Dkt. Slaa: Sitta ni kielelezo cha mfumo uliooza, mlinda mafisadi na ufisadi

Hivi wewe Dr. Slaa unafahamu maana ya mnafiki? wewe ndie umekaa kinafiki zaidi iweje uyaseme leo? Kama ungekuwa mkweli ungeyatoa hadharani siku nyingi; habari ya Sitta na CCJ haina mshiko tena; umesahau unafiki wako? Kwa akili yako unafikiri ni nani atayekuamini zaidi ya wanachadema wenzako; hebu teuleze kati ya hayo mawili ulianza lipi ulianza kujivua upadri ukaingia kwenye zinaa au ulianza zinaa ukajitoa upadri, jiangalie kwenye kioo utajiona ni mnafiki wa kiasi.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu mbona hapa umepwaya sana?
 
Baada umshukuru Dr kwa kukusaidia kujua mambo kiundani na ukweli we una laumu!

Ulitegemea zawadi gani apewe mtu anaye kashfu wenzie?

Kila atakaye jichanganya ata pewa dozi kulingana na uzito alionao.

Hivi wewe Dr. Slaa unafahamu maana ya mnafiki? wewe ndie umekaa kinafiki zaidi iweje uyaseme leo? Kama ungekuwa mkweli ungeyatoa hadharani siku nyingi; habari ya Sitta na CCJ haina mshiko tena; umesahau unafiki wako? Kwa akili yako unafikiri ni nani atayekuamini zaidi ya wanachadema wenzako; hebu teuleze kati ya hayo mawili ulianza lipi ulianza kujivua upadri ukaingia kwenye zinaa au ulianza zinaa ukajitoa upadri, jiangalie kwenye kioo utajiona ni mnafiki wa kiasi.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Nimkweli kuwa kuwa Sitta ni mwanasheria by training, lkn hajawahi practice law hata siku moja, sawa na Pinda tu!

Kwa hiyo it may not be right to refer to him as mwanasheria. Practice makes perfect!
 
WanaSIASA wetu! Sitta anafahamika kwa ukigeugeu na uzabizabina wake. Dr Slaa umetusaidia sana ingawa kwa kuchelewa mno. Jamaa kwenye ziara yake ya Kagera ni kama vile keshateuliwa kugombea URAIS. Nakuomba tu Dr Slaa uendelee kutudungulia mmoja baada ya mwingine hawa "wagombea URAIS wa CCM. Najua unawafahamu wote.
 
We akili yako nzuri kweli? Kwa hiyo sita alimpigia el. Kutaka kugombea uspika kupitia chadema eh,!!!!!???????.ndo mana tunapewaga ban kwa ajili ya mijin...ga ka wewe.
Ish!! Mbona maelelezo haya ni ya EL aliyompa Slaa ili ayaseme. Kalaga baho
 
sikutegemea mtu kama sita kwa nafasi yake na yeye afanye siasa za kina nchemba ..ni kujiabisha kama sio kuaibishwa, amejitakia mwenyewe na amefanya la maana coz ndo yale ya kulazimisha jamii iendelee kulitaja jina lake kwa mambo yasio na msingi (cheap popularity), sidhani kama kulikuwa na ulazima wa kumu attack mtu (mboye) amekurupuka
 
[h=2][/h] Jumamosi, Septemba 01, 2012 06:40 Na Mwandishi Wetu, Iringa

dk.%20slaa.jpg
Dk. Wilbrod Slaa

*Asema ni kiongozi asiye na kumbukumbu
samwel.jpg
Samuel Sitta


*Atoboa siri namna alivyohaha kuhamia Chadema
*Aliahidi kuhama na wabunge 50, akaingia mitini
*Alitaka apewe nafasi ya kugombea U-spika akakosa

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa amemfyatua Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta kuwa, ni mwanasiasa mwenye tamaa na asiyekuwa na kumbukumbu.

