Elections 2010 Dk Slaa ni mkweli: Raia mwaminifu na kiongozi bora

Gobret

JF-Expert Member
Jun 11, 2010
320
88
Nimeamua kutumia maneno hayo kwa sababu nina shindwa kupata neno la kutumia badala yake. Si kawaida kuona watu wa namna hii. Mtu huyu si mbinafsi na amejitoa kwa maslahi ya watu wake. Watu wa Karatu ninawaheshimu sana kwa kumleta na kumruhusu agombee urais wa Tz kwa ridhaa yenu. Watu wa Karatu walikuwa na hofu kuwa kugombea kwake urais wao watapoteza mtu makini lkn kwa sasa wameelewa kuwa si kupoteza bali kupata. Wengi hatumwelewi vizuri Dk Slaa kwa sababu tu tuna desturi ya kuongozwa na CCM. Mwl Nyerere kama mtakumbuka alishasema CCM si mama yake na muda wowote atatoka akitaka. Wengine wana nena kuwa ni mkristu tena mkatoliki. Huu ni upuuzi mtupu. Wengine wamefika mbali kwa kusema ni padri aliyeasi hivyo hafai kuwa kiongozi. Kweli hafai kuwa kiongozi? Kuwa kiongozi tunapima nini? Uaminifu, uzalendo wake na uwezo wake. Hatuongozwi na chama, ukabila, udini wetu bali watu walio na maadili ya uongozi. Watu wenye maadili ya uongozi sasa hawapo CCM, wapo nje ya CCM. Ona wanavyofanya kwenye kura za maoni, hizo ni kufuru. Ni kweli kwamba tunawashabikia watu wa namna hii. Ndio maana wanatukana wanavyopenda hadharani.............sitaki kura zenu........acheni kazi...........Mungu akupe nini sisi binadamu na hali hatuna umaskini wa mawazo. Inatosha sasa. Vijana, wazee, wababa na wamama wakati ni wetu kuionyesha CCM kuwa imetosha, na enzi na nyakati zao zimepita. Tuanza na tumalize na Dk Slaa. God bless DK SLAA.
 
Sina wakati wala nafasi ya kukudanganya, Si wapo wanaokushawishi kwa rushwa.Endelea kushawishika wala usidanganyike. Watanzania waliojeruhiwa safari hii wataamua kumchagua Dk Slaa ili iwe kwa serikali ya CCM isiyosikivu. Watanzania wake kwa waume tujitokeze tumpigie kura Dk Slaa, pamoja na madiwani na wabunge atakaowasimamisha. Tuweke pembeni udini wetu. Tumpe njia. Wale wanaodai mahakama ya kadhi mwulizeni kwa upendo atawasaidia vipi ktk kulitafutia suluhisho la kudumu suala hili. Yeye kama kasisi wa zamani na mwenye shahada ya uzamivu ya sheria ya dini sheria dunia atawasaidia. Naamini ana namna bora ya kulitatua hili jambo si tu kwa waislamu tu bali hata kwa wakristu. Tukumbuka kwamba serikali yetu haina dini ila sisi tunaoichagua serikali tuna dini zetu. Haiwezekani tukashindwa kuelewana kwa misingi ya dini. Serikali ni nini mbele ya watu. Watu huiamulia nini serikali kifanye na kama serikali haitaki kusikia kuna namna nyingi tu ya kuiadhibu serikali kama hii. Mimi kama mkristu ninawapenda sana waislamu na ninaona hoja yao na umuhimu wa mahakama hii. Waislamu ni raia kama raia wengine na wana haki zao za kuamini wanachodhani ndio msingi wa imani yao. Hofu yetu wakristo ni kuwa itakuwaje baada ya mahakama ya kadhi? Hoja si kupinga tu bali nini suluhisho la haya yote? Wakristu nao wanataka mahakama yao? Ni sawa, hakuna ubaya wowote ktk hili. Sasa huu ndio muda mwafaka wa kumhoji DK SLAA atalichukuliaje jambo hili. Hili si suala la lelemama. Tusipolipatia ufumbuzi litatusumbua siku za baadaye, wakati huo wakristu na waislamu hawaelewani, hawasaidiani, hawasalimiani na wengine ni watoto wa baba na mama mmoja lkn hawaongei kisa wametofautiana kiimani. Nini maana ya serikali isiyo na dini? Tuielewe falsafa hii kwanza. Ni serikali ya watu wenye dini/imani tofauti-tofauti isiyoruhusu upendeleo kwa dini/imani moja. Kumbe uwezekano wa kuwa na chombo cha pamoja kushughulikia mambo yetu ya imani kila mtu kwa imani yake ili mradi sheria zingine za nchi za kikatiba hazivunjwi na katiba ikaeleza hivyo na chombo hichi kikaundwa kwa mujibu wa sheria ya nchi. HATUTAKI KUKOSA UELEWANO KATI YETU WATANZANIA. TUMWULIZE DR SLAA NA WATU WAKE WATALICHUKULIAJE SUALA HILI. NINA IMANI KUBWA KWA DR SLAA KUWA ANA MANENO YA BUSARA KULIFANYIA KAZI JAMBO HILI. God bless Dk SLAA.
 
