Do Zombies and Vampires Exist?

jamani do zombies and vampires exist?

Yes, they do exists, tena hapa Tanzania wapo wengi tu,
Zombies ndio Wanachama wa CCM yaana hawajitambu kabisa, wanapelekwa pelekwa tu. Wao kanga na ubwabwa ndo kila kitu.
Vampires ndiohao mafisadi wanyonya uchumi wetu bila haya na ukiwagusa tu wanaweza kukupoteza kwa kasi ya kufa mtu.
Kuwa makini Mkuu, hata hapo ulipo now wapo around wengi tu.
 
Msukule.jpg

Msukule

msukule kapiga chupi ya ukweli du
 
Ananikosha Damon ..ingawa wote kwa pamoja ni wazuri sana ...

DAMÖN!kuna saa unatamani you could date one,ahaha!.kama ni myth bas tena..ila najiulizaga,if they dont,then where did the notion come from?kama they did,je kuna possibility that somehow somewhere bado wapo?
 
DAMÖN!kuna saa unatamani you could date one,ahaha!.kama ni myth bas tena..ila najiulizaga,if they dont,then where did the notion come from?kama they did,je kuna possibility that somehow somewhere bado wapo?

Watu wako kazini..It is a fiction mkuu,
 
Hakuna Vampires na Hakuna Zombies kwa maana halisi. Kuna hallucinations ambapo watu huona visions za vitu visivyokuwepo kutokana na matatizo ya kwenye ubongo au kutokana na kutumia aina fulani fulani za madawa ya kulevya. Vitu hivi huzungumzwa sana kwa sababu wapo watu (wenye matatizo hayo niliyotaja) huviona. Sasa kwa kuwa hivi ni vitu vinavyotengenezwa na akili zenye matatizo (ugonjwa au ulevi) vinaendelea kubaki kwenye legend.

Hawa wanaoitwa eti misukule wanaokamatwa na hawa wachungaji wa "bongo fleva" huwa ni maigizo na wale watu wengi ni watu halisi wanaofanya sanaa tu kuwadanganya watu. Hakuna mtu halisi wala mfu aliyechukuliwa msukule kwa kinachoitwa njia za kichawi. Ni kweli wapo watu hutekwa nyara na kufanyiwa brain-washing ila hili hufanyika kwa kutumia njia za kawaida kabisa.

Uchawi si real, ni sanaa na uongo!
 
Zombie ni neno linalotokana na lugha ya Ki Haiti (zonbi; North Mbundu: nzumbe), wakimaanisha animated corpse, maiti inayotembea.

Hizi simulizi za kuwepo hivi viumbe zipo karibia tamaduni nyingi tangia kale... Hata hapa Tanzania wanaitwa kwa majina tofauti tofauti kulingana na lugha ya kabila fulani, kwa mfano zombie wanajulikana kwa jina maarufu la ndondocha au msukule.

Kuna ambao wanajaribu kuwatofautisha kati ya ndondocha na msukule, wanasema kuwa tofauti kati ya viumbe hivi viwili ni:
Ndondocha ni watu waliorogwa na kubadilishwa akili zao kuwa kama watumwa na wakajikuta wanafanya mambo ya ajabu ajabu.
Msukule kwa upande mwingine ni watu ambao wanaaminiwa kuwa wamekufa lakini kumbe wamechukuliwa kwa madawa ili kumtumikia mganga, mchawi, au mwanamazingara Fulani.

Msukule ndio hao kwa kwa Kiingereza wanaitwa “Zombie” lakini bado wanawatofautisha kati ya msukule na zombie, wanasema kuwa Zombie kwa utamaduni na hadithi za kimagharibi, yaani nchi za ulaya ni watu walioukuwa wamekufa lakini wakarudi wakiwa nusu wafu na wasio na akili timamu. Lakini Msukule ni watu ambao hawajafa kabisa ila wamefanywa waonekane wamekufa na binadamu wengine.

Kiukweli kile unacho kiona kwenye filamu za vampire na zombies ni simulizi tu za kutaka kuburudisha watu si mambo ya kweli, japokuwa wanaweza kushabihisha na matukio ya kweli.

Mawazo ya kufikiria kuwa kuna misukule au zombie ni mawazo ya zamani sana, watu wa ulaya waliamini kuwa wafu wana uwezo wa kufufuka na kuja kusumbua watu walio hai, na hii ni kutokana na wivu waliokuwa nao hao wafu, au wakati mwingine hurudi kuja kutafuta haki walizo dhurumiwa n.k. Sasa ili kuwatisha na kuwafanya wasiwe na uwezo wa kurudi ndio kukabuniwa hizi nguo nyeusi ili kuzitisha roho zinazotaka kurudi duniani.

Ni sawa na hadithi za Halloween, sherehe inayofanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi wa October (tarehe 31). Hii ni sikukuu ambayo usheherekewa usiku kabla ya ile sikukuu ya watakatifu wote, kwa ufupi halloween ni sikukuu ya wafu (Mizimu). Na ilianza miaka 2000 iliyopita uko Ireland, lakini imekuja kuwa maarufu sana kwa nchi za ulaya na haswa ikiusisha uvaaji wa nguo za ajabu ajabu, na uchomaji wa moto na mapambo majumbani.

Mwanzoni ilisemekeana wafu/mizimu walikuwa wakija kusumbuwa watu duniani, na haswa waliharibu mazao, ambayo yalivunwa kipindi cha joto na kuwekwa akiba kwa ajili ya kipindi cha baridi (Winter), sasa ili kuwababaisha wasitambuwe nani ni nani ndio wakabuni haya mambo ya kuvaa kama maiti zilifukuriwa ili kuwachanganya hao magosti.

Lakini wengine wanasema kuwa, uvaaji wa nguo nyeusi misibani ni kweli unatokana na utamaduni wa kimagharibi, na haswa Roma ya kale, (ancient Rome), wao walikuwa wakivaa aina ya nguo inayojulikana kwa jina la toga, ni aina ya shuka ndefu nyeusi inayokadiriwa kufika futi 20 (6 m) kwa urefu wake. Ambayo uzungushwa mwilini, toga ilivaliwa na wanaume na wanawake walivaa stola.

Na wengine wanasema kuwa chanzo cha nguo nyeusi kuvaliwa msibani ni pale malkia Victori, alipokuwa akiomboleza kifo cha mumewe alikuwa akivaa nguo nyeusi tu na alivaa kwa muda mrefu sana... Hii ilipelekea raiya nao kuvaa kila wanapopata msiba ya watu wanao wapenda.

Unaweza kupitia link hizi hapa chini kwa habari za hao zombie na vampire.
Zombie › News in Science (ABC Science)
Zombie
Ghoul
Golem
folk_magic
Jiang_Shi
Mind_control
wiki/Vampire

da aisee bonge la lecture...tumekusoma aisee...
 
ITS TRUE, THEY REAL EXIST ONLY IF YOU BELIEF & WISH TO JOIN UNDERWORLD AFFAIRSS, U WILL BE ABLE TO SEE THIS EARTH IN HOLOGRAM (3D).........ask some 1 to share ILLUMINATI BLOOD WITH U, U WILL HAVE JURISDICTION. YOU ARE WELCOME.
 
ITS TRUE, THEY REAL EXIST ONLY IF YOU BELIEF & WISH TO JOIN UNDERWORLD AFFAIRSS, U WILL BE ABLE TO SEE THIS EARTH IN HOLOGRAM (3D).........ask some 1 to share ILLUMINATI BLOOD WITH U, U WILL HAVE JURISDICTION. YOU ARE WELCOME.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom