Dkt. Slaa: Sitta ni kielelezo cha mfumo uliooza, mlinda mafisadi na ufisadi

Kwani we hujui kama Slaa siku hizi anaitwa mzee wa mipasho kutokana na tabia yake aliyoanza ya kuzungumza kama yuko kwenye kidole juu...
 
Walahi vandugu zangu, Kikwete aliipigia magoti Chadema iwapo CCM wangemtosa angeibukia Chadema? Kama vituko vile lakini ndio hali halisi ya wenye uchu na uroho wa madaraka.
 
Sitta sio kana kwamba ni mnafiki bali ni fisadi wa kutupwa hivyo hana maadili ya uongozi; pale alipokuwa Spika alikuwa anatumia mali za serikali hasa magari kwa kuwahudumia vimada wake na hilo sio siri!!
 
Sina uhakika mtu anaejiita chama ni mtanzania,na kama ni kweli uko Gongo la mboto basi ulipata ajari ya mabomu na hautumii ubongo wako,nakushauri uende Mikocheni B upate baraka za mch,dr& mbunge halafu upite Nzega upate vitumbua na 2000 toka kwa Bash na Kigwange labda na njaa inakutesa.Ukishiba usubirie mazishi ya sisi-m.
 
Dr. Slaa umetenda vema. Kwanza umeonesha ulivyo mkomavu wa siasa kwa kuamua kutomwaga siri nzito kama hizo kwa miaka takribani miwili. Kwa kufanya hivyo, ulijitunzia silaha dhidi ya mnafiki na mbinafsi Sitta. Shetani alivyo wa ajabu na muaibishaji mkubwa alimsahaulisha Sitta mambo yote hayo na kumpatia jeuri ya kutamka mabaya yasiyo na msingi dhidi ya CHADEMA. Sasa cha moto amekiona. Angekuwa ni baba yangu ningemshauri mzee Sitta ajiuzulu siasa na kubwaga manyanga ya uwaziri wake na uongozi wa umma kwa ujumla.
 
images


Mjumbe huyo wa NEC na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga aliyejipambanua kupiga vita ufisadi na vitendo viovu ndani na nje ya CCM, alisema historia ya Waziri Sitta inajionesha wazi kwamba ni 'mkorofi na msaliti mkubwa', kwani mwaka 1966 akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alishiriki maandamano hadi Ikulu kupinga sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).


Alisema katika harakati zao hizo za kupinga sheria hiyo iliyotaka kila mwanafunzi wa Chuo Kikuu lazima ajiunge na Jeshi la Kujenga Taifa, Baba wa Taifa wakati huo akiwa Rais wa nchi na mkuu wa chuo hicho, alilazimika kumchapa viboko Sitta kutokana na usaliti wake huo kwa serikali.


Mgeja alisema mbali na kufanya maandamano hayo, Sitta na wenzake ambao wengine ni marehemu kwa sasa walikuwa na mabango yenye ujumbe mkali kwa serikali, ukiwemo uliosema 'Onyo kali na la mwisho kwa serikali', na kwamba alikuwa akiipinga pia Serikali ya Baba wa Taifa huku akiusifu uongozi wa kikoloni.

"Huyu Sitta ambaye leo hii anawadanganya watu, kipindi hicho akisoma Chuo Kikuu alikuwa akiipinga serikali na kudai afadhali serikali ya kikoloni. Tusipoamini leo usaliti wake huu tunasubiri hadi aje shetani atuambie usaliti wa Sitta ndipo tuamini?
 
