DNA watoto si wetu - Wanawake Mnatuambiaje hapa ?

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
`Nusu ya waliopima DNA watoto si wao`




Na Mwandishi wetu



9th July 2010







Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, imesema nusu ya watu waliokwenda kupima vinasaba (DNA) kutokana na kuwa na mashaka haya na yale, vipimo vimeonyesha kuwa si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Vifaa na Matengenezo wa ofisi hiyo, Emmanuel Gwae, wakati akizungumza katika maonyesho ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema tangu huduma hiyo ianze kutolewa na taasisi hiyo mwaka 2005, watu zaidi ya 2,000 walifika kupata vipimo kujua uhalisia wa watoto wao.
Alisema karibu nusu ya watu hao waliofika na kupimwa ilibainika kuwa watoto waliokuwa nao hawakuwa wa kwao.
Alisema idadi ya watu wanaokwenda kupata vipimo imekuwa ikiongezeka kuliko miaka iliyopita.
“Huduma hii ni kama imechelewa maana watu wanakuja kwa wingi sana kupima uhalisia wa watoto wao na wengi wanaopimwa wanakuta watoto si wao,” alisema.
Alisema kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha matokeo hayo ikiwemo kubadilishana watoto wakati wa kujifungua.
Alisema katika hospitali zenye mlundikano mkubwa wa wanawake wanaojifungua, baadhi ya wanawake kwa makusudi wanaweza kuwabadilishia wenzao watoto.
Alisema hali hiyo pia inaweza kutokea hata bila kukusudia kutokana na mazingira ya hospitali.
Alisema vipimo vya DNA hugharimu shilingi 300,000 na mhusika anaweza kupata majibu ndani ya wiki moja.
Alisema kabla ya mhusika kwenda kupata vipimo lazima apeleke kwa mkemia barua kutoka mahakamani, kwa wakili au ofisi ya ustawi wa jamii na kueleza sababu ya kutaka kupima.
 
Lazima ujue kwamba, mtu anayeenda kupima maana yake tayari ana shaka, kwa hiyo usitegemee kwamba matokeo haya yako reflective of the general population.

Lakini hata baada ya kujua hilo, nusu ni figure iliyo very high. Ukimwi utaisha kweli ?
 
Tatizo ni lipi tena? anyway--inaonekana uaminifu katika ndoa umekwazika kwa kiasi kikubwa--in brief, hakuna tena uaminifu ktk ndoa!! very unfotunate..
 
Na ukihesabu na wanaume wanaopata watoto nje ya ndoa zao au kuwa na vimada lazima utambue kuwa Tanzania bila ukimwi haiwezikani
 
Kama daktari(specialist) anaweza ku operate mguu badala ya kichwa na kichwa badala ya mguu...then uzembe wa nurses kubadilisha watoto utakuwa haulezeki...especially neither of the parents cares.Ni jambo dogo tu la kuhakikisha kuwa mtoto na mama wanawekwa tags immediately after delivery inakuwa ngumu sana ndani ya Bongo.
Sometimes tunagundua kwamba one is NOT biologic father to a kid pale tunapohitaji blood transfusion na kuona ABO are completely un matching.....ukimfanya counselling mother kwa ahadi kuwa hutotoa siri anaweza kukueleza ukweli kwamba ali cheat na unfortunately kupata mtoto.

Awesome
 
Niliposoma hiyo kitu wazo la kwanza lilikuwa ni hii ni "Marketing Campaign" hawa jamaa wa kupima DNA, wanawatisha watu wapate wateja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom