ulichoulizwa tuuu! hawana muda wa kusoma ujumbe yani huo wimbo, wala kuangalia piacha na matusi yaliyo andikwa! je, nyinyi mnafikiri wahusika walipata huo ujumbe kweli? maybe! ni hayo tu!:spy:
 
Absolutely true mr. Julius, umediriki ku-shake system!Being educated never guarantee success, education & achvment r zero r/ship!We as LDCs we 'll continue starvng wc poverty coz of poor cstm we ev 2 addres t!We must change our mindset on edcation 4 dvt!

Wewe naona kaka ulipiga 180 degrees! hiyo lugha yako??!!
 
bado sijakubaliana naye kabisa kwani hata kuwa mwanamuziki mzuri na kuandika mistari iliyo na akili unahitaji hiyo formal education ye aseme tu ni vivu la kusoma basi na alifikiri bila elimu atakuwa bomba wapi. elimu ina umuhimu wake katika kila jambo haswa hilo analotaka kuzama. asiwapotoshe wazazi na vijana bila sababu
 
sasa haya aliandika hiyo mistari katika mtihani wa taifa nini kapata zaidi ya kufanya watu watafute kumjua kwa kituko alichofanya, leo hii hata akitoa hiyo singe au albamu watu wakisikia tu ndio yule aliyoandika mistari katika mtihani kuna mawili waache kabisa kusikiliza kwani watakuwa wameshamzarau au pengine japo kidogo sana wakata kujua kipi atakachokuwa amekifanya.
dogo alichemsha anajitetea tu
 
Sasa ndugu yangu kama ni form four failure without certificate sasa ataenda wapi??? Ndio anataka kwenda kutunga hizi ambazo hazina maudhui yoyote?? Basi badala ya kuandika hiyo bongo flavour alihitaji mshauri ili amsaidie. Kwani angemaliza hata na D mbili au tatu potelea mbali angepata cheti akaenda chuo cha music akiwa na cheti cha kumsaidia. Ndugu yangu si kweli kuwa watu huimba tu bila mpango sahihi wewe si unakumbuka tulivyotunga mashairi na ngonjera p/school?? Anahitaji mtu wa kumsaidia kumfikisha kwenye destiny yake.

ni kweli kabisa usemacho mkuu
pale mlimani watu husomea music pia hujifunza mambo mengi historia na vinginevyo ambavyo huwasaidia kutunga mashairi mazuri yenye maana, mziki si sauti pekee yake bali pia maudhui ya nyimbo.
 
ni wangapi tunawaona waacha shule wakijidanganya watafanya mziki wanaishia kuimba vibarazani kwao, vina havieleweki wanaungaunga hawajui kanuni za vina matokeo yake wanabahatisha tuuuuuuu
 
kwa kuandika hayo madudu katika mtihani anaonesha uwezo wake mdogo wa kufikiri
 
Baadhi ya mistari-
Wanaofanya madudu nawatosa kwenye baraza,
wananitia aibu kwa wananchi wananikwaza,
Nilikuwa kipenzi chao hadi mkasema mi chaguo la Mungu,
Kwenye uchaguzi nikapiga bao ila leo mnaniona mchungu,
Mara mnaiba wanyama mara mnakula cha juu,
Af bado mnataka muongezewe posho huko East Zuu,
Ndo maana maana napenda kusafiri ili nipunguze stress

Hii mistari angefanya colabo na Roma ingekua bomba.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom