Doctors mnavunja sana maadili yenu!!

usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
522
331
Kwenye medical ethics kuna kipengele cha kutotoa taarifa za mgonjwa hata kwa ndugu bila ruhusa ya mgonjwa. Pia ugonjwa wa mtu ni siri yako wewe na mgonjwa, hata madaktari wasiohusika hawaruhusiwi kujua taarifa zake isipokuwa wanaohusika kwenye matibabu.

Kwa waathirika hata spause hatakiwi kujua mpaka aambiwe na mgonjwa mwenyewe au umwambie kwa ruhusa ya mgonjwa. Kama umemshauri amwambie spause wake bila mafaniki(zaidi ya mara 2),sheria inakuruhusu kumpatia taarifa huyo mwenzi wake lakini siyo ndugu wengine cha ajabu taarifa zinafika mpaka kwa wapenzi/wenzi wetu, kwani wanahusika!.

Hairuhusiwi kumpima mtu hiv bila kumshauri na akubali. Hata akikataa, he/she should not be denied from proper treatment. Hizo ni baadhi tu. Siku hizi unakutana na taarifa za mgonjwa zimesambaa kila sehemu na mhusika hazijui taarifa zake. Taarifa zinakuwa disclosed hata kwa watu wasiohusika, mpaka wafagizi wanajua! Zikitoka hapo zinakuwa story za mtaani, this is unethical!! Tunawaambia watu hata wasio wa speciality inayohusika. Hata kwenye vikao vyetu tunageuza wagonjwa ndo story,why?!

Wagonjwa wengi wanapimwa damu zao bila consert na wodi zima linajua kwamba fulani ni muathirika kabla yeye hajajua. Those are distressing information, tunawaumiza watu kisaikolojia tena mara nyingi. Taarifa zenyewe na kuzipata ghafla, impact yake ni kubwa sana! Turudini kwenye maadili, hasa madaktari vijana!

Au medical ethics siku hizi haifundishwi? Kwenye vijiwe vyenu mnakosaga mambo ya kuongea? Imagine ni wewe watu wanakuongelea hivyo, utajisikiaje? Kumbukeni siku hizi awareness ya wananchi ni kubwa na wanasheria wengi wanatafuta kazi. Wakiingia huku tutafungwa wengi au kulipa faini sana kwa vitu vidogo vidogo.!
 
Kaka Hippo nakusubiri utoe kauli juu ya hili! Ni ukweli usiopingika, lakini sometimes sio dr wanatoa hizo taarifa ila mfumo ni mbovu wa kuwapima na kuwahudumia wagonjwa wa VVU.

Nilishawahi shuhudia mwalimu mmoja ambaye alikuwa anafahamiana na daktari anayefanya kitengo cha CTC, baada ya kuona foleni kuonana na daktari ni ndefu alimwomba huyo daktari wa CTC ampe favour, daktari alimchukua na kwenda kumsikiliza CTC, wagonjwa wengine walivyomwona tu yule mwalimu kaingia CTC ikawa gumzo mtaani, ati anaringa tu, chuma lenyewe lishaungua moto.
 
You are right mkuu Usungilo, lakini wakati wote, kwa mfano 1.unapata mgonjwa asiyejua kiswahili wala kiingereza utaongea nae vipi kama si kuweka third part?(disclosure)

2.Sera ya Taifa ya kupunguza maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto(PMTCT) inaruhusu kupima VVU even bila hiyo taarifa,

3.Inapotokea mgonjwa amepata magonjwa yaliyotokana na upungufu sana wa kinga mwili(Opportunistic Infection) mgonjwa hupimwa mara moja.

4.Medical ethics inaruhusu information disclosure kati ya daktari na daktari(au kundi la madaktari) katika kuboresha afya ya mgonjwa (ila inapokuwa inafanywa kama "story" kweli ni kosa)

So, kuna wakati ni ngumu kuweka clear cut line btn the two, ila ni ukweli usiopingika Maadili ya kazi yamepungua mkuu.
 
