Do we really need TAKUKURU?

NDUGU ZANGU WANA JF,NAPENDA KUJUWA HIVI HII TAKUKURU IPO KWA MASLAHI YA NANI? NA INAWAJIBIKA KWA BUNGE AMA KWA SERIKALI KUU? KWANI MIMI BADO SIJAIELEWA TAKUKURU WIKI ILIYOPITA ILIMSAFISHA CHENGE KUWA HAUSIKI NA UNUNUZI WA RADA LENGO NI CHENGE AGOMBEE USPIKA,JUZI UBALOZI WA UINGEREZA UNAKANUSHA KUWA KESI BADO HAIJAPELEKWA MAHAKAMANI HIVYO SWALA LA RADA HALIJAHITIMISWA("Lakini kwa kuwa makubaliano hayo hayajathibitishwa na Mahakama, sio sahihi kusema sasa kwamba, suala hilo limemalizika.").NINGEPENDA KUJUWA KAMA TAKUKURU IPO PALE KWA MASLAHI YA WATU FULANI NI VYEMA KAMA WANAVYO SEMA WASOMI IFUTWE ILI TUWE NA CHOMBO HURU NA MAKINI KULIKO KUWA NA CHOMBO KISICHO NA MWELEKEO WA SURA YA TAIFA.WANA FR HEBU TUSAIDIANE JUU YA TAKUKURU KWANI HII SI MALA YA KWANZA CHOMBO MUHIMU KAMA HIKI KUKANGANYA MAMBO.

MAPINDUZIIIIIIIII DAIMAAAAAAAA
 
Mara kadhaa uongozi wa TAKUKURU unapokosea jambo wananchi mbalimbali huwa wanakimbilia kudai kwamba Taasisi hiyo ifutwe! (Kwa mfano soma Gazeti la Mwananchi la leo) Sijawahi kusikia kwamba Taasisi nyinginezo viongozi wake wanapokosea idaiwe kwamba Taasisi zao zifutwe!
- TRA inawabeba wafanyabiashara wakubwa na wanakwepa kodi kuliko maelezo, sijawahi kusikia hoja kwamba ifutwe.
- Polisi "wanachakachua" rushwa si mchezo na wanaonea mno wananchi, wengine huuawa hata bila kufikishwa mahakamani kila iitwapo leo lakini hatujasikia kwamba Jeshi hilo lifutwe.
- TANESCO wanatukatia umeme mara kwa mara lakini sijawahi kusikia wakidai ifutwe.
- Usalama wa taifa ndio uko likizo si mchezo, ni kama haupo, lakini sijawahi kusikia hoja ya kufutwa kwa Taasisi hiyo nyeti.
nk, nk, nk, nk.....

Kwa nini linapokuja suala la TAKUKURU huwa inatolewa hoja kwamba ifutwe? Wengine hudai kwamba iwe chini ya Bunge. I can't imagine kwamba chombo cha utendaji ambacho kinatakiwa kiwe chini ya executive kinakuwa chini ya Parliament. After all Wabunge (hasa wa CCM) ni wala rushwa wakubwa, sasa TAKUKURU ikiwa chini yao si ndio watang'oa hata yale meno machache ambayo TAKUKURU ilikuwa imebakiwa nayo?
Tujadili wandugu!
 
Nadhani ipo kwa maslahi ya watawala yaan zzm, kulinda maslahi yao mbona kila wakati ina prove wrong.zile rushwa kubwa wanazilinda na kuhangaika na ndogo, hakuna rushwa kubwa hata moja waliyo isimamia kidete na tunazidi kujionea ya rada nayo yameibuka tena kweli mwisho wa siku, kwa busara tu huyo mkurugenz wao na ajiuzulu.
 
