Elections 2010 Dk Slaa, Prof Lipumba mambo bado moto

PJ

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
297
32
Dk Slaa, Prof Lipumba mambo bado moto WAGOMBEA urais kwa tiketi ya vyama vya Chadema na CUF jana waliendelea na kampeni zao wakitumia mbinu tofauti za kujenga hoja, huku Willibrod Slaa akimtaka mkuu wa wilaya kupanda jukwaani na Prof Ibrahim Lipumba akiilaumu serikali kwa kuwabana kodi watu wa chini na kuwachia matajiri na makampuni makubwai.

Akiwa wilayani Same, Dk Slaa ambaye anagombea urais kwa tiketi ya Chadema alimkaribisha mkuu huyo wa wilaya, Ibrahim Marwa kupanda jukwaani kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Kwasakwasa na kuungana na viongozi wengine wa chama hicho, lakini alikataa.

Marwa alisema kuwa hawezi kupanda jukwaani kwa kuwa yeye alifika katika eneo kusikiliza tu hivyo hangeweza kukaa mbele ya wananchi.

Kitendo hicho kilimuudhi Dk Slaa ambapo alisema kuwa kitendo cha mkuu huyo wa wilaya kugoma kupanda jukwaani ni kutoitendea haki Chadema na kitu hicho ni cha kichokozi.

"Unachokifanya mkuu wa wilaya si haki na kitendo hiki ni cha kichokozi," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema kuwa kwa mujibu wa sheria mkuu wa wilaya ni mlezi wa vyama vyote vya siasa hivyo hakupaswa kugoma kukaa jukwaa kuu na viongozi wa Chadema.

"Kikwete akipita hapa na nikiona umekaa jukwaa kuu nitalia na wewe ili mshahara wako ambao ni kodi za wananchi ufutwe na utolewe kwenye kazi hiyo," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema kuwa amefanya kazi na mkuu huyo wa wilaya wakati wa kamati za bunge katika wilaya yake na walikuwa pamoja, lakini haamini kama amegoma kukaa nao jukwaani.

"Sikutegemea kama ungenifanyia hivyo na tumefanya kazi wote," alisema Dk Slaa.

Akiwahutubia wananchi wa eneo hilo Dk Slaa alitumia muda mwingi kumchambua mbunge wa jimbo la Same Magharibi aliyemaliza muda wake, Dk Mathayo David Mathayo kwa kumtaka aache kuwadanganya wananchi kuwa amefanya kitu wakati hakuna kitu chochote alichowafanyia wananchi.

"Mathayo ampishe mwanaume wa Chadema awasaidie wananchi kwa kuwa Mathayo ameshindwa kazi na amekuwa akitoa fedha kwenye shule ambazo haziwezi kuwasaidia kitu chochote,"alisema Dk Slaa.

"Nilikutana na Mathayo bungeni baada ya kutoka jimboni kwake akaniuliza kwa nini nimemshtaki kwa wapigakura wake na mimi nikawaambia nimewaeleza ukweli na ndiyo maana Mathayo hanisalimii," alisema Dk Slaa.

Naye Frank Kimboy anaripoti kutokas Pangani kuwa Prof Lipumba, ambaye anawania urais kwa tiketi ya CUF, ameendelea kujenga hoja kuhusu gharama za safari za mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete akisema zinatafuna fedha za walipa kodi.

Pia alisema serikali imekuwa makini katika kukusanya kodi kwa kampuni ndogo za wazawa ndani ya nchi wakati kampuni kubwa, hasa zile za sekta ya madini zikifurahia misamaha ya kodi.

"Tangu Rais Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, zaidi ya Sh11 trilioni zimepotea na hazina maelezo ya maana na nyingi zimetumiwa vibaya katika rushwa kubwa kubwa kama ile ya mkataba tata wa Richmond na kashfa nyingine ambazo bila shaka mtakuwa mmezisikia,” alisema Prof Lipumba.

Alisema serikali ya CCM imeshindwa kuwajibika kutoa maelezo kuhusu matumizi ya zaidi ya Sh 11.8trilioni katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Alisema kuwa fedha hizo huenda zimetumika kwa shughuli tofauti na matumizi ya serikali au ziliibwa na wanasiasa wasiokuwa na maadili.

Mojawapo ya matumizi mabaya ya fedha hizo alisema Profesa Lipumba na manunuzi ya ndege ya rais ambayo ni ghali inatumia mafuta mengi kiasi cha Sh9 milioni kwa saa moja inapokuwa angani.

"Kutokana na safari nyingi alizozifanya Rais Kikwete nje ya nchi, mnaweza kuona ni kiasi gani cha fedha za walipa kodi kilivyoteketea," alisema Lipumba.
Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Source: Mwananchi

My Take: Kama 11 trilion zinapotea bila maelezo serikali itashindwaje kusomesha watanzania bure kama anavyoadvocate Dr. Slaa. Do we really need foreign aid to sustain our economy? we need abled leaders to make efficient use of available resources for development as a nation
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom