Dkt. James Alex Msekela ateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Katika taarifa yake, Katibu Mkuu Kiongozi Sefue amesema kuwa Rais Kikwete amemteua Dkt. James Alex Msekela kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.

Kabla ya hapo Mheshimiwa Msekela alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Aidha, taarifa hiyo ya Bwana Sefue imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Bwana Ramadhani Muombwa Mwinyi kuwa Naibu Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York.

Kabla ya hapo, Bwana Mwinyi alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Katibu Mkuu kiongozi amesema katika taarifa yake kuwa wateuliwa hao wawili wataapishwa keshokutwa, Alhamisi, Januari 5, 2012.

Imetolewa na
:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM
.
 
Nampongeza Rais kwa kuchanganya ili kuepuka wapotoshaji kama kina malaria sugu
 
Naona mwaka huu umeanza vizuri kwa baadhi ya watu maana vyeo vinamwagwa tu. Nani anachukua nafasi ya Sefue UN?
 
Safari itakuwa ndefu sana kwa mzee wa kaya pindi makundi yanayompinga.Hususani ndani ya chama cha magamba, yatakapomuhoji juu ya uteuzi wako wa kulipa fadhila.
 
Huyu naye si Tabora walimkataa Ubunge?

Walimkataa wakamchagua Rage lakini Rais anamtaka!

Naona na mimi sasa niingie kwenye siasa manake ukipata utaendelea kupata. Ukikataliwa na wapiga kura kama Rais anakutaka atakuteua tu ukale bata. Ngoja nifanye haraka kabla ya katiba mpya manake naona watanzania wanataka eti kila anayeteuliwa aidhinishwe na bunge! Ikiwa hivyo hata maana ya Urais itakuwa hakuna!!
 
Masikini weee Tanzania yangu inatapanywa na ma CCM. Yule Karume anapelekwa wapi sasa maana duh sijui watamshikia wapi .Hivi Msekela what did he do kule Dodoma ?
 
Walimkataa wakamchagua Rage lakini Rais anamtaka!

Naona na mimi sasa niingie kwenye siasa manake ukipata utaendelea kupata. Ukikataliwa na wapiga kura kama Rais anakutaka atakuteua tu ukale bata. Ngoja nifanye haraka kabla ya katiba mpya manake naona watanzania wanataka eti kila anayeteuliwa aidhinishwe na bunge! Ikiwa hivyo hata maana ya Urais itakuwa hakuna!!

Mkuu tuweke facts vizuri Rage in no substitute for Dr Msekela. Rage ni mbunge wa Tabora mjini. Dr Msekela was replaced by Shaffin Mamlo Sumar kuwa mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini.

BTW Hongera sana Dr Msekela, japo ninasikitika kuwa tunazika utaalam wa 'High Voltage' kwenye siasa na kudunisha maendeleo but I hope you are enjoying your royal support to the then wanamtandao na sasa JK mwenyewe.

Wishing you all the best. Hoping Mgombelo anajuta kuwavuruga jamaa.
 
Kuna kitu huwa kinanipa shida kuelewa toka uteuzi wa mabalozi au makatibu wote wanakuwa ni wanachama wa ccm mbaya zaidi wengi wao ni wale walishindwa na kuonekani ni dhaifu na wanaccm wenyewe kwenye michakato ya uchaguzi lakini baada ya muda rais anawateua kuwa mabarozi. Barozi anawakilisha nchi nzima na mbunge anawakilisha jimbo, rais anapomteua mtu ambaye wananchi waliona hafai kuwa mbunge lakini rais anaona anafaa kuwa barozi ni udhaifu mkubwa.
 
Huyu naye si Tabora walimkataa Ubunge?

it is high time kwamba mtanzania yeyote mwenye sifa zinazokubalika aweze kuteuliwa kushika nyazifa kama hizi bila kujali his affiliation to any political party
 
Invisible,
Imekuaje hii taarifa inajikanganya? Paragraph ya kwanza inasema taarifa imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi lakini chini kabisa taarifa inaonekana kutolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais. Na hapa ndipo tunagundua kwamba hiyo kurugenzi ya Rais haina kazi bali ilikuwa ni njia ya kumwezesha Salva nae apate Ugali wa Kula!
 
Kuna kitu huwa kinanipa shida kuelewa toka uteuzi wa mabalozi au makatibu wote wanakuwa ni wanachama wa ccm mbaya zaidi wengi wao ni wale walishindwa na kuonekani ni dhaifu na wanaccm wenyewe kwenye michakato ya uchaguzi lakini baada ya muda rais anawateua kuwa mabarozi. Barozi anawakilisha nchi nzima na mbunge anawakilisha jimbo, rais anapomteua mtu ambaye wananchi waliona hafai kuwa mbunge lakini rais anaona anafaa kuwa barozi ni udhaifu mkubwa.

Tatizo si la Rais tatizo ni la mfumo na mtazamo tulio nao watanzania. Katiba ina mpatia rais madaraka ya kuteua watu bila kuulizwa na chombo chochote kile kama bunge n.k. Hivyo kwake yeye anachokiona ni nani amuwakilishe yeye na si nchi. Na kikubwa zaidi nafasi za uongozi Tanzania huchukuliwa kama nafasi za ulaji, hivyo basi kwa CCM wao wanaamini kabisa kuwa wana nafasi ya kwanza ya kula kabla ya mtu mwingine. Na rais asipofanya hivyo watamzingira na kumuweka mtu kati kwenye vikao vyao vya umma na sahani.

Tukibadili mtazamo huu basi tutakuwa tunaweka nchi mbele kabla ya siasa.Maana leo hii hata nafasi za kitaalam zinaangaliwa wewe ni chama gani kwanza badala ya wewe una nini kichwani cha kuongeza value to the country. This is unfortunate to the country na ndiyo maana hatuendi popote tumekalia blah blah. Tunahitaji mageuzi makubwa ya kifikra kwenye hili.
 
Huyu naye si Tabora walimkataa Ubunge?

Hicho ndicho huwa kinanishangaza siku zote. Inakuwaje mtu ambaye wananchi wa jimbo lake hawamtaki halafu rais anamkabidhi ofisi ya umma kubwa hiyo ya ubalozi!!! Nchi hii ndiyo maana itaendelea kuwa kinara wa umaskini siku zote.
 
Back
Top Bottom