Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 481
Mimi nina kila sababu ya kujivunia kwa hatua tuliyofikia hadi sasa. Kusema ukweli hadi sasa tumefanya vizuri sana. Siwezi kusema kuwa tumeshindwa hadi sasa. majimbo yote ambayo mpaka sasa hayajatangazwa tuelewe kuwa hali ni tete kwa ndugu zetu wa kijani. Moja tu ambalo natamani kuliona ni 2015. Tunaenda kufanya historia hata kama sitokuwepo ila kuna watu wataandika historia hiyo. Take it from me 2015 ni mwisho wa utawala wa watu wa kijani. No matter kuwa ni chama gani kitachukua nchi ila moyo wangu unanituma kuwa wakati umewadia sasa kwa nchi hii kuandika historia na hii ndiyo inayotokea.
Changamoto kuu sasa baada ya uchaguzi huu (kama uchakachuaji utapata fursa) basi wito wangu ni kwa vyama vyote vya siasa kukaa chini na kuacha ubinafsi ili tuweze kujenga umoja wa upinzani. Chonde chonde hebu tukae meza moja na kujua twataka nini ili tuweze kuikomboa nchi hii nzuri yenye kila kitu.
Kumbuka ule wimbo mzuri
Tazama ramani utaona nchi nzuriiiiiiiiiiii
yenye mito mingi na mabonde mengi ya nafakaaaaaaaaaaaa
Mungu ibariki Tanzania