Kauli ya Dk. Slaa, imekuja siku moja baada ya Waziri Sitta, kudai ndani ya CHADEMA, Dk Slaa pekee ndiye anafaa kugombea urais.

Mbali na kauli hiyo, pia Waziri Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki, alidai Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe hana uzoefu wa uongozi, zaidi ya kuwa mzoefu wa kuongoza kumbi za disko.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa jana, Dk. Slaa, alisema hatua ya Waziri Sitta kuingilia masuala ya ndani ya CHADEMA, ni ishara tosha kuwa, ameanza kupoteza mwelekeo.

Alisema badala ya Waziri Sitta kuzungumzia vyama vingine, anapaswa kuhakikisha amani ndani ya chama chake (CCM) inadumu, ili asipate kiwewe cha kujiandaa kukimbia kama alivyotaka kufanya kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Alisema mwaka 2010, Waziri Sitta, Wizara ya Uchukuzi, Dk. Harisson Mwakyembe na aliyekuwa Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe, ndio waasisi wakuu wa Chama cha Jamii (CCJ), ambapo walikutana na viongozi wa CHADEMA katika ofisi za Spika mjini Dodoma.

Alisema katika moja ya azimio lao, waliweka wazi na kusema wanaanzisha CCJ kwa mujibu wa sheria na kama ikishindikana kupata usajili wa kudumu, wangehamia CHADEMA.

“Sitta akiwa Spika wa Bunge, Mwakyembe na Mpendazoe walikuja kwetu kuomba kujiunga na CHADEMA, kama CCJ isingepata usajili wa kudumu, sasa inakuwaje leo anaibuka na mambo ya ajabu,” alisema Dk. Slaa.

Alisema baada ya makubaliano hayo na kuiangalia Katiba ya CCJ kwa kiasi kikubwa, ilikuwa inafanana na ile ya CHADEMA, hivyo kubaini malengo yao yanafanana.

Kutokana na hali hiyo, kwa kauli moja wakakubaliana kwa pamoja Waziri Sitta, awe mgombea urais kupitia CHADEMA, lakini dakika za mwisho aliwageuka wenzake na kuendelea kubaki CCM.

“Jana nimepigiwa simu na waandishi wengi wakitaka kauli yangu, basi kwa kuwa Sitta ameamua kutuchokoza, nami nimeamua kumpiga ngumi…nimeamua kumpa za uso, ili wenzake waone manundu yanayomtoka, anasahau matendo yake aliyofanya siku za nyuma,

…napenda kuwaambieni Sitta ndiye anayetuongoza leo, haaminiki hata ndani ya dhamira yake…tulikutana naye zaidi ya mara 100 na kuandikiana vimemo, yeye akiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania… kama anabisha ajitokeze akanushe juu ya uhaini wake ndani ya CCM.

“Alikuwa ananipigia simu kuanzia saa 6 usiku, baada ya kutoswa na CCM kwa bahati mbaya, simu yangu ilikuwa katika mtetemo na saa 12 asubuhi nikapokea simu ya mke wake, Magreth Sitta, akiniambia… Dk. baba anataka kuongea na wewe na alikutafuta kuanzia usiku.

“Wakati napokea simu ya Sitta, jambo la kwanza aliomba nimzuie Marando asigombee Uspika, ili agombee yeye na kwamba angeitisha mkutano na waandishi wa abarrí, kwa ajili ya kutangaza kujiondoa CCM, kwa kuwa alitoswa kuwania nafasi hiyo,” alisema Dk Slaa.

Alisema wakati huo, Sitta alikuwa akimweeleza kuwa, ana kundi la wabunge 55, ambao walikuwa wamepania kuondoka ndani ya CCM, na wangefanya hivyo siku tatu kabla ya Bunge la mwaka 2010, kuvunjwa.

