Dk. Slaa: UCHAGUZI WIZI MTUPU

Hayo majimbo 3 yaliyoainishwa hapo juu yangetosha kumpa Slaa ushindi?

Mbona mnakuwa na mawazo finyu ma Great Thinkers...Pale ubungo Mnyika alitoa computer zake 2 zisaidie kuhesabu kura kwa mujibu wa gazeti la mwananchi zingekuwa zimetolewa na CCM mngesusia matokeo hata kama Chaadema ingeshinda.

Last but not least huyo Kubenea wa Mwanahalisi ni mwanachama wa chadema mnategemea atakuwa ana report mambo kama yalivyo?

Wake Up great thinkers mtafanya sisi common thinkers tupoteze imani na vichwa vyenu

Kumbe hata wewe usie mwananchama wa Chadema unakubali kuwa kwenye hayo majimbo matatu aliibiwa ila kwa kuwa yasingempa ushindi basi sio ushahidi. Kwa taarifa yako NEC wakikubali kuchakachua kura moja tu JK anaondoka Ikulu sio lazima yawe majimbo matatu.

Kwamba Kubenea ni mwananchama wa chadema unataka kusema Mtanzania, Rai, Sauti Huru, Jambo Leo, Tazama Tanzania, Nipashe, n.k yasomwe na wanan CCM tu kwa kuwa yanamilikiwa na wanachama wa CCM? Kazi ipo
 
muonamambo,
Asante sana kwa comment yako. Najua wengi wangelipenda tutoe Tamko haraka haraka. Mambo magumu hayahitaji ushabiki, wala haraka haraka. Tukumbuke haraka haraka haina baraka. Niseme tu uwizi wa kura mwaka huu ni wa kutisha sana. Hivyo tunajiandaa kikamilifu, ili tutakapotoka kusiwe na shaka lolote. Kuna mambo mawili, tunaweza kutoa Tamko la kisiasa na hatimaye Tamko lenye Data. Lakini pia ujue kuwa Tamko la namna hiyo inatolewa siyo na Dr. Slaa, bali na vyombo vya maamuzi ya Chama,kwani katika siasa hakuna jambo muhimu kama kushirikishana. Naomba subiri, si muda mrefu Tamko litatoka. Ninalotaka kuwahakikishia watanzania ni kuwa hatuwezi kuwaangusha kamwe,
na wala hatuwezi kuwauza.
Tunawaahidi Watanzania kuwa Wabunge takriban 45 wa Chadema wataendeleza jitihada za kumkomboa Mtanzania. Ajenda ya Wabunge wetu licha ya kushughulikia majimbo yao, lakini Wabunge wa Chadema watakuwa katika ujumla wao Wabunge wa Taifa, na watakuwa wakishughulikia kupitia Bunge maswala ya kitaifa ili hatimaye tufikie lengo letu la kumkomboa Mtanzania, wote wanaohitaji ukombozi yaani wakukulima, wafugaji, wafanyibiashara(wasio mafisadi) kwa lugha ya kawaida Walalahoi. Ninachoomba kwa wote wenye nia njema, tuendelee kushikamana, kushirikiana kwani vita vya ukombozi si vya mtu mmoja wala siyo vya kundi la watu au chama fulani tu, bali wote wenye nia na malengo yanayofanana. Najua tuko wengi wenye nia ya aina hii. Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana Wana JF kwa ushirikiano, ushauri, mawazo japo wakati mwingine yamekuwa very critical yametusaidia sana kujielekeza(focused) na kulenga "real issues". Nawashukuru sana wale wote walioniombea muda wote mkono wangu ulipokuwa umevunjika. Nashukuru mkono unaendelea vizuri, na hata sasa kwa mara ya kwanza leo ninafanya "blind typing" kwa mikono yote miwili. Namshukuru sana Mungu. Mungu awabariki nyote na Mungu ibariki Tanzania.
Asante sana Dr. nakuombea katika harakati zako ili hatimaye watanzania wapate haki yao iliyoporwa. Mungu akubariki
 
Sasa nini kifanyike wadau?
Tusiishie kulalamika tu kwani tunazidi kupata vidonda vya tumbo.
Tufanye nini?