You are right mkuu Usungilo, lakini wakati wote, kwa mfano 1.unapata mgonjwa asiyejua kiswahili wala kiingereza utaongea nae vipi kama si kuweka third part?(disclosure)
2.Sera ya Taifa ya kupunguza maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto(PMTCT) inaruhusu kupima VVU even bila hiyo taarifa,
3.Inapotokea mgonjwa amepata magonjwa yaliyotokana na upungufu sana wa kinga mwili(Opportunistic Infection) mgonjwa hupimwa mara moja.
4.Medical ethics inaruhusu information disclosure kati ya daktari na daktari(au kundi la madaktari) katika kuboresha afya ya mgonjwa (ila inapokuwa inafanywa kama "story" kweli ni kosa)

So, kuna wakati ni ngumu kuweka clear cut line btn the two, ila ni ukweli usiopingika Maadili ya kazi yamepungua mkuu.

Dr,
Wewe ni mtu muhimu humu JF ingawa tulikuwa tunatofautiana mitizamo kwenye issue ya Dr Ulimboka...

Unatusaidia kufahamu vitu vingi sana humu JF kwenye maswala ya tiba ushauri wangu kwako punguza jazba kidogo Dr. Mwaminifu.
 
Dr,
Wewe ni mtu muhimu humu JF ingawa tulikuwa tunatofautiana mitizamo kwenye issue ya Dr Ulimboka...

Unatusaidia kufahamu vitu vingi sana humu JF kwenye maswala ya tiba ushauri wangu kwako punguza jazba kidogo Dr. Mwaminifu.

I remember Mkuu Ritz, shukrani nitaufanyia kazi mkuu.
 
suala la unethical disclosure ni kweli na ni baya... ila kulaumu drs wenyewe sio fair. system ya utoaji tiba onampa access ya info hata nurse, maabara na mfamasia... na kwwnue ukimwi ni hadi ndugu au community. care giver

tatizo ni kubwa kuliko. na uonavyo mmomonyoko huu wa maadili kwa swtka ya tiba, ni reflection tu ya tatozo maadili kwa jamii nzima
 
mke/mume ndio mtu pekee anaruhusiwa kujua information kuhusu partnet wao...sasa ukikuta mgonjwa kalala yuko kwenye coma haongei then partner wa huyo mgonjwa ana haki ya kupewa details zote za mgonjwa
 
mke/mume ndio mtu pekee anaruhusiwa kujua information kuhusu partnet wao...sasa ukikuta mgonjwa kalala yuko kwenye coma haongei then partner wa huyo mgonjwa ana haki ya kupewa details zote za mgonjwa

kama yuko kwenye critical condition na hawezi kuongea unamshauri ndugu wa karibu na ndiye utakayempa majibu kama atakubali, lakini sivyo inavyofanyika. Watu wanafanya kiholela tu.
 
Swala hili sio kuhusu Ukimwi tu.
Kuna daktari hapa alikuja na vyeti vya wagonjwa vyenye taarifa yao binafsi natarehe walizohudhuria hospitali. Si sahihi hata kidogo.
 
I remember Mkuu Ritz, shukrani nitaufanyia kazi mkuu.

mkuu hata kama hali yake ni mbaya sana lazima awepo mtu wa kuconcert na awe counseld na akubali kupewa majibu kwa niaba ya mgonjwa. Kinachofanyika sasa hivi ni dr kuchukua damu na kwenda kupima bila hata kumshauri mgonjwa. Majibu yakirudi wanaanza kuambiana kimya kimya, nini umuhimu wa round kufanyika? Kwa nini msinijulishe nijue nini kinaendelea? Daktari wa speciality husika anatakiwa kupewa taarifa kama atasaidia kwenye matibabu lakini si kila anayeitwa daktari. Mgonjwa ni internal medicine lakhni taarifa unazikuta moi, why?
 
