dogo aliyeandika Bongo Fleva kwenye Mtihani Wa Form Four -live

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,347
11,610
Julius Dawson "ELINAJA" (23) mkazi wa Tabata, Segera, asili yao Marangu, Kilimanjaro, ni kijana ambaye aliandika mashairi ya nyimbo za "Bongo Fleva" kwenye mtihani wake wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2011.

Jana katika kipindi cha Power Breakfast "PB" cha redio CloudsFM alisema anashukuru sana kupewa nafasi ya kujieleza katika redio hiyo ili atoe sababu za msingi za ni kwa nini alifanya hivyo kwa kuwa jamii iliupokea ujumbe wake kama mzaha na kejeli, wakati yeye alikuwa akifikisha masaibu na machungu wanayoyapata watoto wenye vipaji lakini hawapewi fursa wala nafasi za kukuza vipaji vyao, badala yake wote wanaelekezwa kufuata mkondo mmoja hata ikiwa hawauwezi.

Ameomba msamaha kwa jamii nzima kwa yeyote yule aliyekwaza kwa alichokifanya, lakini akasisitiza kuwa alifanya hivyo kwa kuwa alitaka kufikisha ujumbe ambao umekuwa ukipuuzwa na Wazazi, Walezi na jamii nzima, wa kuwasaidia watoto kukuza vipaji vyao ambavyo baadaye hugeuka kuwa ajira rasmi na njia kuu ya kipato cha kuendesha maisha.

Bofya kitue cha pleya hapo umsikilize.

Mwishoni wameuweka wimbo wake mmoja kati ya nyingi ambazo amekwisha kuziandaa, ila bado hajafanikiwa kupata fedha za kutosheleza kurezirekodi kwenye studio kwa ajaili ya kuziuza.
 
Smile i don't see the link.
on topic; everybody needs education and form4 is not too much to ask for, hata mastaa Europe/NA wamefika at least Form4.
 
Last edited by a moderator:
Nashindwa kuweka iyo link but si mnaelewa bwanaaa
 
Ata ajitetee je ni upuuzi na upumbavu tu aliofanya na iko siku ktk maisha yake atakuja kujuta kama haanza majuto sasa
 
Back
Top Bottom