Hapa ndiyo umenena. ni sasa tukakaa na kuamua tufanye nini ku rescue situation. Ili kufanikisha hili lazima tushinikize serikali ya JK kubadilisha mfumo wa tume ya uchaguzi. Kwa jinsi ilivyo siyo rahisi kwa vyama vingine kushinda kwani wote waliopo kwenye tume hii ni WATWANA wa CCM/rais ambapo hawawezi kuwaangusha MABWANA wao. Tunaomba wabunge walifikishe hili bungeni na sisi wazalendo tuliunge mkono kwa nguvu zetu zote manake wabunge wa ccm watakataa. Hata hivyo ni vema wadau tuendelee kujadili suala hili ili tufikie muafaka. BIG UP JF family:smile::smile::smile::smile::smile:
 
NYANGE,

ukisoma vizuri waraka wa DK utagundua kuwa amesema bado wanakusanya vielelezo,
nafikiri tuendelee kuwa na subira huku tukiendea kumuombea Ulinzi na Kibali kwa Mungu Ili aweze kusimamia haki kwa mstakabali wa Taifa

"Haki huinua taifa bali ufedhuli ni aibu kwa watu wote"
 
muonamambo,
Asante sana kwa comment yako. Najua wengi wangelipenda tutoe Tamko haraka haraka. Mambo magumu hayahitaji ushabiki, wala haraka haraka. Tukumbuke haraka haraka haina baraka. Niseme tu uwizi wa kura mwaka huu ni wa kutisha sana. Hivyo tunajiandaa kikamilifu, ili tutakapotoka kusiwe na shaka lolote. Kuna mambo mawili, tunaweza kutoa Tamko la kisiasa na hatimaye Tamko lenye Data. Lakini pia ujue kuwa Tamko la namna hiyo inatolewa siyo na Dr. Slaa, bali na vyombo vya maamuzi ya Chama,kwani katika siasa hakuna jambo muhimu kama kushirikishana. Naomba subiri, si muda mrefu Tamko litatoka. Ninalotaka kuwahakikishia watanzania ni kuwa hatuwezi kuwaangusha kamwe, na wala hatuwezi kuwauza.
Tunawaahidi Watanzania kuwa Wabunge takriban 45 wa Chadema wataendeleza jitihada za kumkomboa Mtanzania.
Ajenda ya Wabunge wetu licha ya kushughulikia majimbo yao, lakini Wabunge wa Chadema watakuwa katika ujumla wao Wabunge wa Taifa, na watakuwa wakishughulikia kupitia Bunge maswala ya kitaifa ili hatimaye tufikie lengo letu la kumkomboa Mtanzania, wote wanaohitaji ukombozi yaani wakukulima, wafugaji, wafanyibiashara(wasio mafisadi) kwa lugha ya kawaida Walalahoi. Ninachoomba kwa wote wenye nia njema, tuendelee kushikamana, kushirikiana kwani vita vya ukombozi si vya mtu mmoja wala siyo vya kundi la watu au chama fulani tu, bali wote wenye nia na malengo yanayofanana. Najua tuko wengi wenye nia ya aina hii. Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana Wana JF kwa ushirikiano, ushauri, mawazo japo wakati mwingine yamekuwa very critical yametusaidia sana kujielekeza(focused) na kulenga "real issues". Nawashukuru sana wale wote walioniombea muda wote mkono wangu ulipokuwa umevunjika. Nashukuru mkono unaendelea vizuri, na hata sasa kwa mara ya kwanza leo ninafanya "blind typing" kwa mikono yote miwili. Namshukuru sana Mungu. Mungu awabariki nyote na Mungu ibariki Tanzania.

jamani tazameni hiyo red tuweni na subira.

kinacho takiwa wakusugua goti sugua, wakuomba omba, wakuswali swali, Mungu amtie nguvu DK.
 
mimi ninafikiri tumuachie Dr. nafasi, imani yangu kwa Dr. iliyonifanya mpaka nikampa kura yangu ni kwa sababu yuko makini, kwa imani hii ya umakini wake nina amini atakapo simama na kutamka hoja zake, basi kuzipinga zitakuwa ngumu kwani ushahidi utakuwa ni wa black & white na ni wakati huo sasa kindumbwe ndumbwe kitaanza, mimi binafsi sijachoka kumsubiri Dr. W.P. Slaa. Tuko pamoja.
 