Hapa kuna haja ya kujiuliza mambo machache.
Sababu iliyopelekea Sita kuropoka mambo ambayo alifahamu fika kuwa yatawaudhi watu aliokwisha kufanya nao mikutano ya siri ni nini? Je hakufahamu kuwa wangemjibu?
Ni rahisi baada ya kujiuliza hayo kuona ukweli wa mambo kuwa inawezekana Sita na wenzake wameshona "they underestimated Chadema" a political error and a miscalculated move. Walidhania kuwa hicho chama kingdhoofika kama wasingewakubali jinsi walivyotaka?
Kinyume chake Chama kinazidi kukomaa, na kushika kasi nchi nzima, sasa kuna wanaofikiria kujiunga sasa hivi hawatapata tena ule umaarufu waliokuwa wategemee?
Je inawezekana kuwa sita na wenzake wameanza kuwataka Chadema waanze kuwafuata ili kuwaomba wajiunge nao ili kuwa na viongozi wa kutosha wa kisiasa?
Inawezekana kuwa wameshajua wazi kuwa kwa jinsi hali inavyoendelea hakuna tena uwezekano wa wao kuchaguliwa kuwa wagombea CCM, kwahiyo wanatafuta namna watakavyoshirikiana na Chadema kuunda serikali hapo baadaye wakati wakiunda chama kipya (au wakishajiunga na chama chao kipya)?
Lakini mbona busara zaidi isingetumika wakati wa kuzungumzia mambo haya ili yasiwe kikashfa kashfa namni hiyo?

Bila kusita nashindwa kujizuia kusema tu kuwa Sita hapa hakutumia busara. Nashindwa kuelewa alikuwa anataka kuchuma nini kutokana na kauli zake hizi.
Hapo hapo anajikanganya kwa kusema wazi jukwaani mbele ya wananchi kuwa Chama chake kimegubikwa na Ufisadi na hakiwaletei wananchi matumaini ya mabadiliko kimaendeleo.

Is the politician going bananas so early before its even 2014??
 
MIMI NILIDHANI UNAKANUSHA KUMBE ALIYOSEMA DK SLAAH NI KWELI!!??

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Ndio maana kawaeleza kwamba safu yenu ya uongozi ni nyembamba,bila majeshi ya kukodi hamuwezi kusonga kwa kuwa anaijua chadema kuliko nyie chadema kata wengi kwa yeye alifikia kubembelezwa na chadema ili awasiadie kugombea urais,jiulize huyo slaa wako alikua wapi?na kama ndoa yake ilimshinda nchi ataiweza?amrudie kwanza mkewe ndio tutaona amekomaa,tunaweza kumfikiria kumpa nchi huyo slaa wenu aliekataliwa na kanisa
 
Walahi vandugu zangu, Kikwete aliipigia magoti Chadema iwapo CCM wangemtosa angeibukia Chadema? Kama vituko vile lakini ndio hali halisi ya wenye uchu na uroho wa madaraka.
kwanini chadema haiandai wagombea wake inasubiri mizoga ya ccm kila siku?ni kweli ina safu nyembamba ya watu weny sifa za uongozi au?
 
kwanini chadema haiandai wagombea wake inasubiri mizoga ya ccm kila siku?ni kweli ina safu nyembamba ya watu weny sifa za uongozi au?

Sikufahamu kuwa umempata vizuri Sitta mwenye mawazo hayo.

Tatizo wengi wanafikiri Chadema wakishika nchi basi hawana kazi, la hasha. Kinachobadilika ni mwongoza kiti cha magogoni na safu yake ya mawaziri wakiwemo waandamizi wachache katika ngazi ya taifa ambao ajira ya ukomo wao hushia Rais anapomaliza kipindi chake.

Watumishi wengine watabaki kama walivyo, isipokuwa kama utendaji wao hauridhishi ndipo ufagio wa chuma utakapowapitia na maumivu yatabaki ni mjukuu, na wasahauliwa ndio watakaochukua nafasi kuonyesha uwezo wao wa waliopigania nchi yao kurudisha heshima stahiki.
 
images

images
Dr Slaa: Sitta Mnafiki
images



  • Je, yametimia Samweli Sitta ni manafiki kama alivyosema Dr Slaa?

Baada ya uchaguzi Mkuu uliopita katika moja ya majibu ya Dr Slaa dhidi ya Samwel Sitta alipokuwa anaponda kuhusu vyama vya upinzani, Dr Slaa alijibu kifupi kwamba "Samwel Sitta ni mnafiki." Tamko hilo lilionekana kama jepesi na rahisi mno kwa wakati huo wengi tukijua kwamba Samweli Sitta alijijengea jina zuri alipoliongoza bunge akiwa Speaker wa Bunge la Muungano kwa weledi.