Alisema kutokana na ukigeugeu wa Sitta, haukuishia hapo kwani wakati wa mchakato na hatimaye uchaguzi wa kumpata Spika, alitoswa kitendo kilichomfanya atumie muda mwingi kuwapigia simu viongozi wa CHADEMA, ili apewe nafasi ya kugombea kiti hicho.

“Wakati wakijiandaa kukutana na waandishi wa habari, Sitta alinipigia simu na kuniambia amepigiwa simu kutoka kwa wakubwa ambao wamemuahidi kumpatia nafasi ya naibu waziri, jambo ambalo mimi nililipinga naye.

“Sitta hakukubaliana na nafasi ya unaibu waziri, akaanza kupata mashaka ya kama anaweza kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu…kama kiongozi wa aina hii, anawaza nafasi za juu, badala ya kuwatumikia Watanzania hatufai hata kidogo ndani ya CHADEMA,” alisema Dk. Slaa.

Alisema kwa tabia ya kiongozi huyo, hana uadilifu unaoweza kulingana hata na kiongozi wa ngazi ya kata wa CHADEMA, kwa kuwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuzuia hoja mbalimbali za ufisadi zilizokuwa zikielezwa na wabunge wa CCM.

“Mnakumbuka hoja ya Buzwagi, aliyoitoa Kabwe Zitto, aliyemtuhumu aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, eti amesema uongo na kulidanganya Bunge… Sitta alipindua hoja ya Zitto na kumfungia kwa kipindi cha miezi minne,” alisema Dk. Slaa.

Akizungumzia kauli yaMbowe, kuwa ni muongozaji wa kumbi za disko, Dk. Slaa alisema Sitta kama mwanasheria na waziri aliyepewa fadhila ya kuongoza wizara, anazidi kuiaibisha Serikali, kwa kuwa mamlaka na leseni ya kuendeshea kumbi za starehe zinatolewa na Serikali ya CCM.

“Sitta ni mvivu wa kukumbuka… hakumbuki hata Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wakati alipopata uongozi, hakuwa na uzoefu na nchi hii, bali aliendelea kuwatumia watendaji wa Serikali ya kikoloni, ambao walilazimika kufuata maagizo ya Serikali ya Tanganyika.


[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Dk Slaa amshukia Sitta Send to a friend
Saturday, 01 September 2012 08:05