muonamambo,
Asante sana kwa comment yako. Najua wengi wangelipenda tutoe Tamko haraka haraka. Mambo magumu hayahitaji ushabiki, wala haraka haraka. Tukumbuke haraka haraka haina baraka. Niseme tu uwizi wa kura mwaka huu ni wa kutisha sana. Hivyo tunajiandaa kikamilifu, ili tutakapotoka kusiwe na shaka lolote. Kuna mambo mawili, tunaweza kutoa Tamko la kisiasa na hatimaye Tamko lenye Data. Lakini pia ujue kuwa Tamko la namna hiyo inatolewa siyo na Dr. Slaa, bali na vyombo vya maamuzi ya Chama,kwani katika siasa hakuna jambo muhimu kama kushirikishana. Naomba subiri, si muda mrefu Tamko litatoka. Ninalotaka kuwahakikishia watanzania ni kuwa hatuwezi kuwaangusha kamwe, na wala hatuwezi kuwauza.
Tunawaahidi Watanzania kuwa Wabunge takriban 45 wa Chadema wataendeleza jitihada za kumkomboa Mtanzania. Ajenda ya Wabunge wetu licha ya kushughulikia majimbo yao, lakini Wabunge wa Chadema watakuwa katika ujumla wao Wabunge wa Taifa, na watakuwa wakishughulikia kupitia Bunge maswala ya kitaifa ili hatimaye tufikie lengo letu la kumkomboa Mtanzania, wote wanaohitaji ukombozi yaani wakukulima, wafugaji, wafanyibiashara(wasio mafisadi) kwa lugha ya kawaida Walalahoi. Ninachoomba kwa wote wenye nia njema, tuendelee kushikamana, kushirikiana kwani vita vya ukombozi si vya mtu mmoja wala siyo vya kundi la watu au chama fulani tu, bali wote wenye nia na malengo yanayofanana. Najua tuko wengi wenye nia ya aina hii. Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana Wana JF kwa ushirikiano, ushauri, mawazo japo wakati mwingine yamekuwa very critical yametusaidia sana kujielekeza(focused) na kulenga "real issues". Nawashukuru sana wale wote walioniombea muda wote mkono wangu ulipokuwa umevunjika. Nashukuru mkono unaendelea vizuri, na hata sasa kwa mara ya kwanza leo ninafanya "blind typing" kwa mikono yote miwili. Namshukuru sana Mungu. Mungu awabariki nyote na Mungu ibariki Tanzania.

Dr W. Slaa, salaam. Ninashukururu sana kwa taarifa fupi ktk JF. Wengi wamesema mengi, na mimi pia nasema kuwa: tunangoja matamko yote mawili, tamko la kisiasa na lile lenye data.

Tuna shauku ya kusikia na kuona njia ya namna nchi yetu inavyoweza kuepushwa na uhalifu wa demokrasia na ufisadi. Watu wengi tuna mashaka na ushindi wa Kikwete, lakini bila ya kuchukua hatua hata kama ni ya kutoa tamko kali, hali hii itakubalika na kuzoeleka. Na ikizoeleka, itakuwa utamaduni unaojirudiarudia.

Watu wamekuomba, na mimi nikiwa miongoni mwao, utoe tamko hilo, huenda Bwana anataka kufanya jambo la pekee kupitia kwako, jambo la ukombozi wa nchi hii nzuri inayonajisiwa na mibakaji (mibaka uchumi). Mungu akubariki, akulinde, na kukupigania.
 