Swala hili sio kuhusu Ukimwi tu.
Kuna daktari hapa alikuja na vyeti vya wagonjwa vyenye taarifa yao binafsi natarehe walizohudhuria hospitali. Si sahihi hata kidogo.

maadili yanavunjwa sana kuhusu taarifa za wagonjwa. Kama kuna makosa unahisi jamii inatakiwa kujua futa jina,tarehe na daktari aliyemuona
 
Mhhh...Pole!

ni suala sensitive sana kwenye sekta hii. Siku watz wakianza kudai haki zao za afya mahakamani tutaumia wengi. Kuna daktari years back in mbeya aliuawa na jamaa baada ya kumpima na kumgundua ameathirika. Jamaa akajua yule daktari atavujisha taarifa zake hivyo akaamua kumzima kwa staili hiyo. Huku kwetu watu wanazisambaza taarifa bila sababu zozote za msingi. Unakutana na mgonjwa anaongea, anaakili timamu kwa nini usimshauri kwanza? Kwa nini uanze kuwapa taarifa ndugu wengine bila ruhusa yake? Hata wenye vvu ni mpaka awe THREAT kwa jamii ndipo unatoa riport kwa mamlaka siyo kusambaza mtaani kwa wasiohusi.ka
 
pole mkuu pia jua dr haingii maabara kupima
kwa hivo siri za wagonjwa kuvuja zinanzia hata huko maabara
na pia wale wabeba mafaili.
kwa nchi za wenzetu kila kitu kiko computerised na wana sheria nzuri za data protection ambako ndani yake kipengele cha afya kimeaniswa kama sesnsitive information na adhabu yake ni kubwa kwa atakaekiuka
kwa hivo inakuwa rahisi kumpata mvujishaji wa taarifa.
 
mkuu hata kama hali yake ni mbaya sana lazima awepo mtu wa kuconcert na awe counseld na akubali kupewa majibu kwa niaba ya mgonjwa. Kinachofanyika sasa hivi ni dr kuchukua damu na kwenda kupima bila hata kumshauri mgonjwa. Majibu yakirudi wanaanza kuambiana kimya kimya, nini umuhimu wa round kufanyika? Kwa nini msinijulishe nijue nini kinaendelea? Daktari wa speciality husika anatakiwa kupewa taarifa kama atasaidia kwenye matibabu lakini si kila anayeitwa daktari. Mgonjwa ni internal medicine lakhni taarifa unazikuta moi, why?

Sikubaliani na wewe kwamba muda lazima awepo mtu wa kuconsent!!Otherwise pitia tena Hippocratic Oath vizuri..

1.Suala ulilosema laweza kutokea na ni jambo la kawaida kuona Idara zinashirikishana..mfano umepata mgonjwa mwenye mutiple injuries huyu ataenda MOI lakini kuwepo kwake kule hakuzuii Neurologist(Int. Med) asim-review, ama mtu wa Otorhinolaryngologist( Sikio, Pua na kinywa) kum-review kutokana na uwepo wao na mgonjwa husika.
2.Suala la kupima VVU umelitafsiri in terms of Social impact, ila linapokuwa hospitalini ni suala la OUTCOME zaidi yaani (Prognosis)..this is bse kuwapo kwa ugonjwa fulani let's say mtu ni hypertensive(ana shinikizo la damu), UKIMWI, Kisukari n.k outcome yake ni tofauti mwenye Kisukari pekee..hii hutokana na ugonjwa unavyo udhuru mwili, tiba kuwa muda mrefu nk.. besides kuna dawa huwezi kuanzisha bila kujua muingiliano(interaction ya dawa nyingine).hivyo anapopimwa bila ridhaa yake ni kwa ajili ya manufaa yake mwenyewe na si kwa madakatari "kupiga stori"
 
je, huu utunzaji wa siri ya ugonjwa wa mtu ipo pale anapokuwa hai au hata pale anapokuwa kafariki? Nauliza hivi kwa sababu trend ya jamii yetu kwa sasa hasa kutokana na kuwepo kwa gonjwa la ukimwi kumekuwa na msisitizo mkubwa katika jamii kwamba mtu aliyekufa kwa ukimwi siku ya mazishi ni bora isemwe waziwazi kwamba kafa kwa ukimwi ili kama marehemu aliacha mjane basi watu wawe waangalifu wasijiendee kichwa-kichwa kuomba penzi la mjane. Je, ni sahihi kuusema ugonjwa uliomuua marehemu? Je, marehemu anakuwa katendewa sawa hata kama waliotoboa siri za ugonjwa wake ni ndugu zake?
 
