Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,257
- 105,389
Sio siri kuwa kuna watu wa asili ya Kitusi ambao baba zao walikuja siku nyingi kama wakimbizi na kuishi sehemu za mikoa wa Tabora na Kagera na sasa wana nyadhifa kubwa kwenye serikali yetu. Wengine ndio hao uraia wao ulileta utata enzi ya Mkapa na wengine walipewa ubalozi na Kagame mara alipoingia madarakani na wengine ndio wakina Kamanzi na Rutayisire waliokuwa waalimu IFM na UDSM respectively; baada ya Kagame kuingia madarakani wakatoroka na kurudi kwao!! Sasa kama watu wa usalama wa Taifa wangekuwa wanafanya kazi yao vizuri wangeweza kuwatambua hao watu walioinfiltrate serikali kwani inasemekana wapo mpaka kwenye baraza la mawaziri not to mention mashirika nyeti kama EWURA!! Hiyo ndiyo strategy ya kufanikisha BAHIMA empire!!
Katika hivi vi nationstate vya Afrika mashariki vilivyoanza miaka 50-60 iliyopita, ukjianza kuwa trace watu historia zao hakuna atakayebaki Mtanzania.
Utaambiwa Nyerere Mrundi, Mwinyi na Kinana Wasomali, Mkapa anatoka Msumbiji na Kikwete actually ni Mngazijana na Karume ni Mnyasa wa Malawi.
Na Wakurya wanataka kuchukua jeshi while wachagga wanataka kuchukua biashara huku Wasukuma na Wanyakyusa wakigombea nafasi nono kwenye mashirika ya umma.
Na Wanyakyusa si Watanzania hasa kwa sababu asili yao ni Malawi na Zambia, wakati Wasukuma wametokea Zaire.
Ukiangalia sana Wabantu wote si Watanzania kwa sababu walitokea Nyanda za Kaskazini ya Nigeria na Magharibi ya Cameroon.
Sasa tutaishi vipi hapo?