muonamambo,
Asante sana kwa comment yako. Najua wengi wangelipenda tutoe Tamko haraka haraka. Mambo magumu hayahitaji ushabiki, wala haraka haraka. Tukumbuke haraka haraka haina baraka. Niseme tu uwizi wa kura mwaka huu ni wa kutisha sana. Hivyo tunajiandaa kikamilifu, ili tutakapotoka kusiwe na shaka lolote. Kuna mambo mawili, tunaweza kutoa Tamko la kisiasa na hatimaye Tamko lenye Data. Lakini pia ujue kuwa Tamko la namna hiyo inatolewa siyo na Dr. Slaa, bali na vyombo vya maamuzi ya Chama,kwani katika siasa hakuna jambo muhimu kama kushirikishana. Naomba subiri, si muda mrefu Tamko litatoka. Ninalotaka kuwahakikishia watanzania ni kuwa hatuwezi kuwaangusha kamwe, na wala hatuwezi kuwauza.
Tunawaahidi Watanzania kuwa Wabunge takriban 45 wa Chadema wataendeleza jitihada za kumkomboa Mtanzania. Ajenda ya Wabunge wetu licha ya kushughulikia majimbo yao, lakini Wabunge wa Chadema watakuwa katika ujumla wao Wabunge wa Taifa, na watakuwa wakishughulikia kupitia Bunge maswala ya kitaifa ili hatimaye tufikie lengo letu la kumkomboa Mtanzania, wote wanaohitaji ukombozi yaani wakukulima, wafugaji, wafanyibiashara(wasio mafisadi) kwa lugha ya kawaida Walalahoi. Ninachoomba kwa wote wenye nia njema, tuendelee kushikamana, kushirikiana kwani vita vya ukombozi si vya mtu mmoja wala siyo vya kundi la watu au chama fulani tu, bali wote wenye nia na malengo yanayofanana. Najua tuko wengi wenye nia ya aina hii. Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana Wana JF kwa ushirikiano, ushauri, mawazo japo wakati mwingine yamekuwa very critical yametusaidia sana kujielekeza(focused) na kulenga "real issues". Nawashukuru sana wale wote walioniombea muda wote mkono wangu ulipokuwa umevunjika. Nashukuru mkono unaendelea vizuri, na hata sasa kwa mara ya kwanza leo ninafanya "blind typing" kwa mikono yote miwili. Namshukuru sana Mungu. Mungu awabariki nyote na Mungu ibariki Tanzania.

Tupo pamoja baba, kwa Sala na maombi, na kila lilojema litafanikiwa. Mungu yupo pamoja nawe na tunaomba aendelee kuwa nawe kama alivyokuwa na mtumishi wake Musa na Daudi.
 
Dr.Slaa W.P. nilikuwa na masononeko sana nikiwa natafakari, kwamba;je Dr.atasema chcochote au ndiyo imetoka, lakini nilijipa moyo kuwa lazima ipo siku utatoa neno kuhusu hii catastrophe ya demokrasia, kwa kweli Dr.hili ni JANGA LA KITAIFA ulimwengu unatakiwa utangaziwe kwa njia mbalimbali ili wadau wote duniani wajue huu uozo wa Kikwete.Lakini kwa leo nimefarijika na ninasema endelea kukusanya data ili baadae uweze kutoa informed statement based on informed data.Ni hayo tu
Wewe ndiyo Rais wetu uliyempendeza bwana mungu katika kulitetea Taifa la Tanzania.
 
NYANGE,

ukisoma vizuri waraka wa DK utagundua kuwa amesema bado wanakusanya vielelezo,
nafikiri tuendelee kuwa na subira huku tukiendea kumuombea Ulinzi na Kibali kwa Mungu Ili aweze kusimamia haki kwa mstakabali wa Taifa
Nilimuelewa ila roho inauma, machozi yananitoka nikifikiria!! yaliyotokea. kuona mtu mwenye mzaha asiyejali hali inavyo kwenda anavuruga akili za watu! hili ndilo linalo nisumbua. Naomba tushirikishane pale wanapo kwama. Mi binafsi sijapata kadi ya chama, naamini ntapata tu, ninacho waomba chadema ni kujipanga make hawa watu ni hatari, naamini watatumia fedha nyingi kukivuruga hiki chama. Tafadhari Chadema jipangeni wasije usalama wa taifa wa ccm wakaanza kuvuruga mshikamano uliopo. Hilo ndilo angalizo langu, Maumivu ni mengi, naamini mtu ataumbuka zaidi make bora kuanguka kuliko kukamatwa live unaiba! Ahsanteni.
 
Data zikipatikana, tutaomba Watanzania wote na wale wote wanaoitakia mema Tanzania kama Lisa M Rockerffeller ambao wanapingana vibaya sana na serikali za wizi na ukandamizaji, mara hawa viongozi wote waliobaka Demokrasia wakitokea huko nje ya Mipaka ya Tanzania, basi ni kuandamana na kuwabebea mabango ya kulaani wizi wao.

Nina imani watapunguza hata safari za nje au kuingia na kutoka kimyakimya maana walizoea wakija wanashangiliwa. Hii isijalishe ni PM au Mzee Ruksa maana ni walewale. Watajifanya wamejitenga kwenye uchaguzi ila siku ya mwisho wapo wote pamoja. Wakianza kupata misukosuko mara wanapokuwa nje ya Tanzania, nina imani wataanza kujua Wizi wa Demokrasi si mzuri.

