Dna matching in tanzania

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,859
1,301
WanaJF naomba mnisaidie. Nataka kufanya DNA matching na watoto wangu, Wapi naweza kupata huduma hiyo hapa Tanzania, kwa utaratibu upi na gharama zipi.Asanteni kwa msaada wenu.
 
Humuamini mkeo mkuu? Yapi wamekusibu? Siku hizi ni mpaka upate kibali cha mahakama ili kuelezea sababu ya wewe kufanya DNA!! Gharama inategemea idadi ya DNA but nenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali jirani na Ocean Road Hospital inapakana na the National Institute for Medical Research (NIMR) na utapata Gharama halisi.
 
Bora utulie tuu , uwe mpole kama familia yako ina amani. maana ukikuta watoto wote sio wako itakuwaje?
 
Yote yanawezekana maana kila mtu anatembea na viungo vyake japo mkioana mnaambiwa mmekuwa mwili mmoja.
Ni kweli kuna mambo ukiyajua yatakutesa sana, mojawapo ni hilo la kujua kuwa watoto/mtoto si wako; lakini si ni bora ukajua na mkakubalina na mwenzio kwamba uwe siri au baba za watoto wasaidie malezi? Inawezekana nina watoto kwa wake wa watu na ninasaidia matunzo hivyo hakutakuwa na ubaya kama nami nikasaidiwa matunzo kama kuna mtoto si wangu - au vipi?
 
Kuna profesa mmoja alikuwa nje ya nchi kimasomo, aliporudi akawa na mashaka ya ujauzito wa mkewe, mtoto alipozaliwa vipimo vya DNA vikaonyesha sio wake.Alipoomba ushauri amtimue wife, Ma dr wenzie wakamshauri kama wife anatabia hiyo basi akawapime na wale wengine wawili wakubwu kabla ya kumfukuzi.Inatia uchungu sana kama utalea na kusomesha mpaka chuo kikuu toto amabalo sio damu yako.inauma sana! Kwani wewe umewahi kuhisi/kuambiwa mpenzi wako ana cheat?
 
Yes, nimeambiwa ana-cheat!
 
Haitii uchungu kusomesha watoto wasiokuwa wako. Na usiite litoto. Kakangu mkubwa sikujua kama ana mama yake, nilijua nikiwa 15+ of age. Haikubadiliaha upendo na bond yetu hata leo. Bond inatokana na maisha ya kila siku, na sio mbegu iliyotungisha mimba.

Ningekuwa mimi muuliza swali wala nisingehangaika na dna. Ningeshughulikia tatizo la cheaying kwenye ndoa yangu. Ni muhimu kuongea na mwenzio na kujua kama anataka nini na anategemea nini kwenye ndoa yenu. Pole, tuliza akili usikurupuke. Huenda ukajiumiza zaidi.
Kuna profesa mmoja alikuwa nje ya nchi kimasomo, aliporudi akawa na mashaka ya ujauzito wa mkewe, mtoto alipozaliwa vipimo vya DNA vikaonyesha sio wake.Alipoomba ushauri amtimue wife, Ma dr wenzie wakamshauri kama wife anatabia hiyo basi akawapime na wale wengine wawili wakubwu kabla ya kumfukuzi.Inatia uchungu sana kama utalea na kusomesha mpaka chuo kikuu toto amabalo sio damu yako.inauma sana! Kwani wewe umewahi kuhisi/kuambiwa mpenzi wako ana cheat?
 
Nashukuru kwa michango na ushauru wenu, nadhani jibu nimepata kwamba ni kwa mkemia mkuu wa serikali tu, na kuna procedure lazima nizifuate.
Ninataka kulinganisha hizo DNA ili hata kama nikilea nijue kuwa mimi ni mlezi siyo mzazi! Unajua haya mambo mnaweza kufichaficha lakini iko siku utayajua. Ni vyema ukayajua mapema ukazoea kuliko kuyajua wakati umechelewa; by then itakuuma zaidi maana utakuwa huna hata alternative. Kwa mfano unahangaika hadi mtoto anamaliza chuo kikuu na kupata kazi (miaka 24 -kama alianza akiwa 7 yrs) wewe kama ulisoma na ukawahi kuoa utakuwa na around 52; na hapo ndipo ukajua kuwa mtoto si wako, utafanya nini. (na kumbuka baba wa watoto wa aina hii hujitokeza mtoto anapoanza kufanikiwa)
Ni bora ujue mapema, kama ni kuachana muachane utafute mwingine mapema- au vipi!
 
Back
Top Bottom