Kivumah
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 2,428
- 1,050
Wanajamvi tujadili kama Great Thinkers hapa: issue sio kuwepo au kutokuwepo kwa TAKUKURU, issue ni kwamba TAASISI iliyopo haina Uhuru na haina Meno kupambana na Rushwa. na hata tukisema tuivunje, huyo atakayepewa jukumu hilo naye hatuna Guarantee kuwa atakuwa na Uhuru na Meno(Nguvu) kiasi gani cha kupambana na Rushwa. Mfano, nilisikia ktk Sera ya CHADEMA katika hili ni kwamba wao watakiingia madarakani watakachofanya ni kuipa uhuru na meno TAKUKURU wafanye kazi yao bila kuingiliwa na mtu yeyote, hii ni nzuri kwa maoni yangu mm. Lakini kwa jinsi mfumo/sheria iliyoiunda TAKUKURU hivi sasa, ambapo Mkurugenzi wake Mkuu anateuliwa na Rais, tunategemea nini???, hakuna Uhuru wa Meno hapo!!!!. NASHAURI: Watanzania sasa tudai Katiba mpya ili vyombo vya kisheria/vya Dola kama TAKUKURU, TISS, POLICE,JWTZ etc viwe huru visiingiliwe na wanasiasa kama ilivyo sasa, majirani zetu Kenya wameweza na sasa wanafurahia mabaliko ya Katiba yao. TUACHE KULALAMIKA