Hawana akili kabiisa na wanatia aibu. Kusafisjha kesi iliyo mahakamani! hawapo huru kabisa ila wengine wajanja sana
 
kwanza haina kazi,toka ianzishwe imeshindwa kutushawishi kwamba kwa nini tubaki nayo,kwa nini iendelee kutumia kodi zetu.
kazi zote inazofanya zinaweza kufanywa na jeshi la polisi.kwanza ni watu wenye tamaa ya utajiri wanashindana kununua magari kwa hela haramu.
mimi nashauri ivunjwe mara moja kwa sababu kazi wanayofanya ni tofauti na waliyotumwa(kutetea wala rushwa)
 
Kwa nini Taasisi nyingine nazo zisifutwe?

Kwa sababu TAKUKURU ndiyo polisi wa taasisi hizo nyingine. Ikifutwa TAKUKURU itaanzishwa taasisi imara inayoheshimu wajibu wake na ikiheshimu wajibu wake hizo taasisi nyingine timiza wajibu wake
 
Kwa sababu TAKUKURU ndiyo polisi wa taasisi hizo nyingine. Ikifutwa TAKUKURU itaanzishwa taasisi imara inayoheshimu wajibu wake na ikiheshimu wajibu wake hizo taasisi nyingine timiza wajibu wake

Polisi anayeua jambazi bila hata kulifikisha mahakamani, ambalo ni kosa la jinai, (ambayo hiyo si rushwa) anasimamiwaje na TAKUKURU?
 
kwanza haina kazi,toka ianzishwe imeshindwa kutushawishi kwamba kwa nini tubaki nayo,kwa nini iendelee kutumia kodi zetu.
kazi zote inazofanya zinaweza kufanywa na jeshi la polisi. kwanza ni watu wenye tamaa ya utajiri wanashindana kununua magari kwa hela haramu.
mimi nashauri ivunjwe mara moja kwa sababu kazi wanayofanya ni tofauti na waliyotumwa(kutetea wala rushwa)

Kwa hiyo Jeshi la Polisi ndio halina mapungufu?
 
kwanza PCCB au taasisi ya rushwa ni tamanio la utawala bora. kwa maana nyingine ikle ueleweke kuwa kuna utawala bora nchini inatulazimu tuwe na chombo kama hicho au kinachofanya kazi kama hawa PCCB. mimi kwa maoni yangu kiwe huru sio chini ya rais. kifanye kazi kwa uhuru sio kusafisha kina chenge. kinaweza kikavunjwa kiundwe chombo kingine makini zaidi ambacho politicians hawatakuwa na mamlaka nacho.
PCCB ilisfisha Richmond. ikaongopwa wakati wa uchaguzi. wengine kikawa ni marafiki zao na kuwalinda .ahaaaaa
 
The thing is PCCB ndio ndio mhimili mkuu wa kuanika maovu ya rushwa katika idara zote za serikali....ikiwemo hizo taasisi ulizozitaja hapo kama TRA etc. Kinachokwaza watu ni kwamba kama integrity ya PCCB iko highly questionable, tutarajie kipi cha maana kutoka PCCB kuhusu uwezo wake wa kumulika maovu katika taasisi zingine za serikali ikiwemo TRA???? Hii ina maana kwamba kama PCCB wangekuwa wana high integrity and professional due diligence hata hayo matatizo yaliyoko idara zingine za serikali wangekuwa wameshayaona zamani....kwahiyo vitu kama wafanyabiashara wakubwa kukwepa kulipa kodi ingekuwa ni historia.... PCCB ya sasa ni chombo mahsusi kinachotumiwa na mafisadi kufunika maovu yao.....What a shame!!!!
Mara kadhaa uongozi wa TAKUKURU unapokosea jambo wananchi mbalimbali huwa wanakimbilia kudai kwamba Taasisi hiyo ifutwe! (Kwa mfano soma Gazeti la Mwananchi la leo) Sijawahi kusikia kwamba Taasisi nyinginezo viongozi wake wanapokosea idaiwe kwamba Taasisi zao zifutwe!
- TRA inawabeba wafanyabiashara wakubwa na wanakwepa kodi kuliko maelezo, sijawahi kusikia hoja kwamba ifutwe.
- Polisi "wanachakachua" rushwa si mchezo na wanaonea mno wananchi, wengine huuawa hata bila kufikishwa mahakamani kila iitwapo leo lakini hatujasikia kwamba Jeshi hilo lifutwe.
- TANESCO wanatukatia umeme mara kwa mara lakini sijawahi kusikia wakidai ifutwe.
- Usalama wa taifa ndio uko likizo si mchezo, ni kama haupo, lakini sijawahi kusikia hoja ya kufutwa kwa Taasisi hiyo nyeti.
nk, nk, nk, nk.....