Pia naunga mkono Hoja, Nadhani hii ni nafasi pekee pia kwa watanzania kuweka maslahi ya nchi mbele sio kung'ang'ania mazoea na kuogopa mabadiliko kwa sababu iwayo yote.Ninaona Tanzania yenye sura mpya mbele kwa kumuunga mkono Dr.Slaa.
 
Angalau nimemepata mtu ambaye nadhani labda atasafishe nchi na ushenzi huu ulio jaa Tanzania.Siajabu hata wale watukanaji ndani ya Jamiiforums akawashikisha adabu!ANGALIZO:Kura yangu nitakupa Slaa, lakini usije ukanisaliti.

Nimeamua kutumia maneno hayo kwa sababu nina shindwa kupata neno la kutumia badala yake. Si kawaida kuona watu wa namna hii. Mtu huyu si mbinafsi na amejitoa kwa maslahi ya watu wake. Watu wa Karatu ninawaheshimu sana kwa kumleta na kumruhusu agombee urais wa Tz kwa ridhaa yenu. Watu wa Karatu walikuwa na hofu kuwa kugombea kwake urais wao watapoteza mtu makini lkn kwa sasa wameelewa kuwa si kupoteza bali kupata. Wengi hatumwelewi vizuri Dk Slaa kwa sababu tu tuna desturi ya kuongozwa na CCM. Mwl Nyerere kama mtakumbuka alishasema CCM si mama yake na muda wowote atatoka akitaka. Wengine wana nena kuwa ni mkristu tena mkatoliki. Huu ni upuuzi mtupu. Wengine wamefika mbali kwa kusema ni padri aliyeasi hivyo hafai kuwa kiongozi. Kweli hafai kuwa kiongozi? Kuwa kiongozi tunapima nini? Uaminifu, uzalendo wake na uwezo wake. Hatuongozwi na chama, ukabila, udini wetu bali watu walio na maadili ya uongozi. Watu wenye maadili ya uongozi sasa hawapo CCM, wapo nje ya CCM. Ona wanavyofanya kwenye kura za maoni, hizo ni kufuru. Ni kweli kwamba tunawashabikia watu wa namna hii. Ndio maana wanatukana wanavyopenda hadharani.............sitaki kura zenu........acheni kazi...........Mungu akupe nini sisi binadamu na hali hatuna umaskini wa mawazo. Inatosha sasa. Vijana, wazee, wababa na wamama wakati ni wetu kuionyesha CCM kuwa imetosha, na enzi na nyakati zao zimepita. Tuanza na tumalize na Dk Slaa. God bless DK SLAA.
 
Rushwa inayozidi kuota mizizi kila kukicha, serikali isiyojali wananchi wake (hahitaji kura ya wafanyakazi), serikali inayokumbatia mafisadi, rais mtembeza bakuli kila kukicha (anaomba mpaka net za mbu) ukosefu wa vipaumbele (miaka 5 isiyo na tija hata kidogo, tulichoambulia ni mfumuko wa bei na tabasamu kubwa), kwa hayo na mengine mengi sihitaji kutafuta mchawi wala sihitaji kuwa shabiki wa vyama vya siasa Kura yangu ni kwa Dr SLAA.
 
HATUTAKI KUKOSA UELEWANO KATI YETU WATANZANIA. TUMWULIZE DR SLAA NA WATU WAKE WATALICHUKULIAJE SUALA HILI. NINA IMANI KUBWA KWA DR SLAA KUWA ANA MANENO YA BUSARA KULIFANYIA KAZI JAMBO HILI. God bless Dk SLAA.

Binafsi naamini suala la mahakama ya akdhi ni jambo la muhimu kujadiliwa kwa sasa. Hata hivyo naelewa kuwa hili SIO SUALA LA RAISI bali NI SUALA LA KATIBA. Hakuna raisi mwenye mamlaka ya kubadili katiba, bali ni wananchi wenyewe. Hivyo nina uhakika hata nikimuuliza Dr. Slaa au mgombea mwingine leo juu ya hili na mengine yanayokinzana na katika leo atanijibu kuwa yeye hana maamuzi bali atawaachia wananchi kama wataamua kubadili katiba kihalali na kwa njia zianazokubalika, basi maamuzi yao yatachukua mkondo...
 
Back
Top Bottom