Kwa sasa imesomeka vema kwamba Samweli sita kipindi hicho kwa unafiki wake:
Kwa vile alitengeneza mazingira akubalike na Chadema agombee urais kupitia chama hicho alifanya kila awezacho kujikomba kwa vyama vya upinzani ili aonekane anatenda haki kumbe lengo ili akubalike kugombea urais kupitia Chadema, lakini aliwageuka na kuanzisha chama chake kwa siri ambacho alishirikiana na Nape. Kipindi hicho alianza kampeni kama anazofanya Lowasa sasa hivi kupita makanisani na kutunuku vyeti vya wahitimu vyuoni ili kujitangaza.

Sitta alipowaacha Chadema kwenye makutano ya mataa ya Ubungo, huku Dr Slaa akiwa ameshachukua form ya kugombea ubunge jimbo la Karatu, ikabidi Kamati Kuu Chadema warudi Mtaa wa Ufipa kwenye kikao cha dharura na kumbembeleza Dr Slaa asitishe mbio za ubunge na ashike bendera ya Chadema kupeperusha kugombea nafasi ya Uraisi. Hii ilitokana na unafikiwa wa Samwel sitta.

Kwa sasa napata picha kwamba CCM walikuwa sahihi kumwengua katika kiti cha Uspeaker na kumweka mama laini, legelege na anayefuata upepo Bi Kiroborobo kwa vile Sitta alisomeka ni mnafiki, pengine angeendelea kuwa speaker wa bunge angeharibu zaidi ya Makinda.

Mwenyekiti wa awali katika bunge hilo yule mzee wa Visiwani mwenye mvi nyingi kichwani alitumia busara na kuonyesha hekima sana na katika kamati kadhaa alishirikisha wajumbe toka upinzani pia na tulishuhudia hata wajumbe wa CCM walimsifia Lissu kwa weledi alipoongoza moja ya kitengo cha sheria katika utungaji wa sheria za bunge hilo, na wakadiriki kusema angefaa kama angekuwa mwanasheria wa serikali kuliko Werema.

Sitta alipochaguliwa kukalia kiti cha U-speaker alibadilisha upepo na kufanya bunge kuwa ni la CCM kinyume cha matakwa ya wananchi na sheria ya kuunda bunge hilo ambalo ni la kitaifa. Kwa uongozi wa Samweli Sitta katika bunge la Katiba mpya ameligawa taifa badala ya kuliunganisha zaidi kuwa kitaifa. Ameelemewa na uchama badala utaifa alio nao Warioba. Sitta ameendesha Bunge la Katiba Mpya kwa masilahi binafsi badala ya Kitaifa na matokea yake amechafuka na kupoteza kabisa umaarufu aliokuwa nao.

Dhambi ya unafiki ya Samwel Sitta itamfanya maisha yake anayone machungu zaidi akikumbuka alichowaharibia wananchi haki yao, pia kuchafuka kwa Sitta ni nafuu ya akina Lowasa, sasa huyu ndiye anayetaka kuwa Rais wa Tanzania kwa unafiki huu ataipeleka wapi nchi yetu? Katika biblia inasomeka: "Kimtokacho mtu ndicho kimchafuacho!" Ndicho alichochafuka Sitta.

Mbaya zaidi amemharibia Kikwete heshima aliyojijengea kimataifa kufanikisha kuendesha mchakacho wa Katiba mpya kwa utaratibu na ufanisi bila ushinikishwaji wa vita kama baadhi ya nchi, na sasa Kikwete heshima hiyo imeota mbawa sababu ya unafiki wa Swamwel Sitta.


:juggle: Je, yametimia Samwel Sitta ni mnafiki kama ilivyotamkwa na Dr. Slaa? :juggle:​
 
hakuna mnafki nchi hii kama slaa amesaliti familia.ndoa.kanisa na MUNGU pia hafai kuwa hata mjumbe wa nyuma kumi na cdm itamfia tu
 
Back
Top Bottom