000000000000adkslaaa.jpg
ADAI NI MNAFIKI, MWONGO, NI KUTOKANA NA KAULI YAKE KWAMBA CHADEMA HAKINA VIONGOZI
Waandishi wetu, Iringa
KATIBU Mkuu wa Chadema, Willibrod Slaa amemshukia Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akidai kwamba ni mnafiki, muongo na msaliti na kwamba hafai kuongoza umma wa Watanzania.Dk Slaa alisema hayo katika kikao chake na waandishi wa habari mjini Iringa na kusema amesikitishwa na kauli ya Sitta kwamba Chadema kuna kiongozi mmoja tu; Dk Slaa.
"Nimeamua kuzungumza na nyie kwa vile jana (juzi), wahariri wenu walitaka kujua maoni yangu juu ya kauli aliyoitoa Sitta, akikishutumu Chadema kwamba hakina viongozi na anayestahili kuwa rais bali, ni mimi tu," alisema Dk Slaa na kuongeza:
"Kauli hii inamdhalilisha mwenyekiti wetu na hili linadhihirisha kwamba mtu huyu (Sitta) ni mnafiki, muongo na msaliti...."
Alimtaka Sitta kushughulikia changamoto zinazoikabili CCM ikiwemo kuvunja makundi yanayokimaliza, badala ya kuingilia masuala ya Chadema ambayo alisema hayamhusu.
"Amalize matatizo yanayokihusu chama chake, asituingilie sisi Chadema maana hawezi kutupangia. Sisi tunao utaratibu wetu wa kupata viongozi wetu."
Alisema CCM kimeshindwa kutatua mambo mengi yanayohusu maslahi ya umma kutokana na kuwa na viongozi ambao ni vigeugeu.
Alimlaumu waziri huyo kwamba alipokuwa Spika wa Bunge, alifunga hoja mbalimbali za kupinga ufisadi zilizowasilishwa na Chadema na kwamba alifanya hivyo kwa maslahi ya kukilinda chama chake. Alisema kwa kufanya hivyo, Sitta hakuwatendea haki Watanzania.
Dk Slaa alizitaja baadhi ya hoja hizo kuwa ni mijadala iliyohusu Mgodi wa Buzwagi, kashfa ya wizi kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (Epa), Meremeta na Richmond, ambayo hadi leo haijawahi kutolewa majibu sahihi licha ya Watanzania kutaka kufahamu ukweli.
Alidai kuwa ukigeugeu wa Sitta unadhihirishwa na ushiriki wake katika kuanzishwa kwa Chama Cha Jamii (CCJ) na kwamba hawezi kukwepa tuhuma hizo kwani aliwahi kuketi meza moja na yeye (Dk Slaa), pamoja na Mbowe kujadili suala hilo.
Sitta hakupatikana jana kujibu tuhuma hizo ikielezwa kwamba alikuwa Burundi kikazi. Hata hivyo, mara kadhaa amekaririwa akikanusha kuhusika na CCJ na amekuwa akidai kuwa hizo ni mbinu za wapinzani wake kisiasa kumpaka matope.
Alidai pia kwamba Sitta siyo mwadilifu kama ambavyo amekuwa akijinasibu, akidai kwamba alipokuwa Spika, alitumia mamilioni ya fedha za Watanzania kujenga Ofisi ya Spika, jimboni kwake Urambo akiamini kwamba, angedumu kwenye kiti hicho milele.
"Kama kweli Sitta ni muungwana, ofisi hiyo anapaswa kuirudisha serikalini au vinginevyo, kila Spika anayeingia madarakani aitumie kwa kuwa hakuna Spika wa Urambo ila wa Watanzania wote," alisema Dk Slaa.
Kuhusu Mbowe, Dk Slaa alisema Sitta akiwa mwanasheria, hakupaswa kuzungumzia suala la mwenyekiti huyo kuendesha biashara ya kumbi za disko kwa madai kuwa jambo hilo siyo kosa la jinai.
"Serikali imekuwa ikikusanya ushuru kwa sababu kumbi hizo zina vibali na zimesajiliwa na Serikali ya CCM ambayo Sitta amekuwa akiitumikia," alisema.
Kuhusu Chadema kukosa viongozi wa kuendesha Serikali, Dk Slaa alimtaka Sitta aeleze Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alikopata viongozi waliomsaidia kuiongoza nchi katika kipindi ambacho Tanzania haikuwa na wasomi wa kutosha.
Alisema uongozi si uzoefu, bali maandalizi katika misingi ya uadilifu, uzalendo na weledi, hivyo kauli kwamba Chadema hakina viongozi, haina msingi.
"Ni bora kuwa na viongozi wa kidato cha sita kuliko kuwa na viongozi wasomi wasio na maadili, ikiwa tutaingia madarakani, tutahakikisha sera yetu inatenganisha siasa na watendaji wa Serikali ili kujenga nchi jambo ambalo CCM wameshindwa kwa miaka 50 ya uhuru wa taifa hili," alisema.