Huyu Lisa aliyekuwa kwenye Facebook ya Kikwete na baadaye wakamfungia na kuondoa maelezo yake yote, waweza kusoma baadhi ya mambo aliyoandika siku chache kabla ya uchaguzi na imekuja kuonekana kweli kuwa alichokuwa akisema, ndicho kimetokea:

https://www.jamiiforums.com/uchaguz...-tanzanians-to-reject-kikwete-a-2nd-term.html
 
"You can not foul all the people all time" iko siku ukweli utajulikana kwa nini chama chenye dola kifanye uongo uliodhahiri kiasi hicho siamini kama hao mawakala ni wa kweli
 
kwa hiyo hawa watu wa NEC wametengeneza matokeo :A S angry::A S angry::A S angry::A S angry:
 
mi nimeshaandaaa manati na silaha zote za jadi kwa ajili ya kusubiri Dr.Apulize kipenga auone ntakachofanya...maana hapa nikiongea napigwa BAN kuwa nachochea vita..Vita ni vita muraaaa
 
muonamambo,
Asante sana kwa comment yako. Najua wengi wangelipenda tutoe Tamko haraka haraka. Mambo magumu hayahitaji ushabiki, wala haraka haraka. Tukumbuke haraka haraka haina baraka. Niseme tu uwizi wa kura mwaka huu ni wa kutisha sana. Hivyo tunajiandaa kikamilifu, ili tutakapotoka kusiwe na shaka lolote. Kuna mambo mawili, tunaweza kutoa Tamko la kisiasa na hatimaye Tamko lenye Data. Lakini pia ujue kuwa Tamko la namna hiyo inatolewa siyo na Dr. Slaa, bali na vyombo vya maamuzi ya Chama,kwani katika siasa hakuna jambo muhimu kama kushirikishana. Naomba subiri, si muda mrefu Tamko litatoka. Ninalotaka kuwahakikishia watanzania ni kuwa hatuwezi kuwaangusha kamwe, na wala hatuwezi kuwauza.
Tunawaahidi Watanzania kuwa Wabunge takriban 45 wa Chadema wataendeleza jitihada za kumkomboa Mtanzania. Ajenda ya Wabunge wetu licha ya kushughulikia majimbo yao, lakini Wabunge wa Chadema watakuwa katika ujumla wao Wabunge wa Taifa, na watakuwa wakishughulikia kupitia Bunge maswala ya kitaifa ili hatimaye tufikie lengo letu la kumkomboa Mtanzania, wote wanaohitaji ukombozi yaani wakukulima, wafugaji, wafanyibiashara(wasio mafisadi) kwa lugha ya kawaida Walalahoi. Ninachoomba kwa wote wenye nia njema, tuendelee kushikamana, kushirikiana kwani vita vya ukombozi si vya mtu mmoja wala siyo vya kundi la watu au chama fulani tu, bali wote wenye nia na malengo yanayofanana. Najua tuko wengi wenye nia ya aina hii. Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana Wana JF kwa ushirikiano, ushauri, mawazo japo wakati mwingine yamekuwa very critical yametusaidia sana kujielekeza(focused) na kulenga "real issues". Nawashukuru sana wale wote walioniombea muda wote mkono wangu ulipokuwa umevunjika. Nashukuru mkono unaendelea vizuri, na hata sasa kwa mara ya kwanza leo ninafanya "blind typing" kwa mikono yote miwili. Namshukuru sana Mungu. Mungu awabariki nyote na Mungu ibariki Tanzania.

Thanx Dr wa Ukweli,
Hii Nchi haiwezi ikabaki kwa Wahuni milee, yatakwisha tu, Mi naamini kuwa pamoja tunaweza. Hawatapora haki zetu milele, Mungu akiwepo upande wetu hakuna atakeyetushinda.
 
Hapa hakuna chakujadili wizi umeshafanyika kilamtu anajua hata aliye iba anajua kuwa tulio ibiwa tunajua, sasa tuambizane tunaanzia wapi natuna fanyanini? je tunakubali kutawaliwa na wezi? hiyo hapana hapana lazima tupambane
 
Back
Top Bottom