Kwa nini linapokuja suala la TAKUKURU huwa inatolewa hoja kwamba ifutwe? Wengine hudai kwamba iwe chini ya Bunge. I can't imagine kwamba chombo cha utendaji ambacho kinatakiwa kiwe chini ya executive kinakuwa chini ya Parliament. After all Wabunge (hasa wa CCM) ni wala rushwa wakubwa, sasa TAKUKURU ikiwa chini yao si ndio watang'oa hata yale meno machache ambayo TAKUKURU ilikuwa imebakiwa nayo?
Tujadili wandugu!
 
Polisi anayeua jambazi bila hata kulifikisha mahakamani, ambalo ni kosa la jinai, (ambayo hiyo si rushwa) anasimamiwaje na TAKUKURU?

Takururu ni chombo kilichoundwa kwa lengo la kuthibiti Rushwa na kupambana na wala Rushwa, sasa badala ya kukupambana na wala rushwa ambao ni watumishi ktk vyombo mbalimbali kama TRA, POLISI, nakadhalika zake zote, imekua inapamba rushwa na kuwasafisha wala rushwa na mbaya zaidi wao ndio wala rushwa wenyewe.

Kwa hiyo TAKURURU haijatimiza lengo au kusudi la kuanzishwa kwake, na kama haijatimiza lengo na imekwenda kinyume na kazi iliyotakiwa kufanya, basi na Ifutwe.

Kesi ya polisi kuuwa jambazi ni tofauti kidogo na kesi ya TAKURURU. Kwanza jambazi ni muuaji na anapokuja kukuvamia pale ni ama zako, ama zake, manaka amejiandaa kukumaliza kwa namna yoyote ili mradi apate kile kilichomleta.

Kwa namna ingine naweza kusema jambazi ni adui kama maadui wengine, ni mwanadamu ambaye utu wake umeondoka anaishi kama mnyama mkali anayewinda wanadamu wenzake.

Na kama umevamiwa na jambazi, kama yeye hajakuuwa labda wewe umuue au Mkono wa Mungu ukunusuru katika makucha ya jambazi huyo/hao.

Na polisi nae anapopambana na jambazi ni ama za polisi au za jambazi, ni vita hiyo kati ya polisi na jambazi sasa polisi atamkamata vipi mtu mwenye silaha na uwezo wa kukatisha maisha yake?

Jamani usiombe kuvamiwa na jambazi, wapo watu waliopoteza wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwa unyama wa jambazi, ndio maana nasema jambazi ni adui wa mwanadamu aliyebebwa katika boksi lenye umbo kama mwili wa mwanadamu.

Na Mungu ameturuhusu kupigana ma maadui zetu, tena anasema yeye ni Mungu wa adui zetu na yeye pia ni bwana wa majeshi.
Kwa nguvu zake polisi akimkuta jambazi anavamia akifanikiwa kumuua na amuue tu kwani kinyume na hapo ni yeye anauawa.

Mi naona hata lisiitwe kosa la jinai, lakini polisi akikamatwa anapokea rushwa na akamatwe na akipokea rushwa ili kumtetea jambazi na akamatwe.
 
inabidi ifutwe kwa sababu hizo taasisi nyingine zilikuwepo tokea enzi hizo....takukuru imeanzishwa juzi juzi tu hapa, na haifanyi kazi iliyotakiwa kufanya....na kazi yake ni moja tu....kudeal na mambo ya rushwa.....ambayo haideal nayo......hizo taasisi nyingine zinafanyaka kazi zake, ingawa mara mojamoja zinachemsha lakini kwa ujumla kuna kitu kinafanyika.......TAKUKURU ni kushnehe....na wanaendelea kuharibu....
 