Kuhusu M4C
Katika hatua nyingine Dk slaa alizungumzia kampeni za Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) alisema anaishukuru polisi na Serikali kwa kuwa makatibu wenezi wa Chadema.
Alisema Serikali na polisi wanakitangaza chama hicho cha upinzani kwa umma bila kujua kwa kukifuatafuata katika mambo aliyodai kuwa hayana msingi.
Alisema kuwazuia kwao kufanya kampeni za M4C mkoani Iringa kwa sasa, kumezaa matunda kwani wamefanikiwa kuwafikia wakazi wengi zaidi wa Mkoa wa Iringa kutokana na kutembelea zaidi ya mitaa 150 Iringa mjini pekee.
Alisema mfumo huo ndio watakaoendelea kuutumia katika mikoa mingine.
Awali, Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Zanzibar), Said Issa Mohamed alisema chama hicho hakina udini wala ukabila, huku akiwaasa Waislamu kuacha kutumika kama chombo cha propaganda kuiweka Serikali ya CCM madarakani.
"Ndugu zangu Waislamu jueni Chadema haina udini wala ukabila ila inaongozwa kwa misingi ya katiba. Mnapaswa kufahamu historia ya Chadema na kamwe msikubali kutumika kama chombo cha propaganda," alisema.
Chadema kinatarajia kufanya mkutano wake mkubwa Jumapili kwenye Viwanja vya Mwembetogwa, Iringa eneo ambalo awali, walizuiwa kufanya mkutano ili kupisha shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo inamalizika leo.


 
Nashukuru mungu sijawai kumwamini Sitta hata sekunde moja, hakuna mpambanaji wa ufisadi ndani ya ccm wote ni genge la wasaka vyeo na ulaji. Hata dogo Nape alivyotoswa kugombea ubungo akataka kuamia chadema sema chadema haikumuakikishia kumpa nafac ktk jimbo la ubungo, namshanga sana leo anajifanya eti anamapenzi ya dhati na ccm, nawaonea huruma wanachama wa ccm
 
leo nkitutana na kijani lazma nmtie kofi hata moja tu..unafk wa kikwete,6 na nape hauna tofaut,uroho wa madaraka
 
Duuuuu! Kumbe na Sitta naye ni fisadi kiasi hiki! Basi ndani ya ccm hakuna wa kumfunga mwenzake kengele. Wote wameoza. Hakika Dr Slaa ni kiongozi shupavu na jasiri sana na kwa hakika endapo mwenyezi Mungu atamjalia kuwa Amiri Jeshi mkuu wa taifa letu basi Tanzania itakuwa kiuchumi kwa haraka sana zaidi hata ya Rwanda. Dr Slaa tunakuombea kwa Mungu akuzidishie afya njema na uendelee kuwa na ujasiri huo huo na zaidi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ni article ndefu lakini nimejitahidi kusoma neno kwa neno. Sikuwahi kudhani Samwel ndo alivyo hivi. Anyway, tusubiri tu, mengi bado yanakuja. Thanks dr, unatufungua sana macho aisee

Mkuu nakuunga mkono,sikuwahi kufikiri ndivyo alivyo hivi!Ok ngoja tusubiri majibu yake!
 
Akijibu tu....akinyamaza anaukubali ukweli wa rais wa wananchi,six nyumba yenu as soon itadondoka,poleni sana magamba,peeeople's power
 
samwel sitta ni mnafiki kwelikweli, kuna msemo kwmba ukiwa kijana ukawa mnafiki, ukizeeka atakuwa mchawi
Sasa sitta ameibinua hii kauli! wakati wa ujana alicheza na SANGOMA na sasa ameamua kuwa mnafiki per se!
natamani sita NEC na CC ya magamba IMPIGE chini kugombea na apachikwe fisadi papa E.L tuone atapapukia wapi huyu mzee mchovu labda ADC!
 
Dah! Mnakumbuka wakati heka heka za CCJ zinapamba moto Mzee Mwanakijiji nae akawa anaandika Makala kwenye Tanzania daima Jumatano kwa zaidi ya mara tatu mfululizo juu ya sifa na mazuri ya CCJ. Ingawa namuheshimu sana Mzee Mwanakijiji lakini ile move yake ya kipindi kile ilinitia mashaka sana.

TUMBIRI (PhD, In Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd [/SUP]Overall Best Student in Form Six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com


Mwanakijiji? Wanafiki wana mji wao!
Chama
Gongo la mboto DSM
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom