Dodoma haipaswi kuitwa makao makuu.

Malolella

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
366
111
Jamani huu mji wa Dodoma haupaswi kuitwa makao makuu ya Tz, kwanza barabara za manispaa ni hovyo kabisa, mfumo wa maji taka baadhi ya sehemu tena katikati ya mji ni hovyo kabisa. Stendi kuu ya mabasi haieleweki, kuna mashimo makubwa tena mengi kwnye barabara ya kuingia stendi kuu.

Ukipita maeneo ya majengo sokoni wanaita rev square kuna mashimo kwnye lami ambapo wameamua kuziba kwa kuweka vilaka vya udongo yani vifusi. Hivi wahusika wapo likizo au hili ni shamba la bibi halina mwangalizi? Viongozi wenye dhamana na mji wa Dodoma timizeni wajibu wenu.
 
Ni wakati muafaka kwa Serikali ya Ccm, kutoa tamko rasmi kuhusu Makao makuu ya Serikali Dodoma.
Kwamba kuhamisha makao Makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam na kuhamia Dodoma imeshindika-
na Makao Makuu ya Serikali yatabakia Dar es Salaam, ila Bunge la Jamuhuri litabakia Dodoma.
Serikali ya Ccm aina nia ya kuhama bali kilichokuwepo ni ufujaji wa pesa, huo mradi wa makao Makuu
usimamishwe na pesa ziingizwe katika matatizo makubwa mengine yaliyojitokeza. Bye Bye Dodoma.
 
Malollela. Ktkt ya jiji la Dsm kuna barabara nyembamba za lami,maghorofa marefu,mengi yasiyo na parking na foleni ndefu za magari. Mimi nadhani ni muda muhafaka serikali kuhamia Dodoma ili Dsm ipumue.
 
Uki google Tanzania maelezo yanakuja Dodoma mji mkuu lakini Dar es salaam ndio mji maarufu.Kwa u,aarufu huo wa mji wa Dar bora ndio uwe mji mkuu wa Bongo land kwani viongozi na wengineo ndio wamejazana jijini.
Hamza Kalala aliwahi kuimba kuh jiji la Dar na Dodoma wanakwenda na kuzuga (KURUDI)
 
Kwahiyo ndomana hawataki hata kuuboresha mji wa Dom coz serikali haina mpango wa kuhamia Dom? Je mbunge wa Dom yupo likizo? Nini kazi ya mamlaka ya ustawishaji makao makuu (cda) ambayo ni sera ya serikali ya mwaka 1974 ya kuimarisha mji wa Dodoma?
 
"MAMLAKA YA UZOROTESHAJI MAKAO MAKUU" kwa Wananchi wa Dodoma tunaona hilo ndo jina muafaka la hiyo CDA.
Kwa tunaoijua Dom vema na viongozi wa jimbo,halmashauri,wilaya bado hajapatikana AMBAE ANAIMUDU CDA NA MADUDU YAO YA UZOROTESHAJI(si USTAWISHAJI)
 
kweli mkuu
 
Back
Top Bottom