Kwa nini Taasisi nyingine nazo zisifutwe?

Tatizo hawa wameanza kujihusisha nanani ni kiongozi msafi hapa kwenye ka-Jamhuri ketu...wanapanga nani aitwe mwizi na mwizi gani asiwe mwizi..it's pathetic..that's why......tunataka wafutike kwenye uso wa dunia!
 
Mara kadhaa uongozi wa TAKUKURU unapokosea jambo wananchi mbalimbali huwa wanakimbilia kudai kwamba Taasisi hiyo ifutwe! (Kwa mfano soma Gazeti la Mwananchi la leo) Sijawahi kusikia kwamba Taasisi nyinginezo viongozi wake wanapokosea idaiwe kwamba Taasisi zao zifutwe!
- TRA inawabeba wafanyabiashara wakubwa na wanakwepa kodi kuliko maelezo, sijawahi kusikia hoja kwamba ifutwe.
- Polisi "wanachakachua" rushwa si mchezo na wanaonea mno wananchi, wengine huuawa hata bila kufikishwa mahakamani kila iitwapo leo lakini hatujasikia kwamba Jeshi hilo lifutwe.
- TANESCO wanatukatia umeme mara kwa mara lakini sijawahi kusikia wakidai ifutwe.
- Usalama wa taifa ndio uko likizo si mchezo, ni kama haupo, lakini sijawahi kusikia hoja ya kufutwa kwa Taasisi hiyo nyeti.
nk, nk, nk, nk.....

Kwa nini linapokuja suala la TAKUKURU huwa inatolewa hoja kwamba ifutwe? Wengine hudai kwamba iwe chini ya Bunge. I can't imagine kwamba chombo cha utendaji ambacho kinatakiwa kiwe chini ya executive kinakuwa chini ya Parliament. After all Wabunge (hasa wa CCM) ni wala rushwa wakubwa, sasa TAKUKURU ikiwa chini yao si ndio watang'oa hata yale meno machache ambayo TAKUKURU ilikuwa imebakiwa nayo?
Tujadili wandugu!

Hiyo Quote yote ni upuuzi mtupu, hakuna cha kujadili hapo, zoote TANESSCO, TAKUKURU na nyinginezo doesn't make sense
 
inabidi ifutwe kwa sababu hizo taasisi nyingine zilikuwepo tokea enzi hizo....takukuru imeanzishwa juzi juzi tu hapa, na haifanyi kazi iliyotakiwa kufanya....na kazi yake ni moja tu....kudeal na mambo ya rushwa.....ambayo haideal nayo......hizo taasisi nyingine zinafanyaka kazi zake, ingawa mara mojamoja zinachemsha lakini kwa ujumla kuna kitu kinafanyika.......TAKUKURU ni kushnehe....na wanaendelea kuharibu....

Kwani taasisi kuwepo muda mrefu ndio kuwa na ufanisi?
 
Kitu mhimu ni kuelewa hoseah na chenge wana ukaribu gani na ni kina nani katika nchi hii. yapo maneno kwa familia zao ziko jimbo moja huko kwa obama. kwa hiyo hawana uchungu na nchi hii. kwa nini wasibebane? lakini tumesema mara ngapi kuwa hoseah yupo kuwavuruga watanzania kwa maslahi binafsi? nani asiye jua kuwa chenge akiwa waziri mwenye mamlaka husika alimuuzia hoseah nyumba mbili za serikali katika mazingira tata? hivi kweli katika wakati huu ambao mpasuko unawasumbua watawala, ni muda muafaka wa kuwasafisha mafisadi?
 
Back
Top Bottom