nahisi umepotoka kuwahukumu madaktari bila kuwa na ushahidi wa kutosha.mara nyingi watoaji wa huduma ya upimaji ni manesi,manesi wakunga na wahudumu wa afya.
Madaktari wengi huishia kuandika vipimo flani vifanyike tu.
Kwa bahati mbaya wengi wa wapimaji hao hawajala kiapo cha appolo hivyo usitegemee confidentiality sana.
Hali itakua mbaya zaidi miaka kadhaa ijayo pale madaktari manesi na wahudumu wa afya ambao ni vodafasta watakapomwagika sokoni.
 
Kwenye medical ethics kuna kipengele cha kutotoa taarifa za mgonjwa hata kwa ndugu bila ruhusa ya mgonjwa. Pia ugonjwa wa mtu ni siri yako wewe na mgonjwa, hata madaktari wasiohusika hawaruhusiwi kujua taarifa zake isipokuwa wanaohusika kwenye matibabu. Kwa waathirika hata spause hatakiwi kujua mpaka aambiwe na mgonjwa mwenyewe au umwambie kwa ruhusa ya mgonjwa. Kama umemshauri amwambie spause wake bila mafaniki(zaidi ya mara 2),sheria inakuruhusu kumpatia taarifa huyo mwenzi wake lakini siyo ndugu wengine cha ajabu taarifa zinafika mpaka kwa wapenzi/wenzi wetu, kwani wanahusika!. Hairuhusiwi kumpima mtu hiv bila kumshauri na akubali. Hata akikataa, he/she should not be denied from proper treatment. Hizo ni baadhi tu. Siku hizi unakutana na taarifa za mgonjwa zimesambaa kila sehemu na mhusika hazijui taarifa zake. Taarifa zinakuwa disclosed hata kwa watu wasiohusika, mpaka wafagizi wanajua! Zikitoka hapo zinakuwa story za mtaani, this is unethical!! Tunawaambia watu hata wasio wa speciality inayohusika. Hata kwenye vikao vyetu tunageuza wagonjwa ndo story,why?! Wagonjwa wengi wanapimwa damu zao bila consert na wodi zima linajua kwamba fulani ni muathirika kabla yeye hajajua. Those are distressing information, tunawaumiza watu kisaikolojia tena mara nyingi. Taarifa zenyewe na kuzipata ghafla, impact yake ni kubwa sana! Turudini kwenye maadili, hasa madaktari vijana! Au medical ethics siku hizi haifundishwi? Kwenye vijiwe vyenu mnakosaga mambo ya kuongea? Imagine ni wewe watu wanakuongelea hivyo, utajisikiaje? Kumbukeni siku hizi awareness ya wananchi ni kubwa na wanasheria wengi wanatafuta kazi. Wakiingia huku tutafungwa wengi au kulipa faini sana kwa vitu vidogo vidogo.!

pole sana kaka siku hizi hakuna madokta tanzania si ndio hawa wamejaa kibao hapa jf . wagonjwa kutibu watu hadi wabembelezwe . na huko kutoa siri za wagonjwa ni kawaida yao si unawasikia hapa kila siku , mara ooh kibonde ana ngoma , mara mkewe hanyonyeshi , mara ooh tunampatia dawa za arv. kifupi ni kuwa wale madokta wenyewe as doktaz walishaondoka tanzania wapo nje wanakula maisha . haya yaliyobaki ni makapi tu ya madokta hawana lolote. kazi yao ni kulewa , kuzungumzia siasa, kufuatilia mishahara ya wabunge na safari za kikwete . kutongoza wagonjwa , mwishowe story zikiisha ni kutoa siri za wagonjwa. NDIO MAANA VIONGOZI WOTE HAWATIBIWI HOSPITAL ZA BONGO . HATA MADOKTA WENYEWE WANAJUA NA NDIO MAANA MWENZAO ULIMBOKA WALIMPELEKA SOUTH AFRICA .
 
Kikubwa zaidi ni kutoa siri za wagonjwa , kulewa na kushindana kuwapanga wanawake ndio kazi yao kubwa
 
